Wednesday, November 23, 2016

RAIS BARACK OBAMA ATOA MEDALI ZA RAIS ZA UHURU KWA NYOTA KADHAA NA WATU MASHUHURI

WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2016 WAANZA KAMBI

Warembo wanaoshiriki katika mashindano ya Miss Universe Tanzania 2016 wakiwa wamesimama mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,Fainali itafanyika Novemba 25 katika Hoteli ya Collessium iliyopo Oysterbay.
Warembo wanaoshiriki katika mashindano ya Miss Universe Tanzania 2016 wakiwa wamesimama mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,Fainali itafanyika Novemba 25 katika Hoteli ya Collessium iliyopo Oysterbay.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications L.T.D,Maria Sarungi Tsehai (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,kuhusu kuanza kambi kwa warembo wa Miss Universe Tanzania 2016 ambapo fainali itafanyika Novemba 25 katika Hoteli ya Collessium iliyopo Oysterbay. Kulia ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Collessium,Mustafa Dhanji na Mratibu wa shindano hilo,Mwanakombo Salim.(PICHA NA ELISA SHUNDA)

TAASISI YA VIJANA YA TYVA NA IRI ZATOA ELIMU YA KATIBA KWA VIJANA WA PEMBA NA UNGUJA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la katiba Zanzibar, Profesa Abdul Shariff akizungumza kuhusu umuhimu wa asasi za kiraia kutoa elimu juu ya Katiba Pendekezwa katika kongamano lililofanyika Unguja lililoandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA pamoja na IRI.
Mbunge wa Viti maalum Pemba-Zanzibar, Mheshimiwa Zainabu Mussa Bakari akizungumzia Haki na Wajibu wa mwananchi Kikatiba wakati wa ufunguzi wa Kongamano lililowashirikisha vijana mbalimbali kutoka kisiwani Pemba ili kujadili katiba mpya lililoandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA pamoja na IRI.
Baadhi ya vijana wakipitia katiba wakati wa kongamano lililowakutanisha vijana hao ili kujadili haki na wajibu wa wananachi katika katiba mpya.

BALOZI SEIF AKUTANA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UHANDISI YA NAIF

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhandisi ya Naif { Naif Engeneering Company } Bibi Khadija Naif Alyafei hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

No comments :

Post a Comment