Friday, September 2, 2016

MAJALIWA ATEMBELEA MUHANS - MLOGANZILA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watalaam na wajenzi wa Chuo wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza taarifa kuhusu ujenzi wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Ephata Kaaya wakati alipokagua ujenzi huo eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi na wananchi baada ya kukagua ujenzi wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua jiko wakati alipolea eneo ilipojengwa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016. Watatu kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Ephata Kaaya. . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitaza mashine ya CT Scanner wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa Kampasi Mpya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) eneo la Mloganzila jijini Dar es salaam Septemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KIWANDA CHA SARUJI CHAIPIGA TAFU SHULE YA SEKONDARI YA ILBORU YA ARUSHA

Tanga, KIWANDA Cha Saruji Cha Simba (Simba Cement) cha Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa ujenzi wa vymba vya madarasa.
Akizungumza wakati wa halfa fupi ya makabidhiano leo, Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.

Alisema msaada huo utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika ipasavyo.‘Mifuko hii ya saruji itapunguza changamoto inayoikabili shule yako ikiwemo vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii ya elimu” alisema Malambugi

Alimtaka mwalimu huyo na kamati yake ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu zikiwemo kuondosha changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Ilboru sekondari school , Julias Shulla, alikishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyoombwa.

Alisema shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia. ‘Tunakishukuru kiwanda cha saruji cha simba kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa tutaitumia saruji kama tulivyoiomba” alisema Shulla

Alisema mifuko hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ambazo shule yake inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa shule yake.

Mkuu wa Idara ya Rasilimawatu kiwanda cha Sauji cha Simba Cement cha Tanga, Diana Malambugi, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu shule ya Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa.nyuma kulia ni Mkuu wa fedha Pieter Jaggar na kushoto ni Emmanuel Jonas mhasibu.

MAJALIWA KATIKA SALA YA IJUMAA MKITI WA ANWAR- MSASANI

LIGI KUU YA VODACOM, MECHI NNE KESHO



Raundi ya tatu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 3, 2016 kwa michezo minne wakati kwa Jumapili Septemba 4, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyotolewa na Bodi ya Ligi (TBLB).

Michezo ya kesho ni kati ya Mbao FC na Mbeya City utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Kagera Sugar itazindua uwanja wa nyumbani kwa kucheza na Mwadui ya Shinyanga.

Majimaji itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Majimaji huko Songea na African Lyon itakuwa mgeni wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.

Mchezo wa Jumapili utakuwa ni kati ya Stand United na Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Ligi hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Azam FC itaendelea Jumatano kwa michezo mitatu ambako mabingwa watetezi Young Africans watakaribishwa na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Azam ambayo kwa sasa inangoza ligi hiyo itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine ilihali Simba itakipiga na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

TAIFA STARS KAZINI KESHO

Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kesho Septemba 3, 2016 inatarajiwa kuingia kibaruani kwa kucheza na Super Eagles ya Nigeria katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).

Mchezo huo utafanyika kuanzia saa 11.00 (17h00) jioni kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabo, mjini Uyo katika Jimbo la Akwa Ibom. Muda huo uko mbele kwa saa mbili kamili kwa maana hiyo Taifa Stars itacheza dhidi ya Nigeria saa 9.00 alasiri (15h00).

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

ANDAENI WATAALAMU WA KUTOSHA-MAJALIWA

KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI, UTPC YALILIA MAZINGIRA HURU KWA WANAHABARI KUFANYA KAZI.

Septemba 2,2012 Mwandishi wa Habari, Marehemu Daudi Mwangosi (hayuko pichani), aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Iringa, aliuawa na polisi akiwa kazini katika Kijiji cha Nyololo mkoani Iringa ambapo aliyemuua alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani julai mwaka huu. Na BMG

Kufuatia mauaji hayo, Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini, UTPC ulitenga tarehe hiyo kuwa kumbukumbu ya Kifo cha Daudi Mwangosi ikiambatana pia na tuzo inayotolewa kwa mwanahabari aliyefanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo kupigwa ama kuuawa kutokana na kazi yake.

Leo UTPC imekutana na wanahabari Jijini Mwanza imekutana na wanahabari ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Mwangosi ambapo imelaani mazingira magumu ambayo wakati mwingine wanahabari na vyombo vya habari wanayapitia katika utendaji wao wa kazi ikiwemo vyombo vya habari kufungiwa.

Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji (kushoto) amesema wanahabari wanataka mazingira huru ya kufanya kazi huku akilaani serikali kuvifungia baadhi ya vyombo vya bila kusikilizwa juu ya yale yanayodhaniwa kufanywa na vyombo hivyo kinyume cha sheria.

Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, amebainisha kwamba tunzo ya Daudi Mwangosi mwaka huu pia haikupata mshindi kwa namna ambavyo jopo la tuzo hiyo lilivyoweka vigezo vyake ikiwemo Mwandishi anayepaswa kuichukua awe amepigwa, kuumizwa ama kuuawa akiwa kazini. Mwaka 2013 tuzo hiyo ilichukuliwa na Mwanahabari Absolum Kibanda.
                                                                    Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, amebainisha kwamba tunzo ya Daudi Mwangosi mwaka huu pia haikupata mshindi kwa namna ambavyo jopo la tuzo hiyo lilivyoweka vigezo vyake ikiwemo Mwandishi anayepaswa kuichukua awe amepigwa, kuumizwa ama kuuawa akiwa kazini. Mwaka 2013 tuzo hiyo ilichukuliwa na Mwanahabari Absolum Kibanda.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE JANETH WAZURU KABURI LA DKT. OMAR ALI JUMA

GABRIEL JESUS ATUPIA MBILI WAKATI BRAZIL IKIIFUGA ECUADOR

Mchezaji mpya wa Manchester City, Gabriel Jesus, amechochea ushindi wa Brazil kwa kufunga magoli mawili na kumpatia kocha mpya wa Brazil Tite ushindi wake wa kwanza katika mchezo dhidi ya Ecuador.

Katika mchezo huo uliochezwa eneo lililo juu kwa futi 10,000 kutoka usawa wa bahari, Brazil iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 huku mchezaji nyota wa Brazil Neymar akifunga goli kwa mkwaju wa penati.
Gabriel Jesus licha ya kufunga magoli mawili pia alisaidia kupatikana penati iliyofungwa na Neymar
                               Neymar akishangilia baada ya kufunga goli la mkwaju wa penati

LUIS NANI AIONGOZA URENO KUICHAKAZA GIBRALTAR

Luis Nani ameng'ara wakati Cristiano Ronaldo akikosekana kwa kuifungia Ureno magoli mawili katika ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya taifa changa kisoka la Gibraltar, ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa mabingwa hao wa Ulaya.

Mchezo huo wa kirafiki uliofanyika Porto, ulikuwa pia ni wa kwanza kwa Gibraltar tangu kupata uanachama kutoka kwa shirikisho la soka duniani FIFA Mei mwaka huu, kuelekea kufuzu michuano ya kombe la dunia 2018.
                                                Luis Nani akiruka sarakasi baada ya kufunga goli 
                                    Kipa wa Gibraltar akiwa amekaa chini akimuangalia Nani

MAMIA KWA MAELFU WAANDAMANA KATIKA JIJI LA CARACAS NCHINI VENEZUELA

Mamia kwa maelfu ya watu wameandamana katika Jiji la Caracas nchini Venezuela katika maandamano ambayo yanayohusisha pande mbili hasimu.

Wafuasi wa upinzani wamefanya maandamano makubwa kwa miaka miwili, ya kushinikiza rais
Nicolas Maduro aondoke madarakani kutokana na mgogoro wa uchumi.

Wanaomuunga mkono rais Maduro, nao wamefanya maandamano makubwa wakiwatuhumu wapinzania kwa kutaka kufanya mapinduzi.
               Waandamanaji wakikimbia mabomu ya machozi yaliyorushwa na polisi
          Baadhi ya waandamanaji walikamatwa na polisi kama inavyoonekana hapa

No comments :

Post a Comment