Tuesday, July 5, 2016

WANANCHI WAZIDI KUMIMINIKA BANDA LA PSPF, MKURUGENZI MKUU AWASAIDIA WAFAMYAKAZI WAKE KUHUDUMIA WATEJA




 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akiyekaa, akimuonyesha Mwanachama huyu wa Mfuko huo michango yake papo kwa hapo kwenye banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016. Mamia ya Wananchi wamekuwa wakimiminika kwenye banda hilo, ambapo jambp la kuvutia Mkurugenzi Mkuu huyo aliungana na wafanyakazi wake kutoa huduma kwa wananchi. Maonyesho hayo yanashirikisha jumla ya nchi 30 ambapo banda la PSPF limekuwa na idadi kubwa ya wananchi wanaotembelea kujua huduma zitolewazo kwa wananchi ambao si wanachama lakini pia kuwahudumia wanachama wake. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
 Mama Anna Mkapa, (kulia), Mke wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la EOTF linalokusanya wajasiriamali kutoka mikoa yote ya bara na vuisiwani. Kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, wajasiriamali hao wanaweza kujiunga na Mfuko huo na hivyo kufaidika na mafao mbalimbali yakiwemo ya kuboresha biashara zao
 Mama Salma Kikwete, (kulia), Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, walipokutana kwenye banda la EOTF kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016.
 Mamia ya wananchi wakiwa kwenye banda la PSPF Julai 4, 2016
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo,  Mwanaidi Msangi baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Julai 4, 2016
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo,  Baturi J. Msusi, baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Julai 4, 2016
 Baturi J. Msusi mwanachama mpya wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), akionyesha kadi yake ya uanachama baada ya kujiunga leo Julai 4, 2016 na kupatiwa papo hapo.
 Mwanaidi Msangi, mwanachama mpya wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), akionyesha kadi yake ya uanachama baada ya kujiunga leo Julai 4, 2016 na kupatiwa papo hapo.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, (katikati), na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wizarani hapo, Ben Mwaipaja, wakipatiwa maelezo na Afisa wa UTT-AMIS, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwenye jengo la Wizara ya Fedha, viwanja vya Maonyesho ya Biashaya ya Kimataifa Mwalimu Nyerere, Maarufu kama Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimpatia maelezo ya kiutendaji Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, (watatu kushoto), Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele (wapili kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, (kulia), wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango ambayo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iko chini ya wizara hiyo.
 Afisa wa PSPF, Pensila (kushoto), akitoa elimu kwa wanachi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akimuhudumia Mwanachama huyu aliyefika kujua hali ya michango yake kwenye banda la Mfuko huo Julai 4, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu (aliyekaa0, akisaidiana na wafanyakazi wake kuhudumia wananchi Julai 4, 2016

MULTICHOICE TANZANIA KUBADILI MAISHA YA WATOTO YATIMA

Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kusherekea sikukuu ya Eid El Fitri, Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ndiyo wasambazaji wa ving’amuzi vya DSTV nchini imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima ambao wanaishi katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, misaada ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kusaidia kubadilisha maisha ya watoto hao.
 
Misaada ambayo imetolewa kwa watoto hao ni Cherehani 4, kapeti 12, vikombe 60, sahani 40, magodoro 11, shuka 40, tenga za nguo 3, jagi 6, beseni kubwa 3, sufuria 9, chupa za chai 4 na mikeka 6.
 
Akizungumzia misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo Multichoice imekuwa ikitoa kwa kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia kuishi maisha bora lakini pia kuwapatia msaada ambao unaweza kuwasaidia kuwa na uwezo wa kuingiza kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa kituo cha Al–Madina.
 
“Multichoice tumekuwa tukitoa misaada yetu kwa kituo hiki tangu 2009 na leo tumewaletea mwingine ikiwa ni kila mwaka tunafanya hivyi lakini kwa mwaka huu tumeleta pia Cherehani ambazo zitawasaidia kupata kipato,
 
“Pamoja na hayo pia tumewafungia king’amuzi ambacho watoto watakuwa wakiangalia vipindi balimbali baada ya kurejea nyumbani na tuna chaneli mbalimbali za vipindi vya watoto na burudani kwahiyo tunaamini kuwa watoto watafurahi,” alisema Chande.
 
Nae mlezi wa kituo hicho, Bi. Kuruthum Yusuf aliwataja Multichoice kama kampuni ambayo imekuwa mstari wa mbele kuwapatia misaada na kuyaomba makampuni mengine kuwa na utaratibu kama wa Multichoice wa kuwasaidia misaada kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao wanahitaji misaada ili kuboresha maisha yao.
Mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Al-Madina akizungumza kuhusu msaada ambao wamepokea na jinsi ambavyo Multichoice Tanzania imekuwa ikiwapatia misaada. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande.
 
“Tangu walipotufahamu wamekuwa wakitupatia misaada kila mwaka, niwashukuru sana kwa moyo wao na kutoa sio utajiri ila tu wana moyo wa kutoa na hata wenngine wanatakiwa kuwa na moyo kama wao (Multichoice) wa kusaidia,” alisema Bi. Kuruthum.
Pamoja na hayo pia, Bi. Kuruthum alieleza kuwa kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto ya vifaa vya shuleni kwa watoto ambao wanasoma.
Kutokana na msaada ambao umetolewa na Multichoice kwa watoto wa kituo cha Al-Madina ambacho kina watoto 57, wasichana wakiwa ni 23 na wavulana ni 34 basi ni wazi kuwa kama wakitumia msaada huo vyema basi kwa namna moja au nyingine wanaweza kubadilisha maisha yao kwa hatua fulani ambayo awali hawakuwa nayo kama vile kutumia cherehani kwa kushona nguo na kujiongezea kipato.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Sumalu akitoa neno la ufunguzi kuhusu misaada ambayo imekuwa ikitolewa na Multichoice Tanzania pamoja na historia fupi ya kituo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande akimkabidhi Cherehani, mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf. Wa tatu kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu wakiwa na wafanyakazi wengine wa Multichoice Tanzania.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akimpongeza mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf baada ya kukabidhiwa misaada na Multichoice Tanzania.

TANAPA WAFUNGUA OFISI JIJINI DAR ES SALAAM

 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya TANAPA jijini Dar es Salaam.
(Picha na Francis Dande)
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofisi za TANAPA jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata
utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
Baadhi ya wadau wa sekta ya Utalii wakiwa katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata  utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata  utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiangalia ofisi mpya ya TANAPA iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi. 
Kuangalia ofisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi (kushoto), akifafanua jambo wakati Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kulia) alipokuwa akikagua Ofisi ya Tanapa zilizopo jijijini Dar es Salaam. 
Chumba cha mikutano.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi (kulia), akifafanua jambo wakati Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto). 
Jengo la Ofisi za TANAPA zilizopo Dar es Salaam.

MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA (PS3) WAZINDULIWA MKOANI KIGOMA

 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga akizindua mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) katika mkoa wake wa Kigoma leo. Mradi huo wa miaka mitano unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID)  na utatekelezwa katika mikoa 13 nchini na kushirikisha Halamashauri 93.
 Mkuu wa Mkoa aliwataka watendaji wa Halamashauri hizo kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha mradi unaleta manufaa kwa jamii na mkoa
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Charles Pallangyo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini   Samsoni Anga, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga, Kiongozi wa Mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.
Kiongozi wa mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya akizungumza na kueleza dhumuni la mradi huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga.
 Mwakilishi kutoka Tamisemi, Mrisho Mrisho akizungumza kuhusiana na mradi huo na namna ambavyo serikali imejipanga kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya  Buhigwe, Kanali. Elisha Marco Gaguti, Mkuu wa Wilaya ya  Kakonko    Kanali.Hosea
Malonda Ndagala na
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Peter Bura.
 Mkuu wa Wilaya Kasulu,  Kanali. Martin Elia Mkisi akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Hoza Mlindoko, wakifuatilia mada katika uzinduzi huo. 

No comments :

Post a Comment