Mabalozi 12 kutoka nchi mbalimbali wamefika Tanga kuangalia furasa za uwekezaji kwa kutembelea Bandari ya Tanga, Bohari ya mafuta ya GBP na eneo ambalo litajengwa bombala Mafuta kijiji cha Chongoleani.
Akizungumza katika mkutano na ujumbe huo, Meneja wa Bandari Tanga, Hendry Arika, alisema ujumbe huo umejionea kasi kuelekea ujenzi wa bomba la Mafuta na kuwataka wawekezaji wa ndani kuangalia namna ambavyo nao watawekeza.
Kaimu Meneja Bandari Tanga, Hendry Arika, akiwafahamisha mabalozi wa nchi za Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchini wakati walipotembelea Bandari ya Tanga kuangalia fursa za uwekezaji kufuatia ujio wa mradi wa bomba la mafuta Tanga.
MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI WA UNHCR NCHINI
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimfafanulia
jambo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi
(UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea
Naibu Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la
kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Katikati ni
Mkurugenzi wa Idara ya wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia),
akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia
Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya wakati alipokuwa anamfafanulia jambo
kuhusu masuala ya wakimbizi nchini. Mwakilishi huyo alipomtembelea Naibu
Waziri ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
PAMBANO LA ANTHONY JOSHUA NA WLADIMIR KLISTCHKO KUTOFANYIKA MWAKA HUU
Bingwa wa uzito wa juu wa IBF
Muingereza, Anthony Joshua, hatopigana tena na Wladimir Klistchko
mwaka huu.
Mabondia hao walikuwa wapigane
Desemba 10, lakini Klitschko amepata majeraha madogo wakati akifanya
mazoezi.
Sasa Joshua atapanda ulingoni
Desemba 10 kupigana na David Prince, huku pambano lao na Klitschko
likitarajiwa kufanyika mwezi Machi ama Aprili mwakani.
Bingwa wa IBF Muingereza Anthony Joshua akiwa na mkanda wake.
DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji
wakati wa kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika
utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016
kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 24/10 /2016.
Baadhi
ya Wakurugenzi katika Idara mbali mbali katika Wizara ya
Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wakiwa katika mkutano wa siku moja
unaozungumzia Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa
robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu
Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na
Ikulu.] 24/10 /2016.
Baadhi
ya Wakurugenzi katika Idara mbali mbali za Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano
na Usafirishaji wakiwa katika mkutano wa siku moja unaozungumzia
Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya
kwanza ya Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini
ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 24/10 /2016.
Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Balozi Ali Abeid
Karume (katikati) akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mpango kazi wa
mwaka 2016-2017 katika kikao cha robo mwaka ya kwanza ya
Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya
mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) (kulia) Katibu Mkuu Kiongozi
Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Mohamed
Ahmed Salum,[Picha na Ikulu.] 24/10 /2016.
PROFESA MAGHEMBE AFUNGA MAFUNZO YA ASKARI WANYAMAPORI KITUO MLELE KATAVI
MATUKIO MBALIMBALI UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIUCHUMI WA KOREA NA AFRIKA MJINI SEOUL, KOREA KUSINI
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akipokea zawadi ya
kitabu kinachoelezea njia zilizotumiwa na nchi ya Korea Kusini, kupiha
hatua kubwa ya maendeleo, kutoka kwa Afisa Mikopo wa Benki ya Exim ya
Korea Kusini, Park Gil Jong, kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa
tano wa ushirikiano wa Korea Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini
Seoul, Korea Kusini.
Mawaziri
wa Fedha kutoka nchi 54 za kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Tano wa
ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi Afrika (KOAFEC)
wakiweka alama ya kiganja cha mkono kwenye kibao chenye malighafi
maalumu yanayoshika alama za vidole kuonesha ushirikiano na umoja, baada
ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo katika ukumbi wa Grand
Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa
ameshika kibao alichoweka alama ya kiganja chake, kuunga mkono umoja na
mshikamano wa nchi za Kiafrika zinazohusiana kiuchumi na Korea Kusini
baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Tano wa ushirikiano huo kati ya
Korea Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC) katika ukumbi wa Grand
Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini.
MKUTANO UHUSIANO NCHI ZA KOREA NA AFRIKA WAFUNGULIWA SEOUL, KOREA
MKUTANO wa Tano wa Ushirikiano kati ya Nchi za Kiafrika na Korea Kusini (Korea-Africa Economic Cooperation (KOAFEC), Umefunguliwa leo Jijini Seoul, Korea Kusini, huku agenda kubwa ikiwa ni kuzungumzia namna nchi za Kiafrika zinavyoweza kutumia kilimo katika muktadha wa maendeleo ya viwanda ili ziweze kujikwamua haraka kiuchumi.
Mkutano wa tano wa KOAFEC mwaka huu umebeba kaulimbiu ya kuibadili Afrika kwa njia kilimo na mpango jumuifu wa watu unaolenga kuimarisha sekta ya fedha kwa njia ya mitandao ya simu” (Transforming Africa’s Agriculture through Industrialization and Inclusive Finance)
No comments :
Post a Comment