Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema,
(kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha
Jeshi la Magereza Ukonga jijini
Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la
Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na
Judo.
Akikabidhi
vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko
huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi
za serikali katika kuinua michezo nchini.
“Nyinyi
mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, tunayo
furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza majukumu mazito
ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya lakini pia kuinua
vipaji vyenu,” alisema na kuongeza,
“Nichukue fursa hii kuwahamasisha mjiunge na
PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha
maisha yenu kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi
na kamwe hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi.
Akipokea
vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha
Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari,
aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha
wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya kiuanamichezo.
Baada
ya makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika michezo ya
mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo.
Afisa Matekelezo (Compliance), wa PSPF,
George Mnasizu, (kushoto), akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya kina
ya huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa baadhi ya wanamichezo wa Jeshi la
Magereza
Njaidi akiwa na Mkuu wa Kikosi hicho,
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kikosi Maalum cha Magereza Ukonga jijini
Dar es Salaam, Rajabu Nyange Bakari, na wacheza judo wa kikosi hicho
wakiwa katika picha ya pamoja na vipeperushi vya PSPF.
Njaidi akimkabidhi sehemu ya vifaa hicho, Nahodha wa timu ya mpira wa pete (Netball), wa timu ya Magereza Ukonga, Pili Enzi
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo kocha wa soka wa timu ya Magereza, Sajenti Hassan Mulego
Njaidi akikagua timu ya soka ya
Magereza Ukonga, ambayo ilimenyana na Kikosi Maalum cha Magereza Dar es
Salaam, wakati wa bonanza hilo la michezo
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya MagerezaSoka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
Hizi ndio Gloves na flana zilizotolewa kwa wana masumbwi (ngumi)
Pambano la masumbwi likiendelea
Pambano la masumbwi likiendelea
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF,
Abdul Njaidi, akiwa na Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza jijini Dar es
Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, wakati
akitoa nasaha kwa wanamichezo kabla ya kuanza kwa bonanza hilo
Nasaha za mgeni rasmi kwa wanamichezo
Wanamichezo wakishangilia hotuba
Onyesho la Judo
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo, Kocha na Afisa Michezo wa Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, Inspekta Francis Tabu
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
Mkuu wa
Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna
Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, akizungumza jambo na maafisa wa PSPF, kutoka kulia, Afisa Matekelezo, (Compliance), George Mnasizu, Afisa Masoko, Magira Werema, Afisa Uhsuiano Mwandamizi, Abdul Njaidi, na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Maseka Kadala
|
NA JACQUILINE MRISHO - MAELEZO
HALMASHAURI
ya Manispaa ya Temeke imeandaa
operesheni kabambe katika stendi ya Mbagala ili kuhakikisha biashara zote
zinafanyika katika maeneo yaliyotengwa na yasiyohatarisha afya ya jamii.
Afisa tawala wa wilaya ya Masasi Lincoln Ben Tamba akihutubia wananchi wa Masasi mara baada ya hafla ya ufunguzi wa duka la tigo wilayani hapo ,mapema wiki iliyopita. |
Baadhi ya wafanyakazi wa duka la Tigo Masasi wakifuatilia kwa makini hafla za ufunguzi wa duka la Tigo wilaya ya Masasi mapema wiki iliyopita. |
DK.SHEIN AONANANA BALOZI MDOGO WA INDIA
JACQUELINE MENGI AUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM KWA KUKARABATI NA KUNUNU VITABU VYA MAKTABA
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kinondoni ambapo
aliwahimiza kusoma kwa bidii vitabu hivyo ili kupanua ufahamu wao zaidi
na hata kimasomo pia vitasaidia kuinua viwango vyao vya ufaulu.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maktaba ya Shule ya Msingi Kinondoni jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (katikati) pamoja na Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maktaba ya Shule ya Msingi Kinondoni jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (katikati) pamoja na Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge.
Afisa
Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda na Mkurugenzi wa Dr.
Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi kwa
pamoja wakizundua nembo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi.
Jacqueline Mengi wakipeana mikono na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Raymond Mapunda.SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI, MH. ZUBEIR AHUDHURIA MKUTANO WA CPA MAURITIUS
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid yuko nchini
Mauritius kuhudhuria Mkutano wa 47 wa Umoja wa Mabunge ya Nchi za
Jumuiya ya Madola Kanda ya Afirika (CPA African Region).
i
No comments :
Post a Comment