Tuesday, July 5, 2016

Waziri wa Ajira, Vijana ATEMBELEA BANDA LA LAPF katika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa


Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akipata maelezo ya ujumla kuhusu Mfuko wa Pensheni wa LAPF katika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa. Anayetoa maelezo ni Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko Bi. Rehema Mkamba.
L2 
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mifumo ya Kompyta wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yohana Nyabili kuhusu upatikanaji wa taarifa za michango ya wanachama kupitia tovuti ya Mfuko www.lapf.or.tz na simu za viganjani kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
L3 
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akionyeshwa taarifa yake ya michango ya Hiari LAPF kwenye maonyesho ya biashara ya 40 ya kimataifa jijini DSM. Anayemhudumia ni Afisa Mafao ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bi. Irene Michael.
L4 
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akipata maelezo kuhusu shughuli za uwekezaji za Mfuko wa Pensheni wa LAPF pamoja na mipango ya Mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17, anayetoa maelezo ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko Bw. James Mlowe.
L5 
Baadhi ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kutoka Jeshi la Polisi wakipata maelezo mbalimbali ya Mfuko kutoka kwa Afisa wa Mfuko Bw. Yohana Nyabili kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini DSM.
L6Wanachama na wadau mbalimbali wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakipata maelezo mbalimbali kuhusu manufaa na huduma za Mfuko ikiwemo utaratibu wa kujiunga na kuweka akiba kwa hiari kwenye Mfuko. Anayetoa maelezo ni Afisa mafao wa Mfuko Bi. Judith Lupondo.

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUJITOKEZA WAWEZESHWE KUWEKEZA KWA AJILI YA MAENDELEO

Mkurugenzi wa kitengo cha Africa wa JICA, Hideki Watanabe akielezea Jinsi JICA wanavyofanya shughuli za Maendeleo Afrika
Mdau kutoka Namaingo Bi. Mariam akichangia jambo

Mkurugenzi wa Namaingo Bi.Ubwa Ibrahim akimwelezea jambo mwakilishi wa benki ya rasilimali
(TIB) walipokutana katika semina ya uwezeshaji mitaji kwa ajili shughuli za maendeleo.

Watoa mada kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za kifedha wakijibu maswali kutoka kwa wadau waliohudhuria semina hiyo.

Washiriki wakifuatilia semina
  —————————————–
Wajasiriamali wakubwa kwa wadogo wametakiwa
kujitokeza kwa wingi kutumia fursa zilizopo ili waweze kuwezeshwa mitaji ili
wawekeze katika shughuli za maendeleo ili kupunguza tatizo la ajira hapa nchini
na kusaidia juhudi za serikali na wadau kuleta maendeleo hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Balozi wa Japan hapa
nchini Bwana Masaharu Yoshida alipokua akifungua semina ya wadau wa maendeleo
iliyojadili uwezeshaji wa mitaji kwa wajasiriamali kwa ajili ya shughuli za
maendeleo iliyofanyika jana (5/6/2016) jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo iliyoandaliwa na shirika la
ushirikiano na maendeleo la Japan (JICA) pamoja na taasisi ya sekta binafsi
hapa nchini (TPSF) ilihudhuriwa na mashirika na taasisi za kifedha pamoja na
wajasiriamali kutoka sekta binafsi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, watoa
mada walionesha kuwa kuna fursa kubwa kwa watanzania wote walioamua kuwa
wajasiriamali kwa kufungua viwanda vidogo kwa vikubwa, wakulima na
wafanyabiashara kutumia mashirika na taasisi za fedha kujipatia mikopo nafuu
ili kuwezesha kukuza biashara na viwanda vyao na wanaweza kulipa kwa muda mrefu
kwa riba nafuu.
Semina hiyo ilibainisha kuwa changamoto
kubwa ni kutokua na taarifa kwa watanzania wengi na hivyo kuogopa kuwekeza kwa
kutumia taasisi za fedha jambo lililoungwa mkono na washiriki wengi kwani
imebainika kuwa ni asilimia 16 tu ya watanzania wanatumia huduma za kibenki
hivyo wameaswa kubadilika waweze kunufaika na mitaji ambayo ipo lakini hakuna
wanaokidhi vigezo ambapo wanaofuatilia na kunufaika ni watu wachache.
Mwavuli wa wajasiriamali wa Namaingo
(Namaingo Business Agency) ni moja ya taasisi zilizohudhuria na ziliahidiwa
kupewa ushirikiano na wadau wote wa kuwasaidia kufikia malengo yao kwani mitaji
ipo na Namaingo inakidhi vigezo vyote vya kukopesheka kwani mpango kazi wake
uko kitaalamu na ushiriki wa serikali na taasisi zake unaifanya iwe mkombozi
kwa watanzania wengi maskini.
Akizungumza baada ya semina hiyo Mkurugenzi
wa taasisi hiyo Bi. Ubwa Ibrahim aliwataka watanzania wote wajitokeze kujiunga
na taasisi yake wawekwe katika mpango wa kuwarasimisha na kuwawezesha kuingia
katika mipango ya kuwainua kiuchumi kwani kuna mradi wa kijiji biashara ambacho
wanachama wanatarajia kukopeshwa ardhi, kujengewa nyumba za makazi, kukopeshwa
mradi uliokamilika (kilimo na ufugaji) pamoja na utaalamu na usimamizi wa mradi
husika.
“Kwa sasa tuko katika hatua ya utekelezaji ambapo
tarehe 28 mwezi huu tunasaini mikataba na serikali na wadau wengine Diamond
Jubilee. Naomba watanzania waje washuhudie na kusikia juu ya mradi ili waamini
maanake kuna watu wanaongea bila kutenda, mimi nawakaribisha  waje waone
utendaji na tuwape ushuhuda wa hatua tulizokia kwenye mradi wetu wa kijiji
biashara ambapo serikali imetoa ekari 44,000 kwa ajili ya mradi huu. Maendeleo
hayakusubiri hivyo kila mtu achangamke aje atuone tumweke kwenye mpango rasmi”
alisema Bi.Ubwa.
Mwanasheria wa taasisi hiyo
aliyejitambulisha kwa jina moja la Bwana Payas alisema kila siku kuna mafunzo
katika vituo vya Namaingo vilivyopo Ubungo, Ukonga na Temeke ambapo alisema
wajasiriamali hupewa mafunzo kabla ya kuingizwa rasmi katika mpango wa
kampuni.  “Namaingo tunawezesha
wajasiriamali kusajiliwa TRA, BRELA, TFDA, Bima ya afya, mifuko ya jamii na
kuwaunganisha wao kwa wao. Kila Jumamosi tunakaribisha wanachama wapya
wanaopewa maelekezo na kuelezwa juu ya mradi wetu mkubwa wa kijiji biashara
kilichopo Mbawa, Rufiji ambapo Namaingo inaratibu mradi huo pamoja na wadau wa
maendeleo tukisimamiwa na baraza la uwezeshaji chini ya ofisi ya waziri mkuu”
aliongeza.

Serikali yaipongeza Benki ya Standard Chartered

TZ 
Na: Frank Shija, MAELEZO
——————–
Serikali imeipongeza Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kupeleka huduma za kibenki kwa wananchi wanao ishi katika maeneo ambayo benki hiyo haina matawi hapa nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa.Makame Mbarawa katika hafla fupi ya Iftari iliyoandaliwa na Benki hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
Mbarawa amesema kuwa Sekta ya Benki ni muhimu kwa jamii hivyo kwa Standard Chartered Tanzania kupeleka huduma zao kupitia ushirikiano baina yao na Benki ya Posta katika matawi yake pote nchini.
“Nawapongeza sana kwa kuona haja ya kushirikiana na Benki ya Posta ili kuwapelekea huduma wananchi wengi zaidi katika maeneo ambapo hamna matawi yenu.”Mbarawa.
Aidha Mbarawa alitumia fursa hiyo kuwata Waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla kuwa na mahusiano mema ili kudumisha amani.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Sanjay Rughani amesema kuwa Benki yao imeona umuhimu wa kupanua wigo wa huduma zao kutokana na kuwa na matawi machache nchini nzima.
Aliongeza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kusikia uhitaji wa wananchi hususan wakazi wa Arusha ambao waliomba kuongezewa matawi ya Benki hiyo kutoka tawi moja lililopo sasa.
Benki ya Standard Chartered Tanzania imeingia ubia na Benki ya Posta Tanzania ili kutoa huduma za kibenki kupitia matawi ya Benki ya Posta popote yalipo nchini na kwa kufanya hivyo kunatoa fursa kwa wananchi wengi zaidi kunufaika na huduma za Benki ya Standard Chartered Tanzania.

Megawati 200 kutumia jotoardhi kuanza kuzalishwa 2025

1 
Afisa Uwekezaji Mkuu kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Anitha Ishengoma (kushoto) akizungumza na  vyombo  vya habari kwenye Maonesho ya Kimataifa ya  Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
2 
Wananchi mbalimbali wakiangalia  vipeperushi katika  banda la  Wakala wa Jiolojia  Tanzania (GST) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya  Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
3
Mhandisi Uchenjuaji Madini  kutoka  Wakala wa Jiolojia  Tanzania (GST), Priscus Kaspana (katikati) akionesha kipande cha mwamba na kutoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya  Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
———————————————
Na Greyson Mwase
Imeelezwa kuwa Megawati 200 za  umeme unaotokana na jotoardhi nchini zinatarajiwa kuzalishwa ifikapo mwaka  2025 na kumaliza  changamoto ya ukosefu wa umeme nchini.
Hayo  yameelezwa na  Meneja Katika Masuala ya Sheria na Ukatibu kutoka Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Nchini (TGDC),  Mershil Kivuyo katika maonesho ya kimataifa ya  Sabasaba yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini  Dar es Salaam.
Akielezea  mikakati ya kampuni hiyo, Kivuyo alisema kuwa mpaka sasa maeneo  zaidi ya  50 yenye  viashiria vya  jotoardhi nchini  yamegunduliwa ambayo kwa sasa  yanafanyiwa kazi.
Alisema kuwa kampuni imeweka kipaumbele katika maeneo ya  Ngozi na Songwe mkoani Mbeya, Luhoi mkoani Pwani,  Kisaki mkoani Morogoro na Mount Meru mkoani Arusha.
Aliongeza kuwa utafiti wa kina umefanyika  Ziwa Ngozi ambapo inatarajiwa kuchimbwa visima virefu mwaka 2017.
Akielezea manufaa ya Jotoardhi Kivuyo alieleza kuwa nishati ya jotoardhi  itatumika kuzalisha umeme wa uhakika na hivyo kumaliza changamoto ya  ukosefu wa umeme na hivyo kuongeza uwekezaji kwenye viwanda.
Aliongeza matumizi mengine kuwa ni  pamoja na kukaushia mazao, kilimo cha maua na katika utengenezaji wa mabwawa.
Alisisitiza kuwa wawekezaji wanakaribishwa kwenye uwekezaji wa jotoardhi na kuchangia  kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AWAKUMBUKA WENYE UHITAJI.

Siku chache kabla ya kusherehekea Siku Kuu ya Idd, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (pichani), amekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula kwa watoto ajili ya yatima pamoja na wazee mkoani Mwanza.
Na BMG
Jana Mhe. Mongella alikabidhi mbuzi 20, mafuta ya kula ndoo 20, kila moja lita 20, mchele mifuko 20, kila mmoja ukiwa na kilo 50 pampja na sukari mifuko 20, kila mmoja ukiwa na kilo 25.
Vituo saba vya watoto yatima mkoani Mwanza vilinufaika na msaada huo ni Nabawi Mbugani, Markaz Riyabwa-Nyakurunduma, Markaz Sharif Said-Nyegezi, Markaz Sainaa, Islamic Yatima, Jawhary Butimba, Muuminu Kabuhoro pamoj na Masjid Noor-Nyakato huku kituo cha Wazee Bukumbi nacho kikinufaika na msaada huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (wa tatu kushoto) akikabidhi msaada wa vyakula kwa wahitaji mkoani Mwanza, ili kusherehekea katika sikukuu ya Idd inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi huu.
Baadhi ya ichimburi a.k.a mbuzi zilizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwa ajili ya kitoweo kwa watu wenye uhitaji wakiwemo yatima na wazee mkoani Mwanza ili waweze kusherehekea vyema siku kuu ya Idd.


MUSA SAID ASHIRIKI VYEMA KAMBI YA KIMATAIFA YA COPA COCA- COLA, UFARANSA

Nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari akifurahia na wenzake alioungana nao katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyopo jijini Paris nchini Ufaransa.
Musa Bakari akiwa katika nyuso ya furaha ndani ya kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyopo jijini Paris nchini Ufaransa.
Bakari, mwenye miaka 16, ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Tirav iliyoko wilayani Temeke, ambaye amepata nafasi hiyo kwa udhamini wa Kampuni ya Coca-Cola.
Kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola imefanyika kuanzia 29 June hadi Jumatatu 4 Julai 2016.

MAMA SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUITUNZA AMANI

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir akitoa Nasaha katika futari Maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ambapo  mufti mkuu aliwataka waislam kutojihusisha na matendo ya Kigaidi kwani hayaendani na maelekezo na mafundisho ya Allah.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa neno la shukrani kwa wageni waliojumuika kwenye futari aliyoiandaa nyumbani Oysterbay jijini Dar es Salaam kwake ambapo aliwataka Watanzania kudumisha mani na kuishi kwa upendo
Waalikwa kwenye Futari ilyoandaliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiswali muda mfupi kabla ya kufuturu.
Sehemu ya Wageni waliohudhuria
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya amani Sheikh Alhad Mussa akizungumza na waalikwa kwenye futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Padri John Solomon akitoa salaam za Kamati ya Amani wakati wa futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

No comments :

Post a Comment