Mtendaji Mkuuwa Wakala wa Ufundi na
Umeme TEMESA Dkt. MussaMgwatu ( kushoto) akizungumza na Meneja wa
TEMESA Kigoma Mhandisi Hassan Karonda (kulia) alipotembelea kituoni
hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu( mwenyeshaji la rangi yabluu)
akijadili jambo na mafundi wa karakana ya TEMESA Kigoma alipotembelea
kituoni hapo kujionea utendaji kazi.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt.
Mussa Mgwatu (aliyeketi) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalam James
Frank jinsi mfumo wa kielektroniki wa kukatishia tiketi katika kivuko
cha Ilagala Mkoani Kigoma unavyofanya kazi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (wa pili kulia) akiongozana na Meneja
wa TEMESA Kigoma Mhandisi Hassan Karonda (kulia) baada ya kukagua
kivuko cha MV. Malagarasi kinachotoa huduma ya usafiri katika Mto
Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma.
………………………………………………………………………………
Na Theresia Mwami TEMESA Kigoma.
Shirika la umeme Tanzania TANESCO
linadaiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kigoma kiasi cha
shilingi milioni 41 ikiwa ni malimbikizo ya madeni kutokana na
matengenezo ya magari mbalimbali yaliyofanywa na shirika hilo mkoani
humo.
Hayo yameelezwa na Meneja wa
TEMESA Mkoa wa Kigoma Mhandisi Hassan Karonda alipokuwa akitoa taarifa
ya utendaji kazi kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu
alipotembelea kituoni hapo.
Meneja huyo ameeleza kuwa kwa
sasa TEMESA Kigoma ipo katika operesheni ya kukusanya madeni kutoka kwa
Taasisi na makampuni wanayoyadai.
“Mtendaji Mkuu tunazidai Taasisi
mablimbali kiwemo Shirika la Umeme Tanzania TANESCO shilling million 41
mpaka sasa” alisema Mhandisi Karonda.
Hata hivyo Dkt. Mgwatu alimtaka
Mhandisi Karonda kuhakikisha kuwa anakusanya madeni yote anayodai
mkoani humo haraka iwezekanavyo.
“ Fuatilia ofisi kwa ofisi
kukusanya madeni ili kukiwezesha kituo hiki kufanya kazi zake kwa
ufanisi mkubwa” alisisitiza Dkt. Mgwatu.
Akiwa katika ziara ya kikazi
mkoani humo Dkt. Mgwatu pia alipata fursa ya kutembelea kivuko cha MV.
Malagarasi na kuona utendaji kazi wake.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo
vya TEMESA nchi nzima kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo.
No comments :
Post a Comment