Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(katikati) akiwa kwenye mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofunguliwa leo
kwenye ukumbi wa Mandvulo uliopo Lozitha, Swaziland.
Mfalme
Mswati wa III (kushoto) akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa 36 wa
Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwenye ukumbi wa Mandvulo, Lozitha
Swaziland.
Binti akionyesha bendera ya Tanzania wakati wa kuimba shairi maalum ya ufunguzi wa mkutano wa 36 wa SADC
Wakuu
wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa
mkutano wa 36, Lozitha Swaziland.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisaini ubao wa kumbukumbu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wenye majina ya viongozi waliohudhuria
mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika Lozitha, Mbabane Swaziland.
.......................................
Mwenyekiti anayemaliza muda
wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika -SADC- ambaye pia ni Rais wa
Botswana Luteni Jenerali Dkt. Seretse Khama Ian Khama amempongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kwa
kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.
Rais huyo wa Botswana ametoa kauli hiyo ya pongezi katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika Mbabane- Swaziland ambapo Katika Mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI anawakilishwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais huyo wa Botswana
amesema ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC unaendelea
kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi.
Amesema ana Imani kubwa na Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya amani,uhuru na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa shelisheli kwamba watafanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.
Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC katika mkutano huo wameshuhudia utoaji wa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa insha na kwa wanahabari ambao wameandika habari mbalimbali kuhusu SADC ikiwemo masuala ya huduma ya maji.
Aidha Katika Mkutano huo wa 36 wa SADC viongozi wanaohudhuria watafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama ( SADC Troika)
Katika mkutano huo Wakuu wa nchi na serikali pia watapokea rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali kutoka kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kutia saini. Miongoni mwa rasimu hizo ni mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda (kushoto) akimjulia hali mwanafunzi wa Darasa la 4 wa Shule ya
Msingi ya Mount Kibo ya Mbezi Beach ya Jijini Dar es Salaam, David
Kamoga , anayepatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba, Mifupa, Upasuaji
wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Baada ya kujeruhiwa kwa
kugongwa na Gari aina ya Hiace eneo la Tegeta Namanga, kulia ni baba wa
mtoto huyo, Hudson Kamoga. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akielezea dhamira ya kuanzishwa kwa Ikungi Half Marathon ofisini kwake
Na Mathias Canal, Singida
Ni kama vile kuwa na kiu kizito kinachohitaji maji ya kunywa na kisha
maji yakakutikana kusikojulikana, ndivyo itakavyokuwa Wilayani Ikungi
Mkoani Singida mara baada ya kutangazwa mashindano ya riadha
yanayojulikana kama Ikungi Half Marathon 2016.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Jumamosi Septemba 3, 2016 katika Vijiji 101 vilivyopo Wilayani Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa
maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho
kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu
Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete
akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna
ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua
litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben
Fune
Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa
habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya
kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi.
Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum
kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea
Septemba mosi .
Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum
kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea
Septemba mosi .
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali,Mbeya .
SHIRIKA
la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua
linalotarajia kuonekana Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga
katika
wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI
ya Taifa ya Ruaha
Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya
kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction
ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Pascal Shelutete anasema kuongezeka kwa
geti la Ikoga ni fursa kubwa ya
kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu
linakivutio kikubwa cha wanyama
wa aina mbalimbali .
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema
Wilaya hiyo ina vivutio vingi, hivyo
amewataka wananchi watakaofika kuangalia
kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio
vilivyopo Wilayani humo.
Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi
majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga
Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya .
Mkuu wa Wilaya ya
Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, hii leo akifungua Maonesho
ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Maonesho hayo
yameandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini
TCCIA, yalianza Agosti 26,2016 na yanatarajiwa kufikia tamati Septemba
04,2016 katika viwanja wa Rock City Mall.
Na BMG
Mkuu wa Wilaya ya
Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, akizungumza kwenye Maonesho
ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mara, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.

Picha ya pamoja.
Wafanyabiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
wamehimizwa kuchangamkia fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo katika soko
la pamoja la nchi hizo kutokana na soko hilo kuwa na idadi kubwa ya wateja.
Akifungua maonesho ya 11 ya biashara ya Afrika Mashariki
yanayofanyika kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza,Mkuu wa mkoa wa
Mwanza John Mongela amesema soko lililopo kwenye nchi hizo lina zaidi ya wateja
milioni 140 na hivyo likitumika vizuri litatoa fursa ya kuuziana bidhaa wenyewe
kwa wenyewe.
Kwenye hotuba ya ufunguzi iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya
Ilemela Dkt.Leonard Massale,mkuu huyo wa mkoa amesema badala ya wafanyabiashara hao kutegemea masoko ya
nje yanayofikika kwa gharama kubwa,wanapaswa kuuziana bidhaa ndani ya nchi za
Afrika Mashariki na hivyo kuinua uchumi wa nchi hizo.
Aidha amewahimiza waandaaji wa maonesho hayo chemba ya
wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo nchini, TCCIA, kuyatangaza zaidi ili
yavutie makampuni mengi kutoka nchi zingine.
Katika hotuba yake Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza,
Elibariki Mmari, amesema licha ya kuandaa maonesho hayo kwa miaka 11 mfululizo
bado wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na eneo linalofaa kwa ajili ya maonesho
hayo na hivyo kulazimika kuhama mara kwa mara na kuiomba serikali kuharakisha
upimaji wa eneo la maonesho Nyamuhongolo ili kujenga majengo ya kudumu.
Maonesho ya mwaka huu yanashirikisha zaidi ya washiriki 300
kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Uganda, China na wenyeji Tanzania ambapo
kuna mabanda ya bidhaa mbalimbali pamoja na wanyama hai.
No comments :
Post a Comment