Kamishna Operesheni
na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP),
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu tukio la mauaji ya askari wanne katika Benki ya CRDB Tawi la Mbande yaliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha na waandishi wakiwa bize kupata taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KUFUATIA mauaji ya askari wanne
yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa watu wanaodhaniwa ni majambazi
kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari hao kwa kutumia silaha za moto
jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka wahusika wote
kujisalimisha.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi
limehusisha tukio hilo na Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA)
kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao wamesikika
katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha wafuasi wao wawashambulie
askari wa Jeshi la Polisi.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna
Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya
(CP), wakati akizungumza waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana
ambapo pia alikiri kuwa mazoezi yanayofanywa na polisi yamelenga
kukabiliana na Ukuta.
Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia
alipiga mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata
ikifanyika kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye
mkono wa sheria.
Aidha CP Mssanzya aliwataja askari
waliouawa katika tukio hilo wakati wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761
CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni na
raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya
wote wakiwa wakazi wa Mbande.
"Katika tukio hilo majambazi ambao idadi
yao haikufahamika walifanikiwa kupora silaha mbilo aina ya MSG na
lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki hiyo kuibiwa au kuharibiwa,
ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na kusudio moja tu la
kuwashambiulia askari polisi, " alisema.
Alisema katika hali ya kushangaza baada
ya tukio hilo kuna baadhi ya watu waliandika mitandaoni kubeza na kukeji
mazoezi ya kawaida ya jeshi la polisi na wengine waliandika ujembe wa
kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa askari polisi huku wengine
wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa na polisi Srptemba1
mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari wanaoishi
uraiani na kuwarudisha kambini.
Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu wa amani nchini.
No comments :
Post a Comment