MUUAJI WA POLISI WATANO MAREKANI ALIFANYA TUKIO HILO PEKE YAKE
Micah Johnson, mtuhumiwa anayedaiwa
kuwauwa maafisa polisi watano kwa risasi katika maandamano huko
Dallas nchini Marekani inasaidikiwa alitenda tukio hilo akiwa peke
yake.
Akiongelea tukio hilo lililotokea
wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya Wamarekani weusi, Meya Mike
Rawlings amesema wanaamini kwa sasa mji wa Dallas upo salama.
Vifaa vya kutengenezea bomu, bunduki
aina ya rifle na jarida la kombati vilikutwa nyumbani kwa Johnson
ambaye aliwahi kulitumikia jeshi la Marekani nchini Afghanistan.
Johnson ambaye aliuwawa kwa bomu la
roboti, kabla ya hapo aliwaambia polisi amechoshwa na mauaji ya watu
weusi yanayofanywa na polisi, hivyo analipa kisasi kwa kuwauwa polisi
weupe.
Polisi wakitoka na vitu kwenye nyumba ya Micah Johnson
Aina ya bunduki aliyotumia Micah Johnson kuwadungua kwa risasi polisi
Micah Johnson kulia akiwa na kaka yake Tevin na mdogo wao wa kike Nicole
Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kamati hiyo inaundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi (administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).
Tuzo hizo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora.
HAFLA YA TUZO LIGI KUU YA VODACOM JULAI 17
Hafla
ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu.
Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kamati hiyo inaundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi (administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).
Tuzo hizo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora.
Waliopendekezwa
(nominees) kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ni Shiza Kichuya
(Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na Mohamed Hussein (Simba) wakati kwa
upande wa kipa bora ni Aishi Manula (Azam), Beno Kakolanya (Tanzania
Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga).
Kocha bora wapo Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga (Tanzania Prisons). Waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi ni Farid Mussa (Azam), Mohamed Hussein (Simba), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).
Waliongia kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent Agban (Simba). Waamuzi bora katika kinyang'anyiro hicho ni Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amewapongeza wateule wote waliopendekezwa kuwania tuzo hizo. "Kama wadhamini tuna matumaini makubwa kuwa msisimko wa ligi hii utazidi kuongezeka katika msimu ujao na kuzidi kuwapatia mashabiki wa soka wanaoifuatilia hapa nchini na nje ya nchi."
Alisema Vodacom itaendelea kudhamini ligi hiyo kubwa ya soka nchini ili kutekeleza moja ya malengo yao ya kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji nchini. Pia kuwawezesha wachezaji kujipatia ajira na kuboresha maisha yao kupitia sekta ya michezo bila kusahau kuwapatia burudani wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla.

No comments :
Post a Comment