Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Modi mara baada ya kuwasili
nchini Saa 5 usiku Julai 9, 2016.
Waziri M,kuu Modi, akiwapungia raia wa India waishio nchini wakati wa mapokezi yake
Waziri Mkuu Modi, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Waziri Mkuu Modi, akisalimiana na Balozi Kairuki
Waziri Mkuu Modi, akipokewa nanWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Waziri Mkuu Modi, akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini
Waziri
Mkuu wa Israeli, Benjamin Bibi Netanyahu, (katikati), akitabulishwa na
mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa Waziri wa Mambo ya Nje
wa Tanzania, Balozi Augustin Mahiga, (kushoto)na Rais wa Rwanda, Paul
Kagame (kulia), Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam
Desalegn, kwenye Ikulu ya Naklasero nchini Uganda.
NA K-VIS MEDIA/NA
MASHIRIKAYA HABARI
Waziri Mkuu wa Israeli,
Benjamin Bibi Netanyahu, amekuwa ni kiongozi wa kwanza wa juu wa serikali ya
nchi hiyo aliyeko madarakani kutembelea barani Afrika, tangu Yitzhak Rabin,
aliyepata kuwa waziri Mkuu wan chi hiyo amtembelee Mfalme Hassan II wa Morocco,
mnamo mwaka 1993.
Kituo cha kwanza cha
Netanyahu kutembelea Afrika iliku Uganda, akaenda Kenya, na kumaliziana
Ethiopia.
Akiwa Uganda, Netanyahu alifanya
mkutano na baadhi ya viongozi wa nchi za Kiafrika kutoka Sudan Kusini,
Tanzania, iliyowakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa,
Kikanda na Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga, na Zambia.
Hata hivyo pamoja na mkutano
huo na viongozi wa kiafrika nchini Uganda, vyombo vya habari havikuutilia
maanani zaidi mkutano huo na badala yake viliangazia zaidi tukio la kuzindua mnara
wa kumbukumbu ya miaka 40 ya operesheni ya kijeshi iliyofanywa na Makomandoo wa
Israeli wakati wakiokoa mateka raia wa Israeli kwenye uwanja wa ndege wa Entebe
mnamo mwaka 1976.
Katika operesheni hiyo ya
aina yake, kiongozi wa makomandoo hao, Yonatan Bibi Netanyahu, kaka wa Waziri
Mkuu Benjamin Netanyahu, aliuawa.
Israeli ililazimika kutuma
makomandoo wake kuokoa raia wake waliotekwa nyara wakiwa ndani ya ndege ya shirika
la ndegge la Ufaransa (Air France). Ndege hiyo ilitekwa nyara na wanamgambo wa
Kipalestina, dakika 15 baada ya kuruka kutoka uwanja wa nege wa Tel-Aviv nchini
Israel ikielekea Paris Ufaransa.
Wanamgambo hao wa
Kipalestina, walifanya tukio hilo wakishinikiza wenzao waliokuwa wakizuiliwa
kwenye magereZa nchini Israeli waachiliwe.
Tukio la kuuawa kwa Kakak wa
Waziri Mkuu wa Israeli, ndio lililomsukuma kiongozi huyo kuingia kwenye siasa.
Hata hivyo mataifa mengi ya
kiafrika hususan kusini mwa jangwa la Sahara, yalijuwa hayaiungi mkono Israeli
kutokana na ukandamizaji wake dhidi ya Wapalestina.
Ukiacha Uganda, Netanyahu alikwenda Kenya,
ambako enzi za utawala wa Kenyatta, Israeli ilikuwa swahiba wake, na hata
Netanyahu akisalimiana na Balozi Mahiga
Netanyahu (kushoto0, na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam
Desalegn
Netanyahu akiwa na Rais Museveni kwenye uwanja wa Entebe nchinihumo
Netanyahu akiweka shada la maua kwenye mnara huo wa kumbukumbu
Netanyahu akikagua gwaride la askari polisi nchini Kenya
Netanyahu akikagua gwaride uwanja wa ndege wa Entebe nchini Uganda
Netanyahu akiwa na Rais Uhuru Kenyatta, Ikulu ya Nairobi
Netanyahu akiteta jambo na mwenyeji wake, Rais wa Rwanda, Paul Kagame mjini Kigali |
Kiongozi wa operesheni ya kuokoa mateka wa Israeli, Komandoo Yonatan Bibi Netanyahu. Kaka wa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Bibi Netanyahu. Kiongozi huyo aliuawa kwenye harakati za kuokoa mateka |
Kampuni ya ChemicotexCotex wazalishaji
wa dawa ya meno aina ya Whitdent, imefanya sherehe kubwa ya kutimiza
miaka 25 tangu iingie sokoni kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam, Julai 9, 2016.
Katika sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi
alikuwa Katibu Mkuu wizraa ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
(Anayeshughulikia viwanda), Dkt. Adelhem Meru, imezindua promosheni
kamambe ambapo jumla ya magari mapya 25 yatashindaniwa. Pichani msichana
mrembo akiwa amesimama mbele ya magari hayo wakati wa uzinduzi wa
promosheni hiyo. (PICHA NA ALLY DAUDI-MAELEZO)
Dkt. Meru akionyesha boksi la dawa ya Whitedent wakati wa sherehe hiyo
Dkt. Meru akitoa hotuba yake
NA
ALLY DAUDI-MAELEZO
Tanzania
inatarajiwa kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2020 kwa kutumia sekta ya
viwanda vikubwa, vya kati na vidogo ili kupiga hatua katika maendeleo ya nchi.
Akizungumza
hayo hafla ya kutumiza miaka 25 ya dawa ya meno ya whitedent iliyofanyika leo
jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dk. Adellhem Meru amesema kuwa wameweka mkakati na
malengo ya kukuza uchumi wa kati kwa kutumia Mchango wa viwanda.
“Mpaka
kufikia mwaka 2020 lazima tufikie uchumi wa kati kutokana na Sekta ya viwanda
ili tuweze kuendelea na kupata pato la taifa kutoka
asilimia 7.5 mpaka asilimia 15 na kuwa na uchumi imara kama Watanzania”
alisisitiza Dkt. Meru.
Aidha
Dkt. Meru amesema kuwa katika malengo waliyojiwekea kwa serikali ya awamu hii
ni kuhakikisha mpaka mwaka 2020 ajira nyingi zitatokana na viwanda kufikia
asilimia 40 na kuendelea.
Katibu
Mkuu huyo ametoa rai kwa watanzania kwa kuwataka wwapende zaidi kutumia bidhaa za viwanda vya nyumbani kuliko
kupendelea bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
Mbali
na hayo Dkt. Meru aliwapongeza kiwanda kinachotengeneza dawa ya meno ya
Whitedent Chemi & Cotex kwa kutimiza miaka 25 tangu waanze kuzalisha bidhaa
hiyo na kuwataka waendelee na uzalishaji wao kwa miaka 25 ijayo.
Kwa
upande wa Afisa mkuu wa Chemi & Cotex Bw. Raja Swaminathan alisema kuwa
katika kusheherekea miaka 25 ya bidhaa yao wametaka kuwashirikisha watanzania
kwa kutoa magari 25 ili yashindaniwe na wananchi wote kwa miezi mitatu.
“Tungependa
kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika mafanikio yetu kwa kucheza shindano
hili kwa sababu bidhaa hii ni mali ya watanzania na inatengenezwa Tanzania “
alisisitiza Bw.Swaminathan.
Wafanyakazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo
Dkt. Meru akiteta jambo na Mkuu wa Operesheni wa CHEMICOTEX, Raja Swaminathan
Dkt. Meru akilishwa keki ya maadhimisho ya miaka 25 ya Whitedent kuwa sokoni
Dkt. Meru, akikaribishwa na wenyeji wake wakati akiwasili ukumbini
No comments :
Post a Comment