Tuesday, July 26, 2016

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA MJINI DODOMA


j1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Kushoto ni ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero.
j2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimwangalia  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier akisaini kitabu alichotunga kabla ya kumkabidhi Rais alipomtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016
j3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea kitabu kutoka kwa   Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier alipomtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016.
j4    
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Katikati ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero.j5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier  na ujumbe wake aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, wa tatu kulia ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero, kulia ni Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Fedha za Nje Bw. Johannes Jovin akifuatiwa na Mkrugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy. Kushoto ni Mshauri wa Rais Masuala ya Profesa Longinus Rutasitara akifuatiwa na Mshauri wa Rais masuala ya Diplomasia Balozi Zuhura Bundala.
PICHA NA IKULU

TBL Group yadhamini semina ya wakaguzi wa magari wa polisi Mwanza

1 
Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi wakifuatilia mafunzo wakati wa semina ya ukaguzi wa magari iliyofanika jijini Mwanza.
2 
Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi wakifuatilia mafunzo  ya ukaguzi wa magari kwa vitendo kutoka kwa Mkufunzi Hubert Kubo kutoka kampuni ya CFAO wakati wa semina ya ukaguzi wa magari iliyofanyika jijini Mwanza.
3 4 5 
Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi walitembelea maeneo ya kiwanda 7/8-.Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi  wakishauriana jinsi ya ukaguzi wa magari makubwa wakati wa semina hiyo.
………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu-Mwanza
Katika mkakati wake wa  kushirikiana na serikali na jamii katika kutoa elimu ya usalama,kampuni ya TBL Group imedhamini semina kwa  wakaguzi wa magari kutoka Jeshi la Polisi jijini Mwanza ambayo imefanyika katika kiwanda cha TBL cha Mwanza na kuendeshwa na Mtaalamu wa magari kutoka kampuni ya CFAO,Bw.Hubert Kubo.
Semina hiyo iliendeshwa kwa  njia shirikishi ambapo  washiriki walijadiliana masuala mbalimbali yanayohusiana na usalama barabarani na changamoto zilizopo katika kukagua vyombo vya moto na  jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini.

DK.KIKWETE :NI NGUMU VYAMA VYA UPINZANI KUSHINDA CHAGUZI ZIJAZO

indexMwenyekiti mstaafu wa chama cha mapinduzi (CCM)dk.Jakaya Kikwete akipewa zawadi na baadhi ya wazee wa wilayani Bagamoyo, kwenye sherehe  za kumpokea na kumkaribisha nyumbani baada ya kumaliza muda wake wa uongozi wa chama,sherehe  zilizofanyika juzi ukumbi wa chuo cha sanaa  (TASUBA).
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo- 26,July
MWENYEKITI mstaafu wa chama cha mapinduzi (CCM),dk Jakaya Kikwete amesema ni ndoto vyama vya upinzani kushinda katika chaguzi kuu zijazo kutokana na chama tawala kuwa imara na kujidhatiti katika kutekeleza ilani yake na kuwatumikia wananchi.
Aidha amesema anaimani nchi itaendelea kuwa na maendeleo makubwa na kuinua uchumi kutokana na kasi aliyonayo rais John Magufuli.
Sambamba na hayo dk.Kikwete ameeleza kuwa kwasasa anahitaji kupumzika na atakuwa anajishughulisha kilimo na ufugaji ambapo hayupo tayari kutoa ushauri wa mambo ya kiserikali na chama kwani kazi hiyo ina wenyewe na wanatosha.
Dk Kikwete alisema anashukuru mungu kipindi chake ameongoza na kuiacha nchi ikiwa na utulivu mkubwa licha ya uchaguzi mkuu uliopita kupitia kwenye kipindi kigumu.
Aliyasema hayo jana majira ya jioni huko mjini Bagamoyo kwenye ukumbi wa chuo cha sanaa (TASUBA)wakati wa sherehe za kumkaribisha baada ya kustaafu na kumkabidhi nafasi ya uenyekiti dk.John Magufuli.
“Namshukuru mungu  nchi iko salama na chama kiko imara nami kwa sasa nataka  nipumzike sitajihusisha na masuala ya kisiasa ama kiserikali nataka nipumzike badala yake nitajikita katika shughuli za kijamii ikiwemo kufuga na kilimo”
“Mkija kufuata ushauri pale mtakapohitaji ,lakini naomba mkija mje kwa ajili ya suala la maendeleo nitakuwa tayari na sio kwa suala la kutoa ushauri kuhusu serikali hapana kwani kwa sasa kuna viongozi ambao wanauwezo na nawaamini kwa kiasi kikubwa”alisema Kikwete.
Dk Kikwete hakuna kitu kilichokuwa kikimpa wakati mgumu kama chama ama serikali kushindwa kufanikiwa malengo yake kwenye uongozi wake.
Alisema hali ya kushindwa ilikuwa ikimpa wakati mgumu na kujiona endapo angeshindwa basi angewaangusha Wanabagamoyo na Pwani nzima.
Dk.Kikwete alieleza kwamba anamshukuru mungu katika uongozi wake aliweza kufanya kazi na kuleta maendeleo makubwa na kuiacha nchi mahali pazuri na salama huku ikiwa imetulia.
Aliwataka watanzania kumuombea na kumuunga mkono rais dk. John Magufuli ili aweze kuleta maendeleo .
Awali wabunge wa mkoa huo wakiongozwa na mbunge wa jimbo la Bagamoyo dk Shukuru Kawambwa alisema wataendelea kumuenzi Kikwete kwa kujenga mnara wa kumbukumbu kwenye ofisi ya CCM mkoani Pwani.
Alisema kuwa ujenzi huo utaanza mara moja na watamwalika kuuzindua utakapokamilika ili iwe kielelezo kwa wabunge na kumbukumbu ya kizazi kijacho.
Dk .Kawambwa alisema baada ya kung’atuka mwenyekiti huyo mstaafu wataendelea kuchota hekima na burasa zake zilizomfanikisha kukiongoza chama hicho na serikali kwa kipindi cha miaka 10.
Kwa upande wake katibu wa CCM mkoani Pwani Joyce Masunga alieleza mkoa unampongeza kwa kuiongoza nchi na kuiletea mafanikio makubwa .
Nae mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo ,Maskuzi alisema dk Kikwete alifanikiwa kuleta maendeleo makubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu na mpango wa shule za kata ambao mpango huo umeonyesha mafanikio kwa mwaka huu kuongoza kwenye matokeo.
Alisema eneo jingine la kujivunia ni nishati ya umeme ambayo ni moja ya mafanikio kupitia mpango wa umeme vijijini( REA) na miundombinu ya madaraja makubwa ,vivuko,viwanja vya ndege na barabara kwa kiwango cha lami.

certificate of appreciation to the Marketing Manager of the Dragon Mabati.

New Picture 
Managing Director of the Green Pastures Orphanage Centre, Mr.   Nicolas Kiseu hands over the certificate of appreciation to the Marketing Manager of the Dragon Mabati, Mr Andrew Sun for the company’s   financial and material support to the centre.  The company donated various construction materials worth 10m/= . On the Managing Director left is the Matron Naomi Doglous.

KAMPUNI YA MGODI WA GEITA GOLD MINING (GGM) YAFANIKISHA ZOEZI LA KUKUSANYA PESA KWA AJILI YA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.

 
Mkuu wa wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiongozana na kundi la wapanda mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining (GGM) waliopanda kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi.

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM)  ,Simon Shayo akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya kundi la wapanda mlima wakiwemo wafanyakazi wa mgodi huo waliopanda kwa leongo la kuchangisha fedha  za kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi.

Kiongozi wa kundi la wafanyakazi wa kampuuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining ,Kelvin Yasiwa akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kuwasili wakitokea katika kilele cha Uhuru ,Mlima  Kilimanjaro.

Balozi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto akizungumza mara baada ya kurejea salama kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto Lucy Mashauri(15)baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto Jacob Musa (16) baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

TAMASHA LA MZANZIBARI NI KUWAUNGANISHA WAZANZIBAR KATIKA KUDUMISHA UTAMADUNI-Chimbeni Kheri

PEMBA-ZANZIBAR 
Na Maryam Kidiko/Kijakazi Abdalla-Maelezo Zanzibar  
……………………………..
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema lengo kuu la kufanywa tamasha la Utamaduni wa Mzanzibar ni kuwaunganisha wazanzibar katika kulinda na kudumisha utamaduni huo.
Hayo yameelezwa mshauri wa Raisi katika mambo ya utamaduni Chimbeni Kheri   katika ufungaji wa tamasha la 21la utamaduni wa mzanzibar huko Fukuchani Wilaya ya kaskazini  A”.
Amesema kuwa utamaduni huo pia unawakutanisha wazanzibar kutoka sehemu mabali mbali ili waweze kubadilishana mawazo juu ya njia bora ya kuendeleza utamaduni kupitia njia ya sanaa.
Aidha amesema utamaduni ni roho ya taifa hivyo unahitaji kuenziwa , kuendelezwa, kurithiwa na watoto wetu katika michezo mbali mbali ya kiutamaduni .
“ Utamaduni ni muhimu sana kwani hujenga afya ,kukuwa kwa kiakili na hupata ajira kwani dunia ya sasa inazingatia sekta ya sanaa na utamaduni katika ustawi wa maendeleo ya kimataifa.Alisema Chimbeni.
Hata hivyo ameeleza kuwa majanga mengi katika jamii hujitokeza kwa kuacha mila na desturi za kizanzibar hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuurejesha utamaduni wetu .
Sambamba na hayo amesema kuwa Serikali imeweka mazingira mzuri yakuwawezesha  Wasanii wa fani zote ili kuweza kunufaika na kazi zao ili kuweza kuchangia pato la taifa .
“Katika suala la utamaduni serikali imechukuwa hatua  madhubuti ikiwa ni pamoja na kuifanyia marekebisho sheria inayohusu mambo ya utamaduni ili iendane na mahitaji ya Jamii” Alisema mshauri huyo.
Nae Waziri waHabari Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma amesema Wizara yake itashirikaana na Wizara ya elimu kuhakikisha somo la utamaduni linarudi katika skuli ili watoto waweze kuzijuwa mila na utamaduni wao .
Waziri huyo amefafanuwa zaidi kuwa suala la utamaduni litaendelea kuwepo  na kuwa la kihistoria  na  kila mmoja anatakiwa kuwa balozi wa mwenziwe ili kuweza kuulinda utamaduni huo usipotee katika visiwa vyetu.
Sambamba na hayo Tamasha hilo limejumuisha michezo mbalimbali ya kiutamaduni ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Dumisha utamaduni na amani , piga vita udhalilishaji .
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments :

Post a Comment