Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wa
pili kulia) akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, (wa kwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya
mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari, machapisho, uchapishaji na
vifaa vya ofisini, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, wakati
wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam
kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016.
Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles
Mwijage.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw.
Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi
wa Umoja wa Mataifa wakiwa na tuzo ya ushindi katika banda lao. Kulia
Felister Bwana wa Shirika la UNFPA Tanzania, Didi Nafisa (wa pili kulia)
pamoja na Hoyce Temu (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw.
Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi
wa Umoja wa Mataifa wakiwa na tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kipengele
cha habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini katika banda
lao. Kulia Felister Bwana wa Shirika la UNFPA Tanzania, Didi Nafisa (wa
pili kulia), Hoyce Temu (katikati) pamoja na Edgar Kiliba (kushoto).
Wataalamu wa mawasiliano na
Uhamasishajii (Communications, Advocacy and Partnership-COAP) wa ofisi
ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakifurahia
ushindi huo katika banda lao. Kutoka kushoto ni Edgar Kiliba, Hoyce Temu
na Didi Nafisa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw.
Alvaro Rodriguez (kulia) katika picha ya pamoja na vijana wanaojifunza
kazi ‘Intern’ katika ofisi za Umoja wa Mataifa, Edgar Kiliba (katikati)
na Msafiri Manongi.
Wananchi wakisaini kitabu cha
wageni katika banda la Umoja wa Mataifa lililopo ukumbi wa Karume kwenye
Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa almaarufu Sabasaba katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijni Dar es Salaam.
Kijana Msafiri Manongi
anayejifunza kazi ‘Intern’ (kushoto) wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji
(IOM), akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini sambamba na elimu ya Malengo ya Dunia (Global
Goals) kwa Maendeleo Endelevu kwa kijana mwenzake (jina halikuweza
kupatikana) aliyetembelea banda UN kwenye maonyesho ya Sabasaba
yanaoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
Kijana Msafiri Manongi
anayejifunza kazi ‘Intern’ kwenye Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)
(kushoto) akipozi na kijana mwenzake aliyetembelea banda la UN
kujifunza shughuli mbalimbali za UN Tanzania na kujinyakulia zawadi ya
tisheti.
Kijana Edgar Kiliba
anayejifunza kazi ‘Intern’ katika kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi
ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania (kulia), akitoa elimu ya Malengo ya
Dunia (Global Goals) kwa Maendeleo Endelevu kwa wananchi wanaoendelea
kufurika kwenye banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya Sabasaba
yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Mawasiliano na
Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, Didi Nafisa akitoa maelezo ya kazi mbalimbali za Umoja wa
Mataifa kwa Bw. Rehani Athumani wa NHIF (kulia) aliyetembelea banda la
UN Tanzania katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja
vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Kijana Edgar Kiliba anayejifunza kazi ‘Intern’ katika kitengo cha
Mawasiliano katika Ofisi ya Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
Tanzania.
Makamu wa Rais wa Powerline
Technologies Limited, Bw. Tumu Kaisi (kushoto) akibadilishana uzoefu na
Kijana Msafiri Manongi anayejifunza kazi ‘Intern’ (kushoto) wa Shirika
la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa
kwenye maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Mawasiliano na
Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, Didi Nafisa akimbandika zawadi ya beji ya’ HE 4 SHE’ ya Shirika
la UN Women katika kampeni ya kuhamasisha wanaume waweze kuwasapoti
wanawake katika nyanja mbalimbali kwa mmoja wa wananchi wanaoendelea
kutembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya Sabasaba
yanayoendelea kushika kasi jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni Baadhi
ya wananchi wakisoma vipeperushi na majirada mbalimbali katika banda la
Umoja wa Mataifa lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye maonyesho ya
Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mtoto akisoma moja ya vitabu
vyenye michoro ya katuni ambacho kilimvutia akisome alipotembelea banda
la Umoja wa Mataifa na wazazi wake.
Mmoja wa wananchi aliyetembelea
banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba akifurahia
zawadi ya tisheti yenye ujumbe mzito wa kukomesha ukatili wa kijinsia
inayosomeka “FUNGUKA” Tumia malaka yako KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA.
Kulia ni Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni
ya Zaidi Enterprises, Eng. Allen Kimambo katika picha na mabango ya
Malengo ya Dunia (Global Goals) ambayo ni sehemu anayoyafanyia katika
utekelezaji wa kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.
Mtaalamu wa Mawasiliano
Mwandamizi wa Ukanda wa Afrika wa Jhpiego, Bw. Charles Wanga akiwa na
mabango ya Malengo ya Dunia (Global Goals) kwa Maendeleo Endelevu katika
banda la UN Tanzania.
Mkutubi wa kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Harriet Macha katika picha ya pamoja na mmoja
wa vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya
Sabasaba.
Watoto nao waliwakilisha
Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu. Kulia ni Msafiri Manongi kutoka
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
Vijana wanaojifunza kazi katika
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini ‘Intern’ Edgar Kiliba (kushoto) na
Msafiri Manongi (kulia) katika picha ya pamoja na wananchi
wanaotembelea banda la Umoja wa Mataifa kujifunza shughuli mbalimbali
zinazofanywa na Mashirika hayo nchini.
Shirika la Umoja wa
Mataifa limenyakua tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari,
machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini katika sherehe za uzinduzi
wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye kwenye
viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na mgeni
rasmi Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame na kupokelewa na Mkuu wa Masharika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw.
Alvaro Rodriguez.
Umoja wa Mataifa umekuwa kinara
wa kuelimisha wananchi, kupitia njia mbalimbali ikiwemo redio, magazeti
mitandao ya kijamii na pia kushiriki katika maonyesho ya sabasaba kila
mwaka kwa Zaidi ya miaka 6 na kwa miaka 5 mfululizo wamekuwa wakishinda
tuzo hizo.
Umoja wa Mataifa mwaka huu
umekuja na kampeni ya uhamasishaji wa Malengo ya dunia (Global Goals) na
umuhimu wa watanzania kuyaelewa malengo hayo na kuwa mabalozi katika
kuhakikisha malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs)
yanatekelezeka.
Banda la Umoja wa Mataifa
linapatikana katika ukumbi wa Karume yanakoendelea maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa almaarufu ‘sabasaba’ katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
JAJI MKUU ATEMBELEA BANDA LA GLOBAL LINK EDUCATION VIWANJA VYA SABASABA
Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Chande Othman akiangalia baadhi ya
Ripoti zilizofanyiwa kati na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
alipotembelea Banda la Tume wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya
Biashara (SABASABA) katika viwanja vya JK Nyerere Dar es Salaam.
Ripoti zilizofanyiwa kati na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
alipotembelea Banda la Tume wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya
Biashara (SABASABA) katika viwanja vya JK Nyerere Dar es Salaam.
Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Chande Othman akipata maelezo katika
Banda la Mahakama ya Rufaa Tanzania
Banda la Mahakama ya Rufaa Tanzania
Jaji Mkuu Chande Othman akizungumza na Waandishi wa Habari mara
baada ya kumaliza kutembelea Banda la Mahakama katika viwanja vya Mwl.
JK Nyerere Dar es Salaam.
baada ya kumaliza kutembelea Banda la Mahakama katika viwanja vya Mwl.
JK Nyerere Dar es Salaam.
Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika viwanja vya JK
Nyerere Dar es Salaam wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa
(SABASABA) Picha zote na Munir Shemweta Tume ya Kurekebisha Sheria)
Nyerere Dar es Salaam wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa
(SABASABA) Picha zote na Munir Shemweta Tume ya Kurekebisha Sheria)
Jaji Mkuu , Othman Chande, akiwasili Viwanja vya maonesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es
Salaam.
Biashara ya Kimataifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es
Salaam.
Jaji
Mkuu , Othman Chande akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Global
Link Education, Abdumalik Mollel, wakati alipotembelea banda hilo
katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya
Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Jaji
Mkuu ,Othman Chande akiongozwa na Mkurugenzi wa Global Link Education,
Abdumalik Mollel, wakati alipokuwa akitembelea kuangalia huduma
mbalimbali kwenye Banda hilo jinsi Wananchi wanavyoweza kujiunga na
vyuo vya nje ya nchi, wakati akiwa katika maonesho ya 40 ya Biashara ya
Kimataifa Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Jaji
Mkuu Othman Chande, akioneshwa na Mkurugenzi wa Global Link
Education, Abdumalik Mollel, Tuzo mbalimbali walizowahi kutunukiwa.
Jaji
Mkuu Othman Chande, akioneshwa na Mkurugenzi wa Global Link
Education, Abdumalik Mollel, Tuzo mbalimbali walizowahi kutunukiwa.
Jaji
Mkuu , Othman Chande, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Global
Link Education, Abdumalik Mollel alipotembelea banda hilo
Sehemu ya wananchi wakipata huduma katika banda hilo la Global Link Education.
JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND KUSUMBUA TENA ULAYA,
Kikosi
kazi cha Ngoma Africa Band a.k.a FFU yenye makao yake kule
Ujerumani,wanategemewa kukwea majukwaa ya maonyesho Afrika-Karibik, siku
ya jumamosi 16 Julai 2016 mjini Bayreuth,Ujerumani pia siku ya 23 Julai
2016 katika tamasha kubwa la International Afrika Festival Tubingen,
siku ya 30 Julai 2016 watatumbuiza XXL Afro Sommer Jam mjini Stuttgart katika Kutur Arena. mzimu huo wa muziki wa bongo dansi utaendelea kudatisha washabiki siku 13 Agosti 2016 mjini Frankfurt katika Afro-Karibik viwanja vya Robestock Park,Frankfurt,Ujerumani.

Bendi
hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya imefanikiwa kuwanasa
maelfu washabiki kwa wingi inayoongozwa na mwanamuziki nguli Ebrahim
Makunja. a.k.a kamanda Ras Makunja wa FFU, itapeleka mzimu wake wote wa
dansi katika maonyesho hayo makubwa na ya aina yake kwa mashabiki wa
muziki katika maonyesho hayo, ambapo watakumbana “Jino kwa Jino” na
makombora ya muziki wa Ngoma Africa band.
Bendi
hiyo kwa sasa inatamba nyimbo zake za “Mapenzi ya Pesa” na single CD ya
“La Mgambo” pia msikose kusikiliza nyimbo “Supu ya Mawe” ,”Uhuru wa
Habari” na “Bongo Tambarare” ambazo zipo katika CD ya “BONGO TAMBARARE”
zote zinasikika katika kambi ya FFU au web yao
NAPE ASHUHUDIA GAME YA GOMS UTD NA BUGURUNI UTD WAKATI WA KOMBE LA NDANDA
Waziri
wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwasili kwenye
uwanja wa michezo wa Chuo cha bandari kushuhudia mechi ya mpira wa
miguuu kati ya timu ya Goms united ya Gongo la Mboto na Buguruni United.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwasalimia wachezaji wa timu ya Goms United kabla mechi kuanza
kwenye uwanja wa michezo wa Chuo cha bandari ambapo timu ya Goms United ya Gongo la Mboto ilicheza na na Buguruni
United
kwenye uwanja wa michezo wa Chuo cha bandari ambapo timu ya Goms United ya Gongo la Mboto ilicheza na na Buguruni
United
Mshambuliaji wa Buguruni United akijaribu kutaka kmtoka beki wa Goms unite.
Kipa wa Buguruni United akiruka bila mafanikio na kuruhusu goli la kwanza kufungwa na Goms United.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati mechi ya mpira
wa miguuu kati ya timu ya Goms United ya Gongo la Mboto na Buguruni
United .
wa miguuu kati ya timu ya Goms United ya Gongo la Mboto na Buguruni
United .
Amsha amsha ya mashabiki.
Sehemu ya watazamaji
Waziri
wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi
zawadi mchezaji bora wa siku kutoka timu ya Goms Utd, kushoto ni
Mkurugenzi wa Clouds Media Ndugu Joseph Kusaga.
Timu ya Goms Utd iliibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Buguruni Utd katika mzunguko wa 16 wa michuano hiyo ya Ndondo Cup.
KADI ZA VISA ZA BancABC KUPUNGUZA WIZI WA PESA
Mkuu wa Kitengo Cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo wa BancABC, Bi Joyce Malai akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kadi ya VISA ya BancABC maalum kwa wateja wao na hata wasio wateja wao. BancABC imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana viwanja vya sabasaba
Mkuu wa Masoko wa BancABC, Bi Upendo Nkini, akielezea faida za kadi Mpya ya VISA ya BancABC inayomwezesha mteja kufanya malipo ya mtandaoni kwa urahisi kwa kuwa kadi hiyo inalindwa kwa kutumia teknolojia mpya ya CHIP na PIN.
Wafanyakazi wa BancABC kitengo cha huduma kwa wateja Bw, Ally Miraji kushoto na Bi Neema David wakimuhudumia mmoja wa wateja aliyekuwa akichukua kadi ya VISA ya BancABC bw, Fredrick Israel katika banda la Bank hiyo viwanja vya sabasaba. BancABC imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi na kwamba ni njia bora ya kufanya malipo kupitia mitandao kwa kuwa imeunganishwa na mitandao ya simu kama Airtel Money, TigoPesa, na Mpesa. mteja ili kupata kadi hiyo sio lazima awe na akaunti ya BacABC. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana viwanja vya sabasaba
Wafanyakazi
wa BancABC kitengo cha huduma kwa wateja Bw, Ally Miraji kushoto na
wenzake wakitoa huduma ya maelekezo kwa bw, Ahmad Ibrahim kuhusu
matumizi ya kadi mpya ya VISA ya BancABC katika viwanja vya sabasaba.
BancABC imezindua kadi hiyo ya Visa ili kupunguzia wateja adha kubwa ya
kubeba fedha tasilimu wanaposafiri ndani na nje ya nchi na kwamba ni
njia bora ya kufanya malipo kupitia mitandao kwa kuwa kadi hiyo
imeunganishwa na mitandao ya simu kama Airtel Money, TigoPesa, na Mpesa
hafla ya uzinduzi ilifanyika jana viwanja vya sabasaba.
——————-
Kadi ya VISA ya BancABC ndio kadi pekee inayohudumia wateja wa huduma za fedha za mitandao ya simu.
BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imekuja na tiba ya kukithiri kwa wizi wa pesa ambao husababishwa na baadhi ya watu kuzunguka na fedha nyingi mifukoni mwao kwani imeanzisha kadi mpya ya Visa ambayo itaweza kujazwa pesa kwa kutumia shilingi ya Tanzania, Rand ya Afrika Kusini, Dola ya Kimarekani, Euro na Pauni ya Uingereza.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo Cha wateja binafsi na wafanya baishara wadogo, Bi Joyce Malai alisema kadi hiyo itaweza kutumiwa na wateja walio na wasio na akaunti za BancABC na kwamba itawapunguzia adha kubwa ya kubeba fedha tasilimu wanaposafiri nadani na nje ya nchi na kwamba ni njia bora ya kufanya malipo kupitia mitandao.
Alisema watatumia maonesho ya Saba Saba kuitangaza kadi hiyo na wateja wataweza kupata kadi ndani ya muda mfupi baada ya zoezi fupi la usajili ambalo ni papo kwa papo. “Ukiwa na kadi hii utaepuka usumbufu mkubwa mno kwani huhitaji kubeba fedha tasilimu na pia sio lazima uwe na akaunti ya benki,” alisema.
Alisema watumiaji wataweza kupata huduma masaa 24, siku saba kwa wiki mahali popote kupitia ATM zaidi ya 400 zenye huduma ya Visa nchini Tanzania ambapo ATM za aina hii zinafikia milioni 1.3 duniani na pia watumiaji wanaweza kufanya miamala kwa watoa huduma zaidi ya 1000 Tanzania na zaidi ya milioni 35 duniani kote.
“Tumepata ushuhuda na mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wetu ambao wana watoto wanaosoma nje ya nchi kwani wanaweza kuwatumia fedha za kujikimu kila mwezi bila kuingia gharama za ziada,” alisema.
“Kinachofaya kadi hii ya Visa iwe ya kipekee ni pale ambapo mteja anaweza kuweka fedha kwenye kadi kwa kutumia huduma ya kutuma pesa kupitia simu ya mkononi yoyote na tunajivunia kuwa benki yetu ndio yenye huduma hii pekee kwa sasa,” alisema.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko, Bi Upendo Nkini, faida nyingine za kadi hiyo ni kama vile kufanya malipo ya mtandaoni kwa urahisi zaidi, kuthibiti matumizi kwani utatumia kiasi cha fedha kilichoko kwenye kadi pekee na pia kuwa na amani kwani pesa zinakuwa salama kwani kadi inalindwa kwa kutumia teknolojia mpya ya CHIP na PIN.
Alisisitiza kuwa hii ndio kadi pekee ya Visa Tanzania ambayo unaweza kutumia kwa ruzuku tano ambazoni shilingi ya Tanzania, Rand ya Afrika Kusini, Dola ya Kimarekani, Euro na Pauni ya Uingereza na kwamba kadi hiyo, ambayo inaweza kutolewa kwa mtu kama zawadi, inaweza kutolewa nyingine pindi inapoibiwa au kupotea.
“Kadi hizi zitapatikana katika banda letu lililoko katika maonyesho ya Saba Saba Ukumbi wa Kimataifa lakini pia unaweza kutuma ujumbe mfupi wenye neno VISA ikifuatiwa na Wilaya uliyopo , kwenda namba 15774,” alisema.
Atlas Mara iliinunua BancABC in Juni 2014 huku ikizidi kujitanua Tanzania, , Botswana, Mozambique, Zambia na Msumbiji. Baada ya hapo ilinunua benki mbili nchini Rwanda (BR Commercial na BPR ambazo zinaendelea kukamilisha mchakato wa kuungana).

No comments :
Post a Comment