Monday, November 28, 2016

TANGA YAWATAKA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI INDIA KUWEKEZA ILI KUNUFAIKA NA FURSA ZILIZOPO

Balozi wa India nchini Tanzania ,Sandeep Arya kushoto akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi.
Balozi wa India nchini Tanzania ,Sandeep Arya akizungumza wakati wa kongamano hilo kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na Waziri wa
Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye

Balozi wa India nchini Sandeep Arya kushoto akiteta jambo na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Mnauye
katikati wakati wa kongamano la wafanyabiashara kutoka nchini India na Tanga uliofanyika ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini India na

Tanga wakimfuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias
Mwilapwa wakati akifungua kongamano la
wafanyabiashara juzi kwenye
ukumbi wa hotel ya Tanga Beach Resort
 
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa amewakata wawekezaji kutoka nchini India kuwekeza mkoani hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kiuchumi zikiwemo kilimo,utalii,elimu na Afya ili kuweza kunufaika nazo.
 
Mwilapwa alitoa kauli hiyo juzi wakati akifungua kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India uliofanyika katika
hotel ya Tanga beach jijini Tanga uliowahusisha wafanyabiashara kutoka India na Mkoa wa Tanga.
 
Kongamano hilo lilikuwa na lengo lilikuwa ni kushirikisha mawazo na kuona ni kwa namna gani wanaweza kuzitumia
fursa mbalimbali zilizopo mkoani hapa ili kufanya uwekezaji ambao utaweza kuleta tija ya kimaendeleo.
 
Alisema kuwa India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukuza uchumi kwa baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania hivyo uwepo wao katika suala la uwekezaji linaweza kuwa chachu ya kuweza kuinua kasi ya ukuaji wa maendeleo.
“India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukua kwa uchumi kwa baadhi ya nchi dunia ikiwemo Tanzania kutokana na hilo niwatake muona namna ya kuwekeza mkoani hapa kwani yapo maeneo mengine mnayoweza kufanya hivyo “Alisema.
Awali akizungumza Balozi wa India nchini,  Sandeep Arya alisema ujio wa Waziri Mkuu wa India Tanzania umeongeza ari kwa Taifa ilo kuona haja ya kuendelea kuwekeza na kusaidia katika masuala mbalimbali ya afya, Elimu Bishara na Kilimo.
 
Alisema kuwa soko la India linahitaj bidhaa zenye ubora na rahisi hivyo anaamini kutokana na ushirikiano wa nchi hizi
mbili kufanana mahitaji kutakuwepo na fursa kubwa ya muingiliano wa kibiashara ambao utaleta tija na faida kwa pande zote mbili.
Hata hivyo alisema licha kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo ya maji, matibabu ya kansa lakini
wanatoa nafasi 350 za mafunzo nchini india kila mwaka ili kuwapatia nafasi watu kujifunza jinsi India inavyofanya kazi katika shughuli zake za uzalishaji.
 
Naye, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikaribishwa kuzungumza alisema moja kati ya mipango ya Serikali ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli ni kuhakikisha inakuza uchumi na kuleta maendeleo kwa mwananchi wa hali ya nchi hivyo hakuna haja ya wananchi kukata tamaa.
 Nape alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa kuzitumia fursa zilizopo hapa nchini ili kuhakikisha zinaleta manufaa kwa
wananchi kwa kukuza vipato vyao na hata kuongeza pato la Taifa.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments :

Post a Comment