NA
TIGANYA VINCENT-MAELEZO- DAR ES SALAAM
Novemba 5, mwaka huu ni mwaka
mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli alioapishwa kuwa kiongozi na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama wa nchi hii.
Katika kipindi cha mwaka mmoja
cha utawala wa Rais Magufuli nchini, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF) kwa upande wake umesaidia Watanzania wanaopata huduma za Jamii kupitia
PSPF kuongezeka kutoka 394,494 hadi kufikia 444,679 ikiwa ni sehemu ya
utekeleza wa agizo lake.
Hatua hii ya PSPF imelenga
kutekeza agizo na kutimiza ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania aliyokuwa akitoa ya kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanufaika na
huduma za Hifadhi za Jamii ikiwemo huduma za Bima za afya wakati wa kampeni na
baada ya kuingia madarakani.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka
mmoja kwa upande wa Mfuko wa PSPF iliyotolewa na Costantina Martin kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF ,idadi hiyo hii inajumuisha Watanzania walio katika
sekta rasmi na isiyo rasmi nchini.
Kundi hili kubwa lilikuwa
limesaulika kujumuishwa katika hifadhi ya jamii , lakini baada ya Mhe. Rais
Magufuli kulizungumzia katika kampeni zake hivi sasa mwamko wa kujiunga na
hifadhi ya jamii umeongezeka na PSPF imeanza kulitekeleza agizo hilo kwa
kuwahamasisha wananchi waliopo katika sekta isiyo rasmi na sekta rasmi
kuchangia na kujiunga katika Bima ya Afya.
Katika kuhakikisha kuwa azma hiyo
inatimizwa tayari PSPF imeingia makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya(NHIF) kwa lengo la kufikisha huduma za afya kwa watanzania wengi ambao
wapo katika sekta isyo rasmi na hivyo kujenga jamii yenye afya bora
inayochangia katika ujenzi wa nchi.
Chini ya makubaliano yanawasaidia
wanachama wa PSPF walio katika Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kuweza kupata ya
tiba kupitia NHIF kwa gharama ya shilingi 76,800/- kwa mwaka katika hospitali
mbalimbali ziliingia makubaliano na Mfuko huo wa Bima ya Afya.
Mpango huo wa PSPF unaounga mkono
juhudi za Rais Magufuli za kutaka kuhakikisha kuwa wananchi wengi wanapata
huduma na matibabu nchi nzima kwenye vituo vyote vilivyosajiliwa na NHIF
kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa kwa gharama nafuu.
Hivi sasa huduma hiyo ya PSPF
kuwadhamini wananchama wake kwa ajili ya kupata matibabu imesaidia watanzania
wengi sana kunufaika na huduma hii husasan katika kipindi cha mwaka mmoja wa
Rais Magufuli.
Akifungua rasmi Bunge la 11 la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Rais Magufuli alisema kuwa dhamira ya kujenga
uchumi wa kisasa na suala la kupambana na umaskini linakwenda sambamba na kuwa
na wananchi wenye afya bora.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu
ya Tano itahakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kwa kuhamasisha
wananchi wengi wanajiunga na Bima ya Afya.
Katika kutekeleza hilo PSPF kwa
kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) imeshawafikia Watanzania
2,710 walio katika sekta isiyo rasmi kuanza kunufaika na huduma za Afya
kupitia PSPF.
Mbali na sekta ya afya , katika
kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli PSPF kwa upande wake imesaidia
kuhakikisha kuwa Tanznaia inakuwa Nchi ya Viwanda kwa lengo la kutoa ajira kwa
Watanzania walio wengi.
Viwanda hivyo ambavyo PSPF
imewekeza ni pamoja na 21st Century cha Morogoro, Saruji Tanga.
Martin ameongeza kuwa hivi sasa
PSPF imejipanga kuwekeza katika Kituo cha Biashara cha Kurasini (Kurasini
Logistic Center) kwa lengo la kuchochea uwekezaji wa viwanda na kutoa ajira kwa
wananchi.
Viwanda vingine ambavyo PSPF
imejipanga kuwekeza ni kile cha Nguo cha Urafiki, Morogoro Canvas Mill na
Kiwanda cha Viatu Karanga kilichopo Moshi.
Hatua hiyo iliyoanza kutekelezwa
na PSPF ni sehemu utekelezaji hotuba ya Mhe. Rais Magufuli wakati anafungua
rasmi Bunge 11 mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka jana ambapo alisema kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano itaweka mkazo katika ujenzi wa viwanda ili mwaka 2020
idadi ya ajira itokanayo na viwanda ifikie asilimia 40 ya ajira zote hapa
nchini.
PSPF ilianzishwa kwa sheria ya
Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Watumishi wa Umma namba 2 ya mwaka 199 . sura ya
371 na inatoa huduma za Hifadhi ya Jamii katika Mapngo wa lazimana wa hiyari.
Balozi
wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer
akisalimiana na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha
Nelson Mandela Profesa Karoli Njau, wakati wa ziara ya balozi huyo
chuoni hapo.
Pichani
juu na chini ni Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya EU kwa nchi za Afrika
Mashariki Roeland Van De Geer akihutubia wanafunzi wa vyuo mbalimbali
katika ukumbi Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela ambapo
alifanya ziara ya kutembelea Chuo jijini Arusha.(Picha na Ferdinand
Shayo).
Kaimu
Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela
Profesa Karoli Njau akifafanua jambo katika ziara ya Balozi wa Umoja wa
Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki, Roeland Van De Geer
alipotembelea chuo hicho.
Balozi
wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer
akisalimiana na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha
Nelson Mandela Profesa Karoli Njau, wakati wa ziara ya balozi huyo
chuoni hapo.
Picha
ya pamoja ya washiriki wa semina ya malengo ya dunia ya Umoja wa
Mataifa katika Chuo cha Nelson Mandela wakiwa na Balozi wa Umoja wa
Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki, Roeland Van De Geer.
Picha ya pamoja ya washiriki wa semina ya malengo ya dunia ya Umoja wa Mataifa katika Chuo cha Nelson Mandela jijini Arusha.
Kaimu
Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela
Profesa Karoli Njau (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na
Wawakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu (wa pili kushoto)
na Amon Manyama (kushoto).
Ofisa
mkuu wa Biashara wa Tigo Shavkat Berdiev (kushoto), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kampuni ya Simu
ya Tigo kuja na vifurushi vipya vya intaneti ;Mega Mix'. Kulia ni
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
WAKATI
Bunge la Tanzania wiki hii linatarajiwa kujadili na kupitisha muswada
wa habari, Shirika la Umoja wa mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni
(UNESCO) limehadharisha juu ya uwapo wa sheria zinazotishia uhuru wa
vyombo vya habari.
Akizungumza
katika kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho
ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, Mkuu wa
idara ya mawasiliano na habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe
Legay alisema katika utekelezaji wa maendeleo endelevu sekta ya habari
ni muhimu na hivyo watendaji wake wanatakiwa kuwekewa mazingira huru ya
kiutendaji.
Serikali
ya Tanzania imepeleka muswada wa habari ambao unalalamikiwa na wadau wa
habari kwamba haukupatiwa muda wa kutosha wa kujadiliwa na kuondolewa
kwa vipengele ambavyo vinawanyima waandishi wa habari uwezo wa kuandika.
Mkuu
wa idara ya mawasiliano na habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania,
Christophe Legay akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
kufungua kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho
ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari,
lililofanyika jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari na Zainul
Mzige wa Modewjiblog)
Aidha
ndani ya muswada huo imeelezwa na Jukwaa la Wahariri kwamba kuna
vipengele ambavyo vinakwamisha umahiri wa uandishi na uchunguzi kama
kufutiwa kwa leseni na kuuzwa kwa mitambo kutokana na makosa mbalimbali
ambayo yamegeuzwa ya jinai.
Aidha
wadau hao wanasema kwamba serikali imejitengenezea nafasi ya kuwa na
nguvu kubwa ya kudhibiti habari kupitia Kurugenzi ya Maelezo na Waziri
mwenyewe huku Bodi iliyopangwa kuwa huru ikionekana kwamba haina nguvu
zakutosha.
Akizungumza
haja ya mazingira rafiki Legay alisisitiza kuwaTaifa linastahili
kuhakikisha kwamba kumewekwa mazingira rafiki ya upatikanaji wa habari
na kwamba kila mwananchi anapata haki yake ya kupata, kusambaza habari
kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa na sheria zinazohusu habari za
taifa.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi akizungumza akifungua
kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku
ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole
Gabriel, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Alisema
ingawa haki ya kupata habari imeelezwa waziwazi katika Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vifungu 18 na 21 mambo
yanayojitokeza sasa katika sheria za habari nchini Tanzania yanatishia
haki hiyo, kutokana na sheria hizo kuonekana kubana uchakataji wa
habari. Akitolea mfano wa sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016.
Alisema
katika mkakati wa utekelezaji wa malengo endelevu ya dunia kuna mpango
mkakati wa kulinda waandishi wa habari na upatikanaji wa habari kama
ilivyoelezwa katika lengo namba 16, kifungu kidogo cha 10.
Alisema
kwa sasa dunia inakabiliwa na tishio kubwa la upatikanaji wa habari
kutokana na vitisho vinavyowekwa kwa waandishi wa habari ikiwa na pamoja
na kuuawa, kutiwa kizuini au kupotea bila kujulikana.
Alisema
katika muongo mmoja uliopita waandishi 827 waliuawa na kwamba ni
asilimia 7 tu ya mauaji hayo yalipatiwa ufumbuzi. Aidha alisema mwaka
jana ulikuwa mwaka mbaya zaidi kwa waandishi wa habari, huku waandishi
16 pekee wakiuawa katika bara la Afrika.
Mkurugenzi
wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa
akijadili rasimu ya mkakati wa mpango wa usalama wa waandishi wa habari
wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni
maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa, lililofanyika jana
jijini Dar es Salaam.
Alisema
kitendo cha kuwadhibiti waandishi wa habari kunaashiria udhibiti wa
upatikanaji wa habari huru ambao ndio msingi wa demokrasia na maendeleo
ya jamii.
Aliitaka
jamii kuhakikisha kwamba inakaa pamoja na kuona haja ya kulinda uhuru
wa habari ikiwa na pamoja na kuwalinda wachakataji habari ili kila mtu
anayetaka kupata habari aweze kuipata na kuitumia kwa maendeleo yake,
jamii na taifa.
Akimkariri
Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova, mkuu huyo wa mawasiliano
alisema kwamba ukatili na vitendo vinavyoshabihiana navyo dhidi ya
waandishi wa habari ni kinyume na uhuru na haki ya upatikanaji wa habari
na wanaofanya mambo hayo wanatishia utawala bora wa kisheria na
kusababisha utoaji habari usiokamili kwa hofu ya udhibiti na matokeo
yake jamii nzima inapotoka na kuhangaika. Leo hii tunahitaji dhamira
mpya ya kuhakikisha kwamba tunatengeneza mazingira salama na rafiki kwa
waandishi wa habari.
UNESCO
ni mdau mkubwa wa habari nchini Tanzania na katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari ilikumbushia kazi inayofanya pamoja na wadau wengine
wa habari wakiongozwa na Tanzania Human Rights Defenders Coalition
kutengeneza mpango kazi wa ushawishi wa namna bora ya kuchakata na
kufanyakazi ya uandishi wa habari nchini Tanzania.
Mdau
wa tasnia ya habari, Kenneth Simbaya akiwasilisha fursa na changamoto
walizokumbana nazo wakati wa uandaaji wa rasimu ya mkakati wa mpango wa
usalama wa waandishi wa habari katika kongamano linalohusu ukatili kwa
waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa,
lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kutokana
na mkakati huo mwaka jana kuliundwa kikosi kazi cha kuangalia usalama
wa waandishi wa habari na taarifa inatarajiwa kutolewa wakati wowote
kuanzia sasa namna bora ya kuwawezesha waandishi wa habari kufanyakazi
kwa usalama.
Naye
msemaji wa serikali ya Tanzania akizungumza Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Habari Maelezo, Jamal Zuberi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel
katika tukio hilo alitoa wito kwa taasisi zisizo za kiserikali, taasisi
za sheria na vyombo vya habari kuhakikisha kwamba mazingira ya kufanyia
kazi waandishi wa habari ni salama na haki za upatikanaji wa habari
haudhibitiwi.
Alisema
ili kuwezesha hali hiyo serikali imepeleka muswada wa waandishi wa
habari bungeni na pia ikiwa kama moja ya nchi iliotia saini mikataba ya
kimataifa kuhusu upatikanaji wa habari serikali itafanyakazi kwa pamoja
na wadau kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanapata mazingira
rafiki na salama ya kufanyia kazi.
Mmoja
wadau wa masuala ya sheria akizungumza jambo katika kongamano
linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga
ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Mwanasheria
kutoka Nola, James Marenga akifafanua jambo wakati wa kongamano
linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga
ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi (kushoto) akiwa na
wadau wa tasnia ya habari wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa
waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa
waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Wadau
wa tasnia ya habari na masuala ya Sheria walioshiriki kwenye kongamano
linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga
ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Washiriki
wakitazama moja ya video ya shuhuda inayozungumzia usalama wa waandishi
wa habari wakati wa uchaguzi wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa
waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa,
lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa
Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango
shirikishi
Madiwani, na Wakuu wa Idara na Vitengo
wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu walengwa wa Mradi wa kuijengea
jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Ally Juma Mwanga, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ikungi Bi Rustika Turuka
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu mradi huo
Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo
wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika
kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
Na Mathias Canal, Singida
Shirika la Health Actions Promotion Association (HAPA) la Mkoani
Singida kwa ushirikiano na Shirika la The Foundation For Civil Society
la Jijini Dar es salaam linatarajia kuendesha mradi wa miaka mitatu kwa
vijiji vyote vya Wilaya ya Ikungi kwa lengo la kuijengea jamii uwezo na
mbinu shirikishi kama fursa na vikwazo katika maendeleo.
Mradi
huo utaanza na Vijiji 10 vya majaribio (Pilot Villages) kutoka katika
kata nne na kila kata itakuwa na Vijiji ama viwili ama Vitatu ambapo
uchaguzi wa Vijiji hivyo vya majaribio umezuingatia utayari wa jamii
husika katika shughuli za maendeleo pamoja na gharama za uendeshaji wa
mradi ili kupata matokeo chanya kwa uendelezaji wa mradi husika.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu amesema kuwa Uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea
kushirikisha wadau mbalimbali katika kusaidia kutekeleza shughuli za
maendeleo, kwani kwa uhabarisho wa mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii na
Halmashauri yataendelea katika kuimarisha juhudi za Wilaya zinazoendelea
kuchukuliwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo pia itakuwa ni fursa
kwa jamii kuwa na Uwezo na Nyenzo muhimu katika kutekeleza miradi ya
maendeleo kwa ufanisi.
Amesema kuwa Wilaya ya Ikungi inakabiliwa
na changamoto mbalimbali za kujiletea maendeleo ambapo endapo zitapatiwa
upembuzi yakinifu zitapunguza kadhia zinazowakumba wananchi ambapo
amezitaja changamoto hizo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Vituo vya Afya na
Zahanati (Kata na Vijiji) ambapo kwa sasa Wilaya ina vituo 39 tu vya
kutolea huduma za Afya ambapo upungufu ni Asilimia 60, Ujenzi na
Uboreshaji wa miundombinu ya shule za msingi ambapo kuna nyumba za
walimu 387 ambapo upungufu ni nyumba 854, Ujenzi na Uboreshaji wa
majosho na mifugo kwani kwa sasa yapo majosho 30 huku kati ya hayo
majosho 20 ni mabovu.
Dc Mtaturu alisema kuwa Zipo Asasi
mbalimbali ambazo zimesajiliwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi
lakini zimegeuka na kuwa Asasi zinazofanya kazi za kisiasa tofauti na
usajili wao ambapo amesema serikali haitasita kuzichukulia hatua ikiwemo
kuzifuta Asasi hizo ili ziache kupotosha wananchi.
Dc Mtaturu
alisema kuwa Mradi huo unaotolewa na Shirika la HAPA ni lazima uzingatie
matakwa ya kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu kuwa wana nafasi kubwa
ya kufanikisha maendeleo yao katika jamii hivyo waache kupotoshwa na
baadhi ya wanasiasa kuwa maendeleo yataletwa na serikali pekee.
Msimamizi wa Mradi wa HAPA Noel Makyao amewataja walengwa wa Mradi huo
kuwa ni wananchi wote wa kijiji cha Mradi wa majaribio, Wawakilishi 100
kutoka kila kijiji ambao watachaguliwa ili kuendesha zoezi la
kutengeneza bajeti ya mpango wa kila mradi ulioibuliwa na jamii kwa siku
tatu mfululizo na watu mashuhuri, wakuu wa madhehebu ya dini na makundi
mengine wapatao 20.
Alisema kuwa Jumla ya gharama zote za
kutekeleza mradi wa mbinu shirikishi ya kujenga uwezo wa jamii katika
kuibua, Kupanga, Kutekeleza na kupima matokeo ya Mradi katika vijiji
kumi vya majaribio kwa robo mbili zitakuwa shilingi milioni hamsini
(50,000,000/=).
Makyao alisema katika awamu hii ya vijiji kumi
vya majaribio jumla ya watu wapatao 25,511 watafikiwa kati ya lengo la
watu 25,334 zaidi ya watu 177 ya walengwa wa mradi.
Wachezaji
wa timu za Ruvu Shooting wenye jezi rangi ya bluu na wa African Lyon
wakiwa wamelala chini ikiwa ni kujihami na makundi ya nyuki ambayo
yalikuwa yanapita uwanjani hapo hivyo wachezaji, waamuzi na mabenchi ya
wachezaji wa akiba wote walilazimika kulala chini ikiwa ni kujinusuru
kutokana na hali hiyo. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara. Shooting iliibuka na ushndi wa bao 1-0 lililofungwa na
mshambuliaji mwenye nguvu za miguu Issa Kanduru kunako dakika ya 19.
'Ni kama wanasema 'Nyuki hao bado wapo tuendelee kujificha chini ya viti"
Watu wazima chini ya viti 'Chezea nyuki wewe'
No comments :
Post a Comment