Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), akimsikiliza
Mwanachama wa Mfuko huo, Margareth Mpunga, aliyefika kuhudumiwa wakati wa Wiki
ya PSPF kwenye kitengo cha huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es
Salaam, Oktoba 4, 2016. Wakurugenzi na Mameneja
wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, waliungana nawafanyakazi wa kitengo hicho kuwahudumia wateja ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za wiki hiyo inayofikia kilele Oktoba 7
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa wateja cha PSPF, Laila Maghimbi, (kushoto), akimuhudumia mteja ofisini kwake Oktoba 4, 2016
Judith Mtweve wa kitengo cha mawasiliano (call centre), akiwa kazini
Meneja wa Kitengo cha Hudma kwa Wateja, akimsikiliza mteja
Mkurugenzi Mkuu, akimsikiliza kwa makini mteja
WANACHAMA
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wamepongeza uongozi wa Mfuko huo, kwa huduma bora
na za haraka katika kuhudumia wateja.
Hayo
wameyasema Oktoba 4, 2016 wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwenye makao
makuu ya Mfuko huo jengo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
“Nimefurahishwa
na huduma zilizokuwa zikitolewa, kwani nilipofika nimepokelewa na kuhudumiwa
haraka, sikuchelewa, kilichonileta ni kuwasilisha risiti za benki za michango
yangu,” alisema Mwanachama wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari,(PSS),
Hamid Maxan Haidary.
Hata
hivyo mwanachama huyo alishauri, Mfuko ufanye juhudi kuelimisha umma hususan
wajasiariamali kama yeye wajiunge nao kwani anahakika wengi watajiunga.
“Wafanyakazi
wapelekwa huko kwenye kata, najua zipo juhudi kubwa za kufanya matangazo kwenye
radio/tv, magazeti na mitandao ya kijamii, lakini sio vibaya wafike wenyewe
mitaani kutoa elimu zaidi.” Alishauri.
“Mimi
kama mtu mwenye kipato cha chini, nilikuwa Napata shida sana inapokuja swala la
kuugua au kuuguliwa na watoto au mke wangu, lakini hivi sasa hilo sio tatizo
tena kwangu, kwani kupitia bima ya afya ambayo nimepata baada ya kujiunga na
PSPF, ninatibiwa bila wasiwasi.” Alifafanua Haidary.
Mwanachama
mwingine wa Mfuko huo ambaye ni mstaafu, Peter Protus Mbele (64), alielezea
kufurahishwa kwake na faida anayopata kutoka PSPF yeye kama mstaafu, ambapo
licha ya kuchukua pensehni ya kila mwezi, ameweza pia kukopa fedha benki na
hivyo kuboresha shughuli zake.
“Kwa
ujumla nafurahia huduma za PSPF, nimeweza kupata mkopo benki, panatokea mara
chache kuchelewa kwa palipo ya mwezi ya pensheni, lakini mimi nachukulia kama
ni changamoto ya kawaida, kwani hata nyumbani mama anaweza kuchelewa
kutayarisha chakula, pengine kwa sababu kuni ni mbichi au mkaa hauko vizuri
lakini hatimaye chakula kinawiza na mnakula,” alisema.
Naye
Devotha R. Kayumbe, aliusifu uongozi wa PSPF kwa kuwajali wateja. “Nimejisikia
raha kuhudumiwa na Mkurugenzi Mkuu, hii inaonyesha jinsi watumishi wa umma
wanavyowajibika na kwenda sambamba na kasi dhana ya Hapa Kazi Tu.”. Alisema
Kayumbe.
Naye
Naomi Albert Duma, ambaye alifika kwa nia ya kujiunga na Mfuko kupitia Uchangiaji
wa Hiari, (PSS), alisema, ameridhishwa na huduma aliyopata kwani amehudumiwa
kwa haraka na hakutegemea kama angechukua muda mfupi kumaliza kile kilichomleta.
“Nimefika
kujiunga na PSS, tayari nimehudumiwa na sasa naondoka.”Alisema .
Akizungumzia
Wiki ya Huduma kwa wateja, Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha PSPF,
Laila Maghimbi, alisema, kila mwaka wiki ya mwanzo ya Oktoba Dunia huadhimisha
Wiki ya Huduma kwa Wateja. “Kuanzia Oktoba 3 hadi 7 tutakuwa tukiadhimisha wiki
hii, kwa viongozi mbalimbali wa Mfuko, kupita maeneo mbalimbali ya nchi
kuungana na wafanyakazi wa huko na kuhudumia wateja.” Alifafanua.
Meneja
huyo alisema, katika wiki hii wateja pia watapata fursa ya kutoa maoni yao ili
Mfuko uweze kuyafanyia kazi kwa nia ya kuboresha huduma, alisema.
Baadhi
ya wakurugenzi na mameneja wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam
Mayingu, waliungana na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja, ili kutoa
huduma kwa wanachama waliofika kupatiwa huduma.
Mkurugenzi
mkuu alipata fursa ya kutoa huduma kwa muda wa dakika 35 na baadaye kutoa barua
za pongezi kwa wafanyakazi bora watatu wa kitengo hicho.
Wafanyakazi
hao ni pamoja na Afisa Huduma kwa wateja, January Buretta, Afisa Mwandamizi wa
Uendeshaji, Hilda Mwema na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Matilda Nyallu.
Alitolea
mfano hapo makao makuu ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko, Adam Mayingu, naye
aliungana na wafanyakazi wa kitengo chake kuhudumia wateja.
“Sambamba
na kutoa huduma, lakini pia Wiki hii tutaitumia kuwatunukia wafanyakazi wetu
bora katika kitengo hiki.” Aliongeza
Mkurugenzi Mkuu, akimsikiliza Mteja, Devotha Kayumbe
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Laila Maghimbi, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mkurugenzi Mkuu, akimkabidhi barua ya
pongezi, Mmoja kati ya wafanyakazi watatu bora wa ,kitengo hicho,
January Buretta, ambaye ni Afisa mwandamizi Huduma kwa wateja wa PSPF
Mkurugenzi Mkuu akimkabidhi barua ya pongezi, Afisa Mkuu wa Matekelezo, Matilda Nyallu
Mkurugenzi Mkuu akimkabidhi barua ya pongezi, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji, Hadija Mwema |
Mkurugenzi wa Uendeshaji, wa PSPF,
Neema Muro, (kulia), akifuatilia jinsi Afisa Uendeshaji Mkuu wa Mfuko
huo, Zeinab Dau, (wapili kulia), wakati akimuhudumia mteja
Meneja Matekelezo wa PSPF, Francis Mselemu, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani, Sosthenes Mushema, (kulia), akimsikiliza kwa makini mteja aliyefika kuhudumiwa Oktoba 4, 2016 |
Afisa mwandamizi msaidizi wa nyaraka, Gwamaka Ngomale, (kushoto), akimuhudumia mteja |
Wateja wakipatiwa huduma na wafanyakazi wa PSPF
Wafanyakazi wa PSPF, sehemu ya call centre wakitekeleza wajibu wao
Picha ya pamoja
Paulina Kagaruki, (kulia), Afisa uendeshaji, akimhudumia mteja
Isack Kimaro, (kushoto), akimuhudumia mteja
Afisa wa Uendeshaji wa PSPF, Elizabeth Shayo, akimuhudumia mteja Oktoba 4, 2016
Hadji Jamadary (kulia), akimuhudumia mkuu wa wilaya wa zamani Lephy Gembe, aliyefika kupata huduma za PSPF Oktoba 4, 2016
Afisa Mkuu Huduma kwa Wateja wa PSPF, Queen Edward, (kulia), akimuhudumia mteja
SBL KUWAPATIA MAJI BURE WAKAZI 65,000 WA TEMEKE, ARUSHA
Moja ya Mradi wa maji uliodhaminiwa na SBL Wilaya ya Hanang mkoani Manyara |
Takribani wakazi 65,000 wa maeneo ya Temeke mkoani Dar es Salaam na Likamba mkoani Arusha hivi karibuni wataanza kufurahia upatikanaji wa maji safi na salama bure huduma ambayop itatolewa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo SBL imesema iko mbioni kujenga na kukabidhi miradi miwili ya maji katika maeneo ya Likamba na Temeke kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 170 ili kupunguza changamoto za uhaba wa maji unaowakabili wakazi wa maeneo hayo mawili.
Mkurugenzi wa Mahusioano SBL John Wanyancha amesema katika taaifa hiyo kuwa miradi hiyo miwili ya maji ni sehemu ya programu ya kampuni hiyo ya kusaidia jamii inayojulikana kama Maji kwa Uhai ambayo inalenga kuzipatia jamii nchini upatikanaji rahisi na wa uhakika wa maji safi na salama.
Kwa mujibu wa Wanyancha zaidi ya Watanzania milioni moja wameshanufaika na programu hiyo katika kipindi cha miaka minnne iliyopita kupitia miradi ya maji kama hiyo iliyotekelezwa katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma.
Mradi wa Maji kwa Uhai unajumuisha uchimbaji wa kisima pamoja na mfumo wake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua (sola) na tenki la maji ambapo kiasi cha lita 45,000 za maji huzalishwa kila baada ya saa sita.
“Kwa miaka kadhaa sasa tumeshuhudia maisha ya familia na kaya yakibadilika kijamii na kiuchumi kutokana na miradi hii ya maji hususani wasichana na wanawake ambao hawatumiii tena saa nyingi kutafuta maji safi. Badala yake muda huo hivi sasa wanautumia kuhudhuria shule pamoja na kufanya shughuli nyingine muhimu za uzalishaji,” alisema mkurugenzi huyo.
Mkakati wa kusaidia jamii wa SBL pia unalenga kutoa msaada kielemu kwa watoto wanaotoka katika familia maskini, uhifadhi wa mazingira, kuhamasisha unywaji wa pombe kistaarabu na kuwasaidia wakulima wa ndani kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha ambayo hadi sasa imewasaidia wakulima nchini kwa kuboresha maisha yao na maisha ya jamii.
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akiongea na Waandishi wa
vyombo vya habari juu umuhimu wa uwekaji wa akiba duniani. Kulia ni Meneja
Masoko wa TPB, Grace Majige na Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki, Timotheo
Mwakifulefule.
NA MWANDISHI WETU
BENKI ya Posta nchini (TPB) imezindua mwezi wa uwekaji akiba duniani
inayokwenda sambamba na kampeni iliyopewa jina la “Asante Mteja”.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi huo, Meneja wa
benki ya TPB tawi la Kariakoo, Patrick Swenya alisema kuwa kampeni hiyo
itaendeshwa nchi nzima katika matawi yao. Alisema, lengo la kampeni hiyo ni
kuhamasisha wateja wa TPB kuweka akiba ili kuweza kufanikisha malengo yao
katika maisha ikiwemo ulipaji wa ada za wanafunzi. Meneja huyo alisema
kuwa katika kuhakikisha wateja wao wanafanikiwa watatoka na kutembelea wateja
wao ambao wengi ni wafanyabiashara ili kupata mrejesho wa huduma wanazozitoa
ikiwemo mikopo kama imeweza kuwakomboa.
Alisema, kama watabaini mikopo inayotolewa imewanufaisha watu wengi
basi watahakikisha inaboreshwa zaidi ili kuwakwamua watu wengi kiuchumi.
"Katika wiki hii ya uwekaji akiba duniani tutahakikisha sisi kama TPB
tunaboresha huduma zetu ili kufanikisha zaidi Watanzania ikiwa pia ni moja ya
njia ya kuwashukuru kwa kuchagua Benki yetu", alisema Swenya. Aidha
aliongeza kuwa TPB itaendelea kuboresha huduma ikiwemo mikopo ya vikundi
visivyo rasmi inayotolewa kwa riba nafuu.
Kwa upande wake mmoja wa wateja wa benki hiyo Alex Lwamanya alisema
kuwa mikopo ya riba nafuu inayotolewa na benki hiyo imeweza kumkwamua kiuchumi
kwa kiasi kikubwa.
Alisema, hadi sasa mikopo hiyo imemuwezesha kujenga nyumba pamoja na
kuendeleza biashara zake. "Nashkuru mikopo niliyoipata na ninayoendelea
kupata imenikwamua kimaisha kwa kiasi kikubwa sana kwani hadi sasa nimeweza
kumiliki vitega uchumi vinavyoniingizia kipato", alisema Alex.
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja
ya wateja wa tawi hilo Grace Mgala katika uzinduzi wa mwezi wa akiba duniani. Kushoto
ni Afisa Mwandamizi wa huduma kwa wateja, Glory Mutta.
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja
ya wateja wa tawi hilo Alex Lwamanya katika uzinduzi wa mwezi wa akiba duniani.
Kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki, Timotheo Mwakifulefule
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja
ya wateja wa tawi hilo Grace Mgala katika uzinduzi wa mwezi wa akiba duniani. Kushoto
ni Afisa Mwandamizi wa huduma kwa wateja, Glory Mutta.
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja
ya wateja wa tawi hilo Mohammed Salim katika uzinduzi wa
mwezi wa akiba duniani.
Meneja
wa Benki ya Posta Tawi la Kariakoo, Patrick Swenya akimpa zawadi ya benki moja
ya wateja wa tawi hilo Jumanne Waziri katika uzinduzi wa mwezi wa akiba
duniani.
Kanisa la All-
Nations Christian Tabernacle (ACT) linaloendesha shughuli zake katika ukumbi wa
Utoji, Sinza Mapambano jijini Dar limezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa
kanisa hilo rasmi .
Akizungumza
katika misa iliyofanyika eneo hilo, mchungaji wa kanisa hilo Pastor Sos Mabele
alisema kuwa harambee hiyo imezinduliwa kanisani hapo kwa waumini na watu
mbalimbali kuweka ahadi au kuchangia moja kwa moja fedha kwa ajili ya ujenzi wa
kanisa unaotarajiwa kuanza mwisho wa mwaka huu.
Mbali na
hayo Mchungaji huyo aliwataka watu mbalimbali wajitokeze kuchangia ujenzi wa kanisa hilo bila kujali madhehebu
au dini, kwa kuwa Mungu ni wa wote ambapo
pia alisema kuwa zoezi la harambee
litaisha tarehe 25 mwezi huu kwa walioahidi wote kutimiza ahadi zao.
“Sisi kanisa
letu kama linavyosema kuwa ni All- Nations Christian Tabernacle yaani hekalu la
makanisa ya mataifa yote, hivyo hatubagui mtu kwa dhehebu wala dini na wote
wanakaribishwa kila jumapili kwenye ibada zetu,” alisema Pastor Sos na kuwataka
watu waendelee kuwasiliana naye kwa ahadi na michango kupitia namba 0784935855.
Naye
mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo, bwana Ibrahimu Chanikicha,
aliwashukuru wote wanaoendelea kuchangia kwa hali na mali na kuwaomba waendelee
kuwa na moyo huohuyo.
Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akisali wakati akifungua Ibada hiyo iliyokuwa ni ya ufunguzi wa Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa
Mmoja ya waumini akisoma neno la Mungu wakati Mchungaji akiwaongoza
Waumini wakimsikiliza kwa makini Baba Mchungaji akifundisha neno
Katibu wa kamati ya ujenzi Debora Simon (wa kwanza Kulia) pamoja na waumini mwengine wakifuatilia neno
Mchungaji
wa Kanisa
la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiendelea kutoa
mahubiri wakati wa Ibada hiyo ya uzinduzi wa Harambee ya uchangiaji kwa
ajili ya ujenzi wa Kanisa
Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akifuatilia Ibada kwa makini
Waumini wakiendelea kufuatilia Ibada kwa makini
Mmoja wa watoto akisoma Neno la Mungu wakati wa Ibada hiyo ya Uchangiaji kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa
Wakijiandaa Kumtukuza Mungu
Baadhi ya watoto wakiwa Ibadani
Mchungaji
wa Kanisa
la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiimba nyimbo za Sifa
Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akizungumza neno wakati wa Ibada hiyo
Ibrahim Chanikicha Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi akizungumza jambo
Waimbaji wakiendelea kumtukuza Mungu kwa njia ya Nyimbo za Sifa
Waumini wakiimba nyimbo za Sifa
Muda wa Maombezi ulifika ambapo Mchungaji
wa Kanisa
la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele aliwaombea watumishi mbali mbali
Wakiendelea kusifu na Kuabudu
Picha zote na Fredy Njeje
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes
Mesa wakati alipokutana naye Ikuu leo kwa mazungumzo ambapo
wamezungumzia jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania
katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa
manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.(PICHA KWA HISANI YA OFISI YA
MAKAMU WA RAIS)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Tanzania na Cuba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi zawadi ya picha ya mnyama Chui anayepatikana katika mbuga
za wanyama za Tanzania Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador
Valdes Mesa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba
Mh. Salvador Valdes Mesa , Kulia ni Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
................................................................................................
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali
ya Tanzania na Cuba zimeahidi kuendeleza ushirikiano uliopo, ambao
umeasisiwa na viongozi wa mataifa hayo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
wa Tanzania pamoja na Fidel Castro Rais mstaafu wa Cuba.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Ikulu leo jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, amesema kuwa
Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa ameitikia mwaliko huo
wa kuja nchini kwa vile nchi hizo mbili zimekua na ushirikiano na
mahusiano mazuri kwa muda mrefu.
“Ziara
hii ni moja ya jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania
katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa
manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili ili kuhakikisha mahusiano
yaliyopo yanaimarika zaidi” alisema Makamu wa Rais
Katika
ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Cuba nchini, mambo mbalimbali
yalijadiliwa ikiwemo masuala ya Afya, Elimu, Michezo, na Utamaduni,
ambapo katika sekta ya afya nchi ya Cuba imepiga hatua na kuahidi
kushirikiana na Tanzania ili kujenga kiwanda cha kisasa cha
kutengeneza madawa ya binadamu.
Aliongeza
kuwa Tanzania imeomba Serikali ya |Cuba kuendelea kusaidia sekta hiyo
kwa kufundisha wataalamu wa afya, ambapo tayari madaktari 24 kutoka Cuba
wako nchini kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za kitabibu na mafunzo
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.
Masuala mengine yaliyojadiliwa katika ziara hiyo ni pamoja na ushirikiano katika sekta ya elimu, biashara, utalii na uwekezaji.
Ambapo
pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu
amesisitiza nia ya Serikali ya Tanzania kudumisha ushirikiano huo ikiwa
ni pamoja kupongeza jitihada za kuboresha uhusiano wa Cuba na Marekani.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa
ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuonesha ushirikiano kwa
nchi yake na kuahidi kuendelea kutoa msaada kwa Tanzania.
“Tumeamua
kuendelea kuboresha mahusiano yetu na Tanzania kwa kuongeza ushirikiano
wetu katika sekta nyingine ambazo hatukuwa tunashirikiana hapo awali
kama vile sekta ya utalii” alisema Makamu wa Rais wa Cuba
Aidha,
Mhe. Mesa ameiomba Tanzania kuendelea kuiunga mkono Cuba katika masuala
ya kimataifa ili kuendeleza ushirikiano na kukuza uchumi kwa nchi zote
mbili.
Makamu
wa Rais wa Cuba aliwasili nchini jana jioni kwa ziara ya siku tatu
ambapo alipata fursa ya kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa John Magufuli .
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mara baada ya kuwasili katika
Uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere JNIA.(PICHA NA
IKULU)
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake
wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati nyimbo za
Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa kabla ya ukaguzi wa gwaride
lililoandaliwa kwa ajili ya heshima yake.
Rais wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akikagua gwaride la heshima
lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati kikundi cha ngoma za asili kilipokuwa kinatumbuiza uwanjani hapo |
No comments :
Post a Comment