Mkuu
wa Kitengo cha Mikopo Rahisi, (Easy Banking), wa BancABC,Thompson
Mwasikili, (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha
benki hiyo, Joyce Malai, wakati akizindua huduma mpya ya “Mkoporahisi”,
makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Agosti 2, 2016.
BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imerahisisha upatikanaji wa
mikopo kwa wateja wake ambapo mteja wa benki hiyo ambaye ni mtumishi wa
serikali anaweza kupatiwa mkopo ndani ya masaa 48.
Na Mwandishi Wetu
BANCABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake kwani imeanza kutoa mikopo
ndani ya saa 48 kupitia huduma mpya ya ‘mkoporahisi’.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 1, 2016, makao makuu ya benki hiyo, kwenye jingo la Uhuru Hights jijini Dares
Salaam, Mkuu wa kitengo cha Easy Banking wa BancABC, Thomson Mwasikili, (pichani juu), alisema
wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serekalini ili kuhakikisha wanapata huduma hii kwa haraka.
“Kwa kupitia huduma hii ya mkoporahisi tutahakikisha kuwa wateja wetu ambao ni waajiriwa wa Serikali, wanapata mikopo
yao ndani ya saa 48 kuanzia muda ambao maombi yaliwasilishwa..tutalisimamia hili na kuhakikisha linatekelezeka,” alisema Mwasikili.
Bw. Mwasikili alisema benki yake inatoa mikopo ya hadi Tsh milioni 40 kwa riba ya kiwango cha chini
hadi asilimia 1.6 kwa mwezi ambayo ni miongoni mwa riba za chini kabisa katika soko la sasa.
“Waombaji wataweza kulipa mikopo yao kwa muda mrefu wa hadi miaka 6 na hakuna pingamizi kuhusu lini unaweza kuongeza
mkopo wako,” alisema na kuongeza kuwa muombaji ana uhuru wa kupata mkopo wa muda mfupi hata wa mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa Mwasikili, tofauti na mikopo mingine, waombaji wana uhuru wa kuchagua matumizi ya fedha kwa mfano kulipia ada, kununua gari, kukarabati nyumba, kulipia kodi na kumaliza ujenzi na benki haitamlazimisha mkopaji matumizi ya mkopo wake.
Waombaji pia watapata fursa ya kuchanganya mikopo yao yote na kuwa na mkopo mmoja kwani BancABC inaweza kununua mikopo yote hiyo na kumpunguzia mteja usumbufu.
“Endapo muombaji wa mkopo atafariki, mkopo utafidiwa kupitia bima ya mikopo na fedha kiasi cha Tsh 500,000 taslimu
zitatolewa kugharamia mazishi,” alisema
“Tunatoa rai kwa wateja wetu wote na pia wale ambao hawana akaunti na benki yetu kuchangamkia huduma hii ya mkoporahisi kwani hii ndio benki pekee ambayo inakusogeza karibu na ndoto zako , pata
mikopo ndani ya saa 48,” alisema.
Atlas Mara iliorodheshwa katika soko la
hisa la London Disemba 2013. Atlas Mara ina lengo la kujitanua na kuwa kinara
katika masuala ya kifedha katika ukanda wa sub sahara kwa kutumia uzoefu wake
na uwezo wa kukuza mitaji. Malengo yake ni kuunganisha na kukuza uwezo wa
taasisi za kifedha na pia kuendeleza uchumi katika nchi ambazo inafanya
shughuli zake.
ndani ya saa 48 kupitia huduma mpya ya ‘mkoporahisi’.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 1, 2016, makao makuu ya benki hiyo, kwenye jingo la Uhuru Hights jijini Dares
Salaam, Mkuu wa kitengo cha Easy Banking wa BancABC, Thomson Mwasikili, (pichani juu), alisema
wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serekalini ili kuhakikisha wanapata huduma hii kwa haraka.
“Kwa kupitia huduma hii ya mkoporahisi tutahakikisha kuwa wateja wetu ambao ni waajiriwa wa Serikali, wanapata mikopo
yao ndani ya saa 48 kuanzia muda ambao maombi yaliwasilishwa..tutalisimamia hili na kuhakikisha linatekelezeka,” alisema Mwasikili.
Bw. Mwasikili alisema benki yake inatoa mikopo ya hadi Tsh milioni 40 kwa riba ya kiwango cha chini
hadi asilimia 1.6 kwa mwezi ambayo ni miongoni mwa riba za chini kabisa katika soko la sasa.
“Waombaji wataweza kulipa mikopo yao kwa muda mrefu wa hadi miaka 6 na hakuna pingamizi kuhusu lini unaweza kuongeza
mkopo wako,” alisema na kuongeza kuwa muombaji ana uhuru wa kupata mkopo wa muda mfupi hata wa mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa Mwasikili, tofauti na mikopo mingine, waombaji wana uhuru wa kuchagua matumizi ya fedha kwa mfano kulipia ada, kununua gari, kukarabati nyumba, kulipia kodi na kumaliza ujenzi na benki haitamlazimisha mkopaji matumizi ya mkopo wake.
Waombaji pia watapata fursa ya kuchanganya mikopo yao yote na kuwa na mkopo mmoja kwani BancABC inaweza kununua mikopo yote hiyo na kumpunguzia mteja usumbufu.
“Endapo muombaji wa mkopo atafariki, mkopo utafidiwa kupitia bima ya mikopo na fedha kiasi cha Tsh 500,000 taslimu
zitatolewa kugharamia mazishi,” alisema
“Tunatoa rai kwa wateja wetu wote na pia wale ambao hawana akaunti na benki yetu kuchangamkia huduma hii ya mkoporahisi kwani hii ndio benki pekee ambayo inakusogeza karibu na ndoto zako , pata
mikopo ndani ya saa 48,” alisema.
Atlas Mara iliorodheshwa katika soko la
hisa la London Disemba 2013. Atlas Mara ina lengo la kujitanua na kuwa kinara
katika masuala ya kifedha katika ukanda wa sub sahara kwa kutumia uzoefu wake
na uwezo wa kukuza mitaji. Malengo yake ni kuunganisha na kukuza uwezo wa
taasisi za kifedha na pia kuendeleza uchumi katika nchi ambazo inafanya
shughuli zake.
KATIBU MKUU WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS AZUNGUMZA NA WAANDHISHI WA VYOMBO VYA FM
Katibu
Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Nd,Salum Maulid Salum (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa
vyombo mbali mbali vya Redio za FM kuhusu kongamano la Watanzania
wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika Agosti 24
mwaka huu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Nd,Salum Maulid Salum (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari wa vyombo mbali mbali vya Redio za FM kuhusu kongamano la
Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika
Agosti 24 mwaka huu (kushoto) Naibu Katibu wa Rais Nd,Marium Haji Mrisho
na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Silima Kombo Haji.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Nd,Salum Maulid Salum (kulia) alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari wa vyombo mbali mbali vya Redioza FM kuhusu kongamano la
Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora) linalotarajiwa kufanyika
Agosti 24 mwaka huu (kushoto) Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji.
[Picha na Ikulu.]
WAKALA WA UNUNUZI SERIKALINI GSPA KATIKA MAONYESHO YA NANENANE LINDI
Meneja
masoko na mauzo wa wakala wa ununuzi serikalini GPSA Hamza hasani
(wa kwanza kushoto) akitoa maelezo juu ya huduma zinazotolewa
na wakala hao kwa mteja Bi NURU CHIWAMBA aliyetembelea kwenye
banda la wakala hao kwenye maonyesho ya nanenane viwanja vya
Ngongo mkoani Lindi , (kulia ni Huseni Athumani Muhasibu wa GPSA
mkoa Lindi na katika Meneja wa GPSA Mkoa wa Lindi Mwakiselu
Mwambange )
Mashindano ya Olimpiki 2016 nchini Brazil, wawakilishi wa Tanzania kupeperusha bendera. DSTV, Bodi ya Utalii wajitokeza kuwapa nguvu.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akikabidhi bendera kwa timu ya Tanzania inayoenda kushiriki katika
mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil Agosti 1, 2016.
Mkurugenzi
Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Maharage Chande akishukuru Serikali
kwa fursa ya kuunga mkono jitihada za kuendeleza michezo wakati wa hafla
ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil
katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil Agosti 1,
2016.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano TTB Bw. Godfrey Tengeneza akitoa nasaha
zake kwa wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Olimpiki kwenda
kutangaza utalii wa Tanzania wakati wa hafla ya kuwaaga wanamichezo
wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil katika mashindano ya
Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil Agosti 1, 2016.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Zikiwa zimebaki siku chache kabla
kuanza rasmi michezo ya 31 ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro nchini
Brazil inayotarajiwa kuanza Ijumaa ya Agosti 4, 2016 katika mji wa Sao
Paulo na Rio De Jeneiro nchini Brazil wawakilishi wa Tanzania katika
michuano hiyo wamepata baraka zote kutoka kwa Serikali na kukabidhiwa
bendera ya Taifa kabla ya kwenda kuipeperusha nchini Brazil.
Akikabidhi bendera kwa timu hiyo
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia
Wambura aliwataka washiriki wanaokwenda kuiwakilisha nchi kwenye
mashindano ya Olimpiki mwaka huu huko Rio De Jeneiro nchini Brazil
kujituma na kuhakikisha wanafanya vizuri ili warudi na medali.
Mhe. Annastazia Wambura alisema
kuwa wanapokwenda kuiwakilisha waamini kuwa macho na masikio ya
watanzania wote yapo kwao kwahiyo wajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza
kuhakikisha watakapokuwa wanarejea basi waje wakiwa wamevaa medali zao.
” Mnakwenda katika mashindano ya
Olimpiki macho yote ya watanzania yapo kwenu tunategemea mkiwa mnarudi
basi tutakuja kuwapokea mkiwa na medali zenu kifuani na hilo
linawezekana kama mtajituma mkiwa na ari ya ushindi”.
Aidha Katibu Mkuu wa Kamati ya
Olimpiki Tanzania , Filbert Bayi alisema kuwa kwa mwaka huu washiriki
wamekaa kambi katika sehemu tofauti nchini na wengine wakiwa nje ya nchi
na hilo limefanikisha kuweza kujifua vyema na kujiandaa ili kuweza
kurejesha ushindi nyumbani.
Akizungumzia mara baada ya
kukabidhiwa bendera Kocha wa timu ya kuogelea Bw. Alexandra Mwaipasi
alisema kuwa wachezaji wake wameiva kwani mwanzoni walikuwa na
changamoto ya kupata mabwawa yenye viwango vinavyoendana na mashindano
hayo ili kwa matayarisho aliyowapatia wachezaji wake anahakika watarudi
na medali.
Moja ya washiriki wa mchezo wa
kuogelea katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 Magdalena Mosha
alisema kuwa amejiandaa vizuri na anaamini kwa miaka aliyoshiriki kwenye
mashindano ya Olimpiki ya Beijing na London yamempa uelewa zaidi wa
nini anatakiwa kufanya na kuyafanyia kazi mazoezi aliyoyapata nchini
Australia ili kurudi na ushindi.
Naye mmoja wa wawakilishi katika
mchezo wa Judo, Adrew Thomas alisema amejiandaa vizuri kwa ajili ya
mashindano hayo na yuko tayari kuiwakilisha Tanzania na kuleta ushindi
na pia kuitangaza Tanzania katika michezo na utalii uliopo kwa
kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini.
Kwa upande wake Sara Ramadhani
ambaye ni mwakilishi mwanamke pekee katika mshindano hayo kwa wakimbiaji
wa Marathon alisema yuko vizuri kuipeperusha bendera ya taifa na
kuitangaza Tanzania kimataifa kwa kushindana na kushinda medali hivyo
kuiletea sifa nchini.
Mmoja wa wadhamini wa safari
hiyo kampuni ya Multichoice Africa, imewataka washiriki hao kujituma
zaidi kwani watanzania wote watakuwa wanawaangalia kupitia chaneli zao
zinazopatikana kwenye kisimbuzi cha DSTV.
Katika mchango wao kwa
wawakilishi hao Kampuni ya ving’amuzi ya Dstv imetoa mchango wa
kuwakutanisha pamoja kwa kuandaa hafla ya kuwaaga wawakilishi hao ikiwa
ni moja ya kuwatia moyo waende kupambana na kushinda katika michezo
mbalimbali na kuliletea sifa taifa.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni
hiyo Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Maharage Chande alisema mwaka
huu mashindano yote yatakuwa yakioneshwa moja kwa moja kupitia channeli
za Super Sport na itawapa fursa watanzania kuwashuhudia wawakilishi wao
kwenye mashindano hayo makubwa duniani.
Bodi ya Utalii nayo haikuwa nyuma
kuwapa nguvu na morali wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya
Olimpiki kwenda kufanya vizuri katika mashindano hayo na pia kutangaza
vivutio vilivyopo nchini kwa mataifa mbalimbali yanayoshiriki mashindano
hayo kwa kuwapatia vifurushi kwa ajili ya kusambaza ujumbe kuhusu
utalii wa Tanzania.
Akitoa nasaha zake kwa
wawakilishi hao Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TTB Bw. Godfrey
Tengeneza aliwaasa wawakilishi hao kujituma kwa bidii na kutangaza nchi
kupitia michezo na pia watumie fursa hiyo kutangaza vivutio vilivyopo
Tanzania kwa kueneza habari kuhusu utalii Tanzania.
“Mtakapokuwa huko mbali na
kushiriki katika michezo muitangaze nchi yetu kwa vivutio vilivyopo
nchini ili tuzidi kupata watalii wengi kutoka duniani kote”.
Timu ya Tanzania inayoenda
kushiriki mashindano ya 31 ya Olimpiki nchini Brazil inawakilishwa na
wachezaji saba ambao ni waogeleaji wawili Magdalena Mosha anayeenda kwa
mara ya tatu kwa upande wa wanawake huku Hilal Hilal akienda kwa mara
ya kwanza kwa upande wa wanaume na wote watakuwa ni waogeleaji kwa
umbali wa mita 50.
Wengine ni Fabian Joseph, Said
Juma Makula na Alphonce Felix Simbu watakaokimbia marathon kwa wanaume
na Sara Ramadhani ambaye ni mwanamke pekee anayeiwakilisha Tanzania
katika mbio za marathon.
Na kwa upande wa mchezo wa Judo Tanzania itawakilishwa na Adrew Thomas Mulugu katika uzito wa kilogramu 73.
Katika mashindano ya Olimpiki
mwaka huu takribani M yanatarajiwa kushindana katika michezo mbalimbali
huku Marekani ikiongoza kuwa na wachezaji wengi zaidi katika mashindano
hayo ikiwa na wachezaji 550 ikifuatiwa na Brazil iliyo na wachezaji 450
na China inayowakilishwa na wachezaji 380.
MKANDARASI APEWA WIKI MBILI KURUDISHA VIFAA NA KUENDELEA NA UJENZI
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia)
akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali
Kaisi (kushoto) kuhusu uboreshwaji wa kiwanja hicho wakati alipotembelea
kiwanja hicho.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
Kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw.
Sandali Kaisi (wa kwanza kushoto) wakati alipokagua kiwanja hicho.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala-
Kanazi yenye urefu wa KM 75 alipokagua ujenzi wa barabara hiyo.
MAKALA KUHUSU FALSAFA, DHANA NA UMUHIMU WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
Historia
ya nchi yetu ni pana na ya kuvutia kwa namna ya pekee ukilinganisha na
nchi nyingi za Afrika na Duniani kote. Upekee huu unatokana na uwezo wa
kujenga hoja na uadilifu wa viongozi wetu, hasa mwasisi wa Taifa letu
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipochaguliwa kuwa mjumbe kwenye
Baraza la kikoloni la kutunga Sheria (Tanganyika Legislative Council)
mwaka 1958.
Kwa
kuwa Mwalimu alikuwa na ndoto ya kuiona Tanganyika na Afrika iliyo huru,
mwaka 1958 katika hotuba yake ya kwanza alitamka maneno ya kifalsafa
kwa wajumbe na Spika wa Baraza la kikoloni la kutunga Sheria kwa kusema
“Sisi tunataka Uhuru wa Tanganyika, Mkitupatia tutauwasha Mwenge wa
Uhuru na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje na
mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali
palipo na chuki na heshima palipojaa dharau”.
Maneno
haya aliyarudia tena mwaka 1959 alipohutubia kikao cha 35 cha Baraza la
Umoja wa Mataifa kama Mbunge mwakilishi pekee wa Tanganyika.
Falsafa
hiyo ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa ni kiashiria kikubwa
kwa Waingereza kwamba watu wa Tanganyika wamechoka kutawaliwa. Siku
Tanganyika ilipopata Uhuru tarehe 09 Desemba, 1961. Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere aliuwasha Mwenge wa Uhuru na akamkabidhi Luteni
Alexander Ngwebe Nyirenda na kikosi cha Vijana wenzake wakaupeleka
Mwenge wa Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.
Mwalimu
wakati akitoa hotuba ya siku ya Uhuru; aliwatangazia Watanganyika,
Afrika na Dunia kwa ujumla kwa kusema
“Sisi tumekwisha uwasha Mwenge wa Uhuru na
kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu,
ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini, ulete upendo mahali penye
chuki na heshima mahali palipo jaa dharau”
Luteni
Alexander Nyirenda akipandisha Bendera na Mwenge wa uhuru juu ya mlima
Kilimanjaro usiku wa kuamkia tarehe 9 december, 1961
Baada
ya Uhuru wa Tanganyika na kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru, Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere na viongozi wenzake wa awamu ya kwanza
walielekeza juhudi zao katika kuwaunganisha Watanzania na kuweka misingi
imara ya kulijenga taifa huru la Tanganyika; kudumisha amani, upendo,
umoja, mshikamano na kuweka sera za kukabili maadui ujinga, umaskini na
maradhi.
WAKUU WA IDARA WILAYANI IKUNGI, MAAFISA TARAFA, WATENDAJI WA KATA, VIJIJI NA WENYEVITI WA VIJIJI WAFUNDWA
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasilisha mtazamo wa namna ambavyo anataka Wilaya hiyo iwe.
Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ikungi Rustika Turuka aliyesimama
akizungumza na Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa
Kata, Vijiji, na Wenyeviti wa Vijiji wakati wa kikao hicho cha kazi.
Wakuu
wa Idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Vijiji, na
Wenyeviti wa Vijiji wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji
Kutoka Kushoto ni Mustafa Mtopo kaimu Afisa usalama wa Taifa Wilaya ya
Ikungi, Fortunatus Ndalama Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi, Dijovson
Ntangeki Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Miraji Jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
ikungi Rustika Turuka, na Mkuu wa poiisi Wilaya ya Ikungi Milton Nkyalu
wakifatilia mafunzo kutoka kwa wawasilishaji waliotoka ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Na Mathias Canal, Singida
Wakuu wa Idara na vitengo, Maafisa
Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji
101 vilivyopo Wilayani Ikungi Mkoani Singida hii leo wamepatiwa mafunzo
ya kutambua mipaka ya majukumu yao kiutendaji katika kikao cha kazi
kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ikungi.
Mafunzo hayo yameandaliwa na
uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kutokana na kubainika kuwa
asilimia kubwa ya watendaji hususani wenyeviti wa vijiji na vitongoji
wamekuwa wakiingilia katika majukumu ya kiutendaji.
Akifungua mafunzo hayo yaliyodumu
kwa zaidi ya masaa matano yaliyojikita zaidi kutoa ufafanuzi juu ya
majukumu ya watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa
Vijiji, Mkuu wa Wilaya hiyo Miraji Jumanne Mtaturu amebainisha kuwa
pamoja na mafunzo kwa ajili ya ufahamu wa majukumu ya watendaji hao
lakini amesema kuwa Wilaya ya Ikungi ipo nyuma kielimu kutokana na shule
kuwa mbali na maeneo ya watu, wanafunzi wa kike kuachishwa shule na
kuolewa, baadhi ya viongozi na wataalamu kutotimiza wajibu wao na wakati
mwingine uzembe wa baadhi ya watumishi wa serikali katika kutatua
kadhia za wananchi.
Pamoja na hayo pia DC Mtaturu
amesema kuwa kuna baaadhi ya maeneo kuna shule ambazo zina majengo
mazuri na Hosteli kwa ajili ya wanafunzi lakini wazazi wanakataa
kuwapeleka wanafunzi shuleni ikiwa ni pamoja na shule ya Sekondari
Mkinya iliyopo Kata ya Dung’unyi, Shule ya Sekondari Mtunduru, Shule ya
Sekondari Mwaru na Wembere , huku shule ya Sekondari Issuna ikiwa na
Majengo na Hosteli nzuri lakini wanafunzi wanaosoma hapo ni wale
wanaotoka Wilaya nyingine huku wenyeji wakiwa wamejichimbia ndani.
Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kushirikiana na Polisi
kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua baadhi ya Watendaji wa Kata,
Waratibu wa elimu wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji
wanaoshirikiana na baadhi ya wazazi kuwaachisha wanafunzi shule ili
wakaolewe ambapo amebaini kuwa katika Kata ya Mwaru na baadhi ya Kata
zinazozunguka katika Kata hiyo viongozi wake kwa kushirikiana na
Waratibu elimu Kata wamekuwa wakifanya biashara ya kuruhusu wanafunzi
kuolewa kwa kupewa Ng’ombe.
Hata hivyo pia amewaagiza
Watendaji wa Kata ya Makilawa na Iyumbu kumpatia taarifa ya kamati ya
maendeleo ya Kata (WDC) ili kubaini mpango wa mikakati katika kujenga
shule za Sekondari katika Kata hizo mbili ambazo zimesalia ilihali Kata
28 tayari zina shule za sekondari kati ya Kata 30 zilizopo katika Wilaya
hiyo.
Katika shule 28 ni shule 3 tu
zenye maabara, shule ya Sekondari ya Puma na Wembere ambao nao walijenga
maabara baada ya kupata msaada kutoka Benki ya dunia Mwaka 2013, shule
ya Sekondari Mkinya ina maabara 2 ambazo zilijengwa kwa msaada wa SADC
mwaka 2009 hivyo kupelekea Wilaya nzima ya Ikungi kuwa na Maabara 4
pekee zilizojengwa kwa msaada wa wahisani ambapo hakuna hata maabara
moja iliyojengwa na wananchi ikakamilika kutokana na zuio la kuchangia
walilolipata wananchi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki
Tundu Lissu.
Sawia na hayo pia Mkuu huyo wa
Wilaya amewaagiza Watendaji wa Kata na Vijiji kwa kushirikiana na
Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji kuwaelimisha wananchi kukaa
vikao na kupitisha maadhimio ya kuendelea kuchangisha michango ya ujenzi
wa maabara kwa mujibu wa waraka wa Elimu namba 6 wa mwaka 2015 wa elimu
msingi bila malipo.
Hata hivyo agizo limetolewa pia
kwa Wazazi/Walezi pamoja na wanafunzi wenyewe kuchukuliwa hatua kali za
kisheria kutokana na utoro wa wanafunzi shuleni jambo ambalo linapelekea
kuwa na ufaulu duni wa wanafunzi Wilayani humo.
Dc Mtaturu pia amemuagiza Afisa
Mtendaji wa Katana Afisa Mtendaji wa Tarafa kutumia siku 14 kuhakikisha
madawati yanafika katika shule zenye uhaba wa madawati ili kuondokana na
adha ambayo inaendelea kuwakumba wanafunzi shuleni ilihali madawati
tayari yamepatikana.
Aidha ndani ya siku tano viongozi
hao wameagizwa kuhakikisha kuwa Masoko pamoja na stendi zinaenda katika
maeneo yaliyopangiwa ili ushuru upatikane kwa wakati na kwa kiasi
kilichokusudiwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka amewashukuru Watendaji wa
Kata, Wenyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Vijiji kwa kujitokeza kwa
wingi katika mafunzo hayo jambo ambalo limeonyesha kuwa wananchi hao
wana imani na serikali ya awamu ya nne hivyo amewaomba kuachana na siasa
na kufanya kazi kwa moyo na nguvu zaidi.
Amewataka viongozi wote wa ngazi
ya Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji na vitongoji kutekeleza maagizo yote
yanayotolewa na serikali kwa haraka na kwa ukamilifu.
Turuka amesema kuwa kila kiongozi
anapaswa Kutatua kero za wananchi kwa kutenda haki, kutofanya kazi kwa
mazoea, kutoa majawabu sahihi ya wananchi na kama hawafahamu wanapaswa
kuuliza sehemu husika ili kutozungumza jambo wasilokuwa na uhakika nalo.
Kupitia kikao hicho kilichoitishwa
na mkuu huyo wa Wilaya kilichokuwa na dhumuni la kufahamiana na
kukumbushana majukumu na wajibu wa viongozi na kueleza mtazamo wa Ikungi
mpya inavyotakiwa kuwa Afisa utumishi wa Wilaya sawia na Mkuu wa Polisi
Wilaya wamepewa nafasi ya kuelezea majukumu na wajibu wa kila mmoja
katika maeneo yao.
Kwa upande wao baadhi ya Watendaji
wa Kata, Vijiji na wenyeviti wa vijiji 101 vilivyopo Wilayani humo
wamesema kuwa mafunzo waliyoyapata watayatumia vyema kuwa mabalozi
wazuri kwa wananchi na kuwaelimisha zaidi ili kutambua mipaka yao na
majukumu yao katika kuishauri serikali.
Aidha Maafisa Tarafa, Watendaji wa
Kata, Watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji wote ambao
hawajahudhuria kikao hicho cha kazi wametakiwa kuandika barua za maelezo
kwanini wameshindwa kuhudhuria na zimetakiwa kupitia kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi hadi kufikia tarehe 10 ya mwezi huu wa
nane.
MO Dewji amwaga Simba Mil. 100 za usajili, kutumia zaidi ya Bilioni
Hatimaye ahadi ya shabiki wa Simba, ambaye ni Mkurugenzi wa
Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji
amekamilisha ahadi aliyoisema kabla ya mkutano mkuu wa Simba kwa
kukabidhi Milioni 100 kwa uongozi wa Simba kwa ajili ya kufanya usajili.
MO amekabidhi pesa hizo baada ya kueleza mipango yake kwa Simba ya kuwa kama wanachama wa Simba wataridhia kufanya mabadiliko basi atachangia pesa ya usajili jambo ambalo katika mkutano wake wa Jumatatu na waandishi wa habari kuwa ahadi yake ni kweli na ataikamilisha kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Akizungumza baada ya kupokea cheki kutoka kwa MO, Rais wa Simba, Evans Aveva, amemshukuru MO kwa msaada huo na sasa wanasimba watatembea kwa kujiamini kwani wamepata pesa ya kufanya usajili.
“Nakushukuru MO kwa msaada ambao umetupatia tunaamini ni mapenzi ambayo unayo kwa Simba ndiyo umefanya uwe tayari kutoa pesa hizi na sisi tunaamini zitaweza kutusaidia kupiga hatua na hata tuweze kutembea kifua mbele,” alisema Aveva.
Aidha Aveva alisema kiasi hicho cha pesa bado hakijatosha kwa kufanya usajili ambao wamepanga kuufanya lakini kitawasaidia kupiga hatua ya kufanya usajili ambapo kwa msimu huu wamepanga bajeti ya Milioni 400 lakini pia kumtaja mchezaji wa Ivory Coast ambaye wanataka kumsajili ni Fredrick Blagnon.
Kwa uapnde wa MO alisema ametoa msaada huo kama sehemu ya ahadi aliyoitoa kabla ya mkutano mkuu na hakuna makubaliano yoyote lakini pia kuwapa ahadi mashabiki wa Simba kuwa kama akipata nafasi ataweka bajeti zaidi ya Bilioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya usajili.
Chanzo Mo Blog
MO amekabidhi pesa hizo baada ya kueleza mipango yake kwa Simba ya kuwa kama wanachama wa Simba wataridhia kufanya mabadiliko basi atachangia pesa ya usajili jambo ambalo katika mkutano wake wa Jumatatu na waandishi wa habari kuwa ahadi yake ni kweli na ataikamilisha kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Akizungumza baada ya kupokea cheki kutoka kwa MO, Rais wa Simba, Evans Aveva, amemshukuru MO kwa msaada huo na sasa wanasimba watatembea kwa kujiamini kwani wamepata pesa ya kufanya usajili.
“Nakushukuru MO kwa msaada ambao umetupatia tunaamini ni mapenzi ambayo unayo kwa Simba ndiyo umefanya uwe tayari kutoa pesa hizi na sisi tunaamini zitaweza kutusaidia kupiga hatua na hata tuweze kutembea kifua mbele,” alisema Aveva.
Aidha Aveva alisema kiasi hicho cha pesa bado hakijatosha kwa kufanya usajili ambao wamepanga kuufanya lakini kitawasaidia kupiga hatua ya kufanya usajili ambapo kwa msimu huu wamepanga bajeti ya Milioni 400 lakini pia kumtaja mchezaji wa Ivory Coast ambaye wanataka kumsajili ni Fredrick Blagnon.
Kwa uapnde wa MO alisema ametoa msaada huo kama sehemu ya ahadi aliyoitoa kabla ya mkutano mkuu na hakuna makubaliano yoyote lakini pia kuwapa ahadi mashabiki wa Simba kuwa kama akipata nafasi ataweka bajeti zaidi ya Bilioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya usajili.
Chanzo Mo Blog
Kampeni ya “Nunua, Uza, Shinda na Konyagi yazindi kupamba moto
Mawakala na baadhi ya maofisa wa Konyagi wakiwa wamesimama kando ya moja linalowaniwa kwenye promosheni hii kubwa.
………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Kampeni ya mawakala wa kuuza
vinywaji vya Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL)
inayojulikana kama “Nunua, Uza, Shinda na Konyagi ambayo itawezesha
washindi kujipatia malori ya usambazaji bidhaa inazidi kupamba moto.
Baadhi ya mawakala wa kampuni
hiyo kutoka mikoa mbalimbali wanaendelea na mikakati mizito ya
usambazaji vinywaji ili kufikia lengo la kuingia kwenye droo kila mmoja
akiwa amepania kujishindia lori la zawadi ya kampeni hii.
Meneja Masoko na Udhamini wa TBL
Group,George Kavishe, amesema kuwa baada ya kukamilika zoezi la uzinduzi
kila kanda ambao umekuwa na mafanikio na kuwashirikisha mawakala
wanaouza bidhaa za kampuni hivi sasa kazi kubwa imebaki kwao kufanya
mauzo na kufikia viwango vya kuingia kwenye droo ya kupata washindi.
“Dhumuni kuu la kampuni yetu ya
TDL kubuni kampeni hii ni kuwainua wasambazaji wa biashara zetu.
Tutaweza kufikia lengo hili kwani washindi wawili katika kampeni hii
watajishidia magari mapya mawili ya usambazaji aina ya Eicher yenye
uzito wa tani 3 pia tunazo zawadi mbalimbali ambazo zimetengwa kwa ajili
ya kuongeza motisha kwao katika kipindi hiki cha kampeni”alisema
Alisema kampeni itadumu kwa
kipindi cha wiki 12 na wasambazaji wanaoshiriki wamewekewa viwango vya
mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa
ya kupata mshindi mwezi Oktoba mwaka huu . “Tunaamini kabisa kampeni
hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao watoongezea chachu ya
manunuzi ya bidhaa zetu”.Alisema.
Baadhi ya mawakala wamepongeza
jitihada za kampuni kutenga zawadi kubwa za promosheni ambazo
zitawawezesha washindi kurahisisha biashara zao badala ya zawadi
ndogondogo zisizoweza kumwinua kimaisha mshiriki.
Mmoja wa wauzaji wa bidhaa ya
Konyagi kanda ya Ziwa aliyejitambulisha kama John Masanja amesema kuwa
japo sio mawakala wote watapata malori lakini watakaobahatika kushinda
watakuwa wamepata zawadi ya uhakika na inayofanikisha biashara kukua.
“Kampeni hii ya Konyagi ni kubwa cha muhimu ni kukidhi vigezo vya
kuingia kwenye droo ya kumpata mshindi “.Alisema.
Mpango wa Urasimishaji Makazi Holela Jijini Dar waanza kutekelezwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Urasimishaji makazi holela toka Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Bibi Betha Mlonda akifafanua kwa waandishi wa
Habari kuhusu mpango wa urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholea katika
Jiji la Dar es saaam ambao umeanza kutekelzwa katika eneo la Kimara
Jijini humo .kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari- Maelezo Bi Fatma
Salum na kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Hassan Mabuye.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi na Vyombo vya Habari leo Jijini Dar es salaam.
Moja ya eneo lenye makazi holela katika Jiji la Dar es salaam.
Mmoja wa Wataalamu wa upimaji Ardhi akiweka alama katika eneo lililorasimishwa.
………………………………………………………………………………………….
Fatma Salum-Maelezo
Serikali imeanza kutekeleza
mpango wa kutambua, kupanga na kupima vipande vya ardhi na kuweka huduma
za jamii kama miundombinu ya barabara na mitaro ya maji ya mvua ili
kuboresha mazingira ya makazi na kuongeza usalama wa miliki kwa kutoa
hatimiliki.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Makazi Holela kutoka
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Bertha Mlonda
wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Akifafanua Mlonda alisema kuwa
mpango huo unatekezwa kwa kushirikiana na Halmashuri zote za Jiji la Dar
es salaam na tayari zoezi limeanza katika Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni ambapo wananchi wameonyesha mwitikio mkubwa kwa kuunga mkono
juhudi hizo za Serikali .
Akizungumzia vigezo vinavyofuatwa
katika urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela, Mlonda alibainisha
kuwa ni pamoja na eneo husika liwe limetengwa kwa ajili ya matumizi ya
makazi katika Mpango wa Jumla wa Jiji (Master Plan).
“Mpango huu ni shirikishi,
wananchi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wataalamu
kubainisha mahitaji ya huduma za jamii na miundombinu na siyo makazi
holela yote yana sifa ya kurasimishwa. “Alisisitiza Mlonda.
Aidha, alisema kuwa eneo husika
ni lazima liwe na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika eneo hilo ambao
hawana uthibitisho wa uhalali wa kumiliki ardhi hata kama wanalipia ada.
Kigezo kingine ni kuwepo kwa
ongezeko kubwa la ujenzi wa nyumba katika eneo husika na idadi kubwa ya
wakazi ambao wameishi katika eneo hilo kwa kipindi kirefu.
“Kuna maeneo mengi ambayo
wamiliki wanaendelea kuuza mashamba au viwanja vyao na ujenzi wa nyumba
mpya kwa ajili ya makazi na biashara unaendelea kwa kasi kubwa; ndio
maana tumeona ni vyema tukaanza utaratibu huu wa kurasimisha ili watu
wamiliki hayo maeneo kihalali.” Alifafanua Mlonda.
Pia idadi kubwa ya wakazi wa Jiji
la Dar es Salaam na Asasi za Kijamii wamehamasika na wako tayari
kushiriki katika mipango ya urasimishaji kwa kuchangia gharama za
kupanga, kupima na kumilikisha.
Mlonda alitoa wito kwa wananchi
kushirikiana na viongozi wao wa Serikali za Mitaa kutatua migogoro ya
mipaka na kutoa ardhi kwa ajili ya barabara kwani ndio msingi wa ufanisi
katika zoezi la urasimishaji makazi.
Makazi holela ni makazi ambayo
yamejengwa bila kufuata Sheria, kanuni na taratibu za Mipangomiji.
Ujenzi mijini unaongozwa na Sheria ya Mipangomiji namba 8 ya mwaka 2007
na ile ya Serikali za Mitaa sehemu ya mamlaka za miji ya mwaka 1982.
ambazo zinaelekeza kupata kibali cha ujenzi kabla ya kujenga nyumba.
|
|
WAZIRI MKUU AKATAA KUPOKEA MADAWATI YALIYOTOLEWA NA TFS
Asema huu si wakati wa kupokea vitu vibovu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amekataa kupokea msaada wa madawati uliotolewa na Wakala wa Misitu
Tanzania (TFS) baada ya kubaini yametengenezwa chini ya kiwango.
“Ofisa Elimu njoo kagua haya
madawati yaliyo mazuri nitayapokea na yaliyobaki yarudishwe karakana
yakatengenezwe upya huu si wakati wa kupokea vitu vibovu,“ amesema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumanne, Agosti 02, 2016) wakati alipowasili katika kiwanja cha Mabau,
Mtibwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ambapo alikabidhiwa madawati
hayo na Meneja wa TFS
Alisema anatambua dhamira ya TFS
ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kumaliza tatizo la upungufu wa
madawati lakini hawezi kupokea kupokea madawati yaliyotengenezwa chini
ya kiwango.
Baada ya Ofisa Elimu (Msingi) wa
Wilaya ya Mvomero, Michael Ligola kukagua madawati 102 yaliyoletwa
uwanjani hapo madawati 84 yalibainika kuwa ni mabovu na 14 tu ndiyo
yalikuwa mazima.
Waziri Mkuu alisema hawezi kupokea
madawati hayo yaliyotolewa na Meneja wa Msitu wa Mtibwa, Hamza Kateti
na kuuagiza uongozi wa wilaya ufuatilie suala hilo kwa kuwa walitakiwa
kuyakagua kabla ya yeye kukabidhiwa.
Katika hatua nyingine
aliwasisitiza wazazi na walezi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanawapeleka
watoto wao shule na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Serikali imewapunguzia mzigo kwa
kuwaondolea michango na ada hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuwapeleka
shule watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule na wasimamie masomo
yao,” alisema.
Awali mbunge wa jimbo la Mvomero,
Saddiq Murad alisema miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili wilaya
hiyo ni pamoja na wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba hivyo
amemuomba Waziri Mkuu kuingilia kati suala hilo.
Akizungumzia namna Serikali
ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na
wakulima Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi watahamishiwa
katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa na wenye mifugo
michache watatengewa maeneo katika vijiji.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 02, 2016.
Ilala yashiriki maonyesho ya Nanenane yanayofanyika mkoani Morogoro
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (kulia) akiwa na Mstahiki Meya wa
Manispaa hiyo Mhe. Charles Kuyeko (kushoto) wakihojiwa na mwandishi wa
habari katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika
jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (kulia) akiongea na baadhi ya
Madiwani wa Manispaa hiyo katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima
(Nanenane) iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Msongela Palela (wa pili kushoto)
akipata maelezo ya namna ya upandikizaji wa mbegu za samaki kwa njia za
kisasa toka kwa Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Msongo Songoro (kulia)
katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana
tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kulia) wakijadiliana
jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Msongela
Palela (kushoto) alipotembelea banda la maonyesho la Manispaa hiyo
katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana
tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
DC ILALA,SOPHIA MJEMA AZINDUA UWANJA WA NETIBOLI NA KIKAPU SHULE YA JANGWANI
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akifunga goli wakati wa uzinduzi wa
uwanja wa Netiboli na Mpira wa Kikapu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani
uliojengwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo
kupitia kampeni yake ya “Be Kidotified”. Mjema alizindua uwanja huo leo
katika hafla fupi iliyofanyika katika shule hiy.Kushoto ni Jokate
akishuhudia tukio hilo.
uwanja wa Netiboli na Mpira wa Kikapu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani
uliojengwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo
kupitia kampeni yake ya “Be Kidotified”. Mjema alizindua uwanja huo leo
katika hafla fupi iliyofanyika katika shule hiy.Kushoto ni Jokate
akishuhudia tukio hilo.
PICHA NA MICHUZI JR
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) akitoa hotuba yake
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo (kushoto). Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa
shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo (kushoto). Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa
shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo (Kushoto)
akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa uwanja alioujenga kupitia
kampeni yake ya “Be Kidotified” uliomgharimu kiasi cha Sh Milioni 50. Wa
pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara
Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule
Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa uwanja alioujenga kupitia
kampeni yake ya “Be Kidotified” uliomgharimu kiasi cha Sh Milioni 50. Wa
pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara
Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule
Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
Mrembo wa zamani wa Tanzania, Faraja Kota akizungumza mbele ya Wanafunzi
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo.
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo.
Mandhari ya uwanja wa Mpira wa Kikapu na Netiboli wa shule ya Sekondari ya
Jangwani uliojengwa na Mrembo, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya
“Be Kidotified”.
Jangwani uliojengwa na Mrembo, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya
“Be Kidotified”.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala pichani kati Mh.Sophia Mjema akiwasili kwenye hafla
fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Netiboli na Kikapu wa shule ya
Jangwani leo jijini Dar,Pichani kulia ni Katibu Tawala wilaya ya
Ilala.Ndugu Edward Mpogolo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Kidoti, Jokate Mwegelo.
fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Netiboli na Kikapu wa shule ya
Jangwani leo jijini Dar,Pichani kulia ni Katibu Tawala wilaya ya
Ilala.Ndugu Edward Mpogolo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Kidoti, Jokate Mwegelo.
……………………………………………………….
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alisema kuwa
amefurahishwa na mpango huo wa Jokate kwa kusaidiana na Mo Dewji
Foundation na kuwaomba kuuendeleza kwa shule nyingineza jijini.
amefurahishwa na mpango huo wa Jokate kwa kusaidiana na Mo Dewji
Foundation na kuwaomba kuuendeleza kwa shule nyingineza jijini.
Mjema alisema kuwa Dar es Salaam kuna shule nyingi na angependa kuona hata
shule za Chanika zinafaidika na kampeni ya “Be Kidotified”. Alisema kuwa
amefarijika sana kuona shule aliyosoma yeye kufaidika kwa mradi huo na
kuwaomba wanafunzi na walimu kuutumia uwanja huo kama fursa ya
kuendeleza michezo na taaluma.
shule za Chanika zinafaidika na kampeni ya “Be Kidotified”. Alisema kuwa
amefarijika sana kuona shule aliyosoma yeye kufaidika kwa mradi huo na
kuwaomba wanafunzi na walimu kuutumia uwanja huo kama fursa ya
kuendeleza michezo na taaluma.
Wakati huo huo Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya kuchangia
jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” amejenga uwanja
utakaotumika kwa ajili ya michezo ya mpira wa kikapu na Pete (netiboli)
kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani. Uwanja huo ulizinduliwa jijini leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule
hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa
serikali. Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Shilingi
milioni 50. Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya
michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya
sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha
zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa
changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya
michezo ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua vipaji ambavyo
vitamwezesha mshiriki kupata ajira.
Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazorudisha nyuma maendeleo ya michezo
nchini ni ukosefu wa viwanja bora ambavyo ukwamisha wachezaji chipukizi
kuonyesha vipaji vyao ipasavyo.
Kwa mujibu waJokate, alipokuwa anasoma, alikutana na changamoto hizo,
lakini alipiga moyo konde na kujihusisha na shughuli mbalimbali za nje
ya darasa ikiwa pamoja na michezo na kujifunza mengi.
“Mimi ni mjasiriamali mchanga sana hapa nchini, nimehamasisha kwa kile kidogo
nilichonacho na kwa msaada wa wadhamini niliyotafuta kuhitimisha ujenzi
wa uwanja huu ambao utatumika si kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya
Jangwani pekee, bali hata kwa mechi za shule nyingine, ”
“Nawapongeza wadhamini walioniunga mkono katika mpango huu kama Mo Dewji Foundation,
na wadau ambao walikuwa nyuma yangu katika kuhakikisha kampeni ya ‘Be
Kidotified’ inaanza kwa mafanikio makubwa na kuendelea kwa shule
nyingine za hapa jijini,” alisema Jokate.
Alisema kuwa chapa ya Kidoti ni miongoni mwa chama zinazoongoza hapa nchini
katika mitindo, urembo na burudani kabla ya kuamua kupanua wigo kwa
upande wa michezo tofauti na mpira wa miguu.
Alifafanua kuwa alianza kwa kuanzisha kampuni ya Kidoti (Kidoti Company) na
kuchangia katika soko la ajira nchini na baadaye kuanzisha “kidoti
brand’ akiwa na lengo la kuhamasisha vijana kujihusisha katika shughuli
mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila
siku.
jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” amejenga uwanja
utakaotumika kwa ajili ya michezo ya mpira wa kikapu na Pete (netiboli)
kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani. Uwanja huo ulizinduliwa jijini leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule
hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa
serikali. Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Shilingi
milioni 50. Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya
michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya
sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha
zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa
changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya
michezo ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua vipaji ambavyo
vitamwezesha mshiriki kupata ajira.
Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazorudisha nyuma maendeleo ya michezo
nchini ni ukosefu wa viwanja bora ambavyo ukwamisha wachezaji chipukizi
kuonyesha vipaji vyao ipasavyo.
Kwa mujibu waJokate, alipokuwa anasoma, alikutana na changamoto hizo,
lakini alipiga moyo konde na kujihusisha na shughuli mbalimbali za nje
ya darasa ikiwa pamoja na michezo na kujifunza mengi.
“Mimi ni mjasiriamali mchanga sana hapa nchini, nimehamasisha kwa kile kidogo
nilichonacho na kwa msaada wa wadhamini niliyotafuta kuhitimisha ujenzi
wa uwanja huu ambao utatumika si kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya
Jangwani pekee, bali hata kwa mechi za shule nyingine, ”
“Nawapongeza wadhamini walioniunga mkono katika mpango huu kama Mo Dewji Foundation,
na wadau ambao walikuwa nyuma yangu katika kuhakikisha kampeni ya ‘Be
Kidotified’ inaanza kwa mafanikio makubwa na kuendelea kwa shule
nyingine za hapa jijini,” alisema Jokate.
Alisema kuwa chapa ya Kidoti ni miongoni mwa chama zinazoongoza hapa nchini
katika mitindo, urembo na burudani kabla ya kuamua kupanua wigo kwa
upande wa michezo tofauti na mpira wa miguu.
Alifafanua kuwa alianza kwa kuanzisha kampuni ya Kidoti (Kidoti Company) na
kuchangia katika soko la ajira nchini na baadaye kuanzisha “kidoti
brand’ akiwa na lengo la kuhamasisha vijana kujihusisha katika shughuli
mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila
siku.
MIKATABA YA WACHEZAJI VPL, FDL
Shirikisho
la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) linapenda kuzikumbusha timu
zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwamba hatutatoa leseni
ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati wa maombi ya
usajili, hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 68 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya
Ligi Kuu ya Tanzania toleo la 2016/2017.
Kila timu
inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya
katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze
kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja
kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. Na kumbuka kanuni ya 68(8) inataka
kulipia kiasi cha sh 50,000 kwa kila mkataba wa mchezaji.
Ni matarajio
yetu kuwa kila klabu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya
timu na mchezaji na mchezaji na timu. Tunategemea kupata ushirikiano.
Kadhalika, kwa
mujibu wa kanuni 67 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Daraja la Kwanza
Tanzania ya StarTimes, Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF)
linakumbusha kwamba halitatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu
haikuleta mkataba wakati wa maombi ya usajili.
Kila timu
inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya
katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze
kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji mtakuja
kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. Na kumbuka kanuni ya 67(8) inataka
kulipia kiasi cha sh 25,000 kwa kila mkataba wa mchezaji.
Pia katika hili tunategemea kila timu itatimiza wajibu wake ili kuondoa migogoro kati ya timu na mchezaji na mchezaji na timu.
NAIBU WAZIRI SULEIMANI JAFFO AHIMIZA USAFI KWENYE MAJIJI,AKAGUA MAGARI MAALUMU JIJINI ARUSHA
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya usimamizi miundombinu ya ukusanyaji Taka ngumu wakimsikiliza Naibu Waziri,Suleimani Jaffo. |
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani Jaffo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari. |
PONDAMALI, MANYIKA DARASANI TFF
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanikiwa tena. Safari FIFA –
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu limeipa nafasi Tanzania kuwapa
mafunzo ya juu ya ukocha wa makipa (Advanced Goalkeeping Coach Course)
ikiandika historia kuwa nchi ya pili barani Afrika kwa makocha wa nafasi
hiyo baada ya Botswana.
Makocha wa
makipa 25 hususani wa wa timu za taifa, timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, wanahudhuria kozi hiyo inayoongozwa na Alejandro
Heredia ambaye ni Mkufunzi kutoka FIFA.
Makocha hao ni
Peter Manyika (Taifa Stars ya Tanzania), Saleh Ahmed (Zanzibar Heroes);
Muharami Mohammed (Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka
17 – Serengeti Boys); Mohammed Silima (Timu ya Taifa ya Vijana
Zanzibar) na Elyutery Mhoery (Timu ya Taifa ya Wanawake – Twiga Stars)
na msaidizi wake ambaye pia anachezea JKT Queens, Fatuma Omary.
Wengine ni
makocha maarufu wa makipa wakiwamo Juma Pondamali (Young Africans); John
Bosco (Majimaji ya Songea); Salimu Tupa (Tanga); Bakari Ali Hamadi
(Wete Pemba – Zanzibar); Hafidh Muhidin Mcha (Mkoani Pemba – Zanzibar);
Mussa Wanena (Kagera Sugar); Juma Bomba (African Lyon), Adam Abdallah
Moshi (Simba SC), Idd Mwinchumu (Azam FC) na Hussein Tade (Seeb
Club-Oman/Toto African)
Pia wamo
Khalid Adams (Mwadui FC); Josia Steven (Mbeya City); Herry Boymanda
(Tanzania Prisons); Emmanuel Mwansile (Polisi Morogoro); Ben Kalama
(Stand United); Abdallah Said (JKT Ruvu); Patrick Mwangata (Mtibwa
Sugar); Augustin Malindi (Mkoa wa Kigoma); Raphael Mpangala (Ndanda FC);
Salimu Tupa (Tanga) na nAbdul Mgude (Coastal Union ya Tanga).
“Mjione kwamba
mmepewa kipaumbele,” alisema Heredia akiwanoa makocha hao na kuongeza:
“Kinachohitajika sasa ni juhudi tu. Kozi hii haijafanyika pengine hapa
barani Afrika zaidi ya Botswana. Mjue kuwa mna bahati.”
Akitoa nasaha
wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia
aliishukuru FIFA na CAF kwa namna inavyoshirikiana na TFF katika kuwapa
kozio nyingi za makocha wa timu kwa wachezaji wa mbele, makocha wa
makipa na waamuzi wa madaraja tofauti.
“Hakuna
kipindi TFF imepata kozi za makocha nyingi za makocha kama kipindi hiki
cha uongozi wa Jamal Malinzi,” anasema Karia na kuongeza: “Tumetoka
kwenye kozi ya makocha wa Daraja A sasa tuko kwenu. Lengo ni Tanzania
kuwe na makipa wazuri. Ninyi mtaleta makipa wazuri. Na hii ni kwa
manufaa ya sasa na baadaye kwa upende wetu, timu zetu na taifa kwa
ujumla.”
Karia aliwatia
hamasa makocha hao wanaoshiriki kozi hiyo kuwa, mara baada ya kozi hiyo
ipo siku watakwenda kuwa wakufunzi nje ya mipaka ya nchi kadhalika
makocha ambao wanaweza kupata kazi mahala popote duniani hasa
ukizingatia walimu wa daraja lao wako Tanzania na Botswana tu.
Kadhalika,
Makamu huyo wa Rais wa TFF alielezea kuwa mpira wa miguu una changamoto
nyingi na nyingine husababishwa na watalaamu hao kubweteka kwa
mafanikio. “Hili ni tatizo. Tubadilike kifikra na kivitendo. Msilaze
damu, kuweni active (mahiri).”
SERIKALI ZETU ZINATAMBUA MCHANGO WA WANADIASPORA
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
zinatambua mchango mkubwa wa Wanadiaspora na ndio maana hutayarisha
makongamano ambayo hutoa fursa ya kujadili masuala mbali mbali ya
kimaendeleo kwa lengo la kuimarisha uchumi wa Tanzania na ustawi wa
wananchi wake.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Salum Maulid Salum aliyasema hayo
leo huko Ikulu Mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na waandishi
wa Habari mbali mbali kutoka Redio za FM zinazofanya kazi zake hapa
Zanzibar kuhusu Kongamano la Diapora la Tanzania linalotarajiwa
kufanyika hapa Zanzibar mwaka huu.
Katika maelezo yake Katibu Mkuu
huyo aliyekuwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Silima Kombo Haji, alisema kuwa kwa
miaka miwili iliyopita makongamano hayo yamefanyika Dar-es-Salam na
kusisitiza kuwa mikutano iliyokwisha fanyika imeweza kuleta mafanikio
makubwa.
Alisema kuwa Mkutano wa mwaka huu
unatarajiwa kufanyika hapa Zanzibar kwa muda wa siku mbili kati ya
tarehe 24 na 25 linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli huko katika ukumbi wa
hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa
mada mbali mbali zinatarajiwa kutolewa katika Kongamano hilo ambalo
kauli mbiu yake ya kila mwaka ni “Mtu kwao ndio Ngao’ ambapo pia,
ujumbe mkubwa kwa mwaka huu ni “Mtizamo mpya wa Kuimarisha Utalii wa
Tanzania na uekezaji”
Katika melezo yake Katibu Salum
alisema kuwa tayari matayarisho ya kongamano huo yanaendelea vizuri na
kueleza kuwa Wanadiaspora wamekuwa na mwamko mkubwa katika ushiriki
ambapo kila mwaka idadi ya ushiriki wao imekuwa ikiongezeka huku
akieleza kuwa vyombo vya habari zikiwemo Redio za FM, vina nafasi kubwa
katika kuwaeleza wananchi juu ya mkutano huo.
Aidha, alisema kuwa miongoni mwa
mafanikio yaliopatikana ni pamoja na Wanadiaspora wengi wa hapa nchini
wameweza kutoa michango yao mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha
mirado mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ya afya, elimu na mengineyo.
Katibu Mkuu huyo alitumia fursa
hiyo kueleza juhudi za viongozi hapa nchin i katika kuhakikisha suala
hilo linaimarika huku akitolea mfano juhudi za makusudi zinazochukuliwa
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein katika kuhakikisha ushirikiano kati ya Wanadiaspora na Serikali
zote mbili unaimarika.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Silima Kombo Haji
aliwaeleza waandishi hao wa habari faida zinazopatikana kutokana na
kuunganishwa kwa Wanadiaspora hapa nchini pamoja na changamoto zilizopo.
Balozi Silima alizitaja baadhi ya
nchi zilizopo ndani na nje ya Afrika ambazo zimenufaika na
zinazaendelea kunufaika kutokana na Wanadiaspora wa nchi zao zikiwemo
Kenya, Ethiopia, Ghanam Idia, Pakistan, Ufilipino, Bangladesh na
nyenginezo.
Sambamba na hayo, Balozi Silima
alisema kuwa serikali zote mbili zimeweka mikakati maalum ya kuhakikisha
Wanadiaspora wanapewa kipaumbele sambamba na kushirikishwa katika
masuala mbali mbali ya maendeleo kwa nchi yao.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
WASANII, WATANGAZAJI NA WATU MAARUFU KUVUNA MAPESA KUTOKANA NA MITANDAO YAO YA JAMII
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey
and Clifford, Rashid Tenga alielezea machache mbele ya wageni na
waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo juu ya huduma mpya ya
matangazo katika bara la Afrika utakaowanufaisha watangazaji, wasanii na
watu maarufu uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole
Gabriel na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni
Kihedu. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Katibu Mkuu wa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
(katikati) akimsifia msanii Diamond Platinumz kwa jinsi ambavyo amekuwa
akiitanga Tanzania nje ya nchi kwa muziki wake.
Katibu Mkuu wa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole
Gabrielakimsifia Wema Sepetu jinsi ambavyo amekuwa akilitunza jina lake.
Msanii Diamond Platinuz akitoa shukrani zake za pekee kwa niaba ya wasanii walihudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey
and Clifford, Rashid Tenga (kushoto) akizunguza na Katibu Mkuu wa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole
Gabriel wakati wa uzinduzi wa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya
kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara
zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii iliyofanyika
jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Wageni waalikwa waliohudhuria shughuli hiyo.
Wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.
Waandishi nao hawakuwa nyuma kufuatilia tukio.
Huduma ya matangazo kidigitali kwa kutumia wasanii na watu maarufu yaanzishwa nchini.
—
Kampuni inaoongozwa kwa kutoa
huduma ya matangazo ya biashara nchini ya Aggrey & Clifford
imezindua kitengo cha kutoa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya
kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara
zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii ambayo
itanufaisha pande zote zitazoshiriki kutumia huduma hii .
Huduma hii ya kisasa
inayoendana na wakati wa sasa wa kizazi kipya inawezesha matangazo
kuwafikia walengwa wengi na kwa haraka inasimamiwa na kampuni tanzu ya
masuala ya huduma za matangazo ya biashara kwa kutumia teknolojia ya
kidigitali ya Aggrey&Clifford inayojulikana kama Binary.
Uzinduzi wa kitengo hiki cha
matangazo kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayoleta mapinduzi katika
sekta ya matangazo ya biashara nchini umefanyika jana katika hoteli ya
Hyatt Regency ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na
ilihudhuriwa na wataalamu wa masoko kutoka makampuni ya FMCG, huduma za
mawasiliano,mabenki na taasisi mbalimbali za biashara ikiwemo wasanii na
wanamichezo.
Kampuni ya Binary kwa kuanza
tayari inashirikiana na wasanii na watu maarufu Zaidi zaidi ya 40 ambao
miongoni mwao wapo wasanii wa filamu,wanamuziki,watangazaji maarufu wa
redio na luninga. Kutokana na ushirikiano huu Binary itawatumia katika
huduma za matangazo za wateja mbalimbali wanaotangaza huduma na bidhaa
zao kidigitali ili kuwafikia watumiaji wa huduma/bidhaa wengi na kwa
urahisi.
Huduma hii mpya ya matangazo
katika bara la Afrika unanufaisha watangazaji kwa huduma zao kuwafikia
wananchi ama wateja wengi kutumia umaarufu wa wasanii na watu maarufu
ambao pia wananufaika kwa kupata mapato ya uhakika kutokana na kutumiwa
kwao katika huduma ya matangazo na pia ina unafuu kulinganisha na njia
nyingine za matangazo.
Profesa Elisante Ole Gabriel
alisema kuwa serikali inao dhamira ya kuwasaidia wasanii wa tasnia
mbalimbali na wanamichezo na alipongeza kuanzishwa kwa huduma hii nchini
ambao itaongeza ajira na vipato vya wasanii wakati huohuo kunufaisha
makampuni kwa njia ya matangazo ya biashara zao.
Naye Mkurugenzi wa Ukuzaji
Biashara wa Binary, Eni Kihedu amesema “Huduma hii mpya ni jukwaa la
aina yake lya matangazo ya baiashara kwa kuwa inawezesha matangazo
kuwafikia walengwa kwa asilimia 100% kwa kulinganisha na kutangaza kwa
kutumia magazeti na ama majarida na inaleta unafuu kwa watangazaji ambao
kwa kutumia mtandao wasanii zaidi ya 40 ambao tunashirikiana nao
kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii matangazo yataweza kuwafikia
watumiaji wa bidhaa na huduma zaidi ya milioni 20 nchini na tunao uwezo
wa kufikia watu wengi zaidi”.
Kuhusiana na huduma hii mpya ya
matangazo itakavyonufaisha wasanii Kihedu alisema “Tunatumia fursa ya
kutumia teknolojia ya digitali katika biashara ambayo itaongeza vipato
vyao wakati huohuo vipaji vyao kuendelea kuonekana kwa watu wengi katika
jamii na kuwawezesha kuwekeza zaidi kwenye fani yao na tasnia yao”
Aliongeza kuwa ushirikiano wa
Binary na wasanii katika huduma za matangazo utafanyika kwa uwazi na
kunufaisha pande zote na kutafanyika makubaliano maalumu ya malipo
kutokana na viwango vinavyotozwa kwa kila tangazo litakalowekwa kwenye
akaunti za mitandao yao ya kijamii na kulingana na wafuasi wanaotembelea
akaunti zao.
“Viwango vya matangazo viko
wazi kwa watangazaji na wasanii hivyo tunaamini kila upande utanufaika
inavyostahili .Tunaamini njia hii ni jukwaa la aina yake kwa watangazaji
kufikisha matangazo yao kwa wateja wanaowalenga kwa kuwa njia
zilizokuwa zinatumika awali kutangaza hazina nafasi tena kutokana na
mabadiliko ya tekonolojia“.Alisema
HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAJIPANGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA UFINYU WA BAJETI
Hospitali
ya Taifa Muhimbili imekuwa na mafanikio kadhaa katika utoaji wa huduma
kwa wananchi. Mafanikio haya ni pamoja na uwepo huduma ya uhakika ya
tiba ya figo na kuchuja damu, ikiwa ni jumla ya mashine ambapo kwa sasa
kuna mashine 17, kuboreshwa kwa huduma ya magonjwa ya matumbo na ini.
Aidha tumeanza kwa muda kufanya upasuaji kwa njia ya hadubini
(Laparascopic Surgery )hususani kwa magonjwa ya masikio, pua na koo, na
katika eneo hili idara husika naongoza katika matumizi ya technologia
hii mpya. Tumeanza upasuaji wa macho kwa kutumia vifaa vya kisasa
(retina surgery), kuimarisha huduma za Uuguzi (Super Specialists Nursing
care in Critical Care, Mental Health). huduma nyingine zilizoboreshwa
ni kupanua Idara ya Kinywa na Meno (Preventive Dentistry na Pediatric
Dentistry). Kwa upande wa Maabara kuwa na vifaa vipya vya kisasa katika
kuhakikisha huduma hiyo inatolewa kwa ubora wa hali wa ya juu. Kuna
mashine mpya ya Architect Analyzer C4100 ambapo mashine moja inaweza
kupima vipimo zaidi ya 1,200 kwa saa moja ili kupunguza muda wa wagonjwa
kusubiri majibu kwa muda mrefu. Uwepo wa famasi mbili zinazofanya kazi
kwa saa 24 na kuhakikisha idara zote 18 za tiba zina watalaam wa
ubingwa wa juu (superspecialist).
Pamoja na mafanikio haya, pia
imekuwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali za uendeshaji na katika
utoaji wa huduma kwa wagonjwa zinazojumuisha upungufu wa rasilimali
fedha. Katika makala haya, Hospitali imejipanga kutekeleza yafuatayo ili
kukabiliana na changamoto;
Kuongeza Mapato na Kupunguza Gharama za Uendeshaji.
Hospitali imejipanga katika
kuongeza mapato na kupunguza matumizi ili kuongeza uwezo wake wa
kujiendesha na kutoa huduma za ufanisi kwa wagonjwa.
Kuongeza Mapato
Hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato ikiwemo:-
CCM ZANZIBABAR YASISITIZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA DR.MAGUFULI.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM)
Zanzibar kimewasisitiza watendaji wa Chama na Jumuiya zake kuharakisha
zoezi la kuhorodhesha Mali za taasisi hizo ili kutekeleza kwa vitendo
agizo la chama hicho.
Akizungumza na watendaji wa
chama, jumuiya na watumishi wa chama hicho wa ngazi mbali mbali , Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai huko afisi kuu ya CCM
Kisiwanduzi Unguja.
Alifafanua kwamba hatua hiyo
inatokana na agizo la Mwenyekiti mpya wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli
aliyetaka mali za chama hicho kuhorodheshwa haraka kwa lengo la
kuimarisha chama hicho.
Alisema kwamba CCM Zanzibar
ilianza utaratibu wa kukagua mali zake kabla ya Mwenyekiti huyo kutoa
agizo hivyo anatarajia kwamba watendaji hao watatekeleza kazi hiyo
haraka na kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa ili kuepuka usumbufu
usiokuwa wa lazima.
Alieleza kwamba licha ya Chama
kupata ruzuku kutoka serikali bado kina wajibu wa kutumia rasilimali
zake vizuri kuongeza vyanzo vya mapato ili kuongeza ufanisi wa
kiutendaji ndani ya chama hicho.
Alisema hatua ya kuhorodhesha
mali za chama hicho iambatane na kumaliza kasoro na mapungufu yaliyopo
katika miradi ya chama na jumuiya hasa kupitia upya mikataba ya
ukodishwa ili kuhakikisha inakidhi na kufuata utaratibu wa kisheria.
“ Nawakumbusha watendaji wenzangu
wa CCM kwamba tujiandae vizuri kifikra kwa kuhakikisha tunafanya kazi
kwa bidii kubwa na kuacha tabia za kufanya kazi kwa mazoea kwani huu ni
wakati wa mabadiliko kwa kila sekta ndani ya chama chetu.
Pia mnajua kwamba chama chetu
hivi karibuni kumefanyika Mkutano Mkuu Maalum na kumpata Mwenyekiti Mpya
Dkt. Jonh Pombe Magufuli atakayesaidiana na Makamo Mwenyekiti wake Dkt.
Shein kuhakikisha wanaendeleza kuimarisha na kukuza ustawi wa CCM,
hivyo nasi ni lazima twende sambamba na kasi ya utendaji wao.”., alisema
Vuai.
KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAANZISHA KIFURUSHI KIPYA MAHSUSI CHA MIITO NA DATA KATIKA TAMASHA LA FIESTA 2016
Meneja
Chapa wa Kampuni ya Simu ya Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Kampuni hiyo,
Kijitonyama Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu kampuni hiyo kuanzisha
kifurushi kipya mahsusi cha miito na data katika tamasha la Fiesta 2016.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Tamasha la Fiesta, Sebastian Maganga.
Mwenyekiti wa Tamasha la Fiesta, Sebastian Maganga (kushoto), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya simu ya Tigo imetangaza vifurushi viwili vipya vya miito na data
vinavyofahamika kama ‘Vifurushi vya Fiesta’ (Fiesta packages) ambavyo
vinalenga kuwanufaisha watega wote wa Tigo na wasio wakati wa tamasha la
Fiesta 2016.
Vifurushi hivi vya kuvutia vitakuwa vinapatikana kwa wateja wote watakaohudhuria matamasha na hata wasio hudhuria.
Vifurushi
vipya vitawawezesha wateja kuchagua kati ya data za GB 1 au visivyo
na ukomo ambavyo vinajumuisha dakika 490 Tigo kwenda Tigo, dakika 10
mitandao yote na SMS 100 kwa shilingi 1000 wakati wale ambao sio wateja
wa Tigo ambao wamenunua kadi ya simu ya 4G ya Tigo watapata dakika 60,
sms 60 na MB 60 papo hapo pindi wanapojisajili na baadaye kuchagua kati
ya data na kifurushi kisicho na ukomo.
Akizungumza
katika mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya Tigo,
Meneja Chapa, William Mpinga alisema, “vifurushi hivi vimekuwa ikiwa ni
ahadi tulioyoitoa kwa wateja wetu kuhusu ofa mbalimbali na promosheni
ambazo zitakuwepo wakati wa msimu wa Fiesta 2016. Hali kadhalika
tutaendelea na uanzishaji wa bidhaa na huduma za ubinifu ili kukidhi
mahitaji ya wateja wetu na pia kutoa nafasi kwa wateja wapya.”
Mpinga
alifafanua kuwa tamasha la Fiesta 2016 linawakaribisha Watanzania wote
na kuongeza kuwa pia tukio hilo litatoa shughuli zenye mabadiliko
kijamii.
Mpinga
alisema, “Mwanzoni wa wiki iliyopita tulianzisha kauli mbiu ya tamasha
la fiesta inayosema, “Fiesta 2016 Kwa Kishindo cha Tigo, Imooooo!”
ambapo mantiki iliyopo katika kauli mbiu hii ni kutoa bidhaa na huduma
ambazo ni mahsusi kwa wateja wetu katika kipindi cha tamasha.”
Mwenyekiti
wa Tamasha la Fiesta 2016, Sebastian Maganga alisema, “ Tunafurahi
sana kutangaza kwamba tamasha la Fiesta 2016 litaanza rasmi jijini
Mwanza Agosti 20, 2016. Kwa hiyo wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake
watarajie kupata vifurushi hivi maalum pamoja na shughuli za kufurahisha
katika kipindi cha wiki nzima kabla ya tamasha.”
Tamasha
la Fiesta 2016 linaandaliwa kila mwaka na kampuni ya Prime Time
Promotions, na hivi sasa ni mwaka wa 15 tangu kuanziswhwa kwake na
linatarajiwa kujumuisha mikoa 15 ambayo ni pamoja na Mwanza, Kahama,
Kagera, Musoma, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga,
Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Mbeya na Dar es Salaam.
Tamasha la Fiesta 2016 linafanyika kwa ushirikiano wa Prime Time Promotions na Tigo Tanzania ambayo ni mdhamini mkuu.
TIMU TEULE ZA JESHI KUKABIDHIWA BENDERA KWA AJILI YA KUELEKEA RWANDA KESHO(LEO)
Picha na Maktaba
…………………………………………………………………………………….
Na mwandishi wetu JWTZ
Timu teule za Jeshi la wananchi
wa Tanazania zinazotarajiwa kushiriki mashindani ya majeshi kwa nchi za
Afrika mashariki zinatarajiwa kukabidhiwa bendera ya Taifa Kesho(Leo)
tayari kuelekea Kigali chini Rwanda kwa ajili ya mashindano hayo.
Kwa Mijubu wa Afisa habari wa
Michezo Kutoka makao Makuu ya Jeshi Luteni Selemani Semunyu alisema
mkuu wa Operesheni na mafunzo Meja Jenerali Issa Nassoro ndiye
anayetarajiwa kukabidhi bendera hiyo kwa Niaba ya Mkuu wa majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange.
Luteni Semunyu alisema kuwa
Hatua hiyo inafikiwa baada ya Timu hizo kuweka kambio katika Visiwa vya
Zanziba kwa Michezo minne huku Riadha wakiweka kambi Arusha kabla ya
kambi hiyo kuhamishiwa mbulu Mkoani Manyara kutokan na haliya hewa.
Aliitaja Michezo hiyo kuwa mpira
wa miguu,pete,Mikono,Kikapu na Riadha ambapo wachezaji wako katia ari
ya hali ya juu kutokana na wito wa mkuu wa majeshi kuwatak kurejesha
hshima ya JWTZ katika Michezo.
ASlifafanua kuwa QWachezaji wa
Timu hizo teule walipatikana baada ya kupitia hatua mbali mbali za
mcvhujo kwa kuanzi na kombe la Mkuu wa majeshi ambalo lilishirikisha
kuanzia ngazi ya Viko mpaka kamandi na hivyo kuibua vipaji.
Michezo ya majeshi kwa Nchi za
Afrika Mashariki imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa kuhama nchi wenyeji
kutoka na utarativbu waliojipangia nchi wananchama ndio maan mwaka huu
yanafanyika nchini Rwanda na Mwakani yatahamia katika nchi nyingine
amabayo itatangazwa baada ya kumalizika mashindano haya.
Timu teule za Jeshi zinatarajia
kuanza safari kuelekea Kigali nchini Rwanda Agosti nne siku moja baada
ya kukabidhiwa bendera ili kuwahi ratiba ya kuanza mashindano hayo
yanayotarajia kuanza Agosti saba na Kumalaizika Agosti 17.
MHE. KAIRUKI KATIKA KIKAO KAZI WATUMISHI KUJADILI MATUMIZI YA TEHAMA SERIKALI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia)
akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro
(aliyeinua mkono) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao kazi na
baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais- Utumishi kuhusu utoaji huduma na
matumizi ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi
wa utumishi leo, wa tatu kulia (mstari wa mbele) ni Naibu Katibu Mkuu
Utumishi na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akielekeza
jambo kwa baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Utumishi wakati wa kikao
kazi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA kilichofanyika katika
ukumbi wa utumishi leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimsikiliza
Mkurugenzi wa TEHAMA katika Utumishi wa Umma, Bw. Priscus Kiwango
wakati wa kikao kazi kuhusu utoaji huduma na matumizi ya TEHAMA katika
Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na baadhi ya
Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakijadili kuhusu matumizi ya TEHAMA
katika utoaji huduma Serikalini wakati wa kikao kazi kilichofanyika
katika ukumbi wa utumishi leo.
RIDHIWANI:VIJANA WAJITAMBUE WAACHE KUTUMIWA /WACHANGAMKIE FURSA ZILIZOPO
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akizungumza na vijana wa
Chalinze Saccos iliyoanzishwa jimboni hapo ambapo Ridhiwani ni mlezi wa
saccos hiyo(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Vijana
wa Chalinze saccos wakiwa katika mkutano uliolenga kuzungumzia masuala
mbalimbali ya saccos hiyo ambapo pia walimchagua mbunge wa jimbo la
Chalinze Ridhiwani Kikwete kuwa mlezi wao.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE
wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amewataka vijana wajitambue na
kuacha kutumiwa kama ngazi na baadhi ya watu kwa ajili ya maslahi yao
binafsi na badala yake wajikite kwenye shughuli ndogondogo za
kujiongezea kipato.
Aidha
mbunge huyo amekubali kuwa mlezi wa Chalinze vijana saccos ambayo
itakuwa mfuko wa kuwezesha vijana kiuchumi na kutambulishwa fursa
mbalimbali za kimaendeleo.
Ridhiwani
aliyasema hayo, kwa vijana mbalimbali mjini Chalinze katika mkutano wa
kuchagua viongozi wa muda mfupi wa saccos hiyo na mlezi pamoja na
kujadili masuala ya kimaendeleo .
Alisema
vijana wabadilike kwa kuchangamkia fursa zilizopo sanjali na kujiajiri
ili hali kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Ridhiwani
alisema ipo tabia kwa baadhi ya vijana ambao hushawishiwa kujiingiza
kwenye mambo yasiyo na tija katika maisha yao kuliko kuwashawishi
kuwajengea uwezo wa kuinua uchumi wao kimaisha.
Aliwaasa
vijana kujitambua kwa kutumia fursa chache zilizopo ikiwemo kuanzisha
vikundi vya kiujasiliamali,kutumia mafungu ya fedha zinazotengwa na
halmashauri,licha kuwepo changamoto za mtaji .
Ridhiwani
alisema yupo bega kwa bega na vijana hao bila kujali itikadi za kisiasa
ambapo atahakikisha anawaonyesha fursa mbalimbali.
“Tatizo
ni kwamba vijana hawajazitambua fursa ama kushindwa kuzitumia,kwa
upande mmoja na kwa upande mwingine wale walioziona hawana uwezo wa
kifedha ili kuzifikia”alisema Ridhiwani.
Ridhiwani
alieleza kuwa ni imani yake kama mlezi wa saccos hiyo kuwaonyesha
fursa zilipo na kuzitumia huku akishirikiana nao kupata mitaji kwa
kutumia wafadhili,halmashauri na taasisi zinazojishughulisha na masuala
ya kusaidia vijana.
Hata
hivyo Ridhiwani alisema ameshawezesha vijana wengi jimboni hapo
kujikwamua kiuchumi lakini changamoto ipo kwenye kujitambua na kumtumia
katika kumfikisha kijana husika katika hatua nzuri kimaisha.
Aliwaasa
vijana kuwa na moyo wa kuwa na maendeleo pale wanapopata mtu wa
kuwainua bila ya kufanya makosa ya kutumia nafasi wanayoipata na hatimae
kujutia baadae.
Ridhiwani
aliwataka vijana kujiunga makundi katika shughuli zao na kuacha
ubinafsi ili kuweza kusaidiwa na kufikiwa kirahisi kuliko kuwa mmoja
mmoja.
Kwa upande wa vijana hao wa halmashauri ya Mji wa Chalinze kwa ujumla wao walimchagua Ridhiwani kuwa mlezi wao .
Walisema wameamua kwa pamoja kuunga mkono hatua za serikali kuwezesha vijana kiuchumi kupitia vicoba na saccos.
“Tumeanzisha
Chalinze vijana saccos,ambayo itakuwa mfuko wa kuwezesha vijana
kiuchumi na kutambua fursa za kuzikimbilia ili kujikomboa katika kupiga
vita umaskini’walisema.
MADIWANI MJI WA KIBAHA WAWAASA WATENDAJI/WATAALAMU WA HALMASHAURI KUSIMAMIA ILANI
Madiwani
mbalimbali wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, wakiwa katika kikao cha
baraza la madiwani ambacho kilijadili na kupitisha agenda ikiwemo
taarifa ya maendeleo ya kata,kupokea taarifa ya mapato na matumizi
ambapo waligomea kupitisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
ya mwaka jana baada ya kubaini mapungufu makubwa.(Picha na Mwamvua
Mwinyi)
……………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MADIWANI
wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,wamewataka wataalamu na watendaji wa
halmashauri hiyo kuwa makini katika kuandaa taarifa mbalimbali ikiwemo
ya utekelezaji wa ilani ili kuondokana na usumbufu wa kufanya maboresho
yasiyo ya lazima.
Wamesema
taarifa ya utekelezaji wa ilani ya mwaka jana ambayo ilikuwa
ikijadiliwa katika kikao cha madiwani kilichofanyika ,kujadili mambo ya
maendeleo,ilani na mapato na matumizi ,ina mapungufu makubwa.
Aidha
madiwani hao wamewaagiza wataalamu na watendaji hao kufanya maboresho
na kuirekebisha taarifa hiyo ili mwezi ujao iweze kujadiliwa na
kupitishwa rasmi.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti madiwani hao walisema,agenda ya kupitia taarifa
hiyo muhimu ya uchaguzi ya mwaka 2015 wameiahirisha kwa ajili ya
maboresho kabla ya kwenda chama.
Walielezea
kuwa ni ngumu kuikwepa ilani ya chama tawala kwa kukubali kufanyakazi
za serikali pasipo kuifanyia kazi ilani hiyo ambayo utekelezaji wake
unakwenda sambamba na serikali iliyo madarakani.
Diwani
wa kata ya Visiga ,Mbegu Legeza,alisema watendaji ,wataalamu wa
serikali sambamba na halmashauri wanapaswa kusimamia kikamilifu
utekelezaji wa ilani .
“Tuliyoyaona
kwenye taarifa ya ilani hii mengi yamechotwachotwa na kubambikwa huku
miradi mingine ikiwa haijawekwa kwenye taarifa hiyo”
“Mambo
mengi hayapo sawa ukisema mmekopesha vikundi lazima iainishwe kata
ngapi wamepewa hizo fedha,makundi gani yamepokea fedha,kuna viwanda
vimejengwa na kuwekezwa vingine vimeandikwa vingine havijaandikwa”
“Kuna
vikundi vimefundishwa lakini diwani wa kata husika hajui na kwenye
kabrasha imeandikwa kuna elimu imetolewa kwenye kata hiyo hapo ni lazima
diwani husika akatae”alisema legeza.
Diwani
wa kata ya Mailmoja ,Ramadhani Lutambi alieleza kuwa ,hali hiyo
inaonyesha udhaifu mkubwa kwa wataalamu hao kwa kushindwa kufanya kazi
zao kwa uhakika.
Mwenyekiti
wa halmashauri hiyo Leonard Mloe,alikiri kuwepo kwa mapungufu kwenye
taarifa hiyo ambapo alisema agenda nyingine zilijadiliwa na kupitishwa
bila tatizo.
Agenda
zilizojadiliwa ilikuwa ni pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa
miradi ya maendeleo robo ya nne april-juni 2016 ,taarifa ya maendeleo
ya kata na kupokea taarifa ya mapato na matumizi.
Nae
mwenyekiti wa CCM mji wa Kibaha ,Maulid Bundala, alitoa wito kwa baraza
hilo kubadili utaratibu wa kupitia taarifa ya ilani kwenye baraza hilo
kwa kutenganisha na kuichambua ilani hiyo kwenye vikao vingine ambavyo
haviudhuliwi na viongozi wa vyama.
Alisema
raha ya chakula usikione kikipikwa wala kuandaliwa hivyo ni vyema
ukafanyika utaratibu mwingine wa kujadiliwa taarifa hiyo kwenye kikao
cha madiwani pekee kabla ya baraza.
Hata
hivyo Bundala alisema baada ya kujadiliwa taarifa hiyo ni lazima
itafika katika chama hivyo hakuna sababu ya kujadiliwa wakati wao
wakiwepo.
Alisema
watendaji,watalaamu wa serikali na halmashauri hawawezi kukwepa ilani
ya chama cha mapinduzi ,na kusema anaeona kichefuchefu kutekeleza ilani
hiyo atoke nje wakati wa kuijadili.
“Itakuaje
maziwa ya ng’ombe yawe mazuri halafu ng’ombe wake awe mbaya,serikali
hii inaongozwa na CCM,sasa utakwepaje kuisimamia ilani ya chama
tawala,jamani huu ni wakati wetu na ukifika wa chama kingine itasimamiwa
ilani yao”alisema Bundala.
Bundala
alieleza kuwa hata kama ni mkurugenzi ameajiliwa na serikali ambayo
imenatekeleza ilani ya CCM hivyo kuna kila sababu ya watendaji wote
kufanyakazi kwa moyo na kusimamia majukumu yao.
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Lucy Kimoi alisema
wamepokea ushauri na maagizo yote na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi.
Katika hatua nyingine halmashauri hiyo imekisia kukusanya kwa mwaka 2015/2016 bil 3.744 katika mapato yake ya ndani .
Robo ya nne inayoishia juni
mwaka huu,imekusanya mil.732.102 na kufanya jumla ya mapato
yaliyokusanywa julai /juni 2016 kuwa zaidi ya bil.2.910.866 sawa na
asilimia 78 ya makisio.
Pia imekisia kutumia zaidi ya bil.31.836.942 kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi wa mji huo .
Katika utekelezaji wa shughuli zake kwa robo ya nne iliyoishia juni 2016
imetumia bil.5.950.420 na kufanya jumla ya matumizi kwa julai/juni
mwaka huu kufikia bil.21.614.164 sawa na asilimia 67 ya makisio.
WAZIRI MKUU MAJALIWA AVITAKA VIWANDA VYA SUKARI KUZALISHA ASILIMIA 100 YA MAHITAJI IFIKAPO 2020
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha sukari cha Kagera, Ashuwin Rana baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa Agosti 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, Seif Ali Seif .
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha
sukari cha Mtibwa kukagua uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho,
Agosti 2, 2016. Kulia ni mkewe Mary, wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa
wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Kiwanda cha sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif Ali Seif . Kushoto ni
Kaimu Katibu wa CCM mkoa Wa Morogoro, Kulwa Solobi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya kumwagilia
katika shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mtibwa wakati
alipokitembelea kiwanda hicho, Agosti 2, 2016. Kushoto ni mkewe Mary
na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera na
Mtibwa, Seif Ali Seif .
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya kumwagilia
katika shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mtibwa wakati
alipokitembelea kiwanda hicho, Agosti 2, 2016. Kushoto ni mkewe Mary
na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera na
Mtibwa, Seif Ali Seif.
Waziri
Mkuu, Kassimu Majaliwa na Mkewe Mary wakisalimiana na wafanyakazi wa
kiwanda cha sukari cha Mtibwa wakati alipotembelea kiwanda hicho Agosti
2, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephene Kebwe.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari
cha Mtibwa wakati alipokitembelea kiwanda hicho Agosti 2, 2016.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amevitaka viwanda vya sukari nchini kuongeza mikakati ya uzalishaji
zaidi ili mwaka 2020 Tanzania iwe imefikia kiwango cha kuzalisha
asilimia 100 ya mahitaji yake.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumanne, Agosti 02, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha
Mtibwa kilichoko mkoani Morogoro ambapo amesisitiza viwanda vya ndani
vizalishe zaidi ili kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya
nchi.
Amesema Serikali imejikita katika
kuimarisha na kulinda viwanda vya ndani nchini hivyo ni vema viwanda vya
sukari vikaweka mikakati ya kuzalisha kwa wingi ili kuondokana na
uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje.
“Kiwango cha mahitaji ya sukari
nchini ni zaidi ya tani 400,000, nimeiagiza Bodi ya Sukari kukaa na
wataalamu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kufanya utafiti ili
tujue mahitaji halisi ya sukari,” alisema.
Waziri Mkuu amesema Serikali
imeweka mkakati wa kulinda viwanda vya ndani kwa kuziongezea kodi bidhaa
zinazotoka nje ambazo zinazalishwa na viwanda vya ndani ikiwemo sukari
hivyo wenye viwanda hawana budi kuzalisha kwa wingi zaidi.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka
wamiliki wa viwanda vya sukari nchini kutoa motisha kwa wakulima wa nje
kwa kununua miwa yao kwa bei nzuri na kuwalipa kwa wakati ili nao
wanufaike na uwepo wa viwanda hivyo na kuwa walinzi wa uwekezaji huo.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano
Mwandamizi wa kiwanda hicho, Ibrahim Juma amesema kwa sasa kiwanda
kinazalisha tani 20,000 kwa mwaka na wanatarajia kuongeza uzalishaji
hadi kufikia tani 70,000 ifikapo mwaka 2021.
Juma alisema uzalishaji wa sukari
kiwandani hapo ulipungua kutokana na uingizwaji wa sukari kutoka nje
hivyo aliipongeza serikali kwa kudhibiti uingizwaji holela wa sukari
kutoka nje jambo litakalosaidia ukuzaji wa viwanda vya ndani.
Meneja huyo alisema kuwa kwa sasa
wameanza upanuzi wa mashamba kiwandani hapo ambapo wanatarajia kuongeza
hekta 400,000 lengo likiwa ni kutimiza ndoto ya Serikali ya kuifanya
Tanzania ijitosheleze katika uzalishaji wa sukari.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 02, 2016.
WASIFU WA MAREHEMU KAMISHNA MSTAAFU WA MAGEREZA EGNO KAMILIUS KOMBA
KAMISHNA MSTAAFU WA MAGEREZA MAREHEMU EGNO KAMILIUS KOMBA
………………………………………………………………………………….
Marehemu Kamishna Mstaafu wa Magereza EGNO KAMILIUS KOMBA alizaliwa tarehe 20 Oktoba, 1947 katika
Kijiji cha Mtungu – Kindimba Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma. Mwaka
1956 alijiunga na Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Kindimba na
kuhitimu elimu hiyo mwaka1959. Alijiunga na Shule ya Kati (Middle
School) ya Litembo mwaka 1960 na kuhitimu mwaka 1963. Alijiunga na Shule
ya Sekondari ya Kigonsera mwaka 1964 na kuhitimu Kidato cha Nne mwaka
1967. Mwaka 1968 alijiunga na Shule ya Sekondari
Karimjee iliyopo Mkoani Tanga na kuhitimu mwaka 1968.
Marehemu aliajiriwa na Jeshi la Magereza tarehe 02 Agosti, 1972 na kupelekwa kuhudhuria mafunzo ya awali ya Uaskari katika Chuo cha Usalama – Moshi. Marehemu alihitimu mafunzo hayo tarehe 30 Aprili, 1973 na kupangiwa kufanya kazi Gereza Malya, Mkoa wa Shinyanga.
Mwaka 1975 akiwa mwajiriwa wa Jeshi la Magereza, Kamishna mstaafu wa Magereza, Marehemu EGNO KAMILI US
KOMBA alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya masomo ya
Shahada ya Kwanza katika Uchumi na kuhitimu mwaka 1978.
Marehemu akiwa Jeshini alitunukiwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:-
Afisa Magereza Daraja la III (PO III)– 30/ 04/1973 – 31/09/1973
Afisa Magereza Daraja la I (PO I)- 01/09/1973 – 31/06/ 1976
Afisa Magereza Mkuu (PPO)-01/07/1976 – 30/ 11/1978
Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP)- 01/12/1978 – 31/09/1980
Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) – 01/10/1980 -31/12/1996
Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) - 01/07/1984 -19/09/1989
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP)-20/09/1989-30/ 6/1996
Kamishna wa Magereza (CP) - 01/07/1996 – 30/06/2007 (Alipostaafu kwa umri Mkubwa).
Marehemu alifanya kazi katika vituo vifuatavyo vya Magereza:-
Gereza Malya – Shinyanga - Tarehe 01/05/1973 – 12/05/1974
Makao Makuu ya Magereza - Tarehe 13/05/1974 – 30/06/2007
Katika utumishi wake Jeshini Marehemu pia alitunukiwa nishani mbalimbali kama ifuatavyo:-
Katika utendaji wake wa kazi, Marehemu alikuwa na uwezo
mkubwa wa kujifunza, kutawala na kuyamudu majukumu yake ya
kazi ipasavyo. Viongozi na watumishi wa Jeshi la Magereza tunamlilia
mno kwa Utumishi wake uliotukuka na hazina kubwa ya utendaji aliyoondoka
nayo kwani hata baada ya kustaafu katika Jeshi la Magereza bado
alikuwa akitoa ushauri katika mambo mbalimbali ya Uendeshaji wa Jeshi la
Magereza.
Kamishna Mstaafu wa Magereza EGNO KAMILIUS KOMBA alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa Moyo hadi umauti ulipomkuta mchana ya tarehe 31 Julai, 2016 nyumbani kwake Mvuti, Chanika Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuzikwa kesho Agosti 3, 2016 Shambani kwake Mvuti, Jijini Dar es Salaam.
MWENYEZI MUNGU AIWEKE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU EGNO KAMILIUS KOMBA, AMEN
Marehemu Kamishna Mstaafu wa Magereza EGNO KAMILIUS KOMBA alizaliwa tarehe 20 Oktoba,
Marehemu aliajiriwa na Jeshi la Magereza tarehe 02 Agosti, 1972 na kupelekwa kuhudhuria mafunzo ya awali ya Uaskari katika Chuo cha Usalama – Moshi. Marehemu alihitimu mafunzo hayo tarehe 30 Aprili, 1973 na kupangiwa kufanya kazi Gereza Malya, Mkoa wa Shinyanga.
Mwaka 1975 akiwa mwajiriwa wa Jeshi la Magereza, Kamishna mstaafu wa Magereza, Marehemu EGNO KAMILI
Marehemu akiwa Jeshini alitunukiwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:-
Afisa Magereza Daraja la III (PO III)– 30/
Afisa Magereza Daraja la I (PO I)- 01/09/1973 – 31/06/
Afisa Magereza Mkuu (PPO)-01/07/1976 – 30/
Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP)- 01/12/1978 –
Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) – 01/10/1980
Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) - 01/07/1984
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP)-20/09/1989-30/
Kamishna wa Magereza (CP) - 01/07/1996
Marehemu alifanya kazi katika vituo vifuatavyo vya Magereza:-
Gereza Malya – Shinyanga - Tarehe 01/05/1973 – 12/05/1974
Makao Makuu ya Magereza - Tarehe 13/05/1974 – 30/06/2007
Katika utumishi wake Jeshini Marehemu pia alitunukiwa nishani mbalimbali kama ifuatavyo:-
•
Nishani ya Mstari wa Nyuma ya Vita vya Kagera,
•
Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzania na,
•
Nishani ya Utumishi Uliotukuka.
Kamishna Mstaafu wa Magereza EGNO KAMILIUS KOMBA alikuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa Moyo hadi umauti ulipomkuta mchana ya tarehe 31 Julai, 2016 nyumbani kwake Mvuti, Chanika Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuzikwa kesho Agosti 3, 2016 Shambani kwake Mvuti, Jijini Dar es Salaam.
MWENYEZI MUNGU AIWEKE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU EGNO KAMILIUS KOMBA, AMEN
MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) KATIKA MADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA MKOANI LINDI
Mkuu
wa Kitengocha uhusino na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika
(katikati) akigawa baadhi ya vifaa vya uhamasishaji kwa wadau
waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya sherehe za Wakulima
katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi jana. Maadhimisho ya sikukuu
hiyo, yatafanyika Agost 8, 2016.
Bi.
Sarah Kibonde Msika (kulia) na Bw. Mathayo Mihayo (Kushoto) wakitoa
maelezo mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi waliotembelea banda
la SSRA katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi katika maonesho ya Nane
nane.
Wananchi
mbalimbali wakipata maelezo ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka kwa
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii
(SSRA) katika maonesho ya Nane nane.
Wananchi
mbalimbali wakipata maelezo ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka kwa
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii
(SSRA) katika maonesho ya Nane nane mjini Lindi jana.
Mkulima
akipokea vipeperushi na maelezo toka kwa Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi
na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. David Mathayo
katika maonesho ya wakulima Nane nane mkoani Lindi jana.
Afisa
Uhusiano na Uhamasishaji Bi. Agnes Lubuva akitoa malezo na vipeperushi
kwa wageni waliotembelea banda la SSRA katika Viwanja vya Ngongo mkoani
Lindi wakati wa maonesho ya Wakulima jana.
AMASHA LA MAADILI LILIVYO TIKISA DAR
Mbunge
wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akizungumza katika Tamasha la
maadili kwa vijana lililoandaliwa na Tumaini Media kupitia Jimbo Kuu
la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki lililofanyika Katika uwanja wa Uhuru
juzi
Umati wa wananchi uliohudhuria katika tamasha hilo.
Aliyekuwa
mgeni wa heshima katika Tamasha la Maadili, Balozi Paul Rupia,
akizungumza katika tamasha hilo lililoandaliwa na Tumaini Media kupitia
Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki lililofanyika Katika
uwanja wa Uhuru juzi.
Kwaya
ya Mtakatifu Kizito wakitumbuizaatika Tamasha la maadili kwa vijana
lililoandaliwa na Tumaini Media kupitia Jimbo Kuu la Dar es Salaam la
Kanisa Katoliki lililofanyika Katika uwanja wa Uhuru juzi
No comments :
Post a Comment