Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichoshirikisha
Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena
Lusa- Diese na ujumbe wake, pamoja na wataalam kutoka Wizara ya
Nishati na Madini.
Kutoka kushoto, Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Nishati Dk. Juliana Pallangyo na Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi
Innocent Luoga wakifuatilia mada iliyokuwa inawasilishwa na Mkurugenzi
kutoka Kampuni ya Oil of DR Kongo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo,
Giuseppe Ciccarelli (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akielezea fursa za uwekezaji kwenye
sekta ya mafuta na gesi mbele ya waandishi wa habari. Kushoto ni Waziri
wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa-
Diese.
Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Oil
of DR Kongo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Giuseppe Ciccarelli
akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya
Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese na ujumbe wake
wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao
hicho.
Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya
Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese (kushoto) akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya
Nishati na Madini. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mafuta wa
Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese (kushoto)
WATAALAMU WA TEHAMA WATAKIWA KUWA NA MAADILI.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wataalam wa
Tehama wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao
uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Prof.
Faustine Kamuzora akiongea na wataalam wa Tehama wakati wa uzinduzi wa
mkutano wa siku moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es Salaam
leo.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wanahabari
hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu
hao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Benjamin Sawe)
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia kikao hicho.
WAJUMBE WA BODI STAMICO WATEMBELEA MGODI WA TANZANITEONE
Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa
shirika la madini nchini (STAMICO) wakiwa na baadhi ya watumishi wa
kampuni ya TanzaniteOne na STAMICO walipotembelea mgodi wanaoumiliki kwa
ubia na kampuni hiyo uliopo mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara.
Wajumbe wa bodi ya shirika la madini
nchini (STAMICO) wakiwa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Balozi
Alexiander Muganda, (mwenye nguo ya rangi ya buluu) baada ya kutembelea
mgodi wanaoumiki kwa ubia na kampuni ya TanzaniteOne uliopo mji mdogo wa
Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Wajumbe bodi ya STAMICO wakipanda scip kwa ajili ya kuingia kwenye mgodi wa madini ya Tanzanite uitwao CT.
STATE GRID YA CHINA YAONESHA NIA KUWEKEZA MRADI WA UMEME WA MCHUCHUMA- MAKAMBAKO
Waziri wa Nishati na Madini
(katikati) Profesa Sospeter Muhongo akiwaeleza jambo Balozi wa China
nchini, Dkt. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake waliofika
Ofisini kwa Waziri ili kufahamu namna kampuni hiyo inavyoweza kufanya
kazi katika sekta ya Nishati nchini.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao baina
yake na Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) na
ujumbe wake waliofika Ofisini kwa Waziri ili kufahamu namna kampuni ya
State Grid ya China inavyoweza kufanya kazi katika sekta ya Nishati
nchini.
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni
ya State Grid ya China upande wa Afrika, Mingu Liu, (wa kwanza kulia
mbele) wakati akimweleza Waziri Muhongo azma ya Kampuni hiyo kuwekeza
katika Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme ya Msongo wa kV 400 Mchuchuma
hadi Makambako. Wengine wanaofuatilia ni Balozi wa China nchini Dkt. Lu
Youqing na ujumbe wake.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiangalia Makabrasha kutoka Kampuni
ya State Grid ya China ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa
ujenzi wa njia ya umeme ya Msongo wa kV 400 ya Mchuchuma hadi
Makambako.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo (katikakti) na Balozi wa China nchini Dkt. Lu
Youging (wa pili kushoto) na ujumbe wake wakifurahia jambo mara baada ya
kumalizika kwa kikao baina ya Waziri, Balozi na kampuni ya State Grid.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia avitaka Menejimenti ya Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kupitia upya mitaala na vifaa
Mwalimu wa Ufundi Ricky akionyesha baadhi ya mashine
zinazotumika kufundishia wanafuinzi wanaojiunga na chuo cha Mafunzo ya
Ufundi Stadi VETA Kipawa
Picha ya pamoja kayi ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
Prof Joyce Ndalichako akiwa na watendaji wa Chuo cha VETA Kipawa
pamoja na baadhi ya wanafunzi chuoni hapo
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)juu ya mikakati
ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda ambapo chuo cha VETA Kipawa
inajikita zaidi kutoa mafunzo yanayohusu masuala ya viwanda
Mmoja wa wanafunzi kutoka chuo
kikuu cha Mlimani waliokwenda chuoni hapo kupata mafunzo kwa vitendo juu
ya masuala ya TEHAMA Picha na Beatrice Lyimo-MAELEZO
………………………………………………………………………………………..
SERIKALI KUNUNUA RADA SITA ZA KISASA
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi
Ally Karume mara baada ya kumtembelea ofisini kwake Kisiwani Unguja.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa wakati
viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo Kisiwani Unguja. Kulia
ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Balozi Ally Karume.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Waziri wa
Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Balozi Ally (kulia) Karume wakati alipotembelea taasisi zilizochini ya
Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hiyo Mustafa Abood
Jumbe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mustapha
Abood Jumbe afafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) katika kikao kazi mjini
Unguja.
………………………………………………………………………
No comments :
Post a Comment