Rais Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Kampuni ya Mafuta ya Stat Oil ya
Norway, Bw. Oystein Michelsen Ikulu jijini Dar es Salaam, Agosti 22, 2016, kabla ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi
mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili (LNG Plant)
kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likon'go, Mchinga Mkoani Lindi.
Rais Dkt. John
Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Meneja Biashara wa Kampuni ya Stat Oil ya
Norway Oivind Holm Karlsen (watatu) kutoka kushoto mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Mwakilishi
wa Kampuni hiyo, Bw. Oystein Michelsen. (PICHA
NA IKULU)
![]() |
| Sehemu ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani |
NA MWANDISHI MAALUM
SHIRIKA
la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea kuwatangazia wateja wake wote wa Wilaya
ya Bagamoyo kuwa, kutokana na kukatika kwa waya wa mawasiliano, (Optic Fiber)
kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, Ofisi ya Shirika hilo wilayani Bagamoyo bado
inashindwa kutoa huduma za kupokea malipo na kuuza LUKU kwa muda mpaka hapo
waya huo utakapoungwa.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga akitoa neno la utangulizi kabla
ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman kutoa hotuba yake ya
ufunguzi wa
mafunzo ya siku tatu kuhusu Miongozo ya Luanda juu ya taratibu za ukamataji na ushikiliaji wa watuhumiwa kabla ya kufunguliwa mashtaka mjini Unguja, Zanzibar Agosti 22, 2016
mafunzo ya siku tatu kuhusu Miongozo ya Luanda juu ya taratibu za ukamataji na ushikiliaji wa watuhumiwa kabla ya kufunguliwa mashtaka mjini Unguja, Zanzibar Agosti 22, 2016
Mgeni Rasmi, Jaji Mkuu wa Zanzibar,
Mhe. Omar Othman Makungu leo akifungua rasmi mafunzo ya siku tatu kuhusu
Miongozo ya Luanda juu ya taratibu za ukamataji na ushikiliaji wa watuhumiwa
kabla ya kufunguliwa mashtaka. Mafunzo hayo yanafanyika Zanzibar Beach hotel
mjini Zanzibar na yanawashirikisha takriban maafisa 50 wa Jeshi la Polisi,
Magereza, Vyuo vya Mafunzo, Mahakama na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Mwakilishi kutoka taasisi ya African
Policing Civilian Oversight Forum – APCOF, Bi. Louise Edwards
Mgeni Rasmi, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu (katikati) na Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo kuhusu Miongozo ya Luanda (Luanda Guidelines on the conditions of arrest, police custody and pre–trial detention in Africa) yaliyoanza leo Zanzibar Beach Hotel mjini Zanzibar. Wengine waliokaa kutoka kushoto ni: Katibu Mtendaji wa THBUB, Bibi Mary Massay, Mwakilishi kutoka taasisi ya African Po







No comments :
Post a Comment