Monday, August 29, 2016

NEWS ALERT; LOWASSA, MBOWE WATIWA MBARONI NA POLISI DAR, WANAHOJIWA NA POLISI KWA KUKIUKA AGIZO LA POLISI





ALIYEKUWA mgombea urais wa Tanzania kupitia CHADEMA mwaka 2015 akiungwa mkono na vyama vinavyounda vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wancnhi (UKAWA), Edward Lowassa, na viongiozi wa juu wa chama hicho wamekamatwa jijini Dar es Salaam alasiri hii Agosti 29, 2016.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu, wengine waliotiwa mbaroni na polisini pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dkt. Vincent Mashinji, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, (Zanzibar) na Mbunge wa Goba, John Mnyika.
Kwa mujibu wa Lissu, viongzi hao wamekamatwa wakati wakishiriki kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichokuwa kikifanyika hoteli ya Giraffe Mbezi Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Polisi ilipiga marufuku mikutano yote ya siasa iwe nje au ndani ya ukumbi.
Hata hivyo marufuku hayo ya polisi yamekuwa yakipingwa vikalina wanasiasa hao huku wakishikilia kuwa ni haki yao ya Kikatiba.
CHADEMA imeingia kwenye msuguano na polisi kufuatia kutangaza operesheni UKUTA kuanzia Septemba Mosi mwaka huu itakayofanyikanchi nzima hali ambayo kwa takriban wiki kadhaa sasa, imezua mivutano na baina ya polisi na chamahicho kikuu cha upinzani huku  rai mbalimbali kutoka kila kona, zikihimiza kufanya maridhiano ili kutuliza "joto" hilo. adi kufikia saa 12;30 jioni hii, viongozi hao walikuwa wakishikiliwa kituo kikuu cha polisi kati jijini Dar es Salaam, na hakuna Mwandishi wa habari aliyeruhusiwa kuingia kwenye kituo hicho na kuamriwa kukaa mbali na kituo.
Hali kadhalikawafuasi na wabunge wa chama hicho wamejikusanya jirani na kituo hicho cha polisi wakisubiri hatma ya viongozi wao.Habari zilizopatikana usiku huu zinasema, Viongozi hao wote wameachiwa kwa dhanana.

 Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
 Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji

No comments :

Post a Comment