Thursday, November 24, 2016

SERIKALI YATOA MAFUNZO YA TATHMINI NA UFUATILIAJI KUBORESHA UTENDAJI

sil1
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba akitoa maelezo kuhusu Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
sil2
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi Susan Mlawi, akifungua Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
sil3
Baadhi ya washiriki kutoka Wizara Mbalimbali wakifuatilia mada wakati wa Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
sil4
Mshiriki wa Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi Mariam Silim akitoa neno la shukrani kwenye Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
sil5
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi Sakina Mwinyimkuu akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

No comments :

Post a Comment