Tuesday, September 13, 2016

KUINGIA UWANJA WA TAIFA SASA NI "KUCHANJA" TU, WAZIRI NAPE AKABIDHIWA RASMI MAGETI YA KIELEKTRONIKI


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiweka kadi  katika moja ya geti linalotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki tayari kuingia katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipita katika moja ya geti linalotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

 Waziri Nape, akionyesha kadi ya "kuchanjia" ili kuvuka geti la kielektroniki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai wakitia saini hati za makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika hafla iliyofanyika Septemba 11, 2016 katika Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai wakionesha  hati za makabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika hafla iliyofanyika Septemba 11, 2016 katika Uwanja wa Taifa  Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na watendaji wa  Wizara yake, wadau wa michezo, wanamichezo na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa na kuzindua rasmi mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja huo Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.



Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumzia mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Jamali Malinzi akitoa salamu za wadau wa mchezo wa mpira wa miguu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki kwa Serikali katika Uwanja huo Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.


Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai akizungumzia utekelezaji wa mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki uliotekelezwa na kampuni yake kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.



Mhandisi Mshauri wa mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki Mhandisi Aloyce Mushi akieleza changamoto mbalilmbali kuhusu mradi huo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Senpai Esther Thomas (kushoto) akipangua chudan tzuki (ngumi ya kifua) wakati semina hiyo ikiendelea.
Anafundisha kwa mifano! Shihan Okuma akishambuliwa na Jerome Sensei kama sehemu ya maelekezo katika semina hiyo
Na Daniel Mbega
SEMINA kubwa ya Shotokan Karate kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, imeanza leo hii jijini Dar es Salaam ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo nchini Tanzania, inaongozwa na mkufunzi mkuu, Shihan Koichiro Okuma (6th Dan), kutoka makao makuu ya chama cha karate cha Japan Karate Association/World Federation (JKA/WF), Tokyo, Japan.
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimwombea Hudson Kamoga akiwa amepiga magoti
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, ambaye ameteuliwa mwishoni mwa wiki jana amesema anaamini ni Mungu aliyemuweka kwenye nafasi hiyo ili  awatumikie wananchi wa Mbulu kwa wakati huu. 

Akiongea kwenye ibada ya Jumapili hii  ndani ya  Kanisa la Living Water Center Kawe, wakati alipopewa nafasi na mtumishi wa  Mungu  Apostle Onesmo Ndegi  ili asalimia Kanisa Mheshimiwa Kamonga  alisema, anakwenda kwenye wilaya yenye changamoto nyingi za kimaendeleo ila anaamini Mungu atamwezesha kuzitatua kwa nafasi yake akishirikina na wananchi pamoja na  viongozi wengine kati halimashauri ya Mbulu.

Kamonga alisisitiza kuwa kwa kupata  nafasi hii ya  Ukurugenzi bado  ataendelea na utumishi wake kwa Mungu maana anaamini huo ndio uliomfanya kufikia hatua hiyo,hivyo kuamua kuwa anamtanguliza Mungu kaika kila atakachokuwa anafanya,alisema Kamoga

Pia alitoa shukurani za dhati kwa Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi pamoja na  watumishi wengine kanisani hapo na kusema kuwa kati ya vitu ambavyo hawezi kuvisahau na malezi mazuri ya kiroho pamoja na mafindisho ambayo amekuwa akiyapata kutoka  kwa Apostle Ndegi na watumishi wengine kanisani hapo, akisema mafundisho hayo yamesababisha kuwa vile alivyo sasa! Mwisho Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi  na waumini walifanya maombi kwa ajili yake ili Mungu aambatane naye katika utumishi wake kwenye nafasi hiyo ya Ukurugenzi!.
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake.

Waumini wa Kanisani Living Water Center Kawe wakiwa wamenyoosha mikono kwa Hudson Kamoga kuomba kwa ajili yake

E
 Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA), aliyemaliza muda wake, Hassan Ngubege akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa chama hicho Jesse John katiba ya chama hicho baada ya kufanyika uchaguzi wilayani humo jana.
Mwenyekiti mpya Jesse John, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa chama hicho na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake.

Na Dotto Mwaibale, Kisarawe

MTANGAZAJI nguli wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jesse John amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA) katika uchaguzi uliofanyika jana.

Jesse ambaye aliupata uongozi huo katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa aliibuka kidedea baada ya kupata kura 32 na kumshinda mpinzani wake Karim Wenge aliyepata kura 21.

Katika uchaguzi huo Mohamed Lubondo alichaguliwa kuwa Katibu baada ya kupata kura 30 na kumshinda Francis Mkamba aliyepata kura 27.Katibu Msaidizi alichaguliwa kuwa Amosi Kisebengo, Makamu Mwenyekiti alichaguliwa kuwa Abdul Mogella.

Wasimamizi wa uchaguzi huo kutoka Chama Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), Mweka Hazina wa KIDIFA alichaguliwa Iddo Mtangaze na Mweka Hazina Msaidizi alichaguliwa kuwa Sadiki Nasoro.

Mwakilishi wa klabu kutoka Tarafa ya Mzenga alichaguliwa kuwa Suleiman Mahenge, kutoka Tarafa ya Sungwi alichaguliwa Abdallah Kuga na Mwakilishi wa klabu alichaguliwa kuwa Ally Madega na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa mkoa alichaguliwa kuwa Mohamed Masenga.

Mwenyekiti wa KIDIFA aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege akimkarisha Jesse kushukuru wajumbe aliwataka viongozi wapya kufufua matumaini ya vipaji vya vijana katika soka wilaya ya Kisarawe kwa kuanzisha mashindano mbalimbali yenye lengo la kutafuta vipaji.

Jesse akiwashukuru wajumbe hao aliahidi kushirikiana na wadau wa soka ndani na nje ya wilaya hiyo kupata timu ya wilaya itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kama timu nyingine zinashiriki mashindano hayo.

Mwenyekiti Jesse alisema wilaya ya Kisarawe ambako yeye ni mzaliwa wa asili alisema anaamini vijana wengi hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hivyo atatumia miaka minne ya uongozi kuzalisha vijana wazuri katika soka.


 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Msuguri wakati alipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary (kulia)  wakiwajulia hali wagonjwa  wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary (kulia)  wakimjulia hali  Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Msuguri wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary (kulia)  wakimjulia hali  Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Msuguri wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary (kulia)  wakiwajulia hali wagonjwa  wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary (kulia)  wakiwajulia hali wagonjwa  wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary (kulia)  wakiwajulia hali wagonjwa  wakati walipokwenda kwenye hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam kuona wagonjwa baada ya kushiriki sala ya Iddi El Haji kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es salaam Septemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka mchana tayari kumwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Sita wa Zambia Mhe Lungu uwanja wa Mashujaa kesho Septemba 14, 2016(Picha na IKULU).




Afisa Uhusiano wa Benki ya Posta, Chichi Banda akiwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya madawati, kushoto kwake ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki ya Posta Timotheo Mwakifulefule na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mbande, Mashaka Mwakyambiki (kulia)
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mbande, Mashaka Mwakyambiki akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada huo wa madawati kwa TPB

 Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mbande, Mashaka Mwakyambikiwakati akitoa neno la shukrani

Wanafunzi wakifurahia msaada uliotolewa na TPB shuleni hapo


Afisa Uhusiano wa Benki ya Posta, Chichi Banda akikata utepe kwenye moja ya madawati hayo.



Afisa Uhusiano wa Benki ya Posta, Chichi Banda akiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbande, Mashaka Mwakyambiki na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo George Anania (kushoto), pamoja na baadhi ya walimu wa shule hiyo na wanafunzi


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (wa pili kushoto) wakati akiwasili katika Uwanja wa Karume kuhitimisha mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star Septemba 11, 2016 kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi wakati wa hitimisho la mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star  Septemba 11, 2016.



 Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bw. Sunil Colaso akizungumza kuhusu maendeleo ya mashindano ya Airtel Rising Star wakati wa hitimisho la mashindano hayo ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.


 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi akitoa salamu kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17  Airtel Rising Star katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wanamichezo, wadau wa michezo na wanahabari kabla ya kushuhudia fainali ya mashindano hayo yiliyohitimisha mashindano hayo kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17  Airtel Rising Star katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wanamichezo, wadau wa michezo na wanahabari kabla ya kushuhudia fainali ya mashindano hayo yiliyohitimisha mashindano hayo kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17  Airtel Rising Star katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua wachezaji wa timu ya Morogoro Boys kabla ya kuanza kwa fainali kati yao na timu ya Ilala iliyofanyika katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikabidhi kikombe kwa nahodha wa Timu ya wasichana ya Temeke walioibuka washindi wa mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star kwa upande wa wasichana katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikabidhi kikombe kwa nahodha wa Timu ya wavulana  ya Morogoro walioibuka washindi wa mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star kwa upande wa wavulana katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.


Timu ya wasichana ya Temeke wakishangilia ushindi wao wakishangilia ushindi wao walioupata katika mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star kwa upande wa wasichana kwa kuwafunga Timu ya temeke kwa mikwaju ya penati katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

kwa kuwafunga Timu ya Ilala kwa goli moja kwa bila  katik
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya wavulana  ya Morogoro mara baada ya kumalizika kwa mshindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star yaliyofanyika  katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2016.

 Wachuuzi wa Samaki wakisubiri kununua kitoweo hicho katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Bei ya samaki katika soko hilo imepungua kutokana kwa kupatikana kwa wingi kwa kitoweo hicho.
Mnada wa samaki ukiendelea

Na Dotto Mwaibalae

HALI ya bei ya samaki katika Soko la Kimataifa la Feri jijini Dar es alaam imeshuka kutokana na samaki kupatikana kwa wingi katika kipindi cha mwezi wa Septemba.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com jijini Dar es Salaam leo asubuhi mchuuzi wa samaki katika soko hilo Mohamed Hassan alisema katika kipindi cha wiki mbili bei ya samaki imeshuka ukilinganisha ni mwezi uliopita.

"Sasa hivi samaki aina ya King Fish, Changua wanauzwa kati ya sh.30,000 lakini kipindi ambacho wakiadimika ufikia hadi sh.35,000" alisema Hassan.

Mchuuzi mwingine wa samaki katika soko hilo Shabani Shamte alisema samaki aina ya kibua, ngisi wakati huu uuzwa kati ya sh. 23,000 hadi 25,000 ambapo wakiadimika ufikia hadi sh. 30,000.

Grace Tesha ambaye uuza samaki hao maeneo ya Mabibo Loyola alisema hata wao kipindi hiki biashara yao inakwenda vizuri kutokana na kuwepo kwa samaki wengi.

"Samaki wakiadimika huwa inatuwia vigumu mno kibiashara kwani wateja wetu wamekuwa wakilalamia kuwauzia kwa bei kubwa" alisema Tesha

Wafanyakazi wa Benki ya Azania tawi la Moshi ,wakishusha Mbuzi kwa ajili ya kutoa zawadi ya siku kuu ya Idd kwa baadhi ya wateja wake pamoja na makundi yenye mahitaji maalumu.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akimkabidhi zawadi ya Mbuzi mwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael , Bw ,Bashir Seleman wa kampuni ya Zuhad kwa ajili ya siku kuu ya Idd.
Meneja wa Azania Bank  tawi la Moshi,Hajira Mmambe akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa msimamizi wa kituo cha kulea watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Qadria kilichopo kata ya mji Mpya,Alhaji Taqdir Haji Amir kama sadaka ya siku kuu ya Idd.
Baadhi ya watoto wa kituo cha  kulelea watoto cha Qadria kilichopo kata ya Mji Mpya.
Meneja wa Azania Bank akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa mteja wa Benki hiyo Aman Idd Mushi kwa ajili ya siku kuu ya Idd.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa mwakilishi wa kampuni ya Ibra line ,Bi Mosi Shayo kwa ajili ya siku kuu ya Idd.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza mara baada ya kukabidhi zaadi ya Mbuzi kwa ajili ya siku kuu ya Idd kwa wateja wake pamoja na makundi yenye mahitaji maalumu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (kushoto), na Sheikh Ponda Issa Ponda, wakiomba dua wakati wa swala ya Idd El Haji kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam leo Septemba 12, 2016. (PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID)

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa, amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuitumia sikukuu hii ya Idd el Haji kutenda mema na kuungana na waumini wengine katika kudumisha amani ya nchi yetu.
Waziri Mkuu akiyasema hayo leo Septemba 12, 2016, kwenye ibada ya sala ya Idd el Haji iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam ambapo miongoni mw masheikh maarufu walihudhuria ibada hiyo ni pamoja na Sheikh Shariff, Sheikh Nurdin Kishki,(mwenyeji wa hadhara), Sheikh Ponda Issa Ponda na Sheikh Rajab Katimba.
“Kwa niaba ya serikali yenu, nawatakia sikukuu njema, na ninaomba kuwasilisha salamu za upendo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, pamona na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, na niwaombe ndugu zangu muitumie sikukuu hii kudumisha amani na upendo.” Alisema Waziri Mkuu.
Waziri M,uu pia alitumia fusa hiyo kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kote nchini, kuwaombea wananchi wa mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililosababisha vifo.
Waziri Mkuu ambaye alihudhuria ibada ya kuaga miili ya watu 16 kwenye uwanja wa michezo wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera Jumapili Septemba 11, 2016, alisema kwa sasa kuna majeruhi zaidi ya 100 ambao bado wanapatiwa matibabu. Tetemeko hilo lilillopelekea uharibifu mkubwa wa nyumba lilitokea Jumamosi alasiri Septemba 10, 2016.
Naye mwenyeji wa Ibada hiyo Sheikh Nurdin Kishki, alimshukuru Waziri Mkuu kwa kuungana na waumini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Temeke, katika swala hiyo ya Idd. “Nduhgu zangu napenda nimshukuru Waziri wetu Mkuu kwa kutoka Oysterbay hadi kufika huku Temeke kuungana nasi katika kutekeleza swala hii ya Idd El Haji, mwenyezimungu amjalie heri na busara katika uongozi wake,” Alsiema Sheikh Kishki.

 Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam
 Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam
 Muumini wa Kiislamu akiomba dua
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mikono na Sheikh Ponda Issa Ponda, mara baada ya swala hiyo
 Waziri Mkuu, akiteta jambo na sheikh Ponda
 Waziri Mku, akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Shariff, (kushoto), na Sheikh Nurdin Kishki
 Waumini wa Kiislamu wakiwa kwenye swala
 Waumini wa Kiislamu, wakiomba dua


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Masheikh na viongozi wa serikali mara baada ya swala hiyo
 Sheikh Nurdin Kishki, akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam
 Sheikh Nurdin Kishki, kiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, wakati wa swala hiyo
 Watoto hawa wa Kiislamu, wakionyesha furaha baada ya kushiriki swala ya Idd El Haji, (Mlulu Khalfan (kushoto) na mdogo wake Kuugara.


Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Kisiwa cha Uzi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia hiyo lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico katika viwanja vya Skuli ya Uzi.  
Mc wa Mkutano huo wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi akisoma ratiba ya Uzinduzi huo katika viwanja vya Skuli ya Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Mwanachama wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi Unguja Khadija Said akisoma Quran Tukufu kabla ya Uzinduzi wa Baraza lao la Vijana la Shehia ya Uzi lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe, Moldiline Castico.
Vijana wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakicheza maigizo ya kuhamasisha Vijana kujiunga na Mabaraza ya Vijana kwa Maendeleo yao katika kujikwamua Kiuchumi.  
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu akiwa na Viongozi wa meza kuu wakifuatilia mchezo wa maigizo unaohamasisha Vijana kujiunga na Mabaraza la Vijana katika Shehia zao.,
Mwanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha  Uzi Salma Tunda akisoma risala yao mbele ya Mgeni rasmin wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya skuli ya uzi. 
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Farashuu Mussa akitowa salamu za Baraza lake kwa mgeni rasmin wakati wa uzinduzi huo.
Sheha wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi Hamad Ramadhani akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa Baraza la Vijana wa Kisiwa cha Uzi
Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Mhe Mashavu Sukwa akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Unguja na kuwataka Vijana kutumia Mabaraza la Vijana kwa maendeleo yao katika kujitafutia Ajira. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya yac Kati Unguja Mhe Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi na kuichangia shilingi laki mbili kwa kukuza mtaji wa Baraza hilo katika miradi yao endelevu.  
Waziri Moldiline Castico na viongozi wa meza kuu wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu akitowa salamu za Mbunge wa wake kwa Vijana wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Uzi.
Waziri Moldiline Castico akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Farashuu Mussa fedha zilizotolewa mchango na Mwakilishi wa Jimbo la hilo Mhe Simai Mohammed Said ikiwa ni mchango wake kwa Baraza hilo la Vijana wa Shehia ya Uzi.
Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico akiwahutubia Vijana wa Baraza la Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakati wa kulizindua Baraza hilo na kuwaasa Vijana kubuni miradi ya Maendeleo yatakayowaletea Tija katika kukuza Uchumi wao kupitia Mabaraza hayo. uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Skuli ya Uzi.Wilaya ya Kati Unguja Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Vijana wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakimsikiliza Mgeni rasmin wakati wa uzinduzi wa baraza lao lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico.

Sheha wa Shehia ya Uzi Ngambwa Amour Ali akisoma dua baada ya hafla ya uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi, uliofanyika katika viwanja vya skuli ya Uzi Wilaya ya Kati Unguja Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com.  

 

WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Karim Mattaka wakati alipofanya ziara ya kuzindua gati mpya wilaya ya Pangani Mkoani Tanga katikati ni Meneja wa Tanroad Mkoani Tanga,Mhandisi Alfred Ndumbaro
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa akizundua gati jipya la Bandari ya Pangani ambalo liligharimu zaidi ya bilioni 3 kulia ni Katibu  Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano wa mwisho kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA)Karim Mattaka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
 Kulia ni Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)Karim Mattaka wapili kutoka kulia wakati wa uzinduzi wa gati jipya wilayani Pangani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika akifuatilia mazungumzo hayo

Viongozi waliokaa meza mkuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Gati Jipya wilayani Pangani

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM),Jumaa Aweso wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Gati jipya wilayani Pangani
 Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani na mkoaani Tanga wakifuatilia uzinduzi wa Gati jipya

Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga wakifuatiliaa uzinduzi huo kutoka kulia ni PRO wa Mamlaka hiyo,Moni Jarufu kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Daudi Mayeji
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakifuatilia uzinduzi wa Gati hiyo


Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akisalimiana na wananchi wilayani Pangani mara baada ya kuzindua

No comments :

Post a Comment