Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura eneo eneo la ujenzi wa mageti ya
kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016 Jijini Dar es
Salaam.
Kaimu
Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya (kulia) akitoa maelezo kwa
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
na Katibu Mkuu Wizara ya hiyo Prof Elisante Ole Gabriel kuhusu ujenzi
wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016
Jijini Dar es Salaam.
MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA NANENANE MOROROGORO
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva wakati alipotembelea Banda la Tume ya Taifa
ya Uchaguzi katika Monyesho ya Wakulima Nane mjini Morogoro Agosti 1,
2016, Kushoto ni mkewe Mary. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary (kulia kwake)wakitazama kilimo cha
mbogamboga kwa mtindo wa kilimo kichuguu wakati walipotembelea banda la
Chuo Kikuucha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye maonyeshoya Nanenane
mjini Morogoro Agosti 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama viatu vilivyotengenezwa
katika gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea banda
la Magereza katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoroo
Agosti 1, 2016, kulia ni Mratibu wa Magereza wa maonyesho hayo na Mkuu
wa Gereza la Mtego wa Simba, Oman Msekwa. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (Kulia kwake) wakatazama bwawa la
samaki na banda la kufugia bata wakati alipotembelea banda la
Magereza katika monyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1,
2016. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitazama mboga zilizokaushwa na
mtambo wa kukaushia mboga hizo katika katika maonyesho ya wakulima
Nanene nane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. (Picha na Ofisi a waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua Banda la Maonyesho la wilaya ya
Temeke kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1,
2016. Kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua Banda la Maonyesho la wilaya ya Temeke
kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016.
Kulia kwake ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,
Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidha mbalimbali zinazotokana
na zao la mronge zikiwema, dawa, mafuta na sabuni wakati alipoembelea
meza ya Bibi Salome Kaiza (kulia) kwenye banda la wilaya ya Tameke
katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro, Agosti, 1, 2016.
Kulia kwake ni Mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama matikiti maji wakati
walipotembelea meza ya Bwana Diocresty Theonesy kwenye banda la wilaya
ya Temeke katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakipokezana tikiti maji wakiwa
kwenye meza ya Bwana Diocresty Theonesy kwenye banda la Wilaya ya
Temeke katika Maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakikagua mtama uliopandwa kwenye
eneo la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika maonyesho ya wakulima
Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JPM amaliza mgogoro wa makazi Magomeni Kota
Na Jonas Kamaleki, MAELEZO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemaliza mgogoro wa makazi wa Magomeni Kota uliodumu kwa kipindi kirefu.
Hayo yamesbainishwa leo jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.
William Lukuvi wakati akiongea na Kamati ya Mgogoro wa Makazi ya
Magomeni Kota mbele ya waandishi wa habari.
“Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli amefuta hati na mikataba yote inayohusiana na ardhi ya
yaliyokuwa makazi ya Magomeni Kota, Dar es Salaam”,alisema Lukuvi.
Kwa mujibu wa Lukuvi Rais
ameondoa umiliki wa eneo hilo toka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) na kumilikisha Serikali Kuu ambayo ndiyo itakayosimamia
ujenzi wa nyumba 644 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu kwa waliokuwa wakazi
wa Magomeni Kota.
“Tutajenga nyumba 644 na kuwauzia
kwa bei ya jengo na siyo ya ardhi ili kuwapeni unafuu katika
kununua,”alisema Lukuvi huku akishangiliwa na baadhi ya wakazi wa
Magomeni.
Aidha, Lukuvi amesema kuwa
anampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kumaliza mgogoro huu ambao umedumu
kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ameagiza timu ya wataalamu wa Wizara
kupima na kuchora michoro kwa ajili ya ujenzi.
Lukuvi amesema katika eneo hilo
zitajengwa nyumba za heshima ambazo kila moja itakuwa na vyumba vitatu
ili kukidhi mahitaji ya kifamilia kwani watu hawa wamekaa kwa miaka
takribani 50 hadi wameshapata wajukuu. Ameongeza kuwa kila mmiliki wa
nyumba hiyo atapewa hati yake hata kama nyumba hiyo itakuwa kwenye
ghorofa.
Lukuvi amesema kuwa Rais ameagiza
maeneo kama ya Magomeni Kota katika mikoa ishirini ya Tanzania Bara
nayo yatakuwa katika mfumo huo wa Magomeni. Kwa mujibu wa Lukuvi wazee
ambao wanakaa kwenye nyumba kama hizo sehemu nyingine wasiondolewe kwani
hao walikuwa watumishi wa umma hivyo Rais amesema wasibughudhiwe.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Kamati ya Mgogoro wa Makazi Magomeni Kota, George Abel ameshukur Mhe
Rais Magufuli na Wazir Lukuvi kwa kutatua mgogoro huo ambao anadai
umewasumbua sana.
Ameahidi kutoa ushirikiana kwa Serikali pindi suala la ujenzi litakapokuwa linaendelea ili kuhakikishaujenzi unaenda haraka.
Naye Wakili ambaye alikuwa
akiendesha kesi hiyo kabla ya Mhe. Rais kuingilia kati, Mhe. Twaha
Tasilima ameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.
“Rais Dkt Magufuli na Mhe. Waziri
Lukuvi ni watu wa vitendo na si maneno na kweli wanawajali wanyonge,
nawashukuru sana,”alisema Tasilima.
Uamuzi wa kurudisha eneo hilo kwenye Serikali Kuu umetolewa na Rais Magufuli tarehe 10/7/ 2016.
WAZIRI MKUU AITAKA WIZARA KUWEKA MIKAKATI YA KUENDELEZA UVUVI KATIKA KINA KIREFU CHA BAHARI
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuweka
mikakati endelevu ya kuwawezesha wananchi kuvua katika maji ya kina
kirefu cha bahari kwa kutumia meli kubwa na za kisasa ili Taifa liweze
kunufaika na rasilimali hiyo ambayo imekuwa ikichukuliwa na wavuvi wenye
vyombo vya kisasa kutoka nje ya nchi.
Aidha, amezitaka halmashauri zote
nchini ziweke mikakati na mipango ya kuifanya mito na maziwa mbalimbali
nchini kuwa na uvuvi endelevu kwa kufuatilia kwa karibu shughuli za
wavuvi na kuwaadhibu wote watakaovua kinyume na sheria.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumatatu, Agosti 01, 2016) wakati akifungua maadhimisho ya 23 ya
sherehe za maonesho ya wakulima Kanda ya Mashariki katika Uwanja wa
Mwalimu J.K Nyerere yanayofanyika katika mkoa wa Morogoro ambapo amesema
bado nchi haijaweza kutumia rasilimali hiyo kikamilifu.
Amesema halmashauri zinatakiwa
zihamasishe vijana kuunda vikundi vya kuanzisha miradi ya kufuga samaki
katika maeneo yao na wewezeshwe kupata teknolojia ya ufugaji huo.
Akizungumzia vikundi vya
wajasiariamali wanaovua katika maeneo ya bahari na maziwa alishauri
waelimishwe kuhusu namna ya kupata mikopo ya kununulia zana bora za
kisasa za uvuvi ili shughuli zao ziwe na tija.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
amesema wakulima wanatakiwa kuzingatia matumizi ya kanuni bora za
kilimo ikiwemo matumizi sahihi ya zana za kisasa, pembejeo na viuatilifu
vilivyopendekezwa na wataalam ili kufanikisha mapinduzi ya kilimo
kuelekea kilimo cha biashara.
Akizungumzia kuhusu suala la
usindikaji alisema wakati anatembelea mabanda mbalimbali alipata fursa
ya kuona teknolojia zinazoweza kutumiwa na wakulima, wafugaji na wavuvi
katika kuongeza uzalishaji bora wenye tija.
Amesema amefurahi kuona wakulima,
wafugaji na wafanyabiashara wa mazao, pembejeo na zana za kilimo wana
ari kubwa ya kushiriki katika kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo
ili kwenda sambamba na kasi ya Serikali ya kuifanya nchi kujitosheleza
kwa chakula na kuendeleza uchumi wa viwanda.
“Naamini kuwa pamoja na lengo la
kujitosheleza kwa chakula, wakulima, wafugaji na wavuvi wataongeza ari
ya uzalishaji kwa kushirikiana na sekta za umma na binafsi katika
kuvipatia viwanda vyetu malighafi na kuongeza thamani ya mazao,”
alisema.
Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu
aliziagiza halmashauri zote kuhamasisha uanzishaji na uendelezaji wa
viwanda vidogo vya kusindika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa
kushirikisha taasisi za umma na binafsi, mashirika na vikundi vya
ujasiriamali katika maeneo yao.
Akizungumzia namna Serikali
ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na
wakulima Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi watahamishiwa
katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa na wenye mifugo
michache watatengewa maeneo katika vijiji.
Awali Waziri Mkuu alitembelea
baadhi ya mabanda na maeneo ya vipando vya mazao mbali mbali yaliyoko
katika viwanja hivyo ambapo alisema ameridhishwa na juhudi zilizofanyika
katika maandalizi ya maonesho ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na
uendelezaji wa uwanja huo.
“Napenda kutoa pongezi za dhati
kwa kujenga miundombinu na nyumba za kudumu za kufanyia maonesho. Aidha,
natoa shukrani za pekee kwa Halmashauri zetu, Mashirika yetu ya Umma na
binafsi; na watu binafsi ambao wamejenga na wanaendelea kujenga majengo
mazuri na ya kudumu,” alisema.
Pia alizindua jengo la
Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na kusema kuwa uboreshaji wa viwanja
hivyo unaonesha jinsi wadau wote katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi
na ushirika wanavyotambua umuhimu wa maonesho hayo kama njia ya kuongeza
maarifa na kumuenzi mkulima, mfugaji na mvuvi kwa kutambua mchango wao
katika uchumi wa Taifa.
Kauli mbiu ya maonyesho hayo kwa
mwaka huu ni kilimo, mifugo na uvuvi ni nguzo ya maendeleo: vijana
shiriki kikamilifu (“HAPA KAZI TU”)
Mrema akutana na Madereva Bodaboda wa Kinondoni.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati)akisitiza
jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati
alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa
katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Mwenekiti wa Waendesha Bodaboda na Bajaj wilaya ya Kinondoni Bw. Almano
Mdede na kushoto ni Katibu wake Bw. George Mbwale.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema ( Mwenye Kofia
Katikati) akisisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya
kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali
wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya
Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema wakati akizungumza na madereva wa
pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza
kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo
jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa Madereva wa pikpiki Wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede akifafanua
jambo kwa madereva pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wa Mwenyekiti wa Bodi
ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati) alipowatembelea
madereva hao na kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa
katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Katibu wa
Madereva Pikipiki Wilaya hiyo Bw. George Mbwale.
Baadhi
ya madereva Pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa
Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (hayupo pichani)
alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa
katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na
Eliphace Marwa.
Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo
……………………………………………………………………………………………………
MRI, CT-Scan Zapiga Mzigo Saa 24 Muhimbili, Wagonjwa 41,101 Wapimwa
Mgonjwa
akiwa katika mashine ya MRI LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH). Pembeni ya mgonjwa ni Mtaalamu wa Mionzi, Medard Mallya
akimsaidia mgonjwa kukaa vizuri kwenye mashine hiyo.
Mtaalamu wa Mionzi, Medard Mallya akichukua picha LEO wakati mgonjwa akipimwa mgongo kwenye mashine ya MRI.
Mkuu
wa Idara ya Mionzi katika Hospitali Ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Flora
Lwakatare akifuatilia mgonjwa anavyochukuliwa vipimo LEO mchana katika
hospitali hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Na John Stephen, MNH
Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) inaendelea kutoa huduma bora hasa ya vipimo kwa wagonjwa
mbalimbali na kufanikiwa kupima wagonjwa 41,101 katika mwaka 2015/2016
kutoka wagonjwa 32,010 waliopimwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Buberwa
Aligaesha imeeleza kwamba mashine zinafanya kazi vizuri na kwamba hakuna
mashine mbovu hadi kusababisha wagonjwa kukosa huduma za vipimo.
“Hospitali inahakikisha kila
mgonjwa anayehitaji vipimo anapata na kwa gharama nafuu. Kama mashine
ilisimama kufanya kazi tangu Januari hadu Juni, 2016 ni kwa muda wa kati
ya siku moja hadi mbili kupisha matengenezo kinga,” amesema Bwana
Aligaesha katika taarifa yake aliyoitoa LEO kwa vyombo vya habari.
RAIS DKT MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU NNE MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akihutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani
kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akisalimiana na Mbunge wa Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Mdini Mhe.
Dkt Medard Kalemani baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere
wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
katika picha ya pamoja na madiwani na viongozi wa Katoro na Buseresere
baada ya kuhutubia wananchi wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani
Geita leo Agosti 1, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akimsabahi mtoto Shabani Kalemani (miezi 8) na mama yake Asha Simon
baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea
nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akilakiwa kwa furaha kijijini Bwanga wakati akielekea nyumbani kwake
Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akisalimia wananchi kijijini Bwanga wakati akielekea nyumbani kwake
Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
UGONJWA WA KIPINDUPINDU BADO UPO JIJINI DAR ES SALAAM
Hussein Makame-MAELEZO
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa
kipindupindu bado upo jijini Dar es Salaam baada ya wagonjwa wapya wanne
kugundulika katika Manispaa ya Temeke jijini hapa.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo
ofisini kwake jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa kwa waandishi
wa habari juu ya magonjwa ya milipuko na magonjwa mengine nchini.
Alisema mwenendo wa ugonjwa huo
kuanzia Julai 2016 ulikuwa wa kuridhisha kwani wagonjwa walipungua hadi
kufikia 173 kwa mwezi bila kifo kutoka wagonjwa 555 walioripotiwa mwezi
Juni 2016 na vifo vya watu saba.
“Mkoa wa Morogoro ni mkoa pekee
umekuwa ukiripoti wagonjwa wa kipindupindu kwa kipindi kirefu hadi
sasa.Vilivile mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa haujaripoti wagonjwa tangu
Mei 19, 2016 ila wiki iliyopita siku ya Jumamosi waliripotiwa wagonjwa
wapya wanne katika wilaya ya Temeke” alisema Waziri Ummy.
Alisema katika kipindi cha wiki
iliyopita idadi ya wagonjwa wa kipindupindu imeongezeka hadi wagonjwa 41
kutoka wagonjwa 30 wa wiki iliyotangulia ingawa hakuna aliyepoteza
maisha.
“Hivyo kuna dalili za kuwepo tena
ongezeko la ugonjwa wa kipindupindu jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa
haraka sana na Wizara yangu” alisema.
Alifafanua kuwa Wizara yake
imeelekeza nguvu kubwa kuendelea kuudhibiti ugonjwa huo hapa Dar es
Salaam na huko mkoani Morogoro na inafuatilia ugonjwa wa kuharisha
katika mikoa mingine ili kubaini kama kuna mgonjwa yeyote wa
kipindupindu na kuudhibiti mapema.
Aliongeza kuwa kikosi kazi cha
Taifa kinaainisha maeneo makuu ya kuyafanyia kazi mkoani Morogoro ambapo
yatajumuisha elimu kwa jamii, uvumbuzi wa namna gani ya kupatikana maji
safi na salama na matumizi vya vyoo bora.
Mbali na kueleza mikakati hiyo,
Waziri Ummy alisisitiza mikoa na halmashauri zote nchini kuendelea kutoa
taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu ugonjwa huo ili kuweza kuudhibiti
endapo utabainika kuwepo sehemu yoyote nchini.
Alisema timu ya wataalamu kutoka
ngazi ya Taifa ilifanya tathmini mnamo Juni, 2016 na kubaini upungufu
katika utoaji taarifa katika baadhi ya mikoa na hivyo Wizara yake
inashirikiana na TAMISEMI kuhakikisha inafanyia kazi mapendekezo
yaliyotolewa.
Ugonjwa wa kipindupindu ulianza
nchini tarehe 15 Agost mwaka 2015 na hadi kufikia tarehe 31 Julai, 2016
watu 22,375 wameugua na kati yao wagonjwa 345 walipoteza maisha.
Watu 14 wafariki kwa ugonjwa unaosababishwa na sumukuvu
Hussein Makame-MAELEZO
Watu 14 wamefariki dunia katika
wilaya za Chemba mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara kutokana na
ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama ‘Aflatoxicosis’ unaosababishwa na
sumu kuvu (Aflatoxins) kwenye nafaka iliyoharibika.
Hayo yamesema na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari juu ya magonjwa ya milipuko na magonjwa
mengine leo jijini Dar es Salaam.
“Ugonjwa uliosababishwa na sumu
kuvu (Aflatoxins) uliripotiwa kwa mara ya kwanza tarehe 13 Juni, 2016
katika wilaya za Chemba mkoani Dodoma na baadaye mkoani Manyara katika
wilaya ya Kiteteo” alisema Waziri Ummy na kuongeza kuwa:
“Wagonjwa walikuwa na dalili za
kuumwa tumbo, kuharisha, kutapika, tumbo kuvimba na kuwa manjano sehemu
mbalimbali za mwili ambayo inaashiria kuathirika kwa ini”
Alisema mbali na vifo hivyo, hadi
kufikia Julai 31 mwaka huu wagonjwa 54 waliripotiwa kuugua ugonjwa hu
huku wagonjwa wanne wakilazwa kutokana na kuugua.
“Hadi kufikia tarehe 31, Juni
2016 kulikuwa na wagonjwa 54 na watu 14 walipoteza maisha kutokana na
ugonjwa huo.Aidha katika wiki iliyopita aliripotiwa mgonjwa mmoja mpya
kutoka wilaya ya Kondoa” alisema Waziri Ummy na kufafanua kuwa:
“Jumla ya wagonjwa waliolazwa
wodini ni wanne kati yao mmoja yupo Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na
watatu wapo katika Hospitali ya Kondoa”
Waziri Ummy alitaja wilaya
zilizoripoti wagonjwa hao na idadi ya wagonjwa kuwa ni wilaya ya Chemba
wagonjwa 38, Kondoa wagonjwa tisa , Kiteto wagonjwa watatu, Chamwino
wagonjwa wawili na Dodoma Manispaa mgonjwa mmoja.
“Vijiji vilivyoathirika zaidi na
ugonjwa huo ni kutoka wilaya ya Chemba ambavyo ni Kinkima, Itolwa,
Mwailanje na katika wilaya ya Kondoa ni kijijini cha Ubembeni” alisema
Waziri Ummy.
Hivyo, aliitoa hofu familia
iliyopoteza watu wanne katika kijiji cha Mwaikuzabe na kusema vifo hivyo
havihusiani na uchawi au kuwekewa sumu bali ni chakula cha siku ile
kilithibitika kwamba kilikuwa na sumukuvu.
Kufuatia athari hizo Serikali
itafanya uchunguzi wa kina katika wilaya kumi za Chemba, Kondoa,
Chamwino na Kiteto na wilaya nyingine za mikoa ya Sindida, Dodoma na
Manyara zinazopakana na wilaya hizo.
Alisema uchunguzi huo unalenga
kubaini hali ya usalama wa vyakula vinavyotumiwa na jamii ili kuzuia
kuenea kwa ugonjwa huo na kuwaathiri wananchi wengi zaidi wanaoishi
katika wilaya hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Taifa wa Afya wa Wizara hiyo Dkt. Fausta Mosha alisema wizara imeandaa
vipepereshi vyenye maelekezo yanayotoa elimu juu ya kijikinga kwa
kuandaa chakula kuanzia hatua ya uvunaji shambani hadi wakati wa kula.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa
Serikali Dkt. Otilia Gowelle alisema njia bora ya kupambana na ugonjwa
huo ni kuukinga kwa kuhakikisha sumu kuvu haizalishwi kutoka kwenye
nafaka.
Akifafanua kuhusu udhibiti,
Waziri Ummy alisema wanashirikiana na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi
kutoa elimu kwa wananchi juu ya njia sahihi ya uhifadhi na uandaaji wa
chakula utakaosaidia kupunguza kiasi cha sumukuvu kwa nafaka ambazo
hazijaharibika sana.
“Njia hizi ni pamoja na kuhifadhi
nafaka zilizokauka vizuri na kuchambua nafaka zilizoharibika
(zilizooza, kuvunjika, zilizobadilika rangi), kukoboa mahindi kabla ya
kusaga au kuacha kutumia nafaka zitakazoonekana kuharibika rangi”
alisema.
Waziri Ummy alisisitiza Serikali
kuendelea kuimarisha mikakati ya kitaifa ya kupunguza uchafuzi wa
sumukuvu katika vyakula, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa kupima
sumukuvu katika damu na choo kidogo miongoni mwa taasisi za ndani ya
nchi.
Inaelezwa kuwa ugojwa
wa‘Aflatoxicosis’unaosababishwa na sumu kuvu (Aflatoxins) kwenye nafaka
uliwahi kutokea nchini Kenya mwaka 2004 na kusababisha vifo vya zaida ya
watu 100 huku wengine 200 waliathirika.
Viwanda vya TBL Group vyashinda tuzo ya Kimataifa ya Usalama na Afya
Wakipata burudani ya muziki kusheherekea mafanikio hayo
………………………………………………………………………………………….
Viwanda cha kutengeneza vinywaji
vya TBL Dar es Salaam na TBL Mbeya vimepata tuzo ya utekelezaji kanuni
za Usalama na Afya mahali pa kazi kutoka shirikisho la kimataifa la
kusimamia masuala ya usalama mahali pa kazi lenye makao makuu nchini
Afrika ya Kusini lijulikanalo kama National Occupational Safety
Association (NOSA).
Tuzo hii ambayo viwanda vya TBL
Group vya Mbeya,Mwanza na Dar es Salaam vimeipata mfululizo imekuwa
ikitolewa kutokana na kukidhi viwango vya kimataifa vya utekelezaji
kanuni za afya,usafi na usalama mahali pa kazi ambapo wataalamu kutoka
taasisi ya NOSA wamekuwa wakija nchini kufanya ukaguzi kwenye viwanda
vyake na vimekuwa vikipata alama ya kufanya vizuri kwenye kiwango cha
nyota nne na nyota tano.
Akiongea wakati wa hafla ya
kusherehekea tuzo hiyo mwishoni iliyofanyika katika kiwanda cha
Ilala,Meneja wa kiwanda cha TBL cha Dar es Salaam,Calvin Martin alisema
kuwa kampuni inajivunia kuendelea kufanya vizuri katika suala la Usalama
na Afya mahali pa kazi ambapo mwaka huu imeshinda kwa kiwango cha nyota
tano ambacho ni kiwango cha ufanisi cha hali ya juu
“Tunayo sababu ya kusherehekea
kupata tuzo hii tena katika kipindi cha mwaka huu kwa kuwa
inadhihirisha kuwa kampuni inajali suala la usalama na afya kwa
wafanyakazi na hili ni jambo la msingi kwa kuwa usalama na Afya
ukikosekana mazingira yetu ya kufanyia kazi yatakuwa hatarini na
ufanisi hautakuwepo”.Alisema.
Aliwapongeza wafanyakazi wote kwa
jinsi wanavyoshiriki kuzingatia kanuni na miongozo inayowekwa na
kampuni hali ambayo inachangia kuleta mafanikio na kuvifanya viwanda
vilivyopo chini ya TBL Group kuongoza kufanya vizuri na kuwa mfano wa
kuigwa na viwanda vingine nchini.
Kwa upande wake Meneja wa Usalama
na Afya kwa TBL,Renatus Nyanda,amesema kuwa kampuni imeweka mikakati
kuhakikisha viwanda vyake vyote vinatekeleza kanuni za Afya na Usalama
kwa viwango vya kimataifa na ndio maana inaendelea kupata tuzo hizi za
Usalama kuazia zinazotolewa na taasisi za hapa nchini na nje ya nchi
“Leo tunaposheherekea kupata tuzo hii wenzetu wa Mbeya nao
wanasheherekea na ukaguzi unaendelea katika viwanda vingine”.Alisema
Alitoa wito kwa wafanyakazi wote
wa viwanda vya TBL Group kuendelea kutekeleza miongozo mbalimbali ya
utendaji wenye kuleta ufanisi ili waendelee kuwa kioo hususani katika
suala hili la usalama na Afya kwa kuwa linawagusa moja kwa moja katika
maisha yao ya kila siku.
KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI NA BALOZI WA ITALIA WAKIKAGUA RAMANI YA BARABARA
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala
ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga kushoto akimuonyesha Balozi wa
Italia Bwana Roberto Mengoni baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa
kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala
ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana
Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa
kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni
Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala
ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana
Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa
kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni
Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala
ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana
Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa
kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni
Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA GGM KUTOA UAMUZI
Afisa
Madini wa Geita, Fabian Mshai (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), namna
ambavyo Ofisi yake ilitekeleza maagizo aliyoyatoa kwao kuhusu malalamiko
ya baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita
(GGM) likiwemo suala la mipasuko ya nyumba zao. Wengine pichani ni
maafisa kutoka Wizarani.
Baadhi
ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani),
wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Geita na wawakilishi
wa wananchi kuhusu ripoti ya wataalam wa mipasuko kutoka Wakala wa
Jiolojia Tanzania (GST) juu ya chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba
na majengo yaliyo karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani akizungumza na
wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani kuhusu
uamuzi wa Serikali kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na baadhi
ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwa
shughuli zinazoendeshwa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna mbalimbali.
Mbunge
wa Viti Maalum Geita (CHADEMA), Upendo Peneza, akizungumza wakati wa
kikao baina ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani na
wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani husika
kuhusu malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaoishi
jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwamba shughuli zinazofanywa
na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna mbalimbali.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati) akitoa
maagizo mbalimbali kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuhusu malalamiko
ya baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi huo kuwa shughuli
zinazofanywa na Mgodi zinawaathiri kwa namna mbalimbali. Waliokaa Kulia
ni viongozi kutoka GGM. Kushoto ni baadhi ya wawakilishi wa wananchi wa
Geita wakiwamo wabunge na madiwani na Maafisa wa Wizara ya Nishati na
Madini.
…………………………………………………………………………………………………..
Na Veronica Simba – GEITA
Serikali imetoa siku 30 kwa Mgodi
wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwalipa fidia wananchi wanaoishi ndani ya
eneo la leseni ya Mgodi huo au kuwaruhusu rasmi waendelee kuishi humo na
kufanya shughuli za kiuchumi.
Sambamba na agizo hilo, pia
Serikali imeupa Mgodi huo siku 14 kuziba Tuta lililopasuka ambalo huzuia
maji machafu kutoka Mgodini yasiende katika makazi ya wananchi.
Aidha, kufuatia taarifa
iliyowasilishwa na timu ya wataalam wa mitetemo kutoka Wakala wa
Jiolojia Tanzania (GST), baada ya kukamilisha kazi waliyopewa kutafiti
chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba za wananchi na majengo
mbalimbali yaliyo jirani na Mgodi wa GGM, Serikali imeagiza timu hiyo
kufanya tathmini maalum ya idadi ya waathirika.
Iliagizwa kazi hiyo ifanyike kwa
kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Maafa na Kitengo
cha Mazingira pamoja na uongozi kuanzia ngazi za vijiji mpaka madiwani
na wabunge husika kwa muda wa siku Saba tu kuanzia tarehe 29 mwezi huu
na kuiwasilisha serikalini ili hatua stahiki zichukuliwe.
Maagizo hayo yalitolewa hivi
karibuni mjini Geita na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard
Kalemani katika kikao chake kilichomshirikisha Mkuu wa Mkoa wa Geita na
wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani.
Dkt Kalemani alisema kuwa maagizo
hayo ni kufuatia maelekezo aliyoyatoa mapema mwezi Februari mwaka huu
alipotembelea mkoani humo na kusikiliza kero za wananchi wa vitongoji
vya Katoma na Nyamalembo. Alisema maagizo hayo yasipotekelezwa ipasavyo
hatua kali za kisheria zitachukuliwa, chini ya sheria ya madini na
sheria nyingine za nchi.
Akifafanua zaidi kuhusu masuala
hayo yaliyosababisha Serikali kufikia hatua husika, Naibu Waziri alisema
kuwa mwezi Februari alipotembelea Geita, wananchi walieleza kero kubwa
walizokuwa nazo kuwa ni baadhi ya nyumba zao kupasuka kiasi cha kutoweza
kukalika na nyingine kukalika lakini zimeharibika kutokana na ulipuaji
wa baruti (blasting) wa Mgodi wa GGM.
Malalamiko mengine yalihusu
wananchi ambao wanaendelea kuwa na makazi ndani ya eneo la leseni ya
GGM, ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba 196. 7 ambao walikuwa
wanadai fidia ili waondoke katika eneo husika au waendelee kubaki na
kufanya shughuli zao za maendeleo.
Pia, baadhi ya wananchi wanaoishi
karibu na Mgodi na hasa maeneo ya chini ya Mgodi, walilalamikia maji
machafu ambayo yalikuwa yanakingwa na tuta ambalo lilikuwa limebomoka na
kuruhusu maji kutiririka kuelekea kwenye makazi yao na hivyo kuwepo
uwezekano wa kuathiri afya zao. Walitaka hatua madhubuti zichukuliwe
kuzuia mtiririko huo wa maji.
Alisema kuwa, baada ya kusikiliza
maelezo ya pande zote mbili, kwa suala la mipasuko, aliunda timu ya
wataalam wa Serikali kutoka GST na kuiagiza kufanya utafiti wa kisayansi
ili kubaini chanzo cha mipasuko husika kwa kushirikiana na wawakilishi
wa wananchi wa maeneo hayo.
Timu hiyo ilikamilisha kazi hiyo
na kukabidhi taarifa yake kwa Serikali mwezi Julai mwaka huu ambapo
ilibainisha vyanzo vikuu viwili vya mipasuko hiyo kuwa ni udhaifu wa
majengo yaliyoathirika lakini pia milipuko inayofanywa na GGM hasa ya
miaka ya nyuma hususan kuanzia mwaka 2007 hadi 2010 ambayo ilikuwa na
kipimo cha juu cha mitetemo kinachofikia 57.
Kuhusu wananchi wanaoishi kwenye
eneo la leseni, Dkt Kalemani alisema kuwa alimwagiza Afisa Madini wa
Geita kuwaandikia GGM ili wathibitishe kwa maandishi kati ya kuwaondoa
wananchi wale kwa kuwafidia kama eneo hilo lilivyo kwenye leseni yao au
kuwaruhusu waendelee kuishi na kufanya shughuli za maendeleo, jambo
ambalo Mgodi haukutekeleza badala yake walisema wananchi hao ni
wavamizi.
Aidha, kuhusu suala la Tuta,
Naibu Waziri alieleza kuwa, aliagiza lizibwe mara moja ili kuepusha
madhara ambayo yangeweza kujitokeza kama maji yangeendelea kutiririka
kuelekea kwenye makazi ya wananchi, ambalo pia halijatekelezwa hadi
sasa.
“Ni kutokana na hali hiyo, sasa
Serikali tumeona tutoe maagizo ya mwisho ili yatekelezwe na
yasipotekelezwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa.”
Naibu Waziri alisema kuwa
Serikali haina nia mbaya kwa Mgodi husika isipokuwa ni wajibu wa
Serikali kuhakikisha pia sheria zinafuatwa ili pande zote zipate haki
stahiki.
“Tunapenda sana wawekezaji muwekeze kwa sababu ndiyo mnatupa ajira, mnalipa mirabaha na kodi lakini lazima tuzingatie sheria.”
Dkt Kalemani alizitaka Mamlaka zinazohusika kusimamia zoezi hilo kikamilifu.
MPANGO WA CHANDARUA KLINIKI WAWAFIKIA MWANZA
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha, akimkabidhi Chandarua kwa mtoto Mwasiti Abdallah(miezi 9) aliyebebwa na Mama yake Geni Elias,kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Malaria ujulikanaao kama Chandarua Kliniki,uliofanyika mkoani Mwanza kwa ushirikiano wa serikali na USAID.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha,akimkabidhi chandarua mama mjamzito mkazi wa Mkolani jijini Mwanza Elizabeth Edward, kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Malaria iitwayo Chandarua Kliniki ulioganyika mkoani Mwanza.mradi huo wa chandarua kliniki unatekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali.
Msanii wa muziki wa taarabu Khadija Kopa, akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana Malaria ujulikanao kama chandarua kliniki unaotekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali, uzinduzi ulifanyika jijini
Mwanza jana
Msanii wa muziki wa taarabu Khadija Kopa, akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana Malaria ujulikanao kama chandarua kliniki unaotekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali, uzinduzi ulifanyika jijini Mwanza jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mo Music, akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Malaria Chandarua Kliniki unaotekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali uliofanyika jijini Mwanza jana.
Mpango wa Chandarua Kliniki wagawa vyandarua mkoani Mwanza.
Malaria yapungua mkoani mwanza
Malaria yapungua mkoani mwanza
Mpango wa ugawaji wa vyandarua
unaojulikana kama CHANDARUA KILINIKI ulioanzishwa na serikali ya
Marekani kupitia shirika la USAID umewafikia wananchi wa Mwanza mwishoni
mwa wiki ikiwa lengo lake ni kuendeleza dhamira yake yakupambana na
malaria nchini hasa kwa Mama wajawazito na watoto.
Akitoa taarifa, wakati wa
utambulisho wa mpango na ugawaji vyandarua kupitia kliniki ya wajawazito
na watoto,Mratibu wa Malaria mkoa wa Mwanza Dk Saula Baichumila alisema
Jumla ya wagonjwa 235 wa Malaria katika Mkoa wa Mwanza wamepoteza
maisha kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu
ambapo vifo 121 sawa na asilimia 51.5 ni vya watoto chini ya miaka
mitano.
“Kutokana na vifo hivyo
halmashauri ya Sengerema inaongoza kwa asilimia 27.6, Magu 20.4, Ukerwe
14.5, Nyamagana 11.9, Misungwi 11.1, Kwimba 8.5, Buchosa 3.4 na Ilemela
2.6,” alisema Dk Baichumila
Alisema mkoa umeendelea kupambana
na ugonjwa huo kwa kushirikiana wadau mbalimbali ambapo kumekuwa na
matokeo mazuri kwa ugonjwa huo kupungua hasa toka waliposhirikiana na
USAID kupitia mpango wa CHANDARUA KLININKI mkoani Mwanza hadi sasa jumla
ya vyandarua 142,360 tayari vimesambazwa kupitia vituo vya kutolea
huduma za afya mkoani hapo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza John Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Marry Onesmo,
alisema maambukizi ya ugonjwa wa Malaria mkoani hapo yamepungua kutoka
asilimia 19.1 ya mwaka 2011/12 hadi kufikia asilimia 15.1 mwaka2015/16.
Alisema lengo la mpango huo ni
kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano
vinavyosababishwa na malaria.Alisema takwimu za kitaifa za mwaka 2012
zinaonyesha kuwa kila vizazi hai 1000, watoto 54 hupoteza maisha huku
malaria ikiongoza kuchangia vifo hivyo, huku kila vizazi hai 100,000
wajawazito 432 hupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Mpango wa chandarua kliniki
unatekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks ambao ni mradi wa
miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji na
matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu kwa kushirikikiana
na serikali ambapo wamejiweke lengo kuwa hadi kufikia mwaka 2016
kitaifa iwe imefikia asilimia 6 na mwaka 2020 iwe asilimia 1 kutoka
asilimia 9 ya sasa.
MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI AKABIDHI MADAWATI 537 NA VITABU KWA UONGOZI WA HALMASHAURI
Baadhi
ya walimu,madiwani, watendaji wa serikali wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya kumalizika kwa halfa fupi ya ugawaji wa madawati pamoja
na vitabu sherehe zilizofanyika kwenye shule ya sekondari Kilinaga
langa.
Mbunge
wa jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Juma wa kulia akimkabidhi madawati
537 Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibaha vijijini Mansouri Kisebengo
katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya sekondari
kilanga langa(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
………………………………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WANAFUNZI wa shule za msingi na
sekondari katika halmashauri ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani
waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya uhaba wa madawati na viti na
kusababisha baadhi yao kuwa tabia ya utoro kwa sasa wameanza kunufaika
na agizo la Rais Dr.John Magufuli la kutaka wanafunzi wote nchini
kuhakikisha wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati.
Agizo hilo la Rais
limetekelezwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa
kupitia kupitia fedha ambazo zimepatikana kutokana na kubana matumizi
yasiyo ya lazima katika ofisi yake kwa lengo la kuweza kusaidia katika
kuboresha sekta ya elimu.
Akikabidhi jumla ya madawati
537 Mbunge wa Jimbo hilo kwa uongozi wa halmashauri ya kibaha vijijini
katika halfa fupi zilizofanyika katika shule ya sekondari kilangalanga
iliyopo Mlandizi, amesema kwamba ametoa madawati hao pamoja na vitabu
kwa lengo la kuweza kupunguza kero na kuondokana na adha ambayo
walikuwa wanaipata wanafunzi wa jimbo lake katika siku za nyuma.
Kwa upande wake Afisa elimu
katika halmashauri ya kibaha vijijini Coskansia Mafuru amebainisha
kwamba awali kabla ya agizo la Rais walikuwa wana upungufu wa madawati
1923 kwa shule za msingi, hivyo msaada huo utaweza kumaliza changamoto
zilizokuwa zikiwakabili na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Alisema kwamba kukamilisha
agizo ambalo limetolewa na rais litaweza kuwa ni mkombozi mkubwa sana
kwa wanafunzi na wataweza kuongeza kasi ya ufaulu kwani hapo awali
walikuwa wanasoma katika mazingira ambayo sio rafiki kwao na wengine
kusoma wakiwa wamekaa chini.
“Katika kukamilisha zoezi hili
na agizo lililotolewa na Rais kuhakikisha kwamba tunafanya kila jitihada
ili kuweza kuhakikisha wote wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati na
sio chini hivyo madawati hayo yametokana na kubana matumizi mbali mbali
katika ofisi ya Mbunge hivyo nina imani ni moja ya hatua nzuri katika
kuendelea kuboresha sekta ya elimu katika jimbo langu,”alisema Jumaa.
Pia alisema kwamba pamoja na
agioz hilo pia ataendelea kujitahidi kushirikiana na wa madiwani wote
katika halmashauri ya Kibaha vijiji pamoja na wadau wengine ili kuweza
kuendeleza kutoa sapoti katika kununua mahitaji mengine muhimu ikiwemo
vitabu ambavyo viyaweza kuwapa fursa wanafunzi kuweza kujisomea.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari
Kilangalanga Albert Mabiki, pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya
Kibaha vijijini Mansouri Kisebengo hapa wanazungumza changamoto
zilizokuwa zinawakabili wanafunzi pamoja na kushindwa kufanya vizuri
kutokana na kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wanafunzi pamoja na hali ya
kuwepo kwa utoro.
“Ni kweli changamoto ya watoto
wetu walikuwa wanasoma katika mazingira ya mlundikano, na wakati
mwingine baadhi ya wanafunzi wanakuwa ni watoro hawafiki shuleni nah ii
ni kutokana na kutokuwepo kwa madawati na viti vya kutosha lakini kwa
hali hii na agizo la Rais wetu hakika kwa sasa hata huu utoro
utamalizika katika baadhi ya maeneo.
MADAWATI hayo pamoja na vitabu
ambayo vimetolewa na ofisi ya Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini
vimegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 ambapo kata zote
14 ambapo kuna shule za msingi na sekondari zimeweza kupatiwa mgao huo
kwa baadhi ya shulezenye mahitaji makubwa kwa ajili ya kuweza
kutekeleza agizo lililotolewa na Rais.
Haki Madini waendesha mdahalo wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini Simanjiro.
Mkurugenzi
wa Shirika la Haki Madini, Amani Mustafa Mhinda akizungumzia juu ya
ugatuzi na ugatuaji wa madaraka kwa wadau wa madini ya Tanzanite wa Mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, katika mdahalo wa
siku mbili wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini unaofanyika
Mirerani na kuandaliwa na shirika hilo.
Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Albert
Msole (katikati), Diwani wa Kata ya Mirerani Yohana Onyango, (kushoto)
na Mwenyekiti wa mtaa wa Twiga Anthony Musiba, wakifuatilia mdahalo siku
mbili wa wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini, juu ya
mpango wa uhamasishaji na uwazi katika katika mapato ya madini, gesi
asilia na mafuta unaonyika Mji mdogo wa Mirerani na kuandaliwa na
shirika la Haki Madini.
Wadau
wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara, wakifuatilia mdahalo wa siku mbili wa maendeleo ya
uchumi na uwekezaji kwenye madini uliondaliwa na shirika la Haki Madini.
Ali Kiba kupamba shamrashamra za tamasha la chaneli ya StarTimes Kiswahili
Mkurugenzi
Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li (wa
pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya
Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016
kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
msanii Ali Kiba ambaye atakuwepo kutumbuiza na kutoka kulia ni Msanii
Madee pamoja na Meneja Mauzo wa Huawei, Bw. Zhang Heng, ambao ndio
wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC
FESTIVAL.
Msanii
wa muziki wa bongo flava Ali Kiba (katikati) akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea
miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku
ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini
Dar es Salaam. Wakimsikiliza kwa makini kulia ni Msaidizi wa Masoko na
Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li na kushoto ni Meneja wa
chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian. Huawei ndio wadhamini wakuu
wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Msanii
wa bongo flava kutoka kundi la TipTop Connenction lenye maskani yake
Manzese, Madee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya
Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016
kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Huawei ndio
wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC
FESTIVAL.
Msanii
wa kizazi kipya Bi. Snura alimaarufu ‘Mama Majanga’ akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la
kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes
litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya
Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Msanii Madee wa
kundi la Tip Top Connection.
Msanii
wa muziki wa singeli Eskide akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya
chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi
Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian.
Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la
SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Meneja
wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la
kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes
litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya
Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Huawei ndio wadhamini wakuu wa
tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL. Kulia ni
Msanii Ali Kiba.
Kutoka
kulia ni Meneja Mauzo wa Huawei, Bw. Zhang Heng, ambao ndio wadhamini
wakuu wa tamasha la StarTimes Kiswahili linalokwenda kwa jina la
SEREBUKA MUSIC FESTIVAL, Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes
Tanzania, Bw. Damien Li, Msanii wa muziki wa bongo flava Ali Kiba na
Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian wakikata keki
kuashiria uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya
Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016
kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wasanii wakubwa nchini kulishambulia
jukwaa, wakiwemo Ali Kiba, Lady Jaydee, Yamoto Band, Madee, Juma Nature,
Snura, Stamina, Eskide (msanii wa muziki wa singeli) na bila ya kusahau
wakali wa bongo movie pia watakuwepo.
…………………………………………………………………………………………………..
Wasanii wa muziki wa Bongo Flava
Ali Kiba na Lady Jaydee wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la
kusherehekea miaka miwili tangu kuanzishwa kwa chaneli ya StarTimes
Kiswahili siku ya Jumamosi ya Agosti 13, 2016 katika viwanja vya Posta,
Kijitonyama.
Akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana na tamasha hilo Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na
Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li amesema kuwa tamasha hilo
linadhamiria kusherehekea kwa pamoja na wateja wao mafanikio
yaliyofikiwa na chaneli ya StarTimes Kiswahili katika kuonyesha vipindi
vyenye maudhui ya Kiswahili nchini Tanzania na Kenya.
“Chaneli hii mwaka huu mwezi wa
Agosti inatimiza miaka miwili tangu kuanzishwa kwake mnamo Agosti mosi
mwaka 2014. Chaneli ya StarTimes Kiswahili inaonekana katika nchi mbili
za Tanzania na Kenya na hivyo kutoa wigo mpana kwa wasanii na
watayarishaji wa vipindi hapa nchini kupata fursa ya kuonekana maeneo
hayo. Vipindi vingi katika chaneli hii huangazia masuala ya filamu,
muziki, burudani, vyakula, mitindo ya maisha na mavazi pamoja na
tamaduni za watu wa Afrika ya Mashariki hususani kwa nchi hizo mbili
ambavyo huwasilishwa kwa lugha ya Kiswahili.” Alisema Bw. Li
“Tamasha hili litahusisha
shughuli mbalimbali hususani kuangazia maudhui yanayopatikana kwenye
chaneli ya StarTimes Kiswahili lakini pia litapambwa na burudani kadhaa
kutoka kwa wasanii watakaoalikwa. Siku hiyo watanzania watawashuhudia
wasanii wakubwa wa muziki wa bongo flava jukwaani kama vile Ali Kiba,
Lady Jaydee, Juma Nature, Madee, Yamoto Band, Snura na Stamina. Pia
kutakuwepo na wasanii mashuhuri kutoka katika tasnia ya bongo movie
ambao filamu zao zinaonekana kupitia chaneli hii kama vile Wema Sepetu,
JB, Steve Nyerere na Ray Kigosi.” Aliongezea Bw. Li
Chaneli ya StarTimes Kiswahili
inapatikana katika visimbuzi vyote viwili vya StarTimes yaani cha
antenna kuazia kifurushi cha NYOTA kwa shilingi 6000/- na cha dishi
kuanzia kifurushi cha NYOTA PLUS kwa shilingi 8000/- kama malipo ya
mwezi. Kampuni hiyo inajivunia kuwa ya kipekee nchini Tanzania kwa kutoa
matangazo bora ya dijitali kwa gharama nafuu ambayo kila mtu anaweza
kuimudu.
“Ningependa kutoa wito kwa wateja
wa StarTimes na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika
tamasha hili litakalofanyika siku ya Jumamosi ya Agosti 13 mwaka huu
pale viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Tiketi
zitapatikana kwa bei ya kawaida kabisa ya kuanzia shilingi 5000/- na
kupatikana katika vituo vitakavyoanza kutangazwa kwa njia mbalimbali.
Tamasha hili ni maalumu kwa ajili ya kuwashukuru watanzania kwa kuipokea
vizuri chaneli hii na kuifanya kuwa chaguo lao kubwa pindi watazamapo
luninga, hivyo naomba wajitokeze kwa wingi.” Alimalizia Bw. Li
Naye kwa upande wake msanii wa
bongo flava Ali Kiba akizungumza mbele ya waandishi wa habari amewaahidi
makubwa wateja wa StarTimes na watanzania watakaohudhuria siku hiyo
kuwa watapata burudani ya aina yake.
“Kwanza kabisa ningependa kutoa
pongezi za dhati kwa kampuni ya StarTimes kwa kutambua mchango wa lugha
ya Kiswahili na kuikuza miongoni mwa nchi wanazofanya biashara. Hii ni
fursa ya kipekee kwa wasanii na watayarishaji wa kitanzania kuweza
kupanua wigo wa kazi zao na kuweza kuonekana sehemu zingine. Kusema
ukweli hapo awali wakati matangazo ya dijitali yanaingia nchini sikuweza
kuiona fursa hii lakini sasa ninaona kazi za wasanii wetu zinaonekana
na kutambulika kimataifa.” Alisema Ali Kiba
“Ningependa kutoa wito kwa
StarTimes kupanua wigo zaidi wa chaneli hii ifike katika nchi zingine za
jirani kama vile Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Kongo hata Afrika ya
Kusini kwani kuna watanzania kule na waafrika ambao wanapenda kufahamu
lugha ya Kiswahili na tamaduni za waswahili wenyewe. Na mwisho kabisa
ningependa kuwaalika watanzania wote siku hiyo waweze kuhudhuria kwa
wingi kwani tamasha hili ni lao, nawaomba waje kwa wingi kusherehekea
kwa pamoja maudhui mazuri na ya kusisimua yanayopatikana ndani yake.”
Alihitimisha Ali Kiba au King Kiba kama anavyojulikana miongoni mwa
mashabiki wake
Airtel Money yaingia ubia na NMB bank kuongeza ufanisi kwa wakala wake.
Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colasso akiongea wakati wa kutambulisha
kuhusu Money airtel kuingia ushirikiano na NMB banki ili banki ya NMB
ihudumie wakala wa Airtel Money
……………………………………………………………………………………………………..
Wakala wa Airtel kupata Airtel Money salio kwenye benki ya NMB popote.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya
Airtel Money imeingia ubia na Benki ya NMB ili kutoa huduma kwa wakala
wake wanaotoa huduma za Airtel Money kujipatia huduma ya salio na pesa
taslim katika matawi ya benki hiyo popote nchini.
Akiongelea
ubia huo, Mkurugenzi wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “tunachofanya
Airtel na benki ya NMB ni mundelezo wa mikakati tuliyojiwekea ya
kuhakikisha tunaleta maendeleo katika huduma za kifedha nchini ili
wateja wetu wapate huduma za uhakika na nafuu. Pia kuwepo kwa sera bora
za udhibiti na uwekezaji itachochea wawekezaji kuendelea kuboresha na
kuweka miundombinu bora zaidi ya huduma ili kugusa mahitaji ya wateja
wengi”
Tunajisikia
fahari kuona NMB banki anakuwa nguzo muhimu ya kutoa huduma za Airtel
Money kwa kuwafikishia wakala wetu salio kila walipo ili waweze
kuhudumia wateja wetu, hii inaonyesha dhairi huduma za kifedha kwa
mtandao zinazidi kupanuka kutokana na jitihada na ubunifu wa watoa
huduma kwa lengo la kuwahakikishia wateja usalama na unafuu katika
kufanya malipo, Nina uhakika Tanzania itaendelea kukua katika swala la
huduma za fedha endapo tu kutakuwa na mahusiano ya wadau kibiashara kama
haya ya Airtel Money na Banki ya NMB”
“NMB
itahudumia wakala wetu zaidi ya 45,000 ili kuweka na kutoa salio la
Airtel Money wakati wowote katika matawi yao 160 nchi nzima, haya ni
maendeleo makubwa sana hata kwa biashara yetu”. alieleza Colaso
NMB
na Airtel inaingia Ubia kipindi ambacho Airtel Money pia imezindua
kampeni yake kabambe ya Mr Money kwa lengo la kuwafikishia wateja wake
taarifa za uhakika na unafuu katika huduma za Airtel Money. Airtel Money
imefanikiwa pia kuleta huduma pekee za mikopo isiyokuwa na maharti
magumu ya TIMIZA ambapo inawawezesha wateja na mawakala wake zaidi ya
milioni 2 kujipatia mikopo kila wakati.
DC MTATURU ATENGA SIKU YA JUMAPILI KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akielekezwa jambo na muwekezaji wa miche ya miti Wikayani humo Mr Choi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipokea maelekezo ya
namna ya kuitumia miche iliyooteshwa na muwekezaji Mr Choi
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alipata nafasi ya kukutana
na Club inayopambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na UKIMWI kwenye
Shule ya Sekondari ya Issuna
…………………………………………………………………………………………………………..
Na Mathias Canal, Singida Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu Leo amekagua miradi ya maendeleo katika kijiji cha Utaho A
ambapo inajengwa shule mpya ili kupunguza adha ya watoto kwenda umbali mrefu na kuvuka barabara ambapo pamoja na kupatiwa mafunzo ya usalama barabarani lakini bado ni Hatari kwao.
Mtaturu amewapongeza wananchi kwa kazi nzuri wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki kingu na Diwani wa Kata ya Kituntu kusimamia vyema shughuli za maendeleo na hatimaye kufanikiwa kupaua madarasa mawili na ofisi ya walimu.
Sawia na pongezi hizo Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza viongozi wote katika Wilaya hiyo kwa kusimamia ujenzi wa choo cha wanafunzi ambacho kina jumla ya matundu 12.
Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha serikali inaunga mkono juhudi za wananchi ili kuwasaidie kujenga nyumba za walimu ili kufikia Januari 2017 shule ianze kupokea wanafunzi wa darasa la kwanza.
Mkuu huyo wa Wilaya pia ametembelea vikundi viwili vilivyopo katika Kijiji cha Makyungu, kikundi cha Muungano ambacho kinatarajia kutotolesha vifaranga baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuwanunulia mashine(Equbator )kwa thamani ya shilingi 8,700,000/- na kikundi cha pili kinaitwa Wajefia kinachotarajia kutengeneza chakula cha kuku kwa kutumia mashine maalumu waliyoinunua toka Shirika la Viwanda vidogo SIDO cha Mkoani Mbeya.
Sawia na hayo Mtaturu pia amebaini Changamoto waliyonayo ikiwa ni pamoja na elimu ya kuendesha Shuguli zao kibiashara na mtaji ambapo amewapa nafasi ya kupeleka wajumbe watatu kwa kila kikundi kwenye viwanja vyanane nane mjini
Dodoma kwa ajili ya kupata mafunzo na mtaji wa shilingi milioni moja kwa ajilinya kuwasaidia kuanza ununuzi wa vifaa vya kusaga chakula cha kuku na mayai ili waanze uzalishaji wa vifaranga.
Dc Mtaturu pia amemtembelea Mr Choi raia wa Korea aliyeamua kuanzisha kitalu cha miche ya miti na matunda kwa ajili ya utunzaji wa mazingira katika kijiji cha Kimbwi na pia amewekeza katika elimu ambapo anajenga shule ya Awali hadi kidato cha Sita.
Aidha Dc Mtaturu amempongeza muwekezaji huyo na kuwaalika wawekezaji wengine kwa ajili ya kuwekeza wilayani Ikungi katika sekta mbalimbali kwani kuna ardhi ya kutosha ambapo pia amemwagiza Mkurugenzi wa Halmshauri kuwaelekeza watendaji wa Kata kwa ajili ya kuchukua miche ya miti na matunda kwa Mr Choi ambaye ameamua kuungana na serikali katika kampeni ya kutunza mazingira kwa kugawa miche bure.
“Naomba mfahamu kuwa Gharama za mashine ya kusagia chakula cha kuku ni shilingi milioni 9.1 zilizotolewa na Halmashauri na wananchi walichangia kujenga majengo” Alisema Mtaturu
Mtaturu pia amekagua ujenzi wa maabara uliokwama katika Sekondari ya Mkiwa hadi umeanza kubomoka hivyo
amemuagiza Diwani kukaa na Kamati ya maendeleo ya Kata yake kuweka mikakati ya kuwashirikisha wananchi katika Kata wapatao 2009 ili serikali iwaunge mkono kupaua na hatimaye ifikapo Januari mwakani maabara ianze kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu anatekeleza kauli ya serikali ya awamu ya tano kwa vitendo
ya Hapa Kazi Tu ambapo ametenga Siku ya Jumapili kuwa Maalumu kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo.
Katika kutembelea shughuli za maendeleo Wilayani humo pia Mtaturu alipatanafasi ya kukutana na Club inayopambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na UKIMWI kwenye Shule ya Sekondari ya Issuna ambayo kitaaluma matokeo ya kidato cha nne mwaka jana ilishika nafasi ya 10 bora.
…………………………………………………………………………………………………………..
Na Mathias Canal, Singida Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu Leo amekagua miradi ya maendeleo katika kijiji cha Utaho A
ambapo inajengwa shule mpya ili kupunguza adha ya watoto kwenda umbali mrefu na kuvuka barabara ambapo pamoja na kupatiwa mafunzo ya usalama barabarani lakini bado ni Hatari kwao.
Mtaturu amewapongeza wananchi kwa kazi nzuri wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki kingu na Diwani wa Kata ya Kituntu kusimamia vyema shughuli za maendeleo na hatimaye kufanikiwa kupaua madarasa mawili na ofisi ya walimu.
Sawia na pongezi hizo Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza viongozi wote katika Wilaya hiyo kwa kusimamia ujenzi wa choo cha wanafunzi ambacho kina jumla ya matundu 12.
Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha serikali inaunga mkono juhudi za wananchi ili kuwasaidie kujenga nyumba za walimu ili kufikia Januari 2017 shule ianze kupokea wanafunzi wa darasa la kwanza.
Mkuu huyo wa Wilaya pia ametembelea vikundi viwili vilivyopo katika Kijiji cha Makyungu, kikundi cha Muungano ambacho kinatarajia kutotolesha vifaranga baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuwanunulia mashine(Equbator )kwa thamani ya shilingi 8,700,000/- na kikundi cha pili kinaitwa Wajefia kinachotarajia kutengeneza chakula cha kuku kwa kutumia mashine maalumu waliyoinunua toka Shirika la Viwanda vidogo SIDO cha Mkoani Mbeya.
Sawia na hayo Mtaturu pia amebaini Changamoto waliyonayo ikiwa ni pamoja na elimu ya kuendesha Shuguli zao kibiashara na mtaji ambapo amewapa nafasi ya kupeleka wajumbe watatu kwa kila kikundi kwenye viwanja vyanane nane mjini
Dodoma kwa ajili ya kupata mafunzo na mtaji wa shilingi milioni moja kwa ajilinya kuwasaidia kuanza ununuzi wa vifaa vya kusaga chakula cha kuku na mayai ili waanze uzalishaji wa vifaranga.
Dc Mtaturu pia amemtembelea Mr Choi raia wa Korea aliyeamua kuanzisha kitalu cha miche ya miti na matunda kwa ajili ya utunzaji wa mazingira katika kijiji cha Kimbwi na pia amewekeza katika elimu ambapo anajenga shule ya Awali hadi kidato cha Sita.
Aidha Dc Mtaturu amempongeza muwekezaji huyo na kuwaalika wawekezaji wengine kwa ajili ya kuwekeza wilayani Ikungi katika sekta mbalimbali kwani kuna ardhi ya kutosha ambapo pia amemwagiza Mkurugenzi wa Halmshauri kuwaelekeza watendaji wa Kata kwa ajili ya kuchukua miche ya miti na matunda kwa Mr Choi ambaye ameamua kuungana na serikali katika kampeni ya kutunza mazingira kwa kugawa miche bure.
“Naomba mfahamu kuwa Gharama za mashine ya kusagia chakula cha kuku ni shilingi milioni 9.1 zilizotolewa na Halmashauri na wananchi walichangia kujenga majengo” Alisema Mtaturu
Mtaturu pia amekagua ujenzi wa maabara uliokwama katika Sekondari ya Mkiwa hadi umeanza kubomoka hivyo
amemuagiza Diwani kukaa na Kamati ya maendeleo ya Kata yake kuweka mikakati ya kuwashirikisha wananchi katika Kata wapatao 2009 ili serikali iwaunge mkono kupaua na hatimaye ifikapo Januari mwakani maabara ianze kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu anatekeleza kauli ya serikali ya awamu ya tano kwa vitendo
ya Hapa Kazi Tu ambapo ametenga Siku ya Jumapili kuwa Maalumu kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo.
Katika kutembelea shughuli za maendeleo Wilayani humo pia Mtaturu alipatanafasi ya kukutana na Club inayopambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na UKIMWI kwenye Shule ya Sekondari ya Issuna ambayo kitaaluma matokeo ya kidato cha nne mwaka jana ilishika nafasi ya 10 bora.
MSHAMA: WALIMU WALEVI NA WATORO WASILINDWE/WAFICHULIWE
Mkuu
wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama,akizungumza na walimu wakuu wa
shule za Msingi wilayani humo ambapo alitoa maagizo mbalimbali ikiwemo
kuacha kuwalinda walimu wasio na maadili kazini.Mkuu huyo anaendelea na
zoezi la kukutana na makundi mbalimbali. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKUU wa wilaya ya
Kibaha ,Assumpter Mshama ,ametoa rai kwa walimu wakuu wa shule za msingi
wilayani humo, kuwafichua walimu walevi kazini na watoro pasipo
kuwalinda ili kulinda nidhamu kazini.
Amesema wapo baadhi ya walimu wanaoshindwa kufuata maadili yao ya kazi ambapo hakuna hatua zinazochukuliwa.
Aidha Assumpter amewataka walimu hao wakuu kuacha kuwaonea haya walimu hao wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kazi.
Alitoa rai hiyo ,wakati
alipokuwa anazungumza na walimu wakuu wa shule za msingi wilayani hapa
,katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya.
Assumpter aliwaomba
wasikubali kukalia tabia hizo ikiwemo kulewa wakati wa kazi kwani kwa
walimu wataoshindwa kuwachukulia hatua wanaojihusisha na ulevi,utoro
wanaweza kujiweka katika mazingira magumu ya kazi.
Aliwaasa walimu kufanya kazi kwa wito, ari na molari ya kazi ili kuinua kiwango cha taaluma wilayani Kibaha.
“Kufanya vibaya kwa
baadhi ya shule ,kunasababishwa na changamoto mbalimbali ikiwemo walimu
kujiingiza na vitendo vya ulevi na utoro,wanakuwa kikwazo katika
kuendeleza sekta hii muhimu”
“Walimu wakuu msikubali
kuwafumbia macho walimu wa aina hiyo kwani kama mnavyosikia ngazi za
juu wanavyowatumbua, huku nako wasipokuwa makini tusiwafumbie macho,”
alisema Assumpter.
Nae afisa taaluma
halmadhauri ya wilaya hiyo, Damas Kimaro alielezea changamoto ambazo
zinasababisha kushuka katika ufaulu kitaifa kutoka nafasi ya 4 mpaka ya 9
imechangiwa na mchakato wa uchaguzi mkuu uliomalizika.
Mwalimu Uhai Legeza
,alimtaka mkuu huyo atembelee katika shule mbalimbali ili aweze kujionea
namna walimu hao wanavyofanyakazi katika mazingira magumu .
Alisema kuwa baadhi ya
walimu hukaa katika ofisi ambazo hazina thamani bora ikiwemo viti na
meza wanazotumia hazilingani na nyingi hazina ubora.
“Mkuu tembelea katika shule zetu uone viti na meza tunazotumia katika kutimiza majukumu yetu ya kazi,” alisema Legeza.
Kufuatia ombi hilo Assumpter aliahidi kutembelea shule hizo kujionea hali hiyo .
Anasema baada ya
serikali kumaliza tatizo la madawati sasa itageukia uboreshaji wa
miundombinu ya majengo ili kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka zaidi.
TANZIA: KAMISHNA MSTAAFU WA MAGEREZA EGNO KAMILIUS KOMBA AFARIKI DUNIA JIJINI DAR
Marehemu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Egno Kamilius
…………………………
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini – CGP. John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Sheria na Utawala wa Magereza – CP(Rtd) Egno Kamilius Komba kilichotokea jana Julai 31, 2016 akiwa nyumbani kwake Mvuti, Chanika Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza anatoa pole kwa Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amina.
…………………………
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini – CGP. John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Sheria na Utawala wa Magereza – CP(Rtd) Egno Kamilius Komba kilichotokea jana Julai 31, 2016 akiwa nyumbani kwake Mvuti, Chanika Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza anatoa pole kwa Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amina.
PINK RIBBON ITASHIRIKIANA NA SERIKALI KUFANYA UCHUNGUZI NA TIBA YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea
na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Pink Red Ribbon toka nchini
Marekani Bi.Celina Schocken,shirika hilo limeahidi kushirikiana na
Tanzania kwenye masuala mazima ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi
ili kuwezesha huduma kuwa endelevu,kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNAIDS
Dkt.Warren Naamara
Waziri
Ummy Mwalimu akizungumza kwenye kikao hicho,kushoto ni mkurugenzi
msaidizi wa kitengo cha afya na mtoto-wizara ya afya dkt.Georgina Msemo
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Pink Ribon Red Itinerary Bi. Celina Schocken
SERIKALI YAWASHUKURU WADAU WA MICHEZO KWA KUSHIRIKI KATIKA MAENDELEO YA MICHEZO NCHINI
Picha/Habari na Raymond Mushumbusi
Serikali
imewashukuru wadau wa michezo nchini kwa kujitokeza na kuwa mstari wa mbele kushiriki
na kudhamini michezo mbalimbali nchini.
Shukrani
hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza na wanamichezo wanaokwenda kushiriki mashindano
ya Olimpiki kwa mwaka 2016 yanayofanyika Jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.
Mhe.
Anastazia Wambura amesema kuwa wadau wa michezo wamekuwa wakishirikiana na
Serikali sio katika suala la michezo pekee hata katika habari na Sanaa na
amewapongeza kampuni ya ving’amuzi ya Multichoice Tanzania (DSTV) na Bodi ya Utalii
katika azma yao ya kuunga mkono maendeleo ya sera ya michezo nchini.
“Napenda
kuwashukuru wadau wetu Dstv na Bodi ya Utalii, nawapongeza kwa kuona fursa hii
muhimu na kuitumia kuwatia moyo wawakilishi wa nchi yetu katika michezo ya Olimpiki
kwa mwaka 2016 mueendelee kuiunga mkono Serikali katika kutekeleza sera ya
maendeleo ya Michezo ili kufikia malengo” alisema Mhe. Anastazia.
Aidha
amewataka wawakilishi wa Olimpiki kutumia fursa hii ya wadau wa michezo waliojitokeza
kuwaunga mkono ikiwemo Bodi ya Utalii kutangaza utalii wa Tanzania kwa mataifa mengine watakayo kutana nayo katika mashindano
ya Olimpiki nchini Brazil.
Kwa
upande wake Mkurungezi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.Maharage Chande
ameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa ya kushirikiana na timu ya Olimpiki
kuitangaza michezo na kuitangaza Tanzania kimataifa na kuahidi kuendelea kushirikiana
na Serikali katika kuendeleza michezo nchini.
No comments :
Post a Comment