Wednesday, November 2, 2016

Bodi ya Filamu yaendelea kutoa elimu kwa wasanii kuhusu kutengeneza filamu bora.

fl1
Katibu  Mtendaji  Bodi ya Filamu Tanzania  Bibi Joyce Fissoo (Wa kwanza kushoto ) akizungumza na uongozi wa East Afrika Televisheni  na East Afrika Radio  alipotembelea vituo hivyo  Novemba 2 mwaka huu  Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa vipindi vya EATV Bi Lydia Igarabuza.
fl2
Katibu  Mtendaji  Bodi ya Filamu Tanzania  Bibi Joyce Fissoo (Kushoto ) akifanya mahojiano na watangazaji  wa  EA Radio alipotembelea vituo hivyo Novemba 2  mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
fl3
Katibu  Mtendaji  Bodi ya Filamu Tanzania  Bibi Joyce Fissoo (Kushoto ) akifanya mahojiano na watangazaji  wa EATV   alipotembelea vituo hivyo Novemba 2  mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
fl4
Mkuu wa vipindi vya East Afrika Televisheni  Bi Lydia Igarabuza (wa kwana kulia) akimueleza jambo Katibu  Mtendaji  Bodi ya Filamu Tanzania  Bibi Joyce Fissoo (wa kwanza kushoto) wakati alipotembelea kituo hicho Novemba 2  mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………..
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo amewashauri  wasanii wa filamu nchini  kujiendeleza kielimu ili kuongeza  weledi na kutengeneza filamu zenye ubora.
Akiongea na   uongozi wa Kituo cha  Radio na Televisheni  cha East Afrika  leo   Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji huyo amesema kuwa chombo hicho  kina nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa wasanii hususani namna ya kuandaa  Filamu zenye  bora kwa kuwa wako mstari wa mbele katika kuonyesha kazi za  tasnia hiyo. 
“Kituo chenu kina nafasi kubwa zaidi ya kushawishi wasanii kutengeneza filamu bora kwa kuwa  mmekuwa mkiwapatia fursa ya kutangaza filamu hizo pamoja na kuzionyesha ndani na nje ya nchi hivyo ni muhimu kuwakumbusha  kuzingatia ubora wa filamu .”Alisema Bibi Joyce.
Aidha ameongeza kuwa vyombo vya Habari ni nguzo muhimu katika kuendeleza tasnia ya filamu  hapa nchini hivyo ni budi kwa wasanii kuhakikisha wanatengeneza Filamu bora ambazo zitapata nafasi ya kuonyeshwa katika vyombo hivyo  kwa maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla.
Naye  Mkuu wa vipindi vya televisheni wa   East Afrika Bi Lydia Igarabuza  ameipongeza Bodi ya Filamu kwa  kufanya maboresho katika tasnia ya Filamu nchini na kuishauri kutoa elimu zaidi kwa wasanii  katika  kufuata Sheria ya Filamu na michezo ya kuigiza kabla ya kutengeneza filamu zao.
“Naipongeza Bodi ya Filamu kwa juhudi mnazofanya katika kuboresha tasnia  hii  na msichoke  kutoa elimu hiyo kwani wasanii wetu bado wanahitaji elimu ya filamu na sheria zake kwa ujumla.Alisema Bi Lydia.
Bodi ya Filamu imejidhatiti katika kuhakikisha tasnia ya Filamu inakuwa kwa kutengeneza bidhaa bora ambapo imekuwa  ikitoa mafunzo  kuwajengea uwezo wanatasnia hao  .

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZINDUA BODI YA HOSPITALI YA MNAZIMMOJA


bo1
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmuod Thabit Kombo akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazimmoja katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
bo2
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmuod Thabit Kombo katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazi baada ya kuizindua rasmi Bodi hiyo, wa kwanza (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Jama Malik Akili na (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
…………………………………………………………………………………
Na  Ramadhani Ali-Maelezo Zanzibar .
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka  matarajio makubwa kwa Bodi ya Hospitali ya Mnazi mmoja katika kufanikisha azma  ya kuwa Taasisi yenye mfumo wa kujitegemea baada ya Baraza la Wawakilishi kupitisha Sheria ya kuanzishwa taasisi hiyo.
Amesema Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti mzoefu wa masuala ya Afya Zanzibar Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil inahitaji mashirikiano ya karibu ya  wafanyakazi wa Hospitali hiyo na wananchi katika Kuleta mabadiliko hayo.
Waziri Mahmoud ameeleza hayo Ofisini kwake Mnazimmoja alipokuwa akizindua Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Mnazi mmoja  ambayo lengo lake kuu ni kuifanya Hospitali hiyo  kufikia kuwa ya rufaa inayoshughulikia maradhi maalum yaliyoshindikana katika vituo vya afya na Hospitali za kawaida.
“Tunawataka  wananchi kutoa ushirikiano  kwa kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu nao, vinavyofikia 142, na kuiacha taasisi mpya ya Mnazi mmoja kushughulia magonjwa  makubwa,”alisisitiza Waziri wa Afya.
 Ameitaka Bodi  kuishauri Serikali njia bora za kuchangia matibabu katika maeneo maalum kwa vile Sera ya Serikali bado ni kuendelea kutoa matibabu bila malipo kwa wananchi.
Waziri wa Afya amewaeleza wajumbe wa Bodi hiyo kuwa  Hospitali ya Mnazi mmoja inarasilimali kubwa ya kuaminiwa na wananchi wengi wa Zanzibar na linapotokea tatizo lolote huwa ni la nchi nzima hivyo suala la kuongeza ufanisi lina  umuhimu mkubwa.
Amesema hivi karibuni Hospitali hiyo itafunga majengo mengine mawili mapya ambayo yanavifaa vya kisasa hivyo wafanyakazi watapaswa kuwa waangalifu na kuacha kufanyakazi kwa mazoea.
Amewataka viongozi wa sehemu zote za Hospitali ya Mnazimmoja kuwasimamia wafanyakazi walio chini yao na kuiunga mkono Bodi katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil amesema jukumu walilopewa na Serikali ni kubwa lakini kwa kutumia utaalamu wa wajumbe wa Bodi hiyo watajitahidi kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya kuifanya Hospitali ya Mnazimmoja kuwa ya kujitegemea linafikiwa.
Hata hivyo amewaomba viongozi wa Wizara na wafanyakazi  wa Hospitali ya Mnazimmoja kuwapa ushirikiano na watakuwa tayari kupokea ushauri utakaosaidia  kufikia malengo yaliyopangwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili amewaeleza wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazi mmoja kuwa Wizara itaendelea kusimamia sera lakini Bodi ndio yenye jukumu la kushauri maendeleo ya taaisi hiyo.

DKT MGWATU APONGEZA UTENDAJI KAZI WA TEMESA LINDi


mez1
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kulia) akiongea na Meneja wa TEMESA Lindi Mhandisi Grayson Maleko (kushoto) alipotembelea kituoni hapo.
mez2
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (katikati) akiongea na Mafundi wa TEMESA Lindi walioko kwenye mafunzo ya vitendo, alipotembelea kituoni hapo.
mez3
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto w) akiongea na watumishi wa Karakana ya TEMESA Lindi, alipotembelea kituoni hapo mapema.
mez4
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akiangalia eneo litakalojengwa gati  kwa ajili ya Kivuko cha Lindi Kitundamkoani Lindi.
Picha Zote na Theresia Mwami TEMESA Lindi
…………………………………………………………..
Na Theresia Mwami TEMESA Lindi
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amepongeza utaratibu unaotumika katika kituo cha TEMESA Lindi na karakana zake kwa kuratibu vizuri kazi za kila siku.
“Nawapongeza sana kwa utendaji wenu wa kazi kwa kuweka utaratibu wa kufuatilia kila kazi inayofanywa na wafanyakazi wa kituo” alisema  Dkt. Mgwatu.
Dkt Mgwatu amemuagiza  Meneja wa TEMESA Mkoa wa Lindi Mhandisi Greyson Maleko kuhakikisha kuwa magari yote ya Serikali mkoani Lindi yanafanyiwa matengenezo katika karakana ya TEMESA iliyopo mkoani humo.
Dkt. Mgwatu amemtaka Meneja huyo kuhakikisha anakusanya madeni yote wanayodai kwenye Taasisi, Halmashauri na Idara mbalimbali za Serikali kutokana na matengenezo ya magari na mitambo, sambamba na kulipa madeni yote wanayodaiwa na wazabuni kwa kipindi cha Julai-Septemba, 2016.
Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Lindi alisema kuwa changamoto kubwa inayokabili kituo hicho ni uwepo wa madeni makubwa wanayodai kwenye Taasisi na Halmashauri mbali mbali za serikali zilizopo Mkoani Lindi kutokana na matengenezo ya magari na mitambo lakini wanajitaidi kuendelea kufanya kazi kwa ustadi na kujituma.
Katika hatua nyingine Dkt. Mgwatu alitembelea eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya kivuko kutoka Lindi hadi Kitunda.
Dkt. Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea mikoa ya Lindi na Mtwara ili kujionea hali ya Vituo katika mikoa hiyo pamoja na utendaji kazi wake.

No comments :

Post a Comment