Monday, October 31, 2016

RAIS MAGUFULI ATUA KENYA, ALAKIWA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE BI. AMINA MOHAMMED



Rais John Pombe Magufuli, akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kenya, Bi. Amina Mohammed kwenye uwanja wa ndege kimataifa wa wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi leo Oktoba 31, 2016. Rais yuko nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. (PICHA NA MPIGA PICHAMAALUM)





Mkurugenzi wa Singita Grumeti Stephen Cunliffe (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa msaada wa madawati 500 yenye Thamani ya Tshs Milioni 112 kwa ajili ya Wilaya za Serengeti na Bunda katika hafla  iliyofanyika  Shule ya Msingi Makundusi Wilayani Serengeti.




MFUKO wa Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha hali ya elimu katika Wilaya za Serengeti na Bunda.
Hii imedhihirika kwenye halfa ya kukabidhi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa ili kupunguza uhaba wa madawati katika Wilaya hizo. Aidha Grumeti wamekabidhi nyumba ya kuishi mwalimu iliyojengwa katika Shule ya Msingi Makundusi.
“Tuko hapa kukabidhi madawati haya 500 yenye thamani ya Tshs Milioni 112 kwa Wilaya za Serengeti na Bunda pamoja na nyumba hii yenye thamani ya Tshs Milioni 86” alisema Richard Ndaskoi ambae ni Mkuu wa Huduma za Jamii toka Mfuko wa Singinta Grumeti.
Akipokea misaada hiyo, Dk. Mlingwa alisema “Nawashukuru Singita Grumeti kwa Msaada huu wa madawati pamoja na nyumba hakika mchango wenu katika Mkoa wa Mara unaoneka” Dk Mlingwa amewataka wawekezaji wengine katika Mkoa wa Mara kuchangia madawati katika Wilaya za Serengeti na Bunda kwani bado zina uhaba wa madawati.
Aidha Dk. Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kuwa na mahusiano mazuri na wawekezaji waliopo katika Wilaya hiyo “Tukiwawekea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao hata wananchi pia watanufaika na uwepo wa wawekezaji hawa” alisema Dk. Mlingwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili wote kwa nyakati tofauti wameushukuru Mfuko wa Singita Grumeti kwa msaada huo wa madawati na kuuomba mfuko huo kuendelea kuchangia katika shughuli za maendeleo katika Wilaya za Serengeti na Bunda. “Wilaya hii ina wawekezaji wengi lakini wamekuwa nyuma katika kuchangia shughuli za maendeleo, nawapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kuchangia katika maendeleo ya Wilaya ya Serengeti” alisema Nurdin Babu.
Aidha Bi. Bupilipili ameuomba Mfuko huo kuanzisha kampeni maalumu ya kuongeza kiwango cha ufaulu kwa watoto wa kike kwa shule za sekondari Wilayani Bunda.
Singita Grumeti wamekuwa wawekezaji wenye tija kwa wananchi wa Wilaya za Serengeti na Bunda licha ya kuwa mstari wa mbele kuchangia katika shughuli za maendeleo, kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa ajira kwa wakazi toka wilaya hizo mbili pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi toka wilaya hizo.



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwasha mshumaa ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi wa Kudhibiti Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa njia ya bahari. Mkutano huo unafanyika mjini Colombo nchini Sri Lanka. Picha zote na WMNN.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akisikiliza mada zilizokuwa zinatolewa katika Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi wa Kudhibiti Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa njia ya bahari unaofanyika mjini Colombo nchini Sri Lanka
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi wa Kudhibiti Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa njia ya bahari unaofanyika mjini Colombo nchini Sri Lanka

No comments :

Post a Comment