Tuesday, October 4, 2016

PPF YASAJILI WANAKIJIJI WAJASIRIAMALI 395 KWENYE MPANGO WA WOTE SCHEME HUKO IKWIRIRI MKOANI PWANI

 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kulia), akiwasaidia wanakijiji hawa wa Ikwiriri, Wilayani Rufiji mkoani Pwani, kutuma michango kwa njia ya mtandao wa simu, wakati wa kuandikisha wanachama chini ya mpango wa Wote Scheme kwenye chuo cha Maendeleo ya Jamii, Ikwiriri,  Oktoba 3, 2016. Takriban wanakijiji 395 wakiwemo, wakulima, wafuga nyuki, wavuvi na waendesha bodaboda, wamekabidhiwa kadi za uanachama kupitia mpango huo unaoruhusu mtu yeyote aliye kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi kujiunga kwa kuchangia kila mwezi kima cha chini shilingi 20,000.
 Meneja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari, (Wote Scheme), wakati wa kuandikisha wanachama na kugawa kadi kwenye viwanja vya chuo cha ufundi Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoa wa Pwani, Oktoba 3, 2016.
 Zawadi Hamza Sule, (kushoto), ambaye ni mkulima huko Ikwiriri, akipokea kadi yake ya uanachama wa PPF kupitia Wote Scheme
NA MWANDISHI WETU, IKWIRIRI
MFUKO wa Pensheni wa PPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari, “Wote Scheme”, umesajili karibu wanachama 400  huko Ikwiriri wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la usajili na ugawaji kadi za uanachama kwenye viwanja vya chuo cha Ufundi Ikwiriri, (IFDC), Oktoba 3, 2016, Meneja wa PPF Kanda ya Temeke, Erica Meshack Sendegeya, alisema,  wanakijiji hao wajasiriamali walihamasika kujiunga na mpango huo baada ya Kanda yake kutoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko huo kwani kuna manufaa  mengi.
“Tuliwaeleza, mpango huu wa Wote Scheme umebuniwa ili kutoa fursa ya wananchi walioajiriwa au waliojiajiri wenyewe, wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji, Boda boda  na mama lishe, kujiunga na Mfuko kwa kuchangia kima cha chini cha shilingi 20, 000 kila mwezi. “Fedha hizo unaweza kuzitoa kwa mkupuo au kwa awamu kulingana na uwezo wa mwanachama,” alifafanua Sendegeya.
Akielezea faida za kuwa mwanachama, Meneja huyo alisema, “Mwanachama atafaidika na fao la Afya ambapo atapatiwa bima ya afya kupitia NHIF baada ya kuchangia shilingi elfu 60,000 tu.” Alisema na kuongeza kuwa faida nyingine ni pamoja na mwanachama kujipatia mkopo wa maendeleo ambapo sharti kuu la kupata mkopo huu ni mwanachama kuchangia Mfuko kwa kipindi cha miezi sita, mkopo wa elimu, lakini pia fao la uzeeni, alisema Meneja huyo.
Kuhusu namna mwanachama anavyoweza kuchangia baada ya kujiunga na Mpango huo, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele alisema, “Kuna njia rahisi ya kuwasilisha michango, ambayo ni kutumia mitandao ya simu, Airtel Money, Tigo Pesa na M-Pesa.” Alisema.
Baadhi ya wanakijiji waliojiunga na Mpango huo, wameipongeza PPF kwa kutoa elimu ambayo imewafanya wajiunge na Mfuko huo na ni matarajio yao utasaidia kuboresha shughuli zao.
“Mimi ni mfuga nyuki, kilichonivutia ni jinsi Mfuko huu unavyoweza kutoa mikopo ya maendeleo,” alisema Erasto Joseph, ambaye pia ni mwalimu wa shule.
Naye Ishara Ibrahim ambaye ni mkulima, alisema, ni matarajio yake kuwa kujiunga na PPF, basi ataweza kumudu kupata huduma ya afya kupitia Bima ya Afya.” Alisema.
  Zawadi Hamza Sule, akionyesha kadi yake baada ya kukabidhiwa
 Seif M. Mgumba akionyesha kadi yake ya uanachama wa PPF, kupitia Wote Scheme
 Khadija R. Kitango, akionyesha kadi yake
 Meneja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, akizungumza na wanachama hao wapya wa PPF huko Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Oktoba 3, 2016
 Wanachama wapya wa PPF, wakiwasikiliza viongozi wa PPF 
 Wanachama hawa wapya wakionyeshana kadi zao za uanachama baada ya kukabidhiwa
Wanachama wakisubiri utaratibu wa kukabidhiwa kadi zao na kufanya malipo ya michango ya awali
 Wanachama wapya wa PPF, wakihudumiwa
 Meenja wa PPF, Kanda ya Temeke, Erica (kushoto), na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele, wakiwasaidia wanachama hao kutumia simu zao za mkononi kuweka michango yao 
 Erica, akiwasaidia kuwaelekeza namna ya kutuma michango kupitia simu za mkononi
 Erica (kulia) na Lulu, wakimsikiliza mwanachama huyu wa Ikwiriri baada ya zoezi la kuwapatia kadi za uanachama Oktoba 3, 2016
 Erica, akisoma majina ya wanachama wapya waliojiunga na PPF kupitia Wote Scheme
 Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, akiwaarifu waandishi wa habari kuhusu shughuli nzima ilivyokwenda
 Lulu akisalimiana na wanachama hawa wenye furaha
Wanakijiji wa Ikwiriri wakisubiri kupatiwa kadi zao za uanachama baada ya kujiunga na PPF kupitia uchangiaji wa Hiari, (Wote Scheme) Oktoba 3, 2016

ACT YAZINDUA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA JIJINI DA


Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) linaloendesha shughuli zake katika ukumbi wa Utoji, Sinza Mapambano jijini Dar limezindua harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo rasmi .

Akizungumza katika misa iliyofanyika eneo hilo, mchungaji wa kanisa hilo Pastor Sos Mabele alisema kuwa harambee hiyo imezinduliwa kanisani hapo kwa waumini na watu mbalimbali kuweka ahadi au kuchangia moja kwa moja fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa unaotarajiwa kuanza mwisho wa mwaka huu. 

Mbali na hayo Mchungaji huyo aliwataka watu mbalimbali wajitokeze kuchangia  ujenzi wa kanisa hilo bila kujali madhehebu au dini, kwa kuwa Mungu ni wa wote  ambapo pia alisema kuwa zoezi la harambee  litaisha tarehe 25 mwezi huu kwa walioahidi wote kutimiza ahadi zao.

“Sisi kanisa letu kama linavyosema kuwa ni All- Nations Christian Tabernacle yaani hekalu la makanisa ya mataifa yote, hivyo hatubagui mtu kwa dhehebu wala dini na wote wanakaribishwa kila jumapili kwenye ibada zetu,” alisema Pastor Sos na kuwataka watu waendelee kuwasiliana naye kwa ahadi na michango kupitia namba 0784935855.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo, bwana Ibrahimu Chanikicha, aliwashukuru wote wanaoendelea kuchangia kwa hali na mali na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huohuyo.

Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akisali wakati akifungua Ibada hiyo iliyokuwa ni ya ufunguzi wa Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa
 Mmoja ya waumini akisoma neno la Mungu wakati Mchungaji akiwaongoza
 Waumini wakimsikiliza kwa makini Baba Mchungaji akifundisha neno
Katibu wa kamati ya ujenzi Debora Simon (wa kwanza Kulia) pamoja na waumini mwengine wakifuatilia neno
 Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiendelea kutoa mahubiri wakati wa Ibada hiyo ya uzinduzi wa Harambee ya uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa
 Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akifuatilia Ibada kwa makini
 Waumini wakiendelea kufuatilia Ibada kwa makini
 Mmoja wa watoto akisoma Neno la Mungu wakati wa Ibada hiyo ya Uchangiaji kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa
 Wakijiandaa Kumtukuza Mungu
 Baadhi ya watoto wakiwa Ibadani
 Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele akiimba nyimbo za Sifa
 Mweka Hazina wa Kanisa hilo Bwana Geofrey Raymond akizungumza neno wakati wa Ibada hiyo
Ibrahim Chanikicha Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi akizungumza jambo 
 Waimbaji wakiendelea kumtukuza Mungu  kwa njia ya Nyimbo za Sifa
 Waumini wakiimba nyimbo za Sifa
 Muda wa Maombezi ulifika ambapo Mchungaji wa Kanisa la All- Nations Christian Tabernacle (ACT) Sos Mabele aliwaombea watumishi mbali mbali
 Wakiendelea kusifu na Kuabudu
Picha zote na Fredy Njeje
mao1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakati alipokutana naye Ikuu leo kwa mazungumzo ambapo wamezungumzia jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.(PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
mao2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Tanzania na Cuba.
mao3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi ya picha ya mnyama Chui anayepatikana katika mbuga za wanyama za Tanzania Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa.
mao4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa , Kulia ni Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
................................................................................................
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali ya Tanzania na Cuba zimeahidi kuendeleza ushirikiano uliopo, ambao umeasisiwa na viongozi wa mataifa hayo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania pamoja na Fidel Castro Rais mstaafu wa Cuba.
Akizungumza na waandishi wa habari, Ikulu leo jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, amesema kuwa Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa ameitikia mwaliko huo wa kuja nchini kwa vile nchi hizo mbili zimekua na ushirikiano na mahusiano mazuri kwa muda mrefu.
“Ziara hii ni moja ya jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili ili kuhakikisha mahusiano yaliyopo yanaimarika zaidi” alisema Makamu wa Rais
Katika ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Cuba nchini, mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo masuala ya Afya, Elimu, Michezo, na Utamaduni, ambapo katika sekta ya afya nchi ya Cuba imepiga hatua na kuahidi kushirikiana na Tanzania ili kujenga kiwanda cha kisasa cha kutengeneza madawa ya binadamu.
Aliongeza kuwa Tanzania imeomba Serikali ya |Cuba kuendelea kusaidia sekta hiyo kwa kufundisha wataalamu wa afya, ambapo tayari madaktari 24 kutoka Cuba wako nchini kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za kitabibu na mafunzo katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.
Masuala mengine yaliyojadiliwa katika ziara hiyo ni pamoja na ushirikiano katika sekta ya elimu, biashara, utalii na uwekezaji.
Ambapo pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu amesisitiza nia ya Serikali ya Tanzania kudumisha ushirikiano huo ikiwa ni pamoja kupongeza jitihada za kuboresha uhusiano wa Cuba na Marekani.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuonesha ushirikiano kwa nchi yake na kuahidi kuendelea kutoa msaada kwa Tanzania.
“Tumeamua kuendelea kuboresha mahusiano yetu na Tanzania kwa kuongeza ushirikiano wetu katika sekta nyingine ambazo hatukuwa tunashirikiana hapo awali kama vile sekta ya utalii” alisema Makamu wa Rais wa Cuba
Aidha, Mhe. Mesa ameiomba Tanzania kuendelea kuiunga mkono Cuba katika masuala ya kimataifa ili kuendeleza ushirikiano na kukuza uchumi kwa nchi zote mbili.
Makamu wa Rais wa Cuba aliwasili nchini jana jioni kwa ziara ya siku tatu ambapo alipata fursa ya kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli .

No comments :

Post a Comment