Monday, September 26, 2016

RAIS MAGUFULI "ATINGA" TENA BANDARINI DAR, AKUTA MASHINE MBILI ZA KUKAGULIA MIZIGO KATI YA NNE HAZIFANYI KAZI


Rais Dkt. John Magufuli akikagua eneo la Gati la Mafuta la Kurasini KOJ, wakati alipofanya ziara kwenye bandari ya Dar es Salaam, Septemba 26, 2016. (PICHA NA IKULU)


Rais Dkt. John Magufuli akikagua utendaji kazi na vitendea kazi vya bandari katika eneo la ofisi ya mtambo wa kuhakiki mizigo katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.


Rais Dkt. John Magufuli akikagua utendaji kazi na vitendea kazi vya bandari katika eneo la ofisi ya mtambo wa kuhakiki mizigo katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.


Rais Dkt. John Magufuli akitoa maelekezo kwa Mhandisi Marry Mhayaya katika eneo la Gati la Mafuta la Kurasini KOJ.


Rais Dkt. John Magufuli akisisitiza jambo wakati akielekea eneo la Gati la upakuaji wa mafuta la kurasini  KOJ katika Bandari ya Dar es Salaam.


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Alphayo Kidata akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa Taasisi yake inavyofanyakazi Bandarini huku Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza.


Rais akiongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Mhandisi Deusdedit Kakoko


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho wakitaza utendaji kazi wa mashine mbalimbali katika Bandari ya Dar es Salaam.


Rais Dkt. John Magufuli akisisitiza jambo mara baada ya kukagua eneo la upakuaji wa mizigo mbalimbali katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.


Rais Dkt. John Magufuli akisisitiza jambo mara baada ya kukagua eneo la upakuaji wa mizigo mbalimbali katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekeza jambo wakati akikagua mtambo wa kukagulia mizigo  ulioharibika kwa muda mrefu.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoka kuangalia sehemu ya kupakulia mafuta kutoka kwenye meli katika bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam leo Septemba 27, 2016

ZIARA YA MAJALIWA KIBITI NA KILWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiingia kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti wilayani Kilwa ambapo Waziri Mkuu alihutubia mkutano wa hadhara , Septemba 26, 2016. . Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea magodoro 10 kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Mendeleo ya Wananchi cha Kibiti, Bi. Cecilia Mfuko ukukiwa ni mchango uliotolewa na Chuo hicho kwa Hospitali ya Kibiti. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa michezo mjini Kibiti Septemba 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee Abadallah Ngwele baada ya kupokea madawati 10 yaliyotolewa na wazee wa Kibiti katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti, Septemba 26, 2016. Kushoto ni mkewe Mary na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MASAUNI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA MJINI GEITA LEO

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Makao Makuu, Koplo Faustina Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo jinsi magari mbalimbali yanavyovunja sheria za barabarani. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika Kitaifa mjini Geita, Mhandisi Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yanafanyika Kitaifa katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita, yalipokuwa yanaingia katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuadhimisha wiki hiyo. Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IRAN YAAHIDI KUENDELEA KUTOA FURSA ZAIDI YA MAFUNZO YA ELIMU YA JUU KWA WANAFUNZI WA ZANZIBAR

Mkurugenzi Mkuu kutoka Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Balozi Hussein Mollale Abdullahi akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Jengo la Baraza la Wawakilishi lilipo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu kutoka Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Balozi Hussein Mollale mara baada ya mazungumzo yao. Wa kwanza kutoka Kulia ni Katibu wa kwanza Msaidizi wa Ubalozi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Mjini Dar es salaam bwana Mohammad Dehghani.

Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran imeahidi kuendelea kutoa fursa zaidi ya Mafunzo ya Elimu ya juu kwa wanafunzi wa Zanzibar katika mpango wake wa kuimarisha uhusiano uliopo kati yake na Zanzibar uliodumu kwa muda mrefu sasa.

Fursa hizo zitazingatiwa zaidi katika fani ya Uhandisi kwa vile Visiwa vya Zanzibar tayari viko katika maandalizi ya utafiti wa mafuta na gesi ikijiandaa kuelekea katika uimarishaji wa Sekta ya nishati itakayosaidia kubadilisha uchumi wa Zanzibar katika miaka michache ijayo.

Mkurugenzi Mkuu kutoka Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Balozi Hussein Mollale Abdullahi alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Hussein alisema Iran kwa vile imebarikiwa kuwa na rasilmali nyingi zilizopelekea kuongoza nafasi ya Pili katika uzalishaji wa mafuta na Gesi Duniani imejitolea kuunga mkono Mataifa Rafiki katika azma ya Mataifa hayo kujenga uwezo zaidi wa kujitegemea.

Akizungumzia miradi ya kujitegemea Balozi Hussein alisema Taifa lake lilioko Mashariki ya Kati tarayi limeshatoa msaada mkubwa wa Vifaa na mashine kwa ajili ya chuo cha Amali kiliopo Mkokotoni ili kuwajengea uwezo vijana wanaopata mafunzo ya ujasiri amali kwenye chuo hicho.

MAFUNZO KUHUSU MWONGOZO WA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI WA MIRADI YA UMMA KANDA YA MOROGORO YAFUMGULIWA RASMI

Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma Kanda ya Morogoro kwa Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango. Waliokaa ni Bi. Anna Kimwela, Mchumi, Tume ya Mipango na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Washiriki wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Mkutano katika Chuo Kikuu cha Kilimo Morogroro (SUA).

WAZIRI MKUU AMPA OFISA ELIMU WIKI MOJA KUPELEKA WALIMU RUFIJI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Rufiji.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano na sita licha ya kuwa na shule.

"Hatuwezi kuwa na shule ambazo hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika Rufiji.",alisema Waziri Mkuu.

Akizungumzia suala la upungufu wa watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya kazi ya uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali itaangalia kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo kutangaza ajira.

"Hivi sasa serikali inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na kujua idadi ya watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena kuajiri, tulisitisha kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa.

Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji Waziri, Mkuu alisema watendaji wa halmashauri na vijiji wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa.

Alisema wenyeviti wa vijiji wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora ya ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia kijijini zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria.

"Hatuwezi kuendelea kuwa na watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia wafugaji ni marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima"alisema Waziri Mkuu.

WATANZANIA 10 KWENDA KUFANYA KAZI STARTIMES NCHINI CHINA

1
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (kushoto) akimkambidhi mmojawapo wa washindi wa mashindano ya sauti, Hilda Malecela mfano wa runinga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 40 kutoka kampuni hiyo. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmoja wapo wa washindi wa sindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela akikumbatiana na majaji baada ya shindano ilo kuisha, akishuhudia tukio hilo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao na kulia ni majaji na washindi wengine. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
 washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China. 

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

spi1
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwasili Mjini Zanzibar kwa kutumia Boti wakati alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Wawakilishi mapema leo Septemba 2016.
spi2
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) alipowasili katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kushoto ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
spi3
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia) akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) na Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma wakati alipowatembelea.
spi4
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu toka kulia) akifuatilia kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati alipowatembelea. Wapili kulia ni Spika wa Baraza hilo Mhe Zuberi Ali Maulid na wa kwanza kulia ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.

RAIS DK.SHEIN ATEMBELEA MRADI UJENZI WA NYUMBA ZA KISASA FUMBA

bak1
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(kulia ) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Nd,Ayoub Mohamed Mahmoud,[Picha na Ikulu.]26/09/2016.
bak2
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group,(wa tatu kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Nassor Khamis,akifuatiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohamed,[Picha Ikulu.]26/09/2016.
bak3
Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipanda ngazi ya moja ya nyumba zinazojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Azam Group akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw.Said Salim Bakhresa wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko Fumba wilaya ya Magharibi,Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara maalum kuangalia ujenzi wa nyumba hizo,[Picha Ikulu.]26/09/2016.

TIGO FIESTA YAITIKISA MKOA WA KILIMANJARO

barnaba-na-nandy1 
Wasanii Barnaba na Nandy wakitoa burudani pamoja kwenye tamasha la Tigo Fiesta kwenye uwanja wa Majengo,Moshi mkoani Kilimanjaro usiku wa kuamkia jana.  
                             Barnaba akiendeleza mtiriko wa burudani ya muziki mzuri  
                         Christian Bella naye akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta 
Wasanii Navy Kenzo wakitoa burudani kwenye tamasha la Tigo Fiesta kwenye uwanja wa Majengo,Moshi mkoani Kilimanjaro usiku wa kuamkia jana.

MAJALIWA AWASIMAMISHA MAOFISA MISITU WANNE, APIGA ‘STOP’ UVUNAJI MAGOGO RUFIJI

KILA KITU CHAKAMILIKA MDAHALO WA DONALD TRUMP NA HILLARY CLINTON LEO

CHINA DONATES US$200, 000 TO EAC FOR INTER-BURUNDI DIALOGUE

Mr. Gou Haodong, Minister-Counsellor at the Chinese Embassy in Dar es Salaam, with the Director of Infrastructure at the EAC Secretariat, Mr. Philip Wambugu. On the left is the Dr. James Njagu, the Chef de Cabinet to the EAC Secretary General.
Mr. Gou Haodong, Minister-Counsellor at the Chinese Embassy in Dar es Salaam, with the Director of Infrastructure at the EAC Secretariat, Mr. Philip Wambugu, sign an agreement under which China is to give the EAC $200,000 to support the Burundi peace process. Looking on (standing) is Mr. Xia Riu Jiu, First Counsellor at the Chinese Embassy, and Dr. James Njagu, the CdC to the EAC Secretary General (seated left). 

The People’s Republic of China has donated US$200,000 to the East African Community Secretariat as part of support to the ongoing Inter-Burundi Dialogue.

Making the announcement at the EAC Headquarters in Arusha, Mr. Gou Haodong, the Minister-Counsellor at the Chinese Embassy in Dar es Salaam, Tanzania General reaffirmed China’s commitment to the success of the Burundi peace process.

Mr. Haodong hailed the EAC for playing a leading role in facilitating the talks, adding that China would continue to support the talks until Burundi realized a genuine and lasting peace.

Mr. Philip Wambugu, the Director of Infrastructure at the Secretariat, who received the donation on behalf of the EAC Secretary General, thanked China for its generous contributions which he said have kept the talks going.

Mr. Wambugu said the Summit had at its 17th Extra-Ordinary Meeting held in State House Dar es Salaam on 8th September, 2016 directed the EAC Secretariat to continue mobilizing resources for the purpose of supporting the peace talks.

Also present at the talks were First Secretary at the Chinese Embassy, Mr. Xia Riu Jiu, and Dr. James Njagu, the Chef de Cabinet to the Secretary
 General.

PANYA ROAD' WAIBUKA UPYA NA KUTESA WANANCHI MOSHI BAA JIJINI DAR ES SALAAM


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar. Simon Sirro


Na Dotto Mwaibale

KUNDI la uhalifu la watoto wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama panya road linatishia usalama wa wananchi na mali zao maeneo ya Moshi Baa na vitongoji vingine katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo katika kipindi kisichopungua wiki mbili tayari watoto watatu walikuwa wakidaiwa kuhusika na kundi hilo wameuawa na wananchi wenye hasira kali.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaa leo hii mkazi wa eneo la Moshi Baa Relini aliyejitambulisha kwa jina  la Mwarami Abubakar alisema hali sio shwari katika eneo kufuatia matukio ya kila siku ya kuvamiwa wananchi kujeruhiwa na kuporwa mali zao na kundi hilo.

"Tayari vijana wawili wiki iliyopita wamechomwa moto na wananchi wenye hasira  huku mwingine akipigwa juzi hadi kutolewa utumbo na kufariki papo hapo" alisema Abubakar.

Mkazi mwingine wa eneo la Kwa Mkolemba Khamisi Fadhil alisema kundi hilo limekuwa likifanya vitendo hivyo mchana kweupe na wanatembea kuanzia vijana nane hadi 10 wakiwa na silaha za jadi kama nondo, visu na mapanga na mtu yeyote wanayekutana naye ni  lazima wampige na kumpora.

"Wenye maduka wanalazimika kufunga kuanzia saa moja jioni kuhofia kundi hilo ambalo huvunja milango ya nyumba na kufanya uporaji" alisema Fadhil.

Fadhil alisema maeneo ambayo vijana hao wameshamiri ni Moshi Baa Relini, Kwa Mkolemba, Diwani na Bomba mbili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi (ACP), Salum Hamdan alisema polisi imejipanga vilivyokukabiliana na vitendo hivyo katika mkoa wake.

"Kwanza napenda kukuambia kwamba hakuna kundi linalojiita panya road wote tuna wahesabu ni wahalifu kama walivyo wahalifu wengine na hivi ninavyongea na wewe tupo katika siku ya sita ya operesheni ya kukakamta watu wanaojihusisha na uhalifu wa ujambazi wakiwemo wanaouza pombe haramu ya gongo " alisema Kamanda Hamdan.

Aliongeza kuwa katika mkoa wake hivi karibuni utakuwa shwari baada ya askari wake kusambaratisha watu hao wanaofanya vitendo hivyo.


 Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam jana.
 Wananchi wakivusha relini pikipiki yao.
 Pikipiki ikivushwa.
 Waendesha bodaboda wakivusha pikipiki zao kwenye reli baada ya kufungwa kwa muda barabara katika makutano ya Reli ya Tazara na Barabara ya Mombasa Moshi Baa Dar es Salaam jana wakati mafundi wa  Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara), wakifanya ukarabati katika eneo hilo.
Mafundi wa Shirika la Mamlaka ya Reli  Tanzania na Zambia (Tazara), wakikarabati Reli katika makutano ya Reli na Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale


MAMLAKA ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) imelalamikiwa na wananchi kwa kutozingatia muda muafaka wa kufanyia ukarabati wa reli zake jambo linalowaletea usumbufu.

Malalamiko hayo waliyatoa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi  kuhusu kadhia waliopata baada ya kufungwa kwa muda Barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa kupisha ukarabati eneo la reli inayokutana na barabara hiyo.

"Kazi ya ukarabati wanayoifanya ni nzuri lakini wangekuwa wakiifanya nyakati za usiku ili kuepusha usumbufu huu tunao upata wa kuvusha pikipiki zetu relini" alisema Gedion Robert.

Robert  alisema katika nchi za wenzetu kazi za kusafisha miji na ukarabati wa namna hii hufanyika usiku ili kuondoa adha kwa wananchi wanaotumia barabara kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.

Mkazi mwingine kwa Diwani Stellah Urio alisema amelazimika kulipa sh. 400 kutoka kwa Diwani hadi Relini ambapo pia alilipa sh. 400 baada ya kubadilisha gari ili kufika Ukonga Mombasa na kujikuta akitumia sh.800 badala ya 400.

Jitihada za kumpata msemaji wa Tazara , Conrad Simuchile, ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baada ya kufika ofisini kwake na kuambiwa mwandishi arudi baadae alikuwa nje ya ofisi kikazi.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (kushoto) akimkambidhi mmojawapo wa washindi wa mashindano ya sauti, Hilda Malecela mfano wa runinga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 40 kutoka kampuni hiyo. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
 Mmojawapo wa washindi wa sindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela akikumbatiana na majaji baada ya shindano ilo kuisha, akishuhudia tukio hilo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao na kulia ni majaji na washindi wengine. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
 washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
 Washindi 10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
  Mmoja wa washiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela akionyesha uwezo wake wa kuigiza sauti mbele ya majaji jukwaani. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
 Mmoja wa washiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Rukia Hamdani akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya kuonyesha uwezo wake wa kuigiza. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mshiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Coletha Raymond akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya kuonyesha uwezo wake wa kuigiza. Washindi 10 walipatikana katika shindano.


Na Dotto Mwaibale

Hatimaye shindano la kusaka vipaji vya sauti lililoandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania limemalizika mwishoni mwa wiki hii kwa watanzania 10 kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu yake yaliyopo jijini Beijing.
Akizungumza baada ya shindano hilo Dar es Salaam juzi , Hilda Malecela kutoka Dar es Salaam ambaye ndiye aliyeongoza kwa kupata alama nyingi kutoka kwa majaji alisema kuwa anashukuru sana kupata fursa hiyo ya kuonyesha kila kipaji alichonacho kwani haikuwa kazi rahisi.
‘’Kwanza kabisa nashukuru kwa ushindi huu, haikuwa kazi rahisi kwani ushindani ulikuwa ni mkubwa ukizingatia washiriki walioingia hatua ya fainali wote walikuwa wana uwezo mkubwa sana. Nawashukuru majaji kwa kunipa moyo tangu awali na hatimaye kuniamini kwamba nina kitu ambacho ninaweza kukitoa kwa watanzania kupitia kipaji change cha sauti. Fursa niliyoipata mimi pamoja na washindi wenzangu tisa ni jambo la kujivunia na kuitumia ipasavyo.’’ alisema . Malecela
‘’Napenda kuwaahidi watanzania kuwa nitaitumia nafasi hii vema kuhakikisha nafanya kazi nzuri ili wao waendelea kuburudika na kujifunza zaidi kupitia filamu na tamthiliya. Nawapongeza pia StarTimes kwa kutambua umuhimu wa Kiswahili na kuja ubunifu huu ambao haujawahi kutokea nchini. Mara nyingi tumekuwa tukiona mashindano ya kuimba, kuigiza na kucheza lakini si kwa upande wa sauti. Wamepiga hatua kubwa sana kwa kweli ambayo inastahili kuigwa na makampuni mengine.’’ alimalizia mshindi huyo aliyeongoza kwa kuwa na alama nyingi zaidi kutoka kwa majaji
Naye kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania,  Lanfang Liao amebainisha kuwa amefurahi kuona shindano la kusaka vipaji vya sauti limepokewa kwa muitikio mkubwa na watanzania sehemu mbalimbali za nchi.
‘’Hatukutegemea kama watanzania wengi wangevutiwa na shindano hili lakini imekuwa ni kinyume chake kwani imedhihirika kuwa wapo wasanii wengi sana wenye vipaji vya sauti. Sanaa ina uwanja mpana sana ni namna tu msanii mwenyewe anavyoamua anakitumia vipi kipaji alichonacho. StarTimes tumebaini kutoka kwa wateja wetu kuwa filamu na tamthiliya zilizotafsiriwa na kuingiziwa sauti kwa lugha ya Kiswahili zinapendwa sana. Hivyo tukaona ni vema kuviibua vipaji ili tufanye nao kazi hiyo kwa manufaa ya watanzania.’’ alisema  Liao
‘’Tunaamini kupitia shindano hili tumeweza kutoa ajira kwa watanzania 10 watakaokwenda kujumuika na wenzetu waliopo makao makuu jijini Beijing, China katika kuzalisha kazi zilizo bora kabisa. Nawasihi washindi waliopata fursa hii kuitumia vema kwa kufanya kazi kwa bidii kwani ninaamini wanastahili mpaka kuchaguliwa na majaji kuwa vinara dhidi ya wenzao 18 waliofikia hatua ya fainali. StarTimes tunaahidi kuendelea na zoezi hili wakati ujao kwani bado uhitaji ni mkubwa na sisi siku zote tupo kwa ajili ya kuwapatia kile wateja wetu wanachokitaka.’’ alihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTime nchini
Katika fainali hizo washindi wa kwanza, pili na watatu; Hilda Malecela - kutoka DSM,  Safiya Ahmed kutoka Zanzibar na Sadiq Kututwa - kutoka Zanzibar) walizadiwa runinga za kisasa zenye ukubwa wa inchi 40, 32 na 24 kila mmoja na StarTimes kutokana na kuongoza kwa alama nyingi katika fainali hizo huku washindi saba wakipatiwa simu za mkononi za kisasa kutoka StarTimes.
Kwa ujumla washindi kumi waliopatikana ni;  Hilda Malecela(DSM),  Safiya Ahmed(ZNZ),  Sadiq Kututwa(ZNZ), Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ), Richard Rusasa(DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao(DSM), Jamila Hassan(DSM) na Abraham Richard(DSM). Na wote watapata fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China kwa mkataba wa muda wa mwaka mmoja. 
Katika mashindano hayo takribani washiriki zaidi ya 547 walijitokeza katika usaili uliofanyika katika mikoa ya Arusha (Agosti 27), Zanzibar (Septemba 3) na Dar es Salaam (Septemba 10) na hatimaye washiriki 18 tu wakabakia na kutinga hatua ya fainali.
Washiriki 18 waliotinga hatua ya fainali ni kama ifuatavyo: kwa mkoa wa Arusha ni Mathew Philip Mgeni, Dorcas Francis, Halima Hussein, Janeth N Molely na Hilda Kinabo; Zanzibar ni Safiya Ahmed Said, Sadiq Kututwa Abdalahh, Rukia Hamdan, Imatu Obeid Fabian na Mohamed Said Mohamed; na Dar es Salaam ni Hilda Malecela, Abraham Richard, Happiness Stanslaus ‘Nyamayao’, Richard Rusasa, Emanuel Landey, Coletha Raymond, Jamila Hassan na Maisala Abdul.

No comments :

Post a Comment