Saturday, August 27, 2016

MAJALIWA AKUTANA NA OFISA MTENDAJI MKUU WA GLOBAL FUND

MAJALIWA AKUTANA NA OFISA MTENDAJI MKUU WA GLOBAL FUND

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul (kulia kwake) kwenye hoteli ya Windsor Agosti 26,2016.Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul kwenye hoteli ya Windsor Agosti 26,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Windsor jijini Nairobi, Agosti 26,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Msanii wa Bongofleva Baraka Da Prince  akitumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016 lililofanyika katika uwanja wa Taifa usiku wa jana Mjini Kahama na kuwakutanisha wasaniii wengine nguli hapa nchini katika mziki wa kizazi kipya.



Christian Bella akilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2016 katika uwanja wa Taifa mjini Kahama usiku wa jana .


Chege Chigunda naye alitoa burudani ya kukata na shoka katika uwanja wa Taifa kwenye Tamasha la Tigo Fiesta 2016 Mjini Kahama  usiku wa jana.

Chege Chigunda



Jux akiwa na Dancer wake akitumbuiza wimbo wa Wivu katika jukwaaa la Tigo Fiesta 2016.


Maua Sama naye alipamba Tamasha la Tigo Fiesta 2016 katika Uwanja wa Taifa Mjini Kahama usiku wa Jana.

Rayvany naye akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fista 2016 ambapo aliwasimulia wananchi wa Kahama stori ya "KWETU" na jinsi anavyotafuta "KIKI"

Stamina akitoa michano katika jukwaa  la Tigo Fiesta 2016 usiku wa jana katika Uwanja wa Taifa .

Maelfu ya wakazi wa Kahama na maeneo jirani wakishuhudia burudani mbali mbali toka kwa wasanii waliotumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa jana.


Mashabiki 


IMOOOOOOOOOOOOOOO

Shanngwe zikiendelea katika uwanja wa Taifa wakati Tamasha la Tigo Fiesta likiendelea usiku wa jana Mjini Kahama.

i


Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji kiongozi, Dkt.Daniel Moses Kulola, linapenda kuwakaribisha watu wote kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa jipya na la kisasa linalotarajiwa kujengwa katika viwanja vya kanisa hilo.
Harambee hiyo inatarajiwa kufanyika kesho jumapili Agosti 28,2016 kanisani hapo ambapo watu wote wakiwemo waumini na viongozi wa Madhehebu mbalimbali, Viongozi wa Serikali na Taasisi binafsi, wanakaribishwa ili kuungana na viongozi na waumini wa Kanisa hilo katika kushiriki kwenye harambee hiyo.
Kumbuka "Bwana Hufurahi  Anapojengewa Hekalu Lenye Kufana" hivyo utabarikiwa ikiwa utashiriki katika harambee hiyo. Kwa mawasiliano zaidi, tumia nambari za simu; 076774 90 40 AU 0787 74 90 40.


WAKALA WA VIPIMO NA VIPIMO, WATOA ELIMU YA UZANI KWA WAKULIMA WA KOROSHO MIKOA YA KUSINI

Meneja wa wakala wa vipimo mkoani Mtwara Augustine Maziku akiwaonesha wakulima wa korosho, mkoani humo kusoma kwa usahihi mizani iliyo hakikiwa na wakala wa vipimo

Meneja wa wakala wa vipimo mkoani Ruvuma, Hallet Hassan  akitoa elimu kwa wakulima wa korosho  mkoani humo kabla ya msimu kuanza  ili kuepusha kuzulumiwa na wanunuzi wasio waaminifu. (PICHA ZOTE NA IREN JOHN).


Alfa Mtui, (kulia), afisa vipimo mwandamizi, akitoa elimu kwa wakulima wa korosho mkoani ruvuma namna yakutambua mizani  iliyo hakikiwa na kuruhusiwa kutumika na wakala wa vipimo.

Wakulima wa korosho katika mkoa wa Ruvuma wakipata elimu kupitia vipeperushi vilivyo andaliwa na wakala wa vipimo wakati wa zoezi la utoaji elimu


Meneja wa wakala wa vipimo mkoani Mtwara Augustine Maziku akijibu maswali kutoka kwa wakulima waliokuwa wamefika kupatiwa elimu ya matumizi sahihi ya mizani iliyo hakikiwa na wakala wa vipimo kabla ya msimu wa ununuzi wa korosho kuanza.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakifanya usafi  wakati wa zoezi la usafi nchi nzima linalofanyika kila jumamosiya mwisho wa mwezi. Wafanyakazi hao walikuwa wakifanya usafi leo Agosti 27, 2016 eneo la Double Road mjini Moshi.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa wamebeba vifaa kwa ajili ya kufanya usafi katika eneo la njia mbili maarufu kama Double Road mjini Moshi leo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakivuka barabara tayari kuanza zoezi la kufanya usafi katika eneo la Double Road mjini Moshi leo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakifanya usafi katika maeneo ya maduka yaliyopo eneo la Double Road mjini Moshi.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi Emanuel Kishosha akiowaongoza wafanyakazi wenzake katika zoezi la kufanya usafi .
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakiokota taka zilizokusanywa wakati wa zoezi la usafi lilofanyika katika eneo la Double Road mjini Moshi.
Wafanyakazi wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa na taka zilizokusanywa wakienda kuzitupa katika eneo la kusanyia takataka.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiendelea na usafi katikati ya barabara  .
Meneja wa NMB tawi la Neslon Mandela Emanuel Kishosha akiwa amebeba taka mara baada ya kumaliza kuzikusanya wakati wa zoezi hilo la usafi.
Hivi ndivyo yalivyooonekana maeneo ambayo wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi walishiriki kuyafanyia usafi  mjini Moshi hii leo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

UWANJA WA MAVAZI

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH.3 BILIONI HALMASHAURI YA ARUSHA DC WILAYANI ARUMERU

1MkimbizaMwenge wa Uhuru kitaifa akiwaongoza Askari wa Kikosi cha Kutulia
Ghasia(FFU)kuingia katika halmashauri ya wilaya ya Arusha DC baada ya kumaliza mbizo zake halmashauri ya wilaya ya Meru zote zikiwa katika wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha . 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akivalishwa Skafu na kijana wa Scout wakati wa kuanza kukimbiza Mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya wilaya ya Arusha DC.  
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijima akisalimiana na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha DC kabla ya kuanza kuweka
Mawe ya Msingi na kuzindua miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh 3 bilioni.
 
Mkurugenzi wa New Age Company Ltd,Godson Ngomuo akimwonyesha Samani
zinazotengenezwa na kuuzwa na kampuni yake na kusaidia kutengeneza ajira
kwa vijana wazawa.
 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2016,George Mbijimaakizungumza na maafisa wa taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilaya ya Arumeru
wanaotoa elimu dhidi ya Rushwa.

KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI YATEMBELEA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART) JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Max Malipo, ambayo imeingia ubia wa utendaji na Udart, Mhandisi Juma Rajab, akizungumza na wajumbe hao katika ziara hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (kulia), akiwapatia kadi za kupandia mabasi hayo wajumbe hao.
 Wajumbe wa kamati hiyo wakipita katika eneo la kukatia tiketi kwa kutumia gadi maalumu badala ya tiketi za kawaida.
 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Anjelina Malembeka (kulia), akiteta jambo na Esther Mahawe ndani ya basi la mwendo wa haraka Dar es Salaam leo, walipokuwa katika ziara ya kutembelea mradi wa Udart. Wengine nyumba kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza na Mariam Ditopile.

MAMIA WAMZIKA MWANDISHI SEIF HASSAN, PEMBA

                                                                         Mwandishi Seif Hassan enzi za uhai wake
MAMIA ya wananchi, Waandishi wa habari wakiwa wameubeba mwili wa Marehemu mwandishi wa Habari wa Radio Jamii Mkoani na Mwanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Time School and Journalism (TSJ)Tawi la Pemba, Seif Hassan Mohamed kuupeleka katika makazi yake ya Mwisho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAUMINI mbali mbali wa Dini ya Kiislamu wakimswalia Marehemu Seif Hassan Mohamed, aliyefariki dunia baada ya kupata ajali jana majira ya saa moja na nusu usiku huko Mkoani(Picha na Haji Nassor, PEMBA.)
SHEKH Salmin Sheha Ussi, akiwaongoza wananchi katika mazishi ya Mwandishi wa habari wa Radio Jamii Mkoani Seif Hassan Mohamed, aliyefariki dunia jana usiku na kuzikwa kijijini kwao Stahabu Mkanyageni Wilaya ya Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

ITALIA YAOMBOLEZA VIFO VYA WATU WALIOKUFA KWA TETEMEKO LA ARDHI

BAYERN MUNICH YAANZA BUNDESLIGA KWA KUTOA ONYO KALI

Robert Lewandowski amefunga magoli matatu 'hat-trick' wakati Bayern Munich ikiichakaza Werder Bremen kwa magoli 6-0 katika mchezo wao wa kwanza wa ligi ya Bundesliga.

Mabingwa hao watetezi wa ligi hiyo wanaonolewa na Carlo Ancelotti walipata goli la kwanza safi katika dakika ya tisa kupitia kwa Xabi Alonso.
Kisha mshambuliaji raia wa poland Lewandowski ndipo alipoanza kuonyesha makali yake ya kucheka na nyavu baada ya kupita dakika akiunganisha pande la Franck Ribery. 
                                                        Xabi Alonso akiifungia Bayern Munich goli
                 Robert Lewandowski akifunga goli lake la tatu kwa mkwaju wa penati

No comments :

Post a Comment