Wednesday, November 30, 2016

RAIS MAGUFULI AMUANDALIA DHIFA YA TAIFA MGENI WAKE RAIS WA ZAMBIA, EDGAR LUNGU


 Rais John Magufuli, akiongozana na Mgeni wake, Rais wa Zambia Edgar Lungu, (kushoto), wakati wakisalimiana na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Naibu Spika wa bunge, Dkt.Tulia Ackson, wakati wa dhifa ya kitaifa ambayo Rais Magufuli alimuandalia Mgeni wake usiku wa kuamkia leo Novemba 29/2016 Ikulu jijini Dar es Salaam.(PICHA NA IKULU).




































Rais mpya wa Chama Cha Riadha Tanzania, (RT), Anthony Mtaka

Mwananchi wa Kerege Bagamoyo, akipatiwa matibabu wakati wa zoezi la kambi ya matibabu bure  katika mji huo. Klabu ya Rotary ya Oyster Bay pamoja na madaktari na wafanyakazi wa kujitolea wametoa huduma za matibabu kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo. Kambi hiyo ya matibabu imeeefanyika Jumapili tarehe 27 Novemba katika shule ya Msingi ya Kerege.
Zoezi la Kambi hiyo ya matibabu na upimaji bure likiendelea katika mji huo wa Kerege.
Mmoja wa wananchi wa Kerege (kulia) akipima macho katika kambi hiyo.


Klabu ya Rotary ya Oyster Bay pamoja na madaktari na wafanyakazi wa kujitolea wametoa huduma za matibabu kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo. Kambi hiyo ya matibabu imeeefanyika Jumapili tarehe 27 Novemba katika shule ya Msingi ya Kerege.

Vipimo na matibabu vilitolewa bure kwa magonjwa kama vile malaria, upungufu wa damu, kisukari na shinikizo la damu, masikio, pua na koo (ENT), magonjwa ya ngozi, macho pamoja na meno. Huduma nyingine zilizotolewa zilikuwa pamoja na ugawaji wa miwani zilizotolewa kwa watu waliokutwa na matatizo ya macho.

Huduma za ushauri kwa wajawazito na vifaa vya kujifungulia vilitolewa bure kwa wajawazito; huduma za ushauri nasaha na upimaji wa UKIMWI pia zilitolewa. Kwa mara ya kwanza, elimu ya usafi na taulo za wanawake zilitolewa kwa wasichana.

Akizungumza katika kambi hiyo, Alfred Woiso, Rais wa Klabu ya Rotary ya Oyster Bay alisema, “Ni furaha yetu kuwa hapa kwa mara nyingine tena na tunafurahi kuona wakazi wa Kerege wamejitokeza kuja kupata huduma hizi. Tumetoa huduma kwa watu waliokuwa na matatizo mbalimbali. Tumeona wagonjwa wengi wenye magonjwa sugu kama kisukari na shinikizo la damu. Inaonekana kuna haja ya kupanua wigo wa huduma zetu kwa vile kuna mahitaji ya huduma za matibabu ya magonjwa mengine.”

Kambi hiyo ya matibabu ilihudhuriwa na wagonjwa wapatao 800 kutoka Kerege na maeneo ya jirani. Kambi hii inayoandaliwa na Klabu ya Rotary ya Oyster Bay imefanyika Kerege kwa mara ya sita sasa kwa lengo la kuwasaidia wakazi wa Kerege kupata huduma za matibabu, wakazi ambao kwa kawaida hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Kambi hiyo ya matibabu imedhaminiwa na Diamond Trust Bank na kuandaliwa kwa ushirikiano na Shree Hindu Mandal Hospital, Vital Supplies, Whitedent, vClick Concepts Inc, MAK Books and Brains, ABACUS Pharmaceuticals, Fazel Foundation na wanachama wa Klabu ya Rotary na Rotaractor.
 Rais John Pombe Magufuli, akizungumza huku mgeni wake, Rais wa Zambia, Edgar Lungu, akimsikiliza, wakati Rais alipomkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam, Novemba 28, 2016. (PICHA NA IKULU)
 Rais Lungu akizungumza
 Rais Magufuli akizungumza

 Rais Magufuli na mgeni wake, Rais Lungu, wakifurahia jambo, wakati Rais huyo wa Zambia alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Novemba 28, 2016
 Rais Magufuli, na mgeni wake Rais Lungu, wakitazama ngoma za asili
 Rais Magufuli na mgeni wake, wakipita katikati ya gwaride la wanajeshi wa JWTZ, wakati wa mapokezi yake Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Magufuli akimpokea Rais Lungu alipowasili Ikulu

No comments :

Post a Comment