Monday, October 31, 2016

KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA COMMORO NA TANZANIA KUFANYIKA ZANZIBAR images

images 
Na Mwashungi Tahir -Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya 361 ya Dar es salaam inaandaa Kongamano la pili la biashara baina ya Tanzania na Commoro.

Kongamano hilo ambalo linaratibiwa na Wizara ya Biashara , viwanda na masoko Zanzibar  litafanyika Novemba 19,2016, katika hoteli ya Seacliff iliyopo Kama nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Biashara, viwanda na masoko  Amina Salum Ali  wakati akizungumza na waandishi  wa habari huko ofisini kwake Migombani.
Waziri Amina amesema Mgeni rasmi anaetarajiwa 
kulifungua kongamano hilo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein.
Amesema katika ufunguzi wa Kongamano hilo kutafanyika shughuli za uwasilishaji mada na majadiliano, mikutano ya ana kwa ana (B2B) na maonyesho ya wajasiriamali.
Ameongeza kuwa kutakuwa na mada zitazowakilishwa na kugusa maeneo ya uwekezaji,biashara na miundombinu ya usafirishaji wa bidhaa baina ya Tanzania na Comoro na kuangalia fursa na vikwazo katika biashara ili kurahisisha Sekta ya biashara.
Waziri Amina amesema kongamano hilo la biashara baina ya Tanzania na Commoro ni la pili, ambapo tamasha  la kwanza  kama hilo lilifanyika nchini Commoro  April 23, mwaka jana.
Akielezea kuhusu kongamano la kwanza, amesema washiriki zaidi ya hamsini kutoka Tanzania  wakiongozwa na aliekuwa Waziri wa Mambo ya nchi za nje Benerd Membe walishiriki Kongamano hilo.
“Kongamano la pili la biashara baina ya Tanzania na Commoro linatarajiwa kuwa na washiriki  zaidi ya mia moja wakiwemo wafanyabiashara, wawekezaji , wajasiriamali na wadau kutoka taasisi za umma” alisema waziri Amina.
Balozi Amina ameongeza kuwa  katika  kongamano  hilo atashauri  kuangaliwa upya suala la kodi  kwani wafanyabiashara wengi wamekuwa wakilalamikia  kodi iliyopo kati ya Tanzania na Comoro kuwa ni kubwa.
Naye Balozi wa Commoro  Elbadaoui Fakih amesema Tanzania imekuwa msaada mkubwa kwa nchi yake hasa kwa kusaidia  mambo mengi ikiwemo  biashara na masuala ya kiuchumi

No comments :

Post a Comment