Tuesday, September 6, 2016

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 7 KWA WAPANGAJI NHC KULIPA MADENI, VINGINEVYO AMUAGIZA MCHECHU AWATOE NJE





RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ametoa siku 7 kuanzia leo Septemba 6, 2016 kuwatoa nje wapangaji wote wa Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC), wanaodaiwa.
Rais ameyasema hayo wakati alipotembelea eneo lililokuwa MagomeniKota, wilayani Kinondonijijini Dar es Salaam leo Septemba 6, 2016. “Wapangaji wote wa serikali ndani ya siku 7 wawe wamelipa madeni, wasipolipa watoe nje,  endelea kuwatoa kama ulivyomtoa yule jamaa, awe wa CCM, mtoe nje, awe wa UKAWA, mtoe nje, awe wa  serikali mtoe nje, awe waziri mtoe nje, awe mpangaji huyo ni Rais mtoe nje, ni lazima upate pesa Ili shughuli za ujenziwa nyumba mpya ziendelee.” Alisema Rais Magufuli wakati akihutubia wakazi waliokuwa wakiishi kwenye nyumba hizo za Magomeni Kota ambazo zilivunjwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirikala Nyumba la Taifa (NHC), Nahemia Mchechu, (kulia), akisimama kuashiria amepokea maagizo ya Rais, ambaye alikuwa anahutubia
1
Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Mzizima Auction Mart wakitoa vyombo vya Winfrida Nkungu Mpangaji wa shirika la nyumba NHC nyumba namba 838 Mtaa wa Senegal Upanga jijini Dar es salaam kutokana na kudaiwagharama ya Pango miezi tisa kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tatu 2,300,000. Shirika la Numba la Taifa NHC liko kwenye kampeni kubwa ya kukusanya madeni yake maeneo mbalimbali nchini.
2
Wafanyakazi wa kampuni ya Udalali ya Mzizima Auction Mart wakikusanya nguo na vitu mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwenye nyumba hiyo.
3 4
Wakiewndelea kutoa vyombo nje.
5
Vyombo vikiwa nje baada ya kampuni hiyo kukamilisha kazi ya kutoa vyombo hivyo nje.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na  Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhusu Programu ya  utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kipindi cha mwaka 2015-2020  katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo (wa pili kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na  Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhusu Programu ya  utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kipindi cha mwaka 2015-2020  katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo (wa pili kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee
Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee akifafanua jambo wakati wa  mkutano wa siku moja wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhusu Programu ya  utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kipindi cha mwaka 2015-2020 chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,uliofanyika leo katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja (kushoto) Wizara wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma
Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika mkutano wa siku moja wa Wizara hiyo   kuhusu Programu ya  utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kipindi cha mwaka 2015-2020 chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) uliofanyika leo katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na  Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhusu Programu ya  utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kipindi cha mwaka 2015-2020  katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo (wa pili kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika mkutano wa siku moja wa Wizara hiyo   kuhusu Programu ya  utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kipindi cha mwaka 2015-2020 chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,uliofanyika leo katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja

Mshauri wa Rais masuala ya Uchumi Bw,Abrahmani Mwinyi Mbegu (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Nd,Khamis Mussa Omar (katikati) na Kamishna wa ZRB Nd,Amour Hamil Bakari wakiwa katika mkutano wa siku moja wa Wizara ya Fedha na Mipango uliozungumzia kuhusu Programu ya  utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kipindi cha mwaka 2015-2020 chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,uliofanyika leo katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016. Mkutano wa 4 bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakao dumu kwa takriban wiki mbili, umeanza leo mjini Dodoma ambapo miswada mbalimbaliya sheria inatarajiwa kujadiliwana kupitishwa.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, (kulia),  akizungumza na wabunge kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni, Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Sumbawanga mjini, Aeshi Hilaly kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwenye jengo la Utawala  la Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2016

No comments :

Post a Comment