Makamu wa Rais, mama Samia Suluhu
Hassan, akikabidjiwa mfano pasi ya kupanda ndege ya ATCL, kutoka Dar es
Salaam kwenda Mwanza Jana.Makamu wa.Rais aliisifu ndege hiyo haina ya
Bombardier Q400 kwa usafiri mzuri na kwamba umepunguza gharama kwa
watumishi wa serikali kama yeye, bapo badala ya kukodi ndege, ameweza
kutumia usafiri huo na hivyo kupunguza gharama. Ndege hiyo pia
ilikodishwa na serikali kupeleka viongozi mkoani Tabora kwenye msiba wa
spika mstaafu marehemu Samwel Sitta.
Rais wa Chama cha Madaktari Wanawake
Tanzania (MEWATA), Dkt.Serafina Mkuwa (kulia), akitoa taarifa kwa
wanahabari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi na matibabu ya
Saratani ya Matiti na mlango wa kizazi mkoani Mwanza.
Kampeni hiyo itazinduliwa kesho katika
Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu
Hassan na baadaye kufanyika kwa siku mbili bure.
Na BMG
Kutoka kushoto ni Dkt.Mary Charles
ambaye ni Makamu wa Rais MEWATA, Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald
Subi, Rais wa MEWATI, Dkt.Serafina Mkuwa, Mwenyekiti Kamati ya Kampeni
na Mjumbe kamati tendaji MEWATA, Dkt.Magdalena Lyimo pamoja na Mratibu
wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Mwanza, Secilia Mrema.
Pia watumishi wa afya mkoani Mwanza
wamepatiwa mafunzo kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za uchunguzi
wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi
WASAIDIZI WA KISHERIA WA SHIRIKA LA EfG WAUNGA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KATIKA KUFANYA USAFI
Msaidizi wa sheria kutoka Soko la
Mchikichini Manispaa ya Ilala, Charles Beatus (kushoto), akitoa somo kwa
wafanyabiashara wa soko hilo kuhusu ukatili wa kijinsia.
Shughuli za usafi zikiendelea.
Hapa kazi tu.
Takataka zikiondolewa sokoni hapo baada ya kufanyika usafi.
Na Dotto Mwaibale
WASAIDIZI wa kisheria wanawake kutoka
Shirika la Equality for Growth (EfG), wamemuunga mkono Rais Dk. John
Magufuli katika uhimizaji wa kufanya usafi Soko la Temeke Sterio jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza katika tukio hilo
lililofanyika mwishoni mwa wiki sokoni hapo Ofisa Ufuatiliaji na
Tathmini wa EFG, Shaban Rulimbiye alisema wameamua kufanya usafi wa
mazingira katika masoko sita yaliyopo chini ya mradi wa kupinga ukatili
wa kijinsia masoko unaoendeshwa na shirika hilo.
"Tunamuunga mkono rais wetu kwa jitihada
zake anazozifanya za kuhimiza usafi ndio maana wasaidizi wetu wa
kisheria kutoka katika masoko hayo tupo nao hapa Temeke kufanya usafi na
baada ya hapo watatoa elimu kwa wafanyabiashara ya kupinga ukatili huo "
alisema Rulimbiye.
Alisema ukatili wa kijinsia masokoni si
kumshika maungoni mfanyabiasha na matusi hata pale wanawake wanapofanya
biashara zao kwa kuziweka chini bila ya kuwa katika mazingira mazuri
pia ni ukatili wa kijinsia.
Alisema mpango huo wa kufanya usafi
katika masoko hayo ni endelevu na kuwa kila Jumamosi watakuwa wakifanya
hivyo kumuunga mkono rais.
Rulimbiye aliyataja masoko ambayo yapo
chini ya mradi huo ambayo yatanufaika na usafi huo wa mazingira kuwa ni
Temeke Stereo, Mchikichini, Kisutu, Feri, Gezaulole na Tabata Muslim.
Makamu Mwenyekiti wa soko la Temeke
Sterio, Issa Ndilima alilishukuru shirika hilo kwa mpango huo wa usafi
kwani umeleta hamasa kwa wafanyabiashara wa soko hasa katika mafunzo
wanayopata kupitia wasaidizi wa kisheria kupinga ukati wa kijinsia
masokoni.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye,(kulia), akimkabidhi Bendera ya Taifa, mwakilishi wa Tanzania
kwenye mashindano ya Miss Africa 2016 Julietha Kabete wakati wa mkutano na
waandishi wa habari ofisini kwa waziri jijini Dar es Salaam, Novemba 14, 2016. Mashindano
hayo yatafanyika nchini Nigeria. (PICHA NA
RAYMOND MUSHUMBUSI WHUSM).
NA SHAMIMU NYAKI WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye ameahidi kuendelea kufanya mageuzi makubwa katika
mashindano ya urembo hapa nchini ili kuondoa dosari zinazojitokeza katika
mashindano hayo.
Mhe. Nape ametoa ahadi hiyo leo Jijini Dar es Salaam
wakati akimkabidhi Bendera Mshiriki wa Tanzania katika mashindano ya
urembo Bara la Afrika kwa mwaka 2016 yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu
nchini Nigeria.
Mhe Nnauye ameongeza kuwa lengo la Serikali ni
kuhakikisha kuwa mashindano kama haya yanakuwa na tija kwa Taifa hasa katika
kuleta ajira kwa vijana pamoja na kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
“Serikali nia yake ni kuhakikisha kuwa jambo
hili linakuwa bora, linaminiwa na kuheshimika hivyo watanzania wote
watajivunia uwepo wa mashindano ya urembo nchini” alisistiza Mhe Nnauye.
Aidha Mwakilishi wa Millen Magese group Ltd Bw.
Matukio Aranyande Chuma amesema kuwa shindano hili litailetea sifa Tanzania na
ni kwa mara ya kwanza kufanyika hivyo wataitumia fursa hiyo kuitangaza nchi
kimataifa kupitia urembo.
“ kwa
niaba ya Millen Magese group Ltd tunatoa shukrani zetu kwa Serikali na Kamati
ya Miss Tanzania kwa kutuunga mkono katika jambo hili na tunaahidi kufanya
vizuri katika mashindano haya”Alisema Bw. Chuma.
Kwa
upande wake Mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano hayo Bi.
Julietha Kabete ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono mashindano
mbalimbali ya urembo Tanzania inaposhiriki.
“Naahidi
kuitangaza nchi yangu vizuri katika mashindano haya na naomba watanzania
waniombee na wanipigie kura ili niweze kushinda na kuitangaza Tanzania
kimataifa katika urembo” Alisema Bi Julietha.
Mashindano ya Miss Afrika yameanzishwa mwaka 2016 na
Prof. Bena Yage ambaye ni Gavana wa Jimbo la Cross River nchini Nigeria kwa
lengo kupata mabalozi wa nchi za Afrika watakaosaidia kutangaza na kuelimsha
waafrika kuhusu uchumi unaozingatia utunzaji wa mazingira.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye,(kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo.
Julietha
Kabete,(katikati), akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wake kwenye mashindano hayo
Mwenyekiti
wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga ( katikati) akifafanua jambo kwa
waandishi wa kuhusu mchakato wa kumpata mshiriki wa mashindano hayo kutoka kwa
washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa,
Julietha Kabete
Mwakilishi wa Millen Magese group company Ltd Bw.
Matukio Aranyande Chuma.(katikati) akitoa maelezo kuhusu mashindano ya Urembo
ya Afrika kwa mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo Novemba 14, 2016 Jijini
Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment