Thursday, November 17, 2016

JK AWATUNUKU DIGRII WAHITIMU 1,179 CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DUCE

 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha  Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kutunukiwa digrii za awali.
Digrii walizotunukiwa ni Elimu ya Jamii na Ualimu (B.A.Ed.) wanafunzi 864, Elimu katika Elimu ya Jamii (B.E.D. Arts) wanafunzi 52, Elimu katika Sayansi (B.Ed. Science) wahitimu 73, Sayansi ya Ualimu (B.Sc.Ed.) wahitimu 190.(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kuwatunuku digrii ya awali ya elimu ya jamii  na ualimu  wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo jioni. Jumla ya wanafunzi 864 walitunukiwa digrii hiyo.
 wakivaa kofia zao
 Wakifurahi kwa kucheza muziki
 Ni shangwe na vigelegele
 Mhitimu Bora wa Kike akipatiwa zawadi
 Warda Jumanne akipatiwa zawadi ya kuwa mmoja wa wanafunzi Bora wa Kike
 Mwanafunzi Bora wa Jumla Haji Mohamed akionesha cheti chake
 Makamu Mkuu wa UDSM, akifurahi wakti wimbo wa kabila la wahaya wa Akanana Kalile Kona ukipigwa wakati wa mahafali hayo
 Ni muziki kwa kwenda mbele
 Eva akipatiwa tuzo ya mwanafunzi bora wa kike
 Mwanafunzi Bora wa Kike Gaudencia Mwita akielekea kutuzwa zawadi maalumu ya Mkuu wa Chuo
 Mwanafunzi Bora wa Jumla wa Duce, Haji Mohamed akitoa hotuba ya shukrani kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu
 Dk. Kikwete akifurahia jambo na Ngumbullu
 JK akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo hixo
Wananchi wakiwa na kamera tayari kuwapiga picha ndugu zao walihitimu

No comments :

Post a Comment