Dondoo za hotuba ya Rais John Pombe
Magufuli wakati akizindua ndege mpya za ATCL jijini Dar es Salaam leo Septemba
28, 2016
*“Tulipochukua
hatua ya kuwashika RAS, DED Kagera leo balozi wa Uingereza ametuchangia Bil 6
kwa ajili ya wananchi Kagera”
*"Tunataka
kuanza ujenzi wa treni za umeme Dar, haya si Ulaya tu, hata hapa
yatafanyika"- Rais…
* "RAS
na DED tuliowafukuza jana, leo wameshafikishwa mahakamani
*"Ujenzi
wa daraja la Coco Beach hadi Agha Khan umeanza, Interchange ya Ubungo itaanza
karibuni"-
*“Wengine wameajiriwa na watu fulani kazi yao
kutukana kila linalofanywa na Serikali, vihela wanavyopewa kidogo na wanafikiri
hatuwajui'-JPM
*“Jana TANESCO
wametangaza tenda ya ku-supply nguzo za zege kwa kanda ya mashariki, Kaskazini, Lake
Zone na Southern Highlands
*“kama
huzitaki ndege hizi bora ukae kimya kiherehere chanini.”
* “Huyo
aliyesema ndege hii haikimbii awe mtu wa kwanza mimi nitamlipia nauli halafu
akae mbele akaone mawingu yanavyopiga.”
* "Ndani ya ATCL kuna wake wa Mawaziri,
Shirika halizalishi lakini wake wa Mawaziri wameng'ang'ani tu.”
*“ Kwa
hiyo kulikuwa na wanafunzi hewa, wafanyakazi hewa na mafuta hewa.”
* "ATCL
walikuwa wakinunua mafuta hewa, unaambiwa ndege imeenda Mwanza kumbe iko Dar
uwanjani"
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo
Septemba 28, 2016, amezindua ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400
kwenyeuwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam. Ndege hizo zilinunuliwa ili zitumiwe na Kampuni ya Ndege ya
Tanzania, (ATCL), ambayo inamilikiwa na serikali. Pichani, Rais
amkisalimiana na muhudumu wa ndege hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
(PICHAN A IKULU)
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe akishuka kwenye ndege
mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa
na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth
Magufuli wakiingia kwenye ndege mojawapo baada ya kukata utepe kuzindua
rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa
ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na
viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina
ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la
Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo
Jumatano Septemba 28, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth
Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege
mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400
zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28,
2016
Rais katika picha ya pamoja na viongozi, wahudumu wa ndege na maafisa waandamizi wa serikali
Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Isaya Mwita(mwenye tai nyekundu) na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masanju wakishuka kwenye ndege
mojawapo baada ya Rais Magufuli kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya
Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege
la
Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo
Jumatano Septemba 28, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa
Canada nchini Mhe. Ian Myles baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege
mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar
es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016
Balozi Seif kati kati akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi kwa ajili ya kugharamia uendelezaji wa ujenzi wa jengo la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Kitope. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wiaya ya Kaskazini B Nd. Issa Juma na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Maandalizi na Msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bibi Safia Ali Rijali.
Kulia ya Balozi Seif ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Kitope Mwalimu Suleiman Juma Makame na Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Maabara ya Skuli za Fujoni na Kitope Nd. Yasir De Costa.
Msimamizi wa Ujenzi wa Majengo ya Maabara ya Skuli za Fujoni na Kitope Nd. Yasir De Costa wa kwanza kushoto akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa majengo ya Maabara ya skuli hizo. Picha na – OMPR – ZNZ.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Viongozi na washirika wa maendeleo katika Sekta ya Elimu kuzijengea uwezo zaidi wa miundombinu skuli mbali mbali Nchini ili ziwe na uwezo kamili wa kuhimili ushindani wa kitaaluma uliopo katika kiwango cha Kitaifa na Kimataifa.
Alisema wakati wa sasa ni ule wa sayansi uliobadilika kabisa Kiteknolojia tofauti na uliopita kiasi kwamba jamii inapaswa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira yanayokubalika kivifaa pamoja na walimu waliobobea.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa kumbusho hilo wakati akikabidhi Hundi ya shilingi Milioni 13,078,000/- kwa ajili ya ukamilishaji wa Jengo la Kisasa la Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya Jimbo la Mahonda.
Katika hafla hiyo fupi ambayo pia alikabidhi hundi ya shilingi Milioni 1.7 kukamilisha gharama za ujenzi wa Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni kwa msimamizi wake Nd. Yasir De Costa Balozi Seif aliahidi kutoa vifaa vyote vya Maabara kwa Skuli ya Sekondari ya Kitope mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.
Wananchi wa Kibiti wakimsikiliza
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia Septemba 28, 2016
licha ya mvua kubwa iliyonyesha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, Dk Leornad Akwilapo amewataka vijana kutafuta ajira sehemu
mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo badala ya kutegemea fursa za
serikali.
Kauli
hiyo ameitoa wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, iliyolenga kuweka
mkakati wa pamoja kati ya wadau wa elimu, serikali katika utekelezaji wa
malengo ya maendeleo endelevu lengo la nne.
Alisema
kwamba ni imani yake kwamba elimu waliyonayo vijana inawaruhusu kufanya
shughuli mbalimbali ambazo si lazima kuajiriwa na serikali.
Alisema
hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuajiri kila mmoja lakini elimu
zinazotolewa pamoja na ya Tanzania zinawaandaa vijana kujiajiri wenyewe.
Akizungumzia
warsha hiyo alisema kwamba wadau wanakutana kutengeneza mkakati wa
pamoja wa kutoa elimu bora kwa wananchi wa Tanzania na namna ambavyo
malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) yanavyoshirikishwa katika utoaji
elimu.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leornad
Akwilapo akifungua warsha ya kutengeneza mkakati mmoja kati ya serikali
na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu uliondaliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa NACTE jijini Dar es Saalam.
Alisema
lengo la nne la Maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa linasisitiza
elimu bora isyokuwa ya kibaguzi kwa watu wote na hivyo mkutano wao ni
kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana kutoa elimu bora inayowezesha
watu wake kujiajiri.
Alisema
kwamba mtazamo huo ambao tayari Tanzania ilikuwa nao miaka ya mwanzo ya
uhuru ambapo kulikuwa na kisoma cha watu wazima kitu ambacho kilillenga
kuwafanya watu kuwa na elimu ya kutosha kuhusu mazingira yao na maisha
yao. Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania, Zulmira
Rodrigues alisema kwamba wameandaa warsha hiyo kwa lengo la kuelezana
utoaji bora wa elimu ambao utaendana na matakwa ya sasa ya kumwezesha
anayepata elimu hiyo kujiajiri mwenyewe. Aidha amesema lengo la
kushirikisha wadau wa elimu ni kuhakikisha kwamba lengo la maendeleo
endelevu la nne la Umoja wa Mataifa linashirikishwa katika utoaji elimu
kwani lengo hilo ni kuhakikisha elimu kwa wananchi wote bila ubaguzi
huku hatua zikichukuliwa katika kuwezesha wanawake kusonga mbele.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues
akizungumza kuhusu lake lilivyojipanga kushirikiana na Serikali katika
nyanja mbalimbali ya ukuzaji wa elimu haapa nchini.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu Sayansi na
Teknolojia, Makuru Petro akiwasilisha mada wakati wa kongamano
lililoshirikisha Serikali pamoja na wadau mbalimbali kujadili ni kwa
jinsi gani wanatengeneza mkakati bora ili kuweza kuisaidia serikali
kutoa elimu bora na bila ubaguzi wa aina yoyote.Afisa
Elimu Mkuu Hilda K. Mkandawire kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia akiwasilisha mada wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau
mbalimbali wa elimu.Baadhi ya wadau mbalimbali wa sekta ya elimu wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa unaendelea.Criana
Connal kutoka UNESCO akizungumza jambo wakati wa warsha
iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu ili kujadili mpango mkakati
utakaosaidia kuinua kiwango cha elimu nchini Tanzania.Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Maria Karadenizli
(kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues wakati wa kongamano lililowakutanisha
wadau mbalimbali wa elimu.Mkutano ukiendelea.Baadhi
ya makundi ya wadau wa sekta ya elimu wakijadiliana ili kutengeneza
mpango mkakati wa pamoja kati ya serikali na wadau mbalimbali wa elimu
utakaosaidia serikali kutoa elimu bila ubaguzi wa aina yoyote na kwa
makundi yote ili kufanikisha lengo namba nne la Mpango wa maendeleo
endelevu (SDG’s) linalohusu elimu bora kwa wote.
R
MAJALIWA AWASILI KIBITI KWA ZIARA YA SIKU MOJA
BALOZI SEIF AIKABIDHI SEKONDARI YA KITOPE MILIONI 13 ILI KUKAMILISHA JENGO LAKE LA MAABARA
Mwakilishi
wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Kaskazini “B” Nd. Issa Juma kushoto yake wakikaguwa maendeleo ya
ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Fujoni.
Haiba ya muonekano wa Jengo la Msikiti wa Ijumaa Fujoni unavyoonekana
nje ukiendelea ujenzi wake ambao unatarajiwa kuezeskwa mapema wiki
ijayo.
Balozi Seif kati kati akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi Hundi kwa ajili ya kugharamia uendelezaji wa ujenzi wa jengo la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Kitope. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wiaya ya Kaskazini B Nd. Issa Juma na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Maandalizi na Msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bibi Safia Ali Rijali.
Kulia ya Balozi Seif ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Kitope Mwalimu Suleiman Juma Makame na Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Maabara ya Skuli za Fujoni na Kitope Nd. Yasir De Costa.
Msimamizi wa Ujenzi wa Majengo ya Maabara ya Skuli za Fujoni na Kitope Nd. Yasir De Costa wa kwanza kushoto akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa majengo ya Maabara ya skuli hizo. Picha na – OMPR – ZNZ.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Viongozi na washirika wa maendeleo katika Sekta ya Elimu kuzijengea uwezo zaidi wa miundombinu skuli mbali mbali Nchini ili ziwe na uwezo kamili wa kuhimili ushindani wa kitaaluma uliopo katika kiwango cha Kitaifa na Kimataifa.
Alisema wakati wa sasa ni ule wa sayansi uliobadilika kabisa Kiteknolojia tofauti na uliopita kiasi kwamba jamii inapaswa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira yanayokubalika kivifaa pamoja na walimu waliobobea.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa kumbusho hilo wakati akikabidhi Hundi ya shilingi Milioni 13,078,000/- kwa ajili ya ukamilishaji wa Jengo la Kisasa la Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya Jimbo la Mahonda.
Katika hafla hiyo fupi ambayo pia alikabidhi hundi ya shilingi Milioni 1.7 kukamilisha gharama za ujenzi wa Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni kwa msimamizi wake Nd. Yasir De Costa Balozi Seif aliahidi kutoa vifaa vyote vya Maabara kwa Skuli ya Sekondari ya Kitope mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.
WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA KIBITI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akihutubia mkutano wa hadhara katika Mji wa Kibiti akiwa katika
ziara ya wilaya hiyo Septemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akihutubia mkutano wa hadhara katika Mji wa Kibiti akiwa katika
ziara ya wilaya hiyo Septemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Wananchi wa Kibiti wakimsikiliza
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia Septemba 28, 2016
licha ya mvua kubwa iliyonyesha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments :
Post a Comment