Wednesday, September 7, 2016

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHASEMA UCHUMI WA NCHI KWA KIPINDI CHA MIEZI SITA UMEPUNGUA KWA ASILIMIA NNE

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kabwe Zitto (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho baada ya kufanyika kikao chake cha kawaida jana. Kushoto ni Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho,  Juma Sanani na kulia ni Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Shaban Mambo.
Taswira meza kuu. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho, Juma Sanani Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Shaban Mambo, Makamu Mwenyekiti Tanzania Zanzibar, Ramadhan Ramadhan na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Msafiri Mtemelwa.
Mkutano na wanahabari ukiendelea
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA Cha ACT Wazalendo kimesema katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Dk. John Magufuli uchumi wa nchi umepungua hadi kufikia asilimia nne ukilinganisha na vipindi vingine vilivyopita.

Hayo yamebainishwa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto Dar es Salaam leo wakati akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho kuhusu hali ya nchi baada ya kikao cha kawaida kilichofanyika jana.

Kabwe alisema katika miaka 10-15 iliyopita, nchi yetu imejenga uchumi ambao umekuwa ukikua kwa kiwango cha asilimia 6-7 kwa mwaka katika kipindi chote hiki. Ukuaji huu wa uchumi ulitokana na juhudi za nchi katika kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za uzalishaji mali kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Alisema awamu ya tano ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi imerithi changamoto ya uchumi unaokua bila kuwafaidisha wananchi wa kawaida. Hili ndilo tulitegemea Serikali mpya ishughulike nalo. 

Kamati kuu yetu imeshtushwa na hali ya kuanza kudorora kwa shughuli za uchumi katika kipindi cha miezi kumi ya utawala wa awamu ya tano" alisema Kabwe

 

MUWSA YAKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI MANDELA MJINI MOSH

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.Said Mecky Saidiq akiwasili katika shule ya msingi Mandela iliyopo kata ya Bomabuzi wilaya ya Moshi kwa ajili ya kupokea msaada wa Madawati yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandela wakiimba nyimbo wakati wakipokea wageni waliofika katika tukio la kukabidhi madawati.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq alipowasili katika shule ya msingi Mandela kwa ajili ya kukabidhiwa Madawati.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (kushoto) pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya (kulia) wakati wa makabidhiano ya Madawati kwa ajili ya shule ya msingi Mandela.

WADAU WAJADILI MPANGO KAZI WA KUENDESHA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OGP) WA AWAMU YA TATU

5
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan P. Mlawi akisisitiza jambo kuhusu Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP) wa Awamu ya Tatu wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango huo, uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
2
Mkurugenzi Mtendaji wa TWAWEZA Bw. Aidan Eyakuze akichangia mada katika mkutano wa wadau wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP) wa Awamu ya Tatu, uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP) wa Awamu ya Tatu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo (hayupo pichani) wakati akiwasilisha hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
3 
Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP) wa Awamu ya Tatu uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Ilomo alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb).

WAFANYAKAZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATINGA MAHAKAMANI

Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko.

                                                                                            Na Woinde shizza,Arusha

Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),  wamefungua kesi kumshtaki Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo  kwa madai ya kuvunja mikataba ya ajira.

Kesi hiyo wameifungua katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya  ya Afrika Mashariki (EACJ) kitengo cha awali.

Wafanyakazi watatu kutoka Idara ya Amani na Usalama  Katibu Mkuu huyo alivunja mikataba yao ya ajira kinyume na agizo la Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliyoyatoa kwenye mkutano wa nyongeza
wa 31 na kwa kuzingatia Kanuni ya 96 ya taratibu za wafanyakazi wa EAC ya mwaka 2006.

Wanadai kuwa walipokea barua kutoka Masjala ya EAC yenye notisi ya miezi mitatu ya kusitishwa kwa ajira zao iliyowekwa saini na katibu mkuu huyo, huku ikieleza kuwa EAC haina fedha za kuendeleza mradi wa APSA unaopata fungu kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Umoja wa Afrika (AU).

 

NCHI YA SUDANI KUSINI YAINGIA RASMI KUWA MWANACHAMA WA EAC

Na Woinde Shizza,Arusha
Nchi za jumuiya wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya mwenyekiti wa nchi hizo Dr John Pombe Magufuli hii leo wamepokea hati ya udhibitisho wa nchi ya Sudani Kusini kuwa miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Awali mapema mwaka huu walitia saini makubaliano ya kutaka kujiunga na kuwa mmoja wan chi jumuiya wanachama ambapo wataalamu kutoka nchi wanachama ambapo Rais Magufuli ndiye mwenyekiti kiongozi wa jumuiya hiyo walizingatia vigezo na masharti vya kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo ambapo leo hii yamekamilika.

Awali akizungumza mbele ya wajumbe kutoka sudani kusini katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Liberat Mfumukeko alisema kuwa jumuiya hiyo imepokea hati ya uthibitisho wa wanachama wapya wa jumuiya ya Afrika mashariki na kwamba wanasubiri Mwenyekiti John Magufuli kuidhinisha rasmi katika Mkutano wa wakuu wa nchi unaotarajiwa kufanyika jijini Daresalaam septemba 8 mwaka huu.

Kwa upande wake Mshauri wa Rais wa Sudan kusini katika masuala ya Kiuchumi Aggrey Tisa Sabun ambapo alisema kuwa wamekuwa wakitamani muda mrefu kuwa nchi wanachama na kwamba kuleta hati ya maakubaliano ni hatua moja wapo ya muunganiko huo.

Nao Alex mushi na Vailet mushi wanajumuiya ya Afrika mashariki wanasema kuwa Sudani Kusini Kujuinga na jumuiya hiyo ina faida mbalimbali ikiwemo masuala ya uchumi lakini pia nchi za jumuiya zinapaswa kufikiri Zaidi na kumaliza machafuko ambayo yanaendelea katika nchi hiyo kwani hali hiyo inatia ho

Nae Waziri wa mambo ya nje ushirikiano wa Kimataifa Agustine Maiga ambapo alisema kuwa wamepokea nyaraka hizo kwa niaba ya Mwenyekiti Rais Magufuli na kwamba hivi sasa wanaruhusiwa kushiriki katika vikao vyote kuanzia sasa na wamekuwa wanachama rasmi wa jumuiya hiyo na watapata fursa mbalimbali kama nchi mwanachama.

Kutokana na Sudan ya Kusini kuingia rasmi katika jumuiya hiyo ipo haja ya nchi kuendelea kuwa wamoja na kwamba waweze kukaa pamoja na kutatua changamoto na machafuko yaliyoko katika nchi hizo , ikiwemo kutafuta ufumbuzi wa mapigano nchini humo na kuwezesha wanajumuiya kutafuta fursa za kibiashara nchini humo.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA ENEO LILILOKUWA NA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA, AONGEA NA WAAKAZI WAKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Ardhi Mhe John Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Ali Hapi na viongozi wengine akitembelea eneo lililokuwa Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi wa nyumba za Magomeni Kota Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia alipotembelea na kuongea na wakaazi wa Magomeni Kota wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016
Wananchi wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi wa nyumba za Magomeni Kota Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016

MWENYEKITI WA BODI YA PAROLE AMTEMBELEA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA.

01
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema wakati alipomtembelea ofini kwake ili kujua matatizo mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
02
Afisa wa Jeshi la Magereza (aliyesimama kushoto) akisoma taarifa ya utekelezaji wa sheria ya bodi ya parole kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema (wa kwanza kulia) wakati Mwenyekiti wa Bodi alipomtembelea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja (katikati) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
04
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Magereza (hawapo pichani) wakati alipomtembelea Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja (kushoto)ili kujua matatizo mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Sanaa za Mikono....
Sanaa za Mikono....


Mratibu wa Maonyesho ya Sanaa za Mikono kwa Afrika Mashariki Bi. Nakaaya Sumari akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) na baadhi ya wadau waliokuja kwenye uzinduzi wa Maonyesho hayo kwa vyombo vya habari, vinavyotarajiwa kufanyika mwezi septemba 23 hadi 25 2016, Jijini Arusha



Sanaa za Mikono....
Sanaa za Mikono....
Sanaa za Mikono....














Ramadhani Mvungi (Star Tv ) na Ihucha Adam (EABC-PR)wakiteta jambo....
Mpiga Picha Kapigwa Picha Akionyesha Picha kwa wapigwa picha na mpiga Picha...
Mtangazaji Maarufu wa AZAM TV (Idd Uwesu ) katika Ubora wake....

ADAM IHUCHA,


CRAFTS producers in East Africa will soon be able to sell their products to international markets following the plans to establish an annual professional for Business-to-Business (B2B) trade fair for Home Décor, Fashion Accessories and Lifestyle products in the region.

Currently, there is no B2B trade platform for the crafts sector in the whole of East African region.

The Africa and Middle East World Fair Trade Organization (WFTO) regional director, Mr Bernard Outah said there is need to establish B2B so that producers could easily sell their products to any country of their choice without problem.

He said, at the moment, the only option for producers to reach regional or international buyers is to travel around the region in search of potential buyers or to participate in trade fairs in South Africa, West Africa or International trade fairs in Europe or the US. He said the high cost of participation fails most of African crafts producers from attending international trade fairs.
“Failure to access market opportunities is one of the key challenges that face most of African crafts producers in East African region,” he said. According to Mr Outah, the establishment of B2B will enable East African crafts producers to excel in the area and boost their businesses at both local and international levels.
Meanwhile, the public has been urged to recognize the crafts sector as a key economic sector in the region and offer required support so that it can unfold its potentiality. CBI programme manager for the export coaching programme in East Africa Ms Heiydy van der Ploeg said there is need to promote and give support to craft sector so that it could help in building up East African countries economies.
According to UNESCO, the crafts sector is the second largest employer in the developing world behind agriculture. Most of those engaged in crafts are majority women with little or no education.
The global crafts sector is valued at USD 34bn/- per annum and 65 percent of global crafts exports come from developing countries. East Africa is one of the most important crafts producing regions on the African continent.
Its geographical location has made it a melting pot of different cultures, resulting in a rich diversity of crafts skills and products.
The Chief Executive Officer (CEO) for TradeMark East Africa (TMEA), Mr Frank Matseart said crafts are important part of the East African trade story but it receives little input from various stakeholders.
He added that a growing tourism sector in the region offers the potential to sell products to tourists through souvenir and gift shops.
“Many hotels and lodges, besides sourcing products for their own in-house gift shops also look for interior decoration products to decorate their houses,” he said.
For the first time, professional craft trade fair is scheduled to take place in the country from September 23rd to 25th, this year.

No comments :

Post a Comment