Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu
kutoka Wizara ya Afya, Maendelewo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Christopher Mushi akifafanua jambo wakati wa Kikao Kazi cha siku mbili
kuhusu Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la Watoto 2017-2020
Mwezeshaji kutoka shirika lisilo
la Kiserikali kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Koshuma
Mtengeti akiwasilisha mada wakati wa Kikao Kazi cha siku mbili kuhusu
Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la
Watoto 2017-2020
Mwakilishi wa Katibu Tawala
Wilaya ya Iringa Menrad Dimoson akifungua Kikao Kazi cha siku mbili
kuhusu Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la Watoto 2017-2020
Meneja Mradi kutoka shirika la
Ukatili wa Kijinsia na Ulinzi wa Mtoto(GBV) akichangia mada wakati wa
Kikao Kazi cha siku mbili kuhusu Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la
Watoto 2017-2020
Baadhi ya Washiriki wa Kikao Kazi cha siku mbili kuhusu Mpango Mkakati Utekelezaji wa Baraza la Watoto 2017-2020
Na Anthony Ishengoma
Idara zinazoshughulikia masuala ya
watoto pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Iringa
zinakutana katika kikao kazi cha siku mbili kupata mafunzo ya Mpango
Mkakati wa Utekelezaji wa Baraza la Watoto Kitaifa.
Kikao kazi hiki kuhusu Mkakati wa
Baraza la Watoto wa miaka mitano wa 2017-2020 kinaratibiwa na Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Christopher
Mushi amesema kuwa Mkakati huu kimsingi unatokana na katiba ya Baraza la
Watoto ambayo inataka kuwepo kwa mkakati huu ili kuwawezesha watunga
sera kutekeleza kwa vitendo haki za watoto.
Mwezeshaji kutoka Shirika lisilo
la Kiserikali la Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) Koshuma Mtengeti amesema
Serikali ya Tanzania imeishatimiza malengo makubwa ya kisera kuhusu
watoto hapa Nchini lakini bado kuna changamoto ya utekelezaji wa sera
hizo ndio maana Wizara imeandaa Mkakati huu ili kukabiliana na
changamoto za utekelezaji.
Amesema katika uhandaaji wa
Mkakati huu mambo yote ya msingi kutoka Wizara na Wadau yaliangaliwa
kiundani ili kuhakikisha Mkakati unazingatia masuala yote ili kujenga
uwezo kwa watoto na masuala mtambuka kuhusiana na haki na wajibu watoto
Nchini.
Masuala mbambali zinazowakabili
watoto Nchini nia pamoja na janga la ukimwi, umasikini, ujinga, maradhi
na uelewa mdogo wa masuala ya watoto kutoka jamii inayowazunguka.
No comments :
Post a Comment