Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji akikata utepe kuzindua tawi jipya la Benki ya UBL Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika jana. Kulia ni Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain na kushoto ni Afisa Mtenadaji Mkuu wa UBL
Tanzania, Faisal Jamall.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya United Bank Limited (UBL) la Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika jana.
Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi la Kariakoo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wa pili kutoka kulia akikata keki maalum katika hafla ya uzindua tawi jipya la Benki ya UBL Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika jana. Kulia kwake ni Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain na kushoto ni Afisa Mtenadaji Mkuu wa UBL Tanzania, Faisal Jamall
Rais, Afisa Mtenadaji Mkuu wa United Bank Limited (UBL) Pakistan ambaye pia ni Mwenyekiti wa UBL Tanzania, Bw. Wajahat Husain(kulia) akimkabidhi tuzo maalum Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji katika hafla ya uzindua tawi jipya la Benki ya UBL Kariakoo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye tawi hilo jana.
Wageni mbalimbali na wafanyakazi wa benji ya UBL wakifuatilia uzinduzi wa tawi la benki hiyo jana.
Serikali imesema kuwa Tanzania
ina fursa nzuri katika uwekezaji wa huduma za kifedha na kuwavutia
wawekezaji wa mataifa tofauti na malalamiko ambayo yamekuwa yakienezwa
na baadhi ya taasisi hizo hapa nchini.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wakati wa ufunguzi wa tawi
la jipya la Kariakoo la benki ya United Bank Limited (UBL) Tanzana
Limited.
Hivi kaibuni kulikuwa na
malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya taasisi za kifedha na kutoa
viashiria vya kufirisika, jambo ambali alisema, uzinduzi wa tawi la
Kariakoo la benki ya UBL ni ishara tosha kuwa sekta ya uwekezaji
wahuduma za kifedha hipo imara na kuendelea kuwavutia wawekezaji.
Waziri Kijaji alisema kuwa uchumi
wa Tanzania kwa sasa unakuwa na bodi ya wakurugenzi wa benki ya UBL
imevutiwa nayo na kuamua kuwekeza nchini. Alisema kuwa benki hiyo kwa
sasa imetumia jumla ya dola za Kimarekani milioni 32 (Sh 67.2 bilioni)
kutoa mikopo kwa wateja wake na huduma nyingine
“Benki ya UBL Tanzania ilianza
rasmi Mwezi Septemba mwaka 2013 na kufanikiwa kupata faida iliyopelekea
kuzindua tawi lingine huku ikiwa na mipango ya kufungua matawi kadhaa
katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Arusha, hii ni ishara tosha kuwa sekta
ya huduma ya kifedha Tanzania inakuwa na kupata maendeleo makubwa,”
alisema Dk Kijaji.
Kwa upande wake, Rais na Mtendaji
Mkuu wa UBL Bw. Wajahat Husain alisema kuwa wamefuraishwa na hali ya
uwekezaji hapa nchini na kuamua kuwekeza, ikiwa ni tawi la kwanza la
benki hiyo kwa bara la Afrika.
Husain alisema kuwa wameichagua
Tanzania kutokana kukuwa kwa uchumi, hali bora ya kisiasa, maliasili na
huduma za bandari ya Dar es Salaam ambayo ni kiungo cha wafanyabiashara,
si kwa Tanzania tu, bali hata kwa nchi sita jirani. Alisema kuwa
kupanuka kwa mtandao wa benki hiyo kwa Dar es Salaam kutaifanya benki
hiyo kuwa kiungo muhimu cha masuala ya kiuchumi.
“Tumefurahi kuwekeza hapa nchini,
benki yetu ni miongoni mwa beki kubwa sana nchini Pakistani, tukiwa na
matawi zaidi ya 1,300 na kutoa huduma wengi, tumevutiwa na hali ya
uwekezaji hapa nchini na muda mfupi tuliowekeza, tumeona matunda yake na
kuamua kupanua wigo,” alisema Husain ambaye pia ni Mwenyekiti wa Benki
hiyo nchini.
Alisema kuwa wapo tayari kwa soko
la ushindani la hapa nchini na nyenzo yao kubwa ni kutoa huduma za
kisasa zenye ufanisi mkubwa.
No comments :
Post a Comment