Mwanasheria
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu
(katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao
Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam leo mchana, wakati akitoa
madai ya kushikiliwa kwa wafuasi wa chama hicho zaidi ya 70
wasiofahamika na wengine 10 katika vituo mbalimbali vya polisi jijini
Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya Umoja wa Kupinga
Udikiteta (Ukuta), bila ya kufikishwa mahakamani. Kushoto ni Ofisa
Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
Mwanasheria
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu
(katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao
Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam leo mchana, wakati akitoa
madai ya kushikiliwa kwa wafuasi wa chama hicho zaidi ya 70
wasiofahamika na wengine 10 katika vituo mbalimbali vya polisi jijini
Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya Umoja wa Kupinga
Udikiteta (Ukuta). Kulia ni Mwenyekiti Baraza la Umoja wa Vijana Chadema
(Bavicha), Patrobas Katambi na kushoto ni Ofisa Habari wa chama hicho,
Tumaini Makene.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kinakusudia kufungua
maombi katika Mahakama Kuu ya kuiomba mahakama hiyo kuiamuru Polisi
kuwafikisha mahakamani watu wanaoshikiliwa katika vituo mbalimbali vya
polisi jijini Dar es Salaam.
Hatua
hiyo inatokana na chama hicho kudai kuwa kuna watu 10 ambao
wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) na Kituo cha
Oysterbay vya Dar es Salaam kwa zaidi ya wiki mbili bila kupewa dhamana
ya polisi au kufikishwa mahakamani.
Kauli
hiyo ya Chadema imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu
Lissu wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu yake yaliyo
mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo mchana.
Akifafanua
kuhusu Habeas Corpus alisema, ni mamlaka iliyonayo Mahakama Kuu ya
kuamuru mamlaka yoyote ya kiserikali inayomshikilia mtu kumpeleka mtu
huyo mahakamani.
Lissu
alisema, vijana hao walikamatwa katika mikoa mbalimbali kwa makosa
aliyodai kuwa ni kujihusisha na haraka za kinachoitwa Umoja wa Kupambana
na Udikteta (UKUTA) pamoja na masuala mengine ya kisiasa.
“Kama
ikifika Jumanne hawajapelekwa mahakamani au hawajapewa dhamana ya
polisi, tutakwenda Mahakama Kuu kufungua maombi ya habeas corpus, imuite
IGP au DCI au Ma-RPC au wakuu wa vituo wanakoshikiliwa hao waeleze kwa
kwanini wanawashikilia hao watu kwa zaidi ya wiki mbili,” alisema Lissu
Lissu
alisema tayari wameshaanza maandalizi ya hati hizo ambazo zitapelekwa
Mahakama Kuu ili iweze kuwaita kati ya Mkuu wa Polisi (IGP), Mkurugenzi
wa Makosa ya Jinai (DCI), Makamanda wa Polisi wa Mikoa au Wakuu wa Vituo
vya Polisi wanakoshikiliwa watu hao.
Alifafanua
kuwa alionana na watu hao ambao wamedai mbali na kushikiliwa lakini pia
wamepigwa na kuteswa huku wakidai kuwa wamekuwa wakichukuliwa usiku na
kupelekwa katika eneo lililopo Mikocheni ambako wanateshwa na kurudishwa
polisi.
Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar Mhe,Said Hassan Said (kulia) akiwa na Viongozi wengine wa Wizara
ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora
katika mkutano Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama
cha Mapinduzi CCM mwaka 2015-2020,chini ya Mwenyekiti Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo
pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
View More...
No comments :
Post a Comment