Msemaji wa CCM, Chritopher Ole Sendeka
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara
Zanzibar Ndg Simai Mohammed Said akitiliana saini ya Makubaliano ya
kusaidia Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar na Balozi wa Ujerumani
Tanzania Balozi Egon Kochanke, Ujerumani imekubali kuchangia €5000 sawa na shilingi za Kitanzania milioni 12,hafla
hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Park Hyyat
Shangani Zanzibar leo. Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar hufanyika
kila mwaka katika mwezi wa Febuary na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali
wanaotembelea Zanzibar.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa
Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Dua ya kuwaombea wanafunzi wote wa
Tanzania wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Nne ili wafanye vizuri
akiwa katika Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba
28, 2016.
Baadhi
ya waumini wa dini ya Kiislam wakiomba dua mara baada ya sala ya Ijumaa ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alihutubia
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam
baada ya Sala ya Ijumaa
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafar
Mwanyemba na Sheikh Shabaan Kitila baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti
wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco, Mohammed
VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika
na Waislamu wengine wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil
Soraga katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja Oktoba 28, 2016. Mfalme
Mohammed VI yupo visiwani humo kwa ziara ya kibinafsi. (PICHA NA IKULU YA
ZANZIBAR)
Viongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar
Mfalme
wa Morocco, Mohammed VI(kulia) akisalimiana na Katibu wa Mufti wa
Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia), akipokea mmoja kati ya misahafu 10,000, iliyotolewa na Mfalme wa Morocco,
Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo Oktoba 28, 2016 katika
Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja. Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya
kibinafsi na ujumbe wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani
Mjimkongwe wa Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na Mkuu wa Mkoa
wa Mjini Magharibi Mhe, Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakitoka ndani ya Msikiti
wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya Ijumaa
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada ya kumalizika
kwa swala ya Ijumaa
No comments :
Post a Comment