Aliyewahi kuwa mbunge wa Kasulu Mjini
2010/2015 akiwakilisha chama cha NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia chama cha
ACT-Wazalendo baaada ya kupoteza ubunge, Moses Machali, leo Novemba 21
216, ametangaza kujiunga na CCM...
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE.
Kutoka mezani kwangu Moses Joseph Machali, Tarehe: 21/11/2016
Kutoka mezani kwangu Moses Joseph Machali, Tarehe: 21/11/2016
Napenda
kuutaarifu umma wa Watanzania kupitia kwenu waandishi wa habari kwamba ni jambo
la ajabu na aibu kwa watu makini na wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli Kuacha
kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini Uongozi wa
Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli bila kusahau utendaji makini wa Waziri Mkuu
wake Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa (Mb) pamoja na mawaziri mbalimbali wameonesha
kutaka kufuata mwenendo wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake.
Mimi
Moses Joseph Machali niliyefanya sana siasa za Upinzani hapa nchini na
niliyepiga kelele na kupinga siasa za kifisadi zilizoitawala nchi hii;
niliyepinga pia ufisadi uliokuwa umeitawala serikali huko nyuma kwa nguvu na
uwezo wangu wote nikishirikiana na wapinzani wenzangu, ninaamua kujiunga na watu
wanaonesha dhamira safi ya kuiendeleza nchi yetu Tanzania. Watu wenye mwelekeo
na dhamira ya kuijenga nchi yetu kwa maendeleo enedelevu ni jamii ya akina
Magufuli, Kasim Majaliwa, nk.
Mwaka
mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake kupitia hatua
mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya ufisadi uliokuwa umeigubika nchi yetu,
inatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au
kutokumuunga mkono Rais Magufuli. Mimi nimechagua kumuunga Mkono Rais kwa
vitendo, kwa sababu ninaposoma Rekodi yangu ya enzi nikiwa Mbunge (Hansard) na
kabla ya kuwa mbunge ni kwamba nilipinga mnoo wizi na ufisadi wa kila aina;
Nilipinga Matumizi ya fedha serikalini yasiyo ya lazima na yasiyo na tija kwa
taifa (Rejeeni hotuba yangu ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, nikiwa Waziri
Kivuli wa wizara hiyo ya mwaka 2014/2015 na 2015/2016), vilevile bila kusahau
hotuba zangu mbalimbali Bungeni na nje ya Bunge.
Kwa
kushirikiana na wapinzania wenzangu enzi hizo tulishauri na kupinga ufisadi wa
kila aina, tuliitaka serikali kufanya mambo yenye tija kwa taifa na sasa kila
mwenye macho anaona hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano. Miradi
kama ya Ujenzi wa Reli, Ununuzi wa ndege mbili na mipango ya kununua ndege
zaidi kama namna ya kulifufua shirikia la ATCL ni mambo tuliyoyahitaji kuyaona
wapinzani; sasa yanafanyika. Wale wenye dhamira ya dhati ya kuona nchi yetu
ikipiga hatua, kamwe hatuwezi kubeza mambo hayo bali kuyaunga mkono.
Wale
tuliosema na kupiga kelele kwamba Serikali ni dhaifu ktk kuwachukulia hatua
watu mbalimbali wenye dhamana serikalini walioonekana kufanya vibaya serikalini
ktk nafasi zao, leo tunaona kumekuwepo na kasi nzuri ktk kuwachukulia hatua
watu hao. Hata hivyo leo hii upinzani umepiteza mwelekeo kwa sababu unapingana
na kile ulichokihubiri nchini. Agenda ya kupinga ufisadi siyo ya upinzani tena
bali ya JPM na CCM yake au yao. Wapinzani wamegeuka kuwa watu wanaokataa yale
waliyoyasimamia na kuyahubiri huko nyuma. Hakika huo siyo uungwana bali aina
mpya ya ufisadi nchini na usaliti kwa agenda zao.
Kama
kweli sisi tumeokuwa wapinzani na tulioonesha kupinga kwa nguvu zote ufisadi
ulioiumiza nchi hii tulimaanisha yale tuliyoyahubiri na kuwaaminisha watu basi
tunao wajibu wa kuacha tabia ya kuwa vigeugeu kwa mambo tuliyoyaamini na kuyahubiri.
Kutofanya hivyo basi ni mwendelezo wa ufisadi kwa maslahi binafsi. Ni nani
asiyeona kwamba serikali ya awamu ya tano inafanyia kazi mambo mengi
tuliyoyapigia kelele? Au tunajifanya kutokukubali ukweli unaoishi kwa ule
msingi wa upinzani wa Tanzania kwamba Tukimuunga mkono Mtawala kamwe hatutapata
kuaminiwa na wapiga kura nchini na hivyo tupinge tu hata kama ni ukweli?
Nadhani kinachofanyika ni mwendelezo wa kupinga hata mazuri ili kutafuta fursa
ya wapinzani kukubalika kisiasa zaidi hata kwa njia na mbinu haramu kama
kawaida ya siasa zilizo zoeleka hapa nchini kwa miaka mingi.
Taifa
hili haliwezi kuendelea kwa kuwa na siasa za kutokukubaliana na ukweli
unaoishi. Kama dhamira ya kila mtanzania ikiwemo wapinzani ni kuona nchi ina
move basi hatuhitaji kuwa watu wa kupingapinga hata yaliyo mema bali kuyaunga
mkono yale yaliyo mema bila kujali yanafanywa na nani bali msingi mzuri
unapaswa kuwa ukweli kwa kila jambo. Serikali ya awamu ya tano imeonesha njia
ktk mambo mengi na inastahili kuungwa mkono. Safari ni hatua na ninaamini
kwamba hata yale yanayoonekana kutokufanyiwa kazi ndani ya mwaka mmoja uliopita
na ambayo yalishindikana huko nyuma, bado yanaweza kuja kufanyiwa kazi huko
mbeleni. Serikqli ya JPM imejitahidi sana tukilinganisha na huko tuliko toka.
Uongozi huu unafanana sana na ule wa akina Hayati EDAWARD MORINGE SOKOINE chini
ya hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.
Daima
ninaamini ktk yale ninayoyaamini pasipo kufungwa na ukada bali kuangalia ukweli
ni upi. Hata kelele wanazopiga baadhi ya watu kwamba maisha yamekuwa magumu kwa
sababu ya Magufuli ni propaganda tu kwa sababu hakuna uhusiano wa maisha magumu
na suala la KUDHIBITI wapiga dili wa fedha na mali za umma bali tukubali kwamba
wapiga dili waliozoea kupiga dili na kuziingiza fedha walizopiga ktk mzunguko
kwamba siyo jambo la msingi ktk kujenga uchumi imara. Uchumi imara hauwezi
kujengwa kwa kuruhusu ubadhirifu wa fedha na mali za umma au hata za mtu mmoja
mmoja. Kinachoonekana hivi sasa ni kama nchi inasukwa upya na hivyo tuwaunge
mkono viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa mema wanayoyafanya na
kuwashauri kurekebisha ktk yale ambayo hayajakaa vizuri. Tuachane na siasa
nyepesi za kutaka kuona kwamba mazuri ni yale yanayofanywa na wapinzani huku
mambo hayohayo yakifanywa na ccm yaonekane hayafai na kutajwa kuwa ni ya hovyo.
CCM ya JPM siyo ile ya 2015 kurudi nyuma kidogo. Hii ni tofauti na ninaiunga
mkono.
Hivyo basi leo Tarehe 21/11/2016 ninatangaza rasmi kwamba ninajiunga na timu JPM kwa maslahi ya taifa kwa kuwa sioni sababu ya kupingana na yale niliyoyapigania na itakuwa ni sawa na mtu kupigana na kivuli chake mwenyewe. Kwaherini Upinzani nimeamua kuanza siasa mpya za masuala yale niliyoyaamini na ninayoyaamini. Imani ni Matendo Na Matendo ni imani. Piga vita ufisadi kwa imani na Matendo.
Hivyo basi leo Tarehe 21/11/2016 ninatangaza rasmi kwamba ninajiunga na timu JPM kwa maslahi ya taifa kwa kuwa sioni sababu ya kupingana na yale niliyoyapigania na itakuwa ni sawa na mtu kupigana na kivuli chake mwenyewe. Kwaherini Upinzani nimeamua kuanza siasa mpya za masuala yale niliyoyaamini na ninayoyaamini. Imani ni Matendo Na Matendo ni imani. Piga vita ufisadi kwa imani na Matendo.
Moses
Joseph Machali
X-mbunge, Kasulu Mjini 2010-2015.
X-mbunge, Kasulu Mjini 2010-2015.
No comments :
Post a Comment