Waziri wa elimu, sayansi
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa na chepe ya mchanga katika
ufyatuaji watofali katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Nassibugani
kabla ya kufunga kambi ya ufyatuaji tofali, Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, Evarist Ndikilo, kulia ni Mbunge wa Mkurang Abdallah Ulega.
Waziri wa elimu, sayansi
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa ameshika kibao chenye tofali
pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo kabla ya kufunga kambi
ya ufyatuaji tofali katika katika shule ya Sekondari Wavulana
Nassibugani.
Waziri wa elimu, sayansi
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wazaledo wa vyuo vya ndani na nje ya nchi pamoja na viongozi
mbalimbali baada ya kufunga kambi ya ufyatuaji tofali iliyodumu mwezi
mmoja.
……………………………………………………………….
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema wananchi wa Mkuranga wamejitoa katika kupata Mandeleo.
Profesa Joyce Ndalichako
ameyasema hayo wakati wa kufunga kambi ya kufyatua tofali zaidi ya
45000 kwa ajili ujenzi wa Mabweni Matano na Nyumba tano za walimu katika
shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya Msonga Wilaya Mkuranga.
Profesa Joyce amesema kuwa wananchi wamejitoa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora inayoendana na mazingira.
Amesema kuwa nia yake nikuona Mkuranga inakuwa na Mapinduzi ya Elimu.
Amesema vijana 53 wazalendo
kutoka vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi wameamua kuunga mkono
jitihada za serikali katika suala la elimu kupewa kiupaumbele katika
kusaidia maendeleo ya Taifa.
Amesema ujenzi wa mabweni hayo itakuwa suluhu kwa wavulana kufanya vizuri kutokana kupunguziwa umbali wa kufika shule.
Profesa Ndalichako, amesena jitihada zinaendelea kutatua baadhi ya changamoto za elimu kwa kushirikiana na wananchi.
Katika ufungaji wa kambi hiyo Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema nia yake ni kuona maendeleo yanapatikana yenye tija.
Waliohudhuria ufungaji ni Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula, Mkuu wa
Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, Mkuu wa Wilaya, Filberto Sanga na
viongozi mbalimbali.
No comments :
Post a Comment