Rais Dkt. John
Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Somalia hapa nchini Mohammed Hassan Abdi
mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam Agosti 23, 2016. (PICHA NA IKULU)
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Balozi wa Somalia hapa nchini Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kuwasili Ikulu
kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho
kutoka kwa Balozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni mara
baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni mara
baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni
akisaini kitabu kabla ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais Dkt.
John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea hapa nchini Kim Yong Su mara baada
ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es SalaamMAFUNZO KUHUSU MWONGOZO WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA KWA MIKOA YA KANDA YA ZIWA YAANZA.
Mgeni Rasmi Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu Katibu
Mtendaji, kundi la Uzalishaji, Tume ya Mipango (aliyesimama) akitoa hotuba kwa
ajili ya ufunguzi rasmi wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Rasilimali za
Umma kwa washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Geita and Simiyu. Wengine ni Bi. Lorah
Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango
(kushoto) na Bw. John Mduma, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(kulia).
Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji,
Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue mafunzo hayo ya siku tano. Waliokaa ni Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu
Katibu Mtendaji, Klasta ya Uzalishaji, Tume ya Mipango (katikati) na Bw. John
Mduma, Mhadhiri Mwanamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Muwezeshaji Dr. Kenneth Mdadila, Mhadhiri, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam akishusha nondo kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Washiriki wakisikiliza na kufuatilia kwa makini mafunzo
waliyokua wakipata kutoka kwa muwezeshaji.
Washiriki wakisikiliza na kufuatilia kwa makini mafunzo
waliyokua wakipata kutoka kwa muwezeshaji.
Picha yan pamoja
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akisalimiana na Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
"Millicom Group" akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Unguja kwa
mazungumzo leo (kushoto) Nd,Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa Zanztel.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akisalimiana na Bibi Rachel Samren Naibu Mtendaji Mkuu wa
kampuni ya Millicom Group pia Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Zanztel
(katikati) Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa kampuni ya "Millicom
Group"(wa pili kulia) na (kushoto) Nd,Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa
Zanztel ujumbe huo ulifika Ikulu Mjini Unguja leo kwa mazungumzo na
Rais.
Ujenzi
wa daraja la mto Kavuu wilayani Mlele ambalo Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alikagua ujenzi wake Agosti 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa daraja la mto Kavuu wilayani
Mlele Agosti 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa daraja la Kavuu linalojengwa na kampuni ya Nandra Engineering and Construction Ltd ya mkoani Morogoro na kumtaka mkandarasi huyo kulikamilisha haraka.
Ujenzi wa mradi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 85.34 ulianza Septemba 2013 na ulitarajiwa kukamilika Septemba 27, 2014. Mradi huo wenye thamani ya sh. Bilioni 2.718 unagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100.
“Serikali imedhamiria kuimarisha barabara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja. Ujenzi wa daraja la Kavuu utakamilika katika kipindi cha mwaka huu wa fedha hivyo nawaomba muendelee kuiamini Serikali yenu,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Majimoto, Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele.
“Tumeamua kuwapa kazi wakandarasi wa ndani tunataka mfanye kazi daraja likamilike kwa viwango vyenye ubora ili kuthibitisha kama wasomi wetu mnafanya kazi na hatimaye tuwape kazi nyingine,” amesema.
Wakati huo huo Waziri Mkuu amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kujiepusha na matapeli wanaopita katika maeneo yao na kuwataka wachange fedha za kuanzisha vikundi ili wapewe sh. milioni 50 zilizoahidiwa na Serikali.
“Serikali bado hatujaanza kusambaza fedha hizo. Jihadharini na hao matapeli na wezi hivyo wakija kwenye maeno yenu wakamateni. Zoezi hilo likianza mtajulishwa kupitia halmashauri zenu,” amewasisitiza.
Awali mbunge wa jimbo la Kavuu, Dk. Pudensiana Kikwembe alimuomba Waziri Mkuu kutoa kipaumbele kwenye ujenzi wa daraja la Kavuu ili likamilike mapema na kuwawezesha wananchi kusafirisha mazao yao kwa urahisi.
Pia ameiomba Serikali kutekeleza ahadi ya Mhe. Rais Dk. John Magufuli ya ujenzi wa barabara ya kutoka Majimoto hadi Inyonga yenye urefu wa kilomita 130 kwa kiwango cha lami aliyoitoa wakati wa kampeni. Waziri Mkuu amesema barabara hiyo itajengwa katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha.
| Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwiru Mkoani Mwanza wakiwa wamekalia madawati 60 waliyopewa na kampuni ya Tigo,wakati wa hafla iliyofanyika jana. |
Kampuni ya Simu ya Tigo Tanzania leo imeanzisha rasmi mkakati wake wa nchi nzima wa kutoa huduma kwa jamii kwa kuchangia madawati 385 yenye thamani ya shilingi milioni 64 kwa shule tisa za msingi mkoani Mwanza ambayo yatazinufaisha shule za msingi katika wilaya za Ukerewe, Nyamagana, Ilemela na Sengerema wakati wa msimu wa tamasha la Fiesta 2016 mkoani Mwanza
RAIS WA ZANZIBAR, DK.SHEIN AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA MILLICOM NA UJUMBE WAKE
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akisalimiana na Bibi Rachel Samren Naibu Mtendaji Mkuu wa
kampuni ya Millicom Group pia Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Zanztel
(katikati) Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa kampuni ya "Millicom
Group"(wa pili kulia) na (kushoto) Nd,Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa
Zanztel ujumbe huo ulifika Ikulu Mjini Unguja leo kwa mazungumzo na
Rais.MBUNGE WA ILEJE JANET MBENE ATAKA WALIOKULA FEDHA ZA MRADI WA HOSPITALI WACHUNGUZWE
Mbunge
wa Ileje Mh Janet Mbene, akiwa na watendaji wa Halmashauri hiyo
akikagua sehemu ya juu ya jengo jipya la Hospitali ya Wilaya ya Ileje
Ksata ya Itumba inayojengwa kwa pesa za Serikali ya Tanzania
Mganga mkuu wa Hospitali ya Ileje akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo hilo Mh Janet Mbene alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo jipya la Hospitali hiyo Mbunge wa Ileje Mh Janet Mbene akitoa pole katika wodi ya Wanawake amabao walibahatika kujifungua kwa Upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje.

MAJALIWA AKAGUA JENZI WA DARAJA LA MTO KAVUU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa daraja la Kavuu linalojengwa na kampuni ya Nandra Engineering and Construction Ltd ya mkoani Morogoro na kumtaka mkandarasi huyo kulikamilisha haraka.
Ujenzi wa mradi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 85.34 ulianza Septemba 2013 na ulitarajiwa kukamilika Septemba 27, 2014. Mradi huo wenye thamani ya sh. Bilioni 2.718 unagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100.
“Serikali imedhamiria kuimarisha barabara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja. Ujenzi wa daraja la Kavuu utakamilika katika kipindi cha mwaka huu wa fedha hivyo nawaomba muendelee kuiamini Serikali yenu,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 23, 2016) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Majimoto, Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele.
“Tumeamua kuwapa kazi wakandarasi wa ndani tunataka mfanye kazi daraja likamilike kwa viwango vyenye ubora ili kuthibitisha kama wasomi wetu mnafanya kazi na hatimaye tuwape kazi nyingine,” amesema.
Wakati huo huo Waziri Mkuu amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kujiepusha na matapeli wanaopita katika maeneo yao na kuwataka wachange fedha za kuanzisha vikundi ili wapewe sh. milioni 50 zilizoahidiwa na Serikali.
“Serikali bado hatujaanza kusambaza fedha hizo. Jihadharini na hao matapeli na wezi hivyo wakija kwenye maeno yenu wakamateni. Zoezi hilo likianza mtajulishwa kupitia halmashauri zenu,” amewasisitiza.
Awali mbunge wa jimbo la Kavuu, Dk. Pudensiana Kikwembe alimuomba Waziri Mkuu kutoa kipaumbele kwenye ujenzi wa daraja la Kavuu ili likamilike mapema na kuwawezesha wananchi kusafirisha mazao yao kwa urahisi.
Pia ameiomba Serikali kutekeleza ahadi ya Mhe. Rais Dk. John Magufuli ya ujenzi wa barabara ya kutoka Majimoto hadi Inyonga yenye urefu wa kilomita 130 kwa kiwango cha lami aliyoitoa wakati wa kampeni. Waziri Mkuu amesema barabara hiyo itajengwa katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha.
BONDIA IDDI MKWELA ALIVYO MSAMBALATISHA MWINYI MZANGELA TAIFA
| Mabondia Mwinyi Mzengela kushoto na Iddi Mkwela wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mkwela alishinda kwa point katika mpambano uho wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia
Iddi Mkwela kulia akipiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Upcut' uku akirudi
nyuma wakati mpinzani wake akiwa kamkumbatia Mkwela alishinda kwa pointi
mpambano uho wa raundi sita uliofanyika mwishoni mwa wki iliyopita
katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha
wa kimataifa wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia
akimpatia mahelekezo bondia Iddi Mkwela wakati wa mpambano wake na
Mwinyi Mzengela Mkwela alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita
Picha na SUPER D BOXING NEWS
WATU 1,900 WAMEUAWA NDANI YA WIKI SABA KATIKA MSAKO WA WAUZA 'UNGA' PHILIPPINE
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
Philippine amesema zaidi ya watu 1,900 wameuwawa wakati wa msako
dhidi ya biashara za dawa za kulevya katika muda wa wiki saba
zilizopita.
Mkuu huyo Ronald dela Rosa ametoa
maelezo hayo mbele ya baraza la seneti kuhusiana na ongezeko kubwa la
mauaji tangu rais Rodrigo Duterte awe rais wa nchi hiyo.
Amesema kuwa operesheni za polisi
zimeuwa watu 750, lakini vifo vingine bado vinafayiwa uchunguzi.
Rais Duterte alishinda urais akiwa
na sera zake za msimamo mkali za kutokomeza biashara ya dawa za
kulevya.
Rais wa Philippine Rodrigo Duterte

No comments :
Post a Comment