Tuesday, August 23, 2016

MAJALIWA AHUTUBI AMKUTANO WA HADHARA KIJIJI CHA MAJIMOTO, MKOANI KATAVI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati walipokutana katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu,   kwenye kijiji cha Majimoto wilayani Mlele Agosti 23, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda wakati Waziri Mkuu, alipohutubia mkutano wa hadara kwenye kijiji cha Majimoto wialayani MleleAgosti 23, 2016. Wapili kulia ni Mbunge wa Kavuu, Dkt. Pundeciana Kwembe

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitazama ngoma ya asili ya Wapimbwe wakati walipowasili kwenye uwanja wa kijiji cha Majimoto wilayani Mlele kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 23, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitazama ngoma ya asili ya Wapimbwe wakati walipowasili kwenye uwanja wa kijiji cha Majimoto wilayani Mlele kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 23, 2016. Katikati ni Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.
Wananchi wa kjiji cha Majimoto wilayani Mlele wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia huku wengine wakionyesha mabango yanayoelezea hisia zao, Agosti 23, 2016
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwiru Mkoani Mwanza wakiwa wamekalia madawati 60 waliyopewa na kampuni ya Tigo,wakati wa hafla iliyofanyika jana.


Kampuni ya Simu ya Tigo Tanzania leo  imeanzisha rasmi  mkakati wake wa nchi nzima wa kutoa huduma kwa jamii  kwa kuchangia madawati 385  yenye thamani ya shilingi milioni 64 kwa shule tisa za msingi mkoani Mwanza  ambayo  yatazinufaisha shule za msingi katika wilaya za  Ukerewe, Nyamagana, Ilemela na Sengerema wakati wa msimu wa tamasha la Fiesta 2016 mkoani Mwanza

 Mganga Mku wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) ambaye alikwenda kuitembelea hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kuangalia changamoto zinazowakabili
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akisisitiza jambo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita

 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari kutoka katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Sunshine Muslim Volunteer huku wakishirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi za Uingereza, Afrika kusini, Canada na Pakistani waliokuja kuweka kambi ya siku tano kwa ajili ya kutoa matibabu bure ya Fistula.
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF), Mussa Mbaruku ameombwa kuangalia namna ya kuweka mkakati wa kuvisaidia vituo vya afya na Zahanati zilivyopo ndani ya Jiji la Tanga ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo inayohudumia wagonjwa wa mkoa mzima.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments :

Post a Comment