Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya
Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi.
Veila Shoo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya
Utendaji Kazi kwa Wajumbe kutoka katika Wakala mbalimbali za Serikali
katika ukumbi wa Wakala za Serikali katika kikao kilichofanyika ukumbi
wa Wakala kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo. Katikati ni Mkurugenzi wa
Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw.
Mick Kiliba na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA), Bw. Dominic Rwekaza.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi
na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba akifungua
kikao cha Mrejesho wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Mifumo na Viwango
vya Utendaji kazi kwa Wakala za Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa
Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi
na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba akiongoza
mjadala katika kikao cha Mrejesho wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa
Mifumo na Viwango vya Utendaji kazi kwa Wakala za Serikali
kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao
(TaGLA) leo.
Baadhi ya washiriki kutoka Wakala
Mbalimbali za Serikali wakifuatilia mada katika kikao cha Mrejesho wa
Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji kazi kwa
Wakala za Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa
Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Henry Mambo akichangia mada kuhusu
taarifa ya utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kwa
Wakala mbalimbali za Serikali katika ukumbi wa Wakala za Serikali katika
kikao kilichofanyika ukumbi wa Wakala kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.
No comments :
Post a Comment