Tuesday, August 30, 2016

TANESCO KUBORESHA KITUO KIKUU CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME CHA ILALA, MAENEO KADHAA KUATHIRIKA NA UPATIKANAJI UMEME JIJINI DAR ES SALAAM




NA K-VIS MEDIA
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), linapenda kuuarifu umma kuwa kutakuwepo na katizo la umeme KUANZIA Septemba 3, 2016 kwenye maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kutokana na kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza cha Msongo wa Kilovolti 132 cha Ubungo-Ilala.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano ya Shirika hilo, Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016, katizo hilo la umeme litaanza rasmi Septemba 3 na umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016.
Taarifa hiyo imetaja maeneo yatakayoathirika na zoezi hilo kuwa ni pamoja na eneo lote la katikati ya jiji (City centre), Maeneoyote ya Upanga, maeneo yote ya Kariakoo, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Mbagala, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Ilala, Maeneo yote ya Chang’ombe, Maeneo ya Temeke, Uwanja wa Taifa, Unilever, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jamana printers, Quality Plaza, Notco, Bima ya Afya, Bandari Gate pamoja na maeneo ya jirani.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa ili jiji la Dar es Salaam lipate umeme ulio bora na wa uhakika, Shirika laUmeem Tanzania (TANESCO), limemruhusu mkandarasi, (TAKAOKA), kubadilisha vikombe na nyaya na kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa za njia mbili (Two-lines) za Msongo wa Kilovolti 132.
Kuboresha vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Ilala na Ubungo kwa kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa zaidi.
Kubadilisha vifaa vya kupima umeme kwenye njia mbili (Two-lines) za Ubungo-Ilala.


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kumi na nne ya Siku ya Wahandisi yatakayofanyika Septemba mosi hadi pili jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo ya siku mbili yanatarajiwa kukutanisha zaidi ya wahandisi elfu mbili kutoka ndani na nje ya nchi ili kupata fursa ya kufanya majadiliano ya kitaaluma, kufanya maonesho ya kiufundi na kibiashara, kuwatambua na kuwazawadia wahandisi wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo yao ya mwisho na kuwaapisha wahandisi waliokidhi vigezo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote, (pichani juu), amesema mada kuu katika maadhimisho hayo itakuwa ni “Tanzania kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati na kuwa nchi ya viwanda: nini jukumu la wahandisi”.
“Tumejipanga Siku ya Wahandisi mwaka huu iwe na mvuto wa pekee kwa sababu mada yake ni ya kitaifa ikiangalia Dira ya Maendeleo ya Taifa na mwelekeo wa nchi kuwa nchi ya viwanda” amesema Eng. Mlote.
Maadhimisho ya wahandisi Tanzania yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 2013, lengo likiwa ni kuiwezesha jumuiya ya wahandisi nchini kuionesha jamii kile ambacho wahandisi wanaweza kukifanya katika kuleta maendeleo ya nchi.
Takribani wahandisi elfu 17 wanakadiriwa kuwepo nchini katika sekta mbalimbali, lengo likiwa ni kuwa na wahandisi elfu 83 ili kukidhi mahitaji ya nchi kuwa ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.(PICHA NA BENJAMIN SAWE-MAELEZO)


Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongoenzi za uhai wake
 

Familia ya marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo (pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi, kwa ajali ya gari.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawiro akipokea msaada wa madawati 235 kwa mkoa wa Kagera toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande jana kwenye shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Vijijini  Deodatus Kinawiro akihutubia wakazi wa Bukoba baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi Kagera makabidhiano hayo yalifanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba 

 Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande  akitoa hotuba kwa wageni waalikwa na wanafunzi mara baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi za mkoa wa  Kagera ,katika hafla iliyofanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakishuhudia makabidhiano  ya madawati 235 kwa shule za msingi mkoani Kagera   toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakiwa wameketi kwenye moja ya dawati kuonyesha kuwa wamepokea madawati toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.



 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbeneakipokea Risala kutoka kwa Ocd Wilaya Ileje
 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene, akikabidhi Laptop kwa OCD wa Wilaya ya Ileje kw ajaili ya kusaidia kazi katika Wilaya hiyo
 Mbunge wa Ieje , Mh Janet Mbene, akikabidhi Matairi kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi  Wilaya ya Ileje Hamida Mbogo
 Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akipokea mkono wa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje  Joseph Mkude mara baada ya kukabidhi laptop, Photocopy Mashine, Matairi na lim tano



Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,(katikati), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya wiki  ya promosheni ya”Kamata Mpunga”ambapo Hassan Mfaume, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam aliibuka mshindi wa wiki wa kitita cha shilingi Milioni 5/- kupitia promosheni hiyo inayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Jumla ya washindi 224 wamepatikana tangu kuanza kwa promosheni hiyo.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali,Wengine katika picha kushoto ni Ofisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania,Abdallah Hamed na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Mathew Kampambe.

1
Bw . Mohamed Seif Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume hiyo akikabidhi kwa Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015, Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye mgahawa wa Mokka City Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam.
2
Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015 mara baada ya kukabidhiwa rasmi.
3
Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015


Wakurugenzi hao wametakiwa kuyachukua haraka madawati hayo na kuyapeleka Katika shule zenye kadhia hiyo ikiwa ni ishara ya kuamsha taswira ya elimu kwa wanafunzi mchini kuondokana na mateso ya kukaa chini wakiwa darasani.

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa makabidhiano hayo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa huo huku akisifu wadau na Taasisi mbalimbali kujitolea kuunga mkono uchangiaji wa madawati ambao awali ulianza kwa ngazi ya Halmashauri kabla ya kuhusisha taasisi mbalimba sambamba na wadau wa maendeleo Mkoani humo.
Mtigumwe amesema kuwa Hali ya Madawati katika Mkoa ilikuwa chini ya asilimia 40% lakini chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na wadau 67 wa Maendeleo wameweza kuchangia jumla ya shilingi milioni 42,626,500 hivyo kufanikisha lengo la utengenezaji wa madawati kufikia asilimia 98% ambapo hata hivyo upungufu Mkubwa ulikuwa zaidi katika Halmashauri za Singida na Manyoni.

No comments :

Post a Comment