Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwasili kwenye ardhi ya mji wa Mbabane nchini Swaziland tayari
kuhudhuria mkutano wa 36 wa SADC wa Wakuu wa nchi na Serikali ambao
utafanyika tarehe 29 Agosti mjini hapo.
Sehemu ya Mabinti wa Swaziland wakiimba na kucheza wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokelewa na ngoma mbali mbali mjini Mbabane nchini Swaziland.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kushoto) akizungumza na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
Phiwayinkhosi Mabuza wa Swaziland ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha
mara baada ya kuwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mfalme
Mswati III.
...............................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo kwa
ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika
mkutano huo ambao utafanyika tarehe 29 Agosti 2016 ambapo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa
nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Mkutano huo wa 36 wa SADC ni maalum kwa
wakuu wa nchi na serikali wanaounda Kamati ya siasa,ulinzi na usalama ambao watajadili
kwa kina hali ya siasa na usalama, demokrasia na maombi ya Burundi na Comoro
kwa ajili ya kujiunga na SADC.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika
msafara wake amefuatana na Waziri wa
Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Augustine
Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa
Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amina Salum
Ali.
Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa katikati akimtoka, Omar Salum kushoto na kufanikiwa kumtoka mlinda mlango wa goli la Lyon, Youthe Rostand |
MABINGWA
watetezi, Yanga SC wameanza vizuri Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya African Lyon Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Pongezi
kwa wafungaji wa mabao hayo, viungo Deus David Kaseke aliyefungua pazia kipindi cha kwanza, Simon Msuva na Juma Mahadhi.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Rajab Mrope wa Ruvuma, Mirambo
Tshikungu wa Mbeya na Janeth Balama wa Iringa, hadi mapumziko Yanga
walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na Kaseke dakika ya 18, akimalizia pasi ya winga Simon Msuva, ambaye leo alikuwa katika kiwango chake.
Donald Ngoma wa Timu ya Yanga (jezi 11)
katikati akijaribu kuwatoka mabeki ya Lyon, kulia ni Abdul Hilary na
namba 26 mgongoni ni Amani Peter
Wanachama wa Timu ya Yanga wakimpungia mikono SimonMsuva
Simon Msuva, akiwapungia mikono wanachama na wapenzi waliokuwa wakimpungia mikono katika Uwanja wa Mpira wa Taifa
Mchezo ulianzia hapa kutoka kwa Harun
Niyonzima kwa kmpatia pasi Simon Msuva kwa kupachika mpira katika nyavu
za goli la Afikan Lyon, angalia picha tatu za chini na kufanikiwa
kumtoka Kipa wa Lyon
Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa
katikati akimtoka Omar Salum kushoto na kufanikiwa kumtoka mlinda mlango
wa goli la Lyon, Youthe Rostand
Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa
katikati akimtoka, Omar Salum kushoto na kufanikiwa kumtoka mlinda
mlango wa goli la Lyon, Youthe Rostand
Simon Msuva wa Timu ya Yanga akiwa
kulia akimtoka, Omar Salum na kufanikiwa kumtoka mlinda mlango wa goli
la Lyon, Youthe
Rostand, hapa mlinda mlango akishuhudia kwa macho mpira unavyo tinga
golini, mpira uliopigwa kwa kicha na Simon Msuva katika mchezo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar
es Salaam
Simon Msuva kulia akifurahi baada ya kuipatia timu yake goli akiwa na Juma Mahadhi
Donald Ngoma akiwana Mpira
Wanachama wa Timu ya Simba wakiwa na butwaa kutoamini kinacho tokea Uwanjani hapo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Kuna
Sherehe za aina mbalimbali mkoani Mara. Leo BMG inakujuza juu ya
Shereze ya kuchinja Mbuzi ili kutengeneza supu. Hii hufanywa zaidi kwa
wanajamii wa kabila la Wakurya mkoani humo.
Sherehe
hizi hazina msimu maalumu bali hufanyika kadri familia moja na nyingine
ama mtu na mtu walivyokubaliana. Mfano mtoto kumchinjia mzazi wake
mbuzi kwa ajili ya supu (umusuri) au dada kumchinjia kaka ama mtu yeyote
kulingana na makubaliano yao ambapo inaaminika mtu akiinywa supu hiyo
husafisha tumbo.
Huchukuliwa
kama Heshima kubwa pindi sherehe za aina hii zinapofanyika katika
familia fulani ambapo ndugu, jamaa na marafiki hujumuika pamoja kama
picha zinavyoonekana katika sherehe ya Chacha Kuchenga alipoenda
kumchinjia mbuzi mdogo wake, Leah Marwa Binagi (Binti Kuchenga).
Na BMG
Supu huandaliwa
Supu hii huchemshwa kwa masaa kadhaa bila kuungwa
Muda wa kunywa supu.
Katika supu hiyo, huchanganywa damu mbichi ili kuongeza ladha
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi.
Wanyange wa Lete Raha Miss Kinondoni
2016 wakionesha moja ya shoo katika Bonanza walioandaliwa na Mdhamini
wao Mkuu Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd lililofanyika
ufukwe wa Jangwani Sea Breeze Mbezi jijini Dar es Salaam jana lenye
lengo la kuwaweka fiti kabla ya shindano lao litakalofanyikaa Septemba
mbili Hoteli ya Denfrances Sinza jijini Dar es Salaam.
Wanyange hao wakiwa na waandaaji wa shindano hilo litakalofanyika Septemba 2, 2016 Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Warembo hao wakiwa wameshika chupa za
Windhoek kinywaji kinachosambazwa na kuuzwa Mdhamini wao Mkuu Kampuni ya
Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd.
Wanyange hao wakitosti kinywaji hicho
Mratibu wa Shindano hilo, Rahmat George
ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Rahmat Entertainment iliyoandaa
shindano hilo, akizungumza na wanahabari kuhusu kukamilika kwa
maandalizi ya shindano hilo.
Mwakilishi wa Kampuni ya Mabibo, Abdallah Ngoma, akizungumzia udhamini shindano hilo na shabaha ya kuandaa bonanza hilo.
Mshauri wa shindano hilo, Boy George, akizungumza na wanahabari.
Burudani zikiendelea katika bonanza hilo.
Wanyange hao wakishiriki kucheza mpira wa mkono kwenye bonanza hilo.
Wadau wa Windhoek wakicheza soka la ufukweni katika
bonanza hilo.
Soka la ufukweni likiendelea.
Mchezo wa kuogelea ukiendelea ndani ya kiota cha Jangwani Sea Breeze huko Mbezi jijini Dar es Salaam.
Na Dotto Mwaibale
MDHAMINI Mkuu wa Lete Raha Miss Kinondoni 2016 Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd imewaandalia Bonanza wanyange wa shindano hilo ili kuwaweka fiti kuelekea shindano lenyewe litakalofanyika Septemba 2 Ukumbi wa Denfrances uliopo Sinza.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa
Kampuni hiyo, Abdallah Ngoma alisema wameamua
kuwa andalia bonaza hilo ili kuwafanya wawe fiti kabla
ya kuingia kwenye shindano lenyewe Sptemba 2.
" Katika bonaza hilo warembo hao wameweza kushiriki
mpira wa miguu, mikono na kucheza" alisema Ngoma.
Mratibu wa shindano hilo Rahmat George alisema maandalizi
yote yamekwisha kamilika ambapo warembo 20 watapanda
jukwaani kuwania nafasi ya Miss Kinondoni 2016.
Alisema kama kawaida warembo hao watapanda jukwaani
wakiwa katika vazi la ufukweni, ubunifu na kujibu maswali wata
kayoulizwa na majaji.
George ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wa
mashindano hayo kufika kupata burudani safi itakayotolewa na mwanamuziki
nguri Christian Bela na kikosi cha promosheni cha kampuni ya
Mabibo.
Na Dotto Mwaibale
MDHAMINI Mkuu wa Lete Raha Miss Kinondoni 2016 Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd imewaandalia Bonanza wanyange wa shindano hilo ili kuwaweka fiti kuelekea shindano lenyewe litakalofanyika Septemba 2 Ukumbi wa Denfrances uliopo Sinza.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa
Kampuni hiyo, Abdallah Ngoma alisema wameamua
kuwa andalia bonaza hilo ili kuwafanya wawe fiti kabla
ya kuingia kwenye shindano lenyewe Sptemba 2.
" Katika bonaza hilo warembo hao wameweza kushiriki
mpira wa miguu, mikono na kucheza" alisema Ngoma.
Mratibu wa shindano hilo Rahmat George alisema maandalizi
yote yamekwisha kamilika ambapo warembo 20 watapanda
jukwaani kuwania nafasi ya Miss Kinondoni 2016.
Alisema kama kawaida warembo hao watapanda jukwaani
wakiwa katika vazi la ufukweni, ubunifu na kujibu maswali wata
kayoulizwa na majaji.
George ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wa
mashindano hayo kufika kupata burudani safi itakayotolewa na mwanamuziki
nguri Christian Bela na kikosi cha promosheni cha kampuni ya
Mabibo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa taarifa juu ya kusimama kwa ujenzi wa Zahanati hiyo.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya ya ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsikiliza kwa
makini Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri wakati akitoa maelezo wakati wa
kikao cha serikali ya kijiji
Mkurungezi
mtendaji wa Asasi ya Fedha Jafari Selemani akisitiza jambo wakati wa
ufunguzi wa warsha iliyofanyika katika Chuo cha Kilimanjaro Insitute college na
kuwakutanisha wanavyuo zaidi ya mia 2 hapa jijini Dar es salaam ambapo
alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwa na tabia ya kuweka akiba na
kujiandaa na maisha ya uzee ambapo Moto wa asasi hiyo ni "UHURU WA
KIFEDHA NI WAJIBU WAKO " kulia kwake ni mtaalamu wa biashara na
mhamasishaji wa vijana Fasili Boniface mapema mwishoni wa wiki
iliyopita.
Mmoja wa wanachuo waliohudhuria warsha hiyo akiuliza swali kwa mwongoza Mada Musa Mashauri. |
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakisiliza kwa makini mada toka kwa Mkurungezi Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele mapema mwa wiki iliyopita. |
Mkurungezi Mtendaji wa Koncept akiongoza washiriki wa warsha hiyo kula kiapo kuwa wanaamini nguvu ya mafanikio ipo ndani yao na ni wajibu wao kutafuta fursa na kutimiza ndoto zao |
No comments :
Post a Comment