Ofisa
Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Shavkat Berdiev (kulia),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
kuhusu kampuni hiyo kutangaza ofa ya Krismas ya Smartphone. Kushoto ni
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni
inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imetangaza
kuzindua ofa mpya ya Tecno Y3+ Music Smartphone ambayo imejengewa
ndani yake zana kubwa ya kuchezesha ambayo inatoa nafasi ya
kutiririsha kupitia mtandao na hivyo kuwawezesha wateja kufurahia na kusherehekea na wapendwa wao wakati wa kipindi hiki cha kipekee kinachohusiana na Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Akitangaza
ofa hiyo katika mkutano wa waandishi wa habrai jijini Dar es Salaam,
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigom, Shavkat Berdiev alisema kuwa Simu ya
mpya ya kisasa ya Smartphone tayari ipo katika maduka yote ya Tigo na
mawakala nchi nzima na inapatikana kwa gharama ya shilingi 99,999 tu.
Hii ni aina ya kwanza ya simu ya kisasa ya Techno Smartphone kuingizwa
katika soko ikiwa na zana kubwa (Boom App) ilibeba miziki ya ndani.
“Tunaamini
ofa hii itawawezesha wateja wengi wa Tigo kufurahia manufaa ya simu
hii ya kisasa inayouzwa kwa bei ya reja reja ambayo mteja anaimudu,
ikiwemo kupata mtandao wa intaneti ambao uko pamoja na kujikita kwetu
katika kuboresha mabadiliko katika maisha ya kidijitali,’ alisema
Berdiev.
Aliongeza,
“Hali kadhalika imekuwa ni utamaduni wetu kuwapatia wateja simu nzuri
ya kisasa wakati wa msimu wa sikukuu. Hivyo natoa wito kwa wateja
wetu wote hususani wale wanaosafiri kwenda mikoani hadi maeneo ya
vijijini kuungana na familia zao kuchukulia faida ya kuwepo kwa ofa
hii.”
Akizungumza
katika tukio hilo Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga
aliongeza;Pindi mteja anaponunua simu, moja kwa moja Tigo inamzawadia
mteja huyo GB 1 ya data za intaneti na muda wa maongezi shilling
5,000 Tigo kwenda Tigo kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja (miezi
12).
Simu
ya Kisasa ya Y3+ imekuja na vitu mahsusi vya kipekee ambavyo
vinajumuisha betri iliyoboreshwa maisha, sehemu mbili za kadi za
simu, uwezo wa kuhifadhi data kwa kiwango cha GB 8 pamoja na kasi ya
ufanisi 512 (RAM) ambazo zinaifanya kuendesha na kuhifadhi data.
No comments :
Post a Comment