Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkaribisha Balozi wa
Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke katika ofisi za Wizara hiyo
jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ardhi Mhe. William
Lukuvi akimfafanulia Balozi Sarah Cooke mapinduzi makubwa yanayoendelea
kufanyika katika sekta ya Ardhi nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisalimiana na Afisa Maendeleo
kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania wakati akimuaga Balozi wa
Uingereza nchini Tanzania.
Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania Mhe. Sarah Cooke akielezea kufurahishwa kwake na mafanikio
makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Ardhi.
………………………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na Balozi wa Uingereza
nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alipotembelea katika ofisi za Wizara
hiyo.
Balozi Sarah alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Ardhi kwa kipindi kifupi.
Miongoni mwa mafanikio hayo ni
pamoja na Mpango wa Serikali kupanga, Kupima na Kumilikisha kila kipande
cha ardhi nchini pamoja na Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS)
ambao unalinga kutoa huduma za ardhi kwa wananchi kielektroniki pamoja
na utoaji hati za kielektroniki.
Aidha, Balozi huyo amepongeza
mchakato wa kuandaa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 2016 na jinsi ulivyo
shirikisha wananchi na wadau wote wa sekta ya ardhi nchini.
Mhe. William Lukuvi alimueleza
Balozi huyo ambaye alifurahishwa zaidi na juhudi za Serikali za
kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi katika kujiletea maendeleo yao,
pamoja na juhudi za kuwawezesha wananchi wanaoishi katika makazi holela
kupimiwa na kumilikishwa makazi yao pamoja na kupatiwa hati miliki za
ardhi
No comments :
Post a Comment