Wanafunzi wa shule ya sekondari, Pugu
wakishusha sehemu ya magodoro yaliyokabidhiwa na benki ya UBA kwa ajili
ya wanafuzni wenye mahitaji
maalum shuleni hapo
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA,Piter Makao akiwa meneja operesheni
Omary wakikabidhi mafuta ya ngozi kwa kijana mwenye ulemavu wa ngozi
,Daudi Nyangusi na Meneja ufadhili wa eleimu kutoka TEA , Tito Mganwa.
Wafanyakazi waUnited Bank of Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wenye ulemavu wa shule ya Sekondari ya wavulana pugu jijini
Dar es Salaam
Afisa masoko wa UBA , Evance Chandarua akimkabidhi begi, Ramadahani Juma
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Benki ya
United Bank of Africa, (UBA), leo imetoa msaada wa viti, Magodoro, Magongo ya
kutembelea na vitabu vya kujisomea kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa
shule ya sekondari ya wavulana, Pugu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa kutoa vifaa hivyo Meneja wa benki hiyo nchini ,Peter Makao,
amesema
kuwa wamechagua kutoa vifaa hivyo katika shule hiyo kutokana na mahitaji
ya wanafunzi hao ambao wamekuwa wakisoma katika mazingira magumu.
“Vitu hivi
ambavyo tumevitoa leo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia watoto hawa
wenye mahitaji maalum shida zinazowakabili wakati wa kusoma na hivyo kusongwa na mawazo ”Amesema Makao
Ameto wito kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii hili
waweze kufanikiwa katikamaisha yao na jamii kwa ujumla.
Wanafaunzi wenye ulemavu wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya bwalo la shulehiyo.
No comments :
Post a Comment