Monday, October 31, 2016

TANZANIA YANG’ARA MAONYESHO YA BIASHARA NA UTALII SAUD ARABIA

Balozi Hemed Mgaza, wakati anaapa baada ya kuapishwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia.
Katika maonyesho hayo ambayo bidhaa mbalimbali zilionyeshwa
ukiwamo eneo maalum la mlima Kilimanjaro, nguo za Kitanzania na viatu pamoja na
bidhaa nyingine muhimu zilizoonekana kuwapendeza wengi waliohudhuria maonyesho
hayo.
Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Mheshimiwa Hemed Mgaza, alisema kwamba wananchi wengi waliohudhuria maonyesho hayo walionekana kuvutiwa zaidi na nchi ya Tanzania kutokana na vivutio vyake.
 
Alisema hali hiyo imekuja kutokana na aina ya bidhaa zilizoonyeshwa pamoja na ubunifu wa kutangaza bidhaa zao na nchi kwa ujumla, wakiamini kuwa utachochea wageni wengi wa kutoka nchini hapa kwenda kutembelea nchini Tanzania kwa mambo mbalimbali.

“Binafsi nimefarijika mno kutokana na wenyeji kuandaa
maonyesho haya na kutuaalika Watanzania ambao watumishi wa ofisi yangu pamoja
na mimi mwenyewe wote tulihakikisha kwamba tunayatumia vizuri kutangaza nchi
yetu Tanzania.
“Tumewahakikishia kwamba mbali na nchi yetu kujawa na
vivutio vingi kutoka Tanzania Bara na Visiwani, lakini bado tumejawa na amani
kiasi kwamba unapokuwa kwenye ardhi ya Tanzania huna sababu ya kuwa na wasiwasi
wowote kwa sababu wananchi wake wanaishi kwa upendo,” alisema Balozi Mgaza.
 
Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, maonyesho hayo kwenye ofisi yao
waliyapa jina la Visit Tanzania the land Kilimanjaro, Serengeti and Zanzibar,
ambapo pia walitangaza bidhaa za chai, kahawa, viatu vya kimasai, vinyago vya
wanyama na nguo za utamaduni.

No comments :

Post a Comment